Ibrahim bin Mahzyar
Ibrahim bin Mahzyar Ahwazi (Kiarabu: إبراهيم بن مهزيار الأهوازيّ), mpokezi wa hadithi wa Kishia wa karne ya tatu Hijria alikuwa mmoja wa masahaba wa Imam Jawad (a.s) na aliyekuwa akinukuu hadithi kutoka kwa Imamu Hadi (a.s) na Imam Askari (a.s).
Katika vyanzo vya hadithi vya Shia, kuna hadithi zilizonukuliwa kutoka kwa Ibrahim bin Mahziyar. Kulingana na Ayatullah Khui, jina lake linaonekana katika zaidi ya simulizi 50. Wanachuoni wa Kishia wametofautiana kuhusu kuwa na itibari hadithi za Ibrahim bin Mahziyar. Ili kuthibitisha kutegemewa na kuaminika kwake, imetolewa hoja kwamba jina lake limejumuishwa katika nyaraka za baadhi ya hadithi za Kitabu cha Kamil Al-Ziyarat.
Histori ya Maisha Yake
Ibrahim alitoka Dauraq, Khuzestan.[1] Kwa mujibu wa Najashi, baba yake alikuwa Mkristo na alisilimu.[2] Hakuna taarifa kamili na makini kuhusu tarehe ya kuzaliwa na kifo cha Ibrahim bin Mahziyar. Hata hivyo, baadhi ya watafiti wamekadiria kwamba, zama za maisha yake kuwa ni kipindi cha kati ya mwaka 195-265 Hijria, wakitaja baadhi ya sababu.[3] Sababu hizo ni pamoja na kwamba alikuwa mmoja wa masahaba wa Imamu Jawadi (a.s) (aliyeuawa shahidi mwaka 220 Hijria)[4] na alikuwa hai baada kuuawa shahidi Imam Hassan Askari (a.s) (kuuawa shahidi mwaka wa 260 H)[5] na katika hadithi, anajulikana kama mmoja wa masahaba wa Imam Mahdi (a.t.f.s)[6].
Ali na Muhammad walikuwa watoto wa Ibrahim Mahziyar; Muhammad alikuwa mmoja wa masahaba wa Imam wa 11[7] na kwa mujibu wa riwaya, alikutana na Imam wa Zama (a.t.f.s).[8] Kwa mujibu wa Ali Akbar Ghafari, jina la Ali halikuonekana katika vitabu vya Rijaal (vitabu vya kueleza wasifu wa wapokeaji wa hadithi).[9]
Katika baadhi ya vyanzo vya vitabu hivyo (vya Rijaal) na hadithi vya Kishia, kuniya yake imetajwa kuwa ni Abu Is'haq.[10]
Sahaba wa Maimamu
Sheikh Tusi amemhesabu Ibrahim bin Mahziyar kuwa ni mmoja wa masahaba wa Imamu Jawad (a.s)[11] na Imam Hadi (a.s)[12]. Kwa mujibu wa riwaya iliyosimuliwa katika Kitabu cha al-Kafi kutoka kwa Muhammad ibn Ibrahim ibn Mahziyar, inaelezwa kuwa, baba yake, Ibrahim ibn Mahziyar, alikuwa wakala na mjumbe wa Imam wa 11 wa Mashia.[13] Ayatullah Khui ameiona riwaya hii kuwa dhaifu.[14]
Kukutana na Imamu wa Zama (a.t.f.s)
Kwa kuzingatia riwaya iliyosimuliwa na Sheikh Saduq, Ibrahim bin Mahziyar alikutana na Imam wa Zama (a.t.f.s) huko Makka.[15] Hata hivyo Ayatullah Khui alitilia shaka itibari na usahihi wa riwaya hii.[16] Aidha katika hadithi kumeashiriwa mawasiliano na maingiliano yake na wajumbe na mawakala wa Imamu Mahdi (a.t.f.s). [17] Fadhl bin Tabarsi amemchukulia kuwa mmoja wa mabalozi na wawakilishi wa mtukufu Mahdi.[18] Allamah Hilli kwa mtazamo wake riwaya hii ni dhaifu.[19]
Nafasi Yake katika Wapokezi wa Hadithi
Kwa mujibu wa Ayatullah Khui, wasomi na wataalamu wa elimu ya wasifu wa wapokezi wa hadithi wa Kishia wana tofauti ya maoni kuhusu Ibrahim bin Mahziyar; Allama Majlisi alimchukulia kama mtu wa kuaminika [20] na Ibn Dawud Hilli alimchukulia kama mtu aliyesifika [21].[22] na Abdul Nabii Al-Jazairi alimjumuisha katika sehemu ya watu dhaifu katika kitabu chake cha Hawi al-Aqwal.[23]
Mamaqani na baadhi ya wengine wakiwa na lengo la kuthibitisha kuaminika Ibrahim Mahziyar pamoja na kusifika kwake wametegemea baadhi ya sababu; ikiwa ni pamoja na kuwa kwake wasii aliyeainishwa na Ali bin Mahziyar, na kuwa kwake balozi wa Mahdi (a.t.f.s)[24]. Sayyid Abul-Qassim Khuii, mwandishi wa kitabu cha Muu'jam Rijal al-Hadithi chenye juzuu 33 ameziona hoja za kumsifu na kumsadikisha kuwa ni dhaifu na yeye mwenyewe akiwa na lengo la kuthibitisha kuaminika Ibrahim bin Mahziyar ametoa hoja ya kuweko jina lake katika kitabu cha Kamil Al-Ziyarat.[25][26] Baadhi ya watafiti wa zama hizi wamezingatia nukuu ya msimuliaji katika kitabu kamili cha Al-Ziyarat kuwa ni uthibitisho wa jumla wa kuwa kwake mtu wa kuaminika na kutegemewa;[27] kwa sababu Ibn Qulawayh amesema katika utangulizi wa kitabu cha Kamil Al-Ziyarat kwamba alinukuu tu kutoka kwa wapokezi wa kuaminika; katika kitabu hiki.[28]
Hadithi
Kuna hadithi zilizonukuliwa na Ibrahim bin Mahziyar katika vyanzo vya hadithi ya Shia, vikiwemo Kutub al-Ar’baa (Vitabu Vinne).[29] Kulingana na Ayatullah Khui, jina lake linaonekana katika zaidi ya simulizi 50. [30]
Ibrahim bin Mahziyar amenukuu hadithi kutoka kwa Imamu wa 10 na 11[31] wa Mashia kwa njia ya moja kwa moja.[32] Yeye amenukuu hadithi kupitia wapokezi kama vile kaka yake Ali,[33] Salih bin Sandi, Ibn Abi Umayr, Husayn bin Ali bin Bilal, Khalilan bin Hisham na kaka yake Dawud bin Mahziyar.[34]. Pia, Abdullah bin Jafar Humayr,[35] Saad bin Abdullah Ash'ari,[36] Muhammad bin Ahmad bin Yahya na Muhammad bin Ali bin Mahbub ni miongoni mwa wapokezi waliosimulia hadithi kutoka kwake.[37]
Ibrahim, amepokea hadithi katika nyanja kama vile wakati wa kufa shahidi na umri wa Maimamu, [38] fadhila za kuswali katika Msikiti wa Mtume[39] na Msikiti wa Kufa,[40] malipo ya kumzuru Imam Hussein (a.s).[41] Kadhalika amepokea hadithi kuhusu hukumu za Sala[42] na Hija.[43] Baadhi ya mafaqihi wa Kishia, kama Sahib Jawahir, wamenukuu riwaya kutoka kwake kuhusu hukumu za Sala.[44]
Najashi amekinasibisha kitabu kiitwacho al-Bisharaat kwa Ibrahim bin Mahziyar.[45]Baadhi ya wanachuoni wamesema kuwa kuna uwezekano kwamba al-Bisharaat ni kitabu kile kile cha kaka yake Ibrahim Mahziyar yaani Ali bin Mahziyar[46], ambacho kimesimuliwa na Ibrahim bin Mahziyar[47] na Najashi amekinasibisha naye.[48]
Rejea
- ↑ Najashi, Rijal al-Najashi, 1365 S, uk. 253, 1365 S.
- ↑ Najashi, Rijal al-Najashi, 1365 S, uk. 253, 1365 S.
- ↑ Guzashte, Ibrahim bin Mahziyar, juz. 2, uk. 458.
- ↑ Tusi, Rijal al-Tusi, uk. 373, 1373 S.
- ↑ Kulaini, al-Kafi,, juz. 1, uk. 518. 1407 H.
- ↑ Saduq, Kamal al-Din, uk. 445-453. 1395 H.
- ↑ Tusi, Rijal al-Tusi, uk. 402, 1373 S.
- ↑ Saduq, Kamal al-Din, juz. 2, uk. 442, 1395 H.
- ↑ Saduq, Kamal al-Din, juz. 2, uk. 466, 1395 H.
- ↑ Najashi, Rijal al-Najashi, uk. 16, 1365 S, Mamaqani, Tanqih al-Maqal, juz. 5, uk. 17, 1431 H.
- ↑ Tusi, Rijal al-Tusi, uk. 374. 1373 S.
- ↑ Tusi, Rijal al-Tusi, uk. 383. 1373 S.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 1, uk. 518. 1407 H.
- ↑ Khui, Mu'jam Rijal al-Hadith, juz. 1, uk. 305. 1410 H.
- ↑ Saduq, Kamal al-Din, uk. 445-453. 1395 H.
- ↑ Khui, Mu'jam Rijal al-Hadith, juz. 1, uk. 305. 1410 H.
- ↑ Kashi, Rijal Kashi, uk. 531-532. 1409 H.
- ↑ Tabarsi, I'lam al-Wara, uk. 416. 1390 H.
- ↑ Allamah Hilli, Khulasah al-Aqwal, uk. 51, 1417 H
- ↑ Allamah Majlisi, al-Wajizah fi al-Rijal, uk. 16; Mamaqani, Tanqih al-Maqal, juz. 5, uk. 31, 1431 H.
- ↑ Ibnu Daud Hilli, Kitab al-Rijal, uk. 19. 1342 S.
- ↑ Khui, Mu'jam Rijal al-Hadith, juz. 1, uk. 304. 1410 H.
- ↑ Jazairi, Hawi al-Aqwal, juz. 2, uk. 249, 1418 H.
- ↑ Mamaqani, Tanqih al-Maqal, juz. 5, uk. 18-31, 1431 H; Nuri, Mustadrak al-Wasail, juz. 4, Khatamah, uk. 26-29. 1408 H.
- ↑ Tazama: Ibnu Qaulawiyah, Kamil al-Ziyarah, uk. 21, 25, 31, 49, 85, 155 va 191, 1356 H.
- ↑ Khui, Mu’jam Rijal al-Hadith, juz. 1, uk. 307, 1410 H.
- ↑ Irwani, Durus Tamhidiyyah Fi al-Qawad al-Rijaliyyah, uk.5, 1431 H.
- ↑ Ibnu Qaulawiyah, Kamil al-Ziyarah, uk. 4, 1356 S.
- ↑ Tazama: Kulaini, al-Kafi, juz. 1, uk. 457, 461, 463, 1407 H, Saduq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, juz. 1, uk. 263, juz. 2, uk. 444, 1413 H.
- ↑ Khui, Mu'jam Rijal Hadith, juz. 1, uk. 307 1410, H.
- ↑ Tazama: Saduq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, jld. 1, uk. 263, 1413 H.
- ↑ Khui, Mu'jam Rijal Hadith, juz. 1, uk. 307 1410, H.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 1, uk. 457, 461, 463, 1407 H.
- ↑ Khui, Mu'jam Rijal Hadith, juz. 1, uk. 307 1410, H.
- ↑ Tazama: Kulaini, al-Kafi, juz. 1, uk. 307, 1407 H.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 1, uk. 457, 1407 H
- ↑ Khui, Mu'jam Rijal Hadith, juz. 1, uk. 307 1410, H.
- ↑ Tazama: Kulaini, al-Kafi, juz. 1, uk. 457, 461, 463, 472, 475,486, 491, 497, 518, 1407 H.
- ↑ Ibnu Qaulawiyah, Kamil al-Ziyarah, uk. 21, 1356 S.
- ↑ Ibnu Qaulawiyah, Kamil al-Ziyarah, uk. 31-32, 1356 S.
- ↑ Ibnu Qaulawiyah, Kamil al-Ziyarah, uk. 155, 1356 S.
- ↑ Saduq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, juz. 1, uk. 263. 1413 H.
- ↑ Saduq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, juz. 1, uk. 444. 1413 H.
- ↑ Najafi, Jawahir al-Kalam, juz. 8, uk. 63; Amili, Miftah al-Karamah, juz. 5, uk. 458, 1419 H.
- ↑ Najashi, Rijal al-Najashi, uk. 16, 1365 S.
- ↑ Tusi, Fehrest Kitab al-Shiah, uk. 265, 1420 H.
- ↑ Najashi, Rijal al-Najashi, uk. 254, 1365 S.
- ↑ Guzashte, Ibrahim bin Mahziyar, juz. 2, uk. 458.
Vyanzo
- Ibn Dawud al-Hilli, Ḥasan bin Ali. Kitab al-rijal. Tehran: Danishgah-i Tehran, 1342 S.
- Ibn Qulawayh, Ja'far bin Muḥammad. Kamil al-ziyarat. Tas-hih: 'Abd al-Ḥusayn Amini. Najaf: Dar al-Murtadhawiyya, 1356 S.
- Irawani, Muḥammad Baqir al-Durus tamhidiyya fi al-qawa'id al-rijaliyya. Qom: Intisharat-i Madyan, 1431 H.
- Jaza'iri, 'Abd al-Nabi. Hawi l-aqwal fi ma'rifat al-rijal. Qom: Muʾassisa al-Hidaya li-Iḥyaʾ al-Turath, 1418 H.
- Khui, Sayyid Abu l-Qasim al-Mu'jam rijal al-hadith. Qom: Markaz-i Nashr-i Athar al-Sh'ia, 1410 H.
- Saduq, Muḥammad bin 'Ali al-Kamal al-din wa itmam al-ni'ma. Tas-hih: 'Ali Akbar Ghaffari. Tehran: Islamiyya, 1395 H.
- Saduq, Muḥammad bin 'Ali al-Man la yahdhuruh al-faqih. Tas-hih: 'Ali Akbar Ghaffari. Qom: Daftar-i Intisharat-i Islami, 1413 H.
- Tabarsi, Fadhl bin Hassan I'lam al-wara bi a'lam al-huda. Tehran, Bita, 1390 H.
- Sheikh Tusi, Muḥammad bin Hassan Rijal Tusi. Tas-hih: Jawad al-Qayyumi. Qom: Jama'at al-Mudarrisin fi al-Ḥawza al-'Ilmiya Qom: Mu'assisa al-Nashr al-Islami, 1373 S.
- Sheikh Tusi, Muḥammad bin Hassan Fihrist kutub al-Shi'a wa usulihim wa asma' al-muṣannifin wa as-hab al-usul. Tas-hih: 'Abd al-'Aziz Ṭabaṭabai. Qom: Maktabat al-Muḥaqiq Tabatabai, 1420 H.
- Amili, Sayyid Jawad. Miftaḥ al-kirama fi sharḥ qawa'id al-'llama. Tas-hih: Muḥammad Baqir Khalisi. Qom: Daftar-i Intisharat-i Islami, 1419 H.
- Hilli, Hassan bin Yusuf al-Khulasat al-aqwal fi ma'rifat al-rijal. Tas-hih: Jawad al-Qayyumi, Mu'assisa al-Nashr al-Islami, 1417 H.
- Kashshi, Muḥammad bin Umar al-Rijal al-Kashshi. Tas-hih: Muṣṭafawi, Ḥasan. Mashhad: Intisharat-i Danishgah-i Mashhad, 1409 H.
- Kulayni, Muḥammad bin Ya'qub Al-Kafi. Tas-hih: 'Ali Akbar Ghaffari & Muḥammad Akhundi. Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyya, 1407 H.
- Guzashte, Nasir Madkhal Ibrahim bin Mahzyar Dar dayere al-ma'rifa buzurg Islami, Tehran, 1368 S
- Mamaqani, Mirza 'Abd Allah al-Tanqih al-maqal fi ahwal al-rijal. Tas-hih: Muḥyi al-Din va Muḥammad Ridha Mamaqani. Qom: Muʾassisat Al al-Bayt li-Ihyaʾ al-Turath, 1431 H.
- Majlisi, Muḥammad Baqir al-Al-Wajiza fi al-rijal. Tas-hih: Muḥammad Kadhim Rahman Sitayish. Tehran: Wizarat-i Farhang wa Irshad-i Islami.
- Najashi, Ahmad bin Ali al-Rijal al-Najashi. Tas-hih: Sayyid Musa Shubayri Zanjani, Qom: Jama'at al-Mudarrisin fi al-Ḥawza al-'Ilmiya bi Qom: Mu'assisa al-Nashr al-Islami, 1365 S.
- Najafi, Muḥammad al-Ḥasan al-Jawahir al-kalam fi sharḥ shara'i al-Islam. Tas-hih: 'Abbas Quchani & 'Ali Akhundi. Beirut: Dar Ihyaʾ al-Turath al-'Arabi, 1404 H.
- Nuri, Mirza Husayn al-Mustadrak al-Wasaʾil. Qom: Muʾassisat Al al-Bayt, 1408 H.