Kuzikurubisha nyoyo

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Kutia nguvu nyoyo)


Kutia nguvu nyoyo (Kiarabu: المؤلفة قلوبهم) ni msaada na himaya ya kiuchumi ya Mtume (s.a.w.w), Imamu (a.s) na mtawala wa Kiislamu kwa makafiri, wanafiki au Waislamu ambao wana imani dhaifu na hilo hufanyika kwa lengo la kuwafanya wawe pamoja na Waislamu na wautetee Uislamu. Wanaopatiwa himaya na msaada huu kwa lengo hili wanatambulika kwa jina la ((الْمُؤَلَّفَة قُلُوبُهُمْ)) au ((مُؤَلَّفَةُ القُلُوب)) "watu wa kutiwa nguvu nyo zao". Katika sira na mwenendo wa Bwana Mtume (s.a.w.w) watu miongoni mwa washirikina walikuwa wakitiwa nguvu nyoyo zao.

Qur'an Tukufu imebainisha moja ya sehemu ya matumizi ya zaka ni kupatiwa watu wa kutiwa nguvu nyoyo zao. Baadhi ya mafakihi wa Kishia wanaamini kwamba, hukumu hii ya kifiq'h (kisheria) sio maalumu na mahususi katika zama za Bwana Mtume (s.a.w.w.) au zama za uwepo wa Imamu Maasumu (a.s), bali inatekelezwa pia katika zama za ghaiba.


Utambuzi wa maana na nafasi yake

Ili kujua zaidi angalia pia hapa: Aya ya zaka

Kutia nguvu nyoyo ni maudhui za kifiq'h ambayo ina maana ya kutoa msaada na himaya ya kiuchumi kwa kundi miongoni mwa makafiri, wanafiki au Waislamu ambao imani yao ni dhaifu (wana hali ya kulegalega katika imani) [1], ambapo hilo hufanyika ili kuwafanya wawe katika njia ya kuutetea Uislamu. Hilo hufanywa na Mtume (s.a.w.w), Imamu Maasumu (a.s) au mtawala wa Kiislamu. [2] Watu hawa wanafahamika kama wa kutia nguvu nyoyo zao. [3]

Qutb Rawandi (aliyefariki 573 Hijiria) anasema kuwa: Lengo la Mtume (s.a.w.w) kulipatia zaka kundi hili ni kuwafanya wamili na kuelekea kwa Uislamu na kuwaimarisha. [4] Kwa mujibu wa ripoti ya ibn Kathir (mmoja wa wanahistoria na wasomi wa elimu ya hadithi wa Ahlu-Sunna katika karne ya 7 Hijiria) ni kwamba, himaya ya kifedha ya Mtume (s.a.w.w) kwa baadhi ya Washirikina baada ya Fat'h Makka (kukombolewa Makka) ilipelekea takribani watu 2,000 miongoni mwao kufuatana na Mtume katika vita vya Hawazin. [5]

Mafakihi wakitumia Aya ya 60 ya Surat at-Tawbah wametambua kuwa, moja kati ya sehemu nane za matumizi ya zaka ni kutia nguvu nyoyo. Muhammad Jawad Mughniyah (1322-1400 Hijiria), mfasiri wa Kishia anasema kuwa, moja ya sababu za kutoa himaya ya kiuchumi kwao ni kuondoa na kujikinga na shari yao. [7]

Sira ya Mtume (s.a.w.w)

Katika zama za uhai wa mbora wa viuumbe Mtume Muhammad (s.a.w.w) watu miongoni mwa washirikina mithili Safwan bin Umayya na watu miongoni mwa wanafiki kama Abu Sufyan walikuwa watu wa kutia nguvu nyoyo. [8] Safwan bin Umayya alipigana vita bega kwa bega na Waislamu katika Vita vya Hunayn na alinufaika pia na hisa ya ghanima. [9] Hassan bin Farhan Maliki (alizaliwa 1390 Hijiria), mmoja wa Maulamaa wa Ahhlu Sunna anaamini kwamba, Mtume wa Allah baada ya Fat'h Makka (kukombolewa Makka) alilipa mali kundi miongoni mwa walioachiliwa huru kama Abu Sufyan, Muawiya, Safwan bin Umayya na Mut'i bin Asud katika mlango wa kutia nguvu nyoyo. [10]


Mifano ya kutia nguvu nyoyo

Mafakihi wana mitazamo tofauti kuhusiana na ni akina nani hasa ambao ni watu wa kutia nguvu nyoyo. Baadhi yao ni:

  1. Makafiri: Sheikh Mufid (336 au 338-423 Hijiria) anaamini kwamba, kutia nguvu nyoyo ni kwa ajili ya kuwavutia makafiri kwa ajili ya kushirikiana na Waislamu katika jihadi. [11] Muhaqqiq Hilli (602 Hijiria) katika kitabu chake cha al-Mu'tabar amemtambuua Sheikh Tusi kuwa mmoja wa wafuasi wa nadharia hii pia. [12] Muqaddas Ardebili (aliyefariki 993 Hijiria) naye pia ameungana na nadharia ya Sheikh Tusi. [13]
  2. Wanafiki: Ibn Junayd (mmoja wa mafakihi wa Kishia wa karne ya 4 Hijiria) anaamini kwamba, kuutia nguvu nyoyo kunajumuisha wanafiki tu [14] ili kwa njia hiyo nyoyo zao zilainike na waachane na nifaki. [15]
  3. Waislamu ambao ni dhaifu wa imani: Kwa mujibu wa baadhi ya mafakihi kama Qut al-Din Rawandi katika kitabu cha Fiqh al-Qur'an na Sheikh Yusuf Bahrani (aliyefariki 1186 Hijiria) katika kitabu cha al-Hadaiq al-Nadhirah ni kuwa, asili ya kutia nguvu nyoyo inajumuishha Waislamu ambao wana imani ya tawhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) lakini mpaka sasa Utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) bado haujaingia ndani ya nyoyo zao. [16]
  4. Makafiri, wanafiki na Waislamu: Mtazamo mwingine ni huu kwamba, asili ya kutia nguvu nyoyo, asili yake ni aam yaani jumuishi na na inajumuisha makafiri, wanafiki na Waislamu ambao ni dhaifu wa imani, Waislamu wanaoishi mipakani na mfano wao. [17] Aghalabu ya mafakihi kama Shahid al-Awwal, [18] Shahid al-Thani, [18] Muhaqqiq Karaki, [19] Swahib Jawahir [20] na Imamu Khomeini [21] ni miongoni mwa wafuasi wa nadharia na mtazamo huu. [22] Mwandishi wa makala ya "Taalif al-Qulub va Siyasat" anaamini kwamba, inawezekana kutumia hisa ya "kutia nguvu nyoyo" kwa malengo ya Kimwenyezi Mungu na kuziunga mkono kifedha baadhi ya harakati za kupigania ukombozi ulimwenguni; ili kwa njia hiyo iwezekane kudhamini asili ya kulingania mwito wa tawhidi na itikadi nyingine na thamani nyingine za kidini. [23]


Hukumu ya kutia nguvu nyoyo katika zama za ghaiba

Kuhusiana na kwamba, hukumu ya kutia nguvu nyoyo katika zama za ghaiba (zama hizi ambazo Imamu Mahdi yuko ghaiba) inatekelezwa au la, kuna tofauti za kimtazamo baina ya mafakihi. [24] Baadhi yao kama Muhaqqiq Hilli, Imamu Khomeini na Jawadi Amoli wanasema: Katika zanma za ghaiba pia, hukumuu hii inatekelezwa. [25] Kundi jingine kama Sheikh Tusi anaamini kwamba, kutia nguvu nyoyo sharti lake ni kipindi cha kufanyika jihadi na anasema kwamba, kwa kuwa jihadi ni sharti awepo Imamu (a.s), hisa hii pia nayo haipo.[26]

Fadhil Miqdad amelinasibisha na Maulamaa wa Kishia suala la kudondoka (kutofanyiwa kazi) hisa ya kutia nguvu nyoyo katika zama za ghaiba. [27] Shafii na Abu Hanifa ambao ni miongoni mwa mafakihi wa Ahlu-Sunna wanaamini kwamba, kutia nguvu nyoyo ni hukumu ambayo haitekelezwi baada ya zama za Mtume (s.a.w.w) na kwamba, hukumu hii ya kifiq'h imefutwa. [28]

Rejea

Vyanzo