Hukumu ya kuuawa Salman Rushdie
Hukumu ya kuuawa Salman Rushdie (Kiarabu: الحكم بقتل سلمان رشدي) mi fatwa ya Imamu Khomeini ya kuritadi na hukumu ya kunyongwa Salman Rushdie mwandishi wa kitabu cha Aya za Shetani (The Satanic Verses) na wachapishaji waliokuwa na ufahamu wa maudhui ya kitabu hicho. Fatwa hii ilitolewa 14/02/1989. Hukumu hii ilitambuliwa kuwa ishara ya wazi ya kuonyesha nguvu ya Umarjaa wa Shia katika kutetea Uislamu. Madhehebu yote ya Kiislamu yaliunga mkono fatwa hiii. Baada ya kutolewa fatwa hiyo, murtadi Salman Rushdie alikimbia kutoka nyumbani kwake katika mji wa London nchini Uingereza na katika kipindi cha miezi mitano akiwa chini ya usimamizi wa polisi alibadilisha makazi yake ya kuishi mara 57. Baada ya kutangazwa hukumu ya kuuawa Salman Rushdie, 15/02/1989 (26 Bahman 1367 Hijria Shamsia) nchini Iran kulitangazwa maombolezo ya nchi nzima. Wananchi wa Iran walifanya maandamano katika maeneo mbalimbali sambamba na kukusanyika katika misikiti na Husseiniya na kuonyesha hasira na chuki zao dhidi ya kuchapishwa kitabu cha Aya za Shetani na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa hukumu na fat’wa ya Imamu Khomeini. Waislamu wa mataifa mbalimbali walitoa taarifa na kufanya maandamano na wakatangaza himaya na uungaji mkono kwa fat’wa ya kuuawa Salman Rushdie. Mustafa Mazeh, kijana wa Kilebanon 05/08/1989 na Ibrahim Atai mwaka 1989 walikusudia kumuua Salman Rushdie lakini hawakufanikiwa baada ya kuuawa shahidi wa walinzi wa murtadi huyo. Oktoba 2022 Hadi Matar alimshambulia Salman Rushie mjini New York. Rushdie alipoteza jicho moja... Alipata majeraha makubwa matatu shingoni mwake. Mkono mmoja ulipooza kwa sababu mishipa kwenye mkono wake ilikatwa. Na alipata majeraha zaidi ya 15 kwenye kifua na mwilini mwake kufuatia shambulio hilo. Baadhi ya mafakihi wameitambua hukumu na fatwa ya kuuawa Salman Rushdie kwamba, inaendana na hukumu ya anayemtusi Mtume (s.a.w.w) na Murtadd Fitri (ambaye baba na mama yake au mmoja kati yao alikuwa Mwislamu wakati yeye anazaliwa na kisha baada ya kubaleghe akaritadi na kutoka katika Uislamu).
Tukio la Hukumu ya kuuawa Salman Rushdie na Umuhimu Wake
Mwaka 1988 kulichapishwa na kusambazawa kitabu kilichokuwa na jina la The Satanic Verses (Aya za Shetani) ambacho kwa mujibu wa itikadi ya Waislamu wengi, kilikuwa kikitusi na kuuvunjia heshima Uislamu na Mtume Muhammad (s.a.w.w). Imam Khomeini Marjaa Taqlidi na Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran 14/02/1989 alitoa fatwa na kumhukumu kifo Salman Rushdie mwandishi wa kitabu cha Aya za Satani na wachapishaji ambao walijua kuhusu maudhui yake. [1]
Fat’wa ya Imamu Khomeini (ra)
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu انا لله وانا الیه راجعون Hakika Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake Tutarejea. Nawafahamisha Waislamu wa dunia wenye ghera kwamba, mwandishi wa kitabu cha Aya za Shetani ambacho kimeandaliwa, kuchapishwa na kusambazwa kikiwa dhidi ya Uislamu, Mtume na Qur’ani na vilevile wachapishaji waliokuwa wakijua maudhui ya kitabu hicho hukumu yao ni kifo. Nawataka Waislamu wenye ghera na wivu wawanyonge mara moja popote pale watakapowakuta, ili asije akathubutu mtu kuyatukana mambo matakatifu ya Waislamu, na atakayeuawa katika njia hii ni shahidi, Insh’Allah. Isitoshe, ikiwa mtu ana uwezo wa kumpata mtunzi wa kitabu, lakini hana uwezo wa kumuua, amtambulishe kwa watu ili aadhibiwe kwa matendo yake. Wassalaam Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Ruhollah Mousavi Khomeini [2]
Umuhimu
Hukumu ya Imamu Khomeini ya kuuawa Salman Rushdie imezingatiwa kuwa ni hukumu ya kihistoria na ishara ya uwezo na akili na upeo wa maarifa wa Umarjaa wa Shia dhidi ya njama za wapinzani wa Uislamu na uwezo wa kutetea matukufu ya dini. [3]. Fat’wa hii iliungwa mkono na madhehebu yote ya Kiislamu. [4] Sayyid Abdullah Bukhari, Imamu wa Sala ya Jamaaa wa Ahlul Sunna wa New Delhi India aliitambua fat’wa ya Imamu Khomeini kuwa ishara na kielezo cha upeo na maarifa ya hali ya juu ya Imamu Khomeini. Ahmad Kaftaru, Mufti Mkuu wa wakati huo wa Syria naye 01/03/1989 alitoa fat’wa iliyokuwa ikieleza ulazima wa kuhukumiwa na kuadhibiwa Salman Rushdie. [5] Ayatullah Khamenei anaamini kwamba, hukumu hii ilikuwa pigo madhubuti dhidi ya uistikbari na wafuasi wa Kimagharibiwa kitabu cha Aya za Shetani (The Satanic Verses) ambayo iliwalazimisha kutetea na kudhoofisha ari yao. [6] Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah alisema pia kuwa, nchini Lebanon fat’wa hii pia ilikuwa pigo kubwa dhidi ya ulimwengu wa kiistikvari na Kimagharibi. [7]
Misingi ya Kifikihi ya Hukumu ya Kuuawa Salman Rushdie
Baadhi ya mafaqihi wameorodhesha hukumu ya kifo dhidi ya Salman Rushdie kuwa imechukuliwa kutoka katika hukumu za sheria. Kwa mujibu wa Seyyed Hadi Khosrowshahi, hukumu ya kifo ya Salman Rushdie ni hukumu ya mwenye kumtusi Mtume (s.a.w.w) na murtadi [8], ambayo wanazuoni wote wa dini ya Kiislamu wanakubaliana nayo [9]. Akibainisha fat’wa hii Mousavi Ardebili amemtambua Salman Rushdie kuwa ni Murtadd Fitri (Murtadd Fitri ambaye ambaye baba na mama yake au mmoja kati yao alikuwa Mwislamu wakati yeye anazaliwa na kisha baada ya kubaleghe akaritadi na kutoka katika Uislamu) ambaye kwa mujibu wa Uislamu, toba yake haikubaliwi. [10]
Radiamali ya Salman Rushdie
Baada ya kutolewa fat’wa hii, hasira za walimwengu zilishadidi na kufikia kilele chake. 18 Februari 1989 Salman Rushdie akiwa ameingiwa na hofu ya mustakabali wake, alitoa taarifa na kuomba msamaha. [11] Baada ya kutolewa fat’wa hiyo Salman Rushdie alikimbia kutoka nyumbani kwake mjini London Uingereza na katika kipindi cha miezi mitano akiwa chini ya usimamizi wa polisi alibadilisha makazi yake ya kuishi mara 57. [12] Katika mahojiano aliyofanyiwa na gazeti la Daily Mirror alielezea hisia yake ya kwanza baada ya kusikia hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi yake ambapo alisema: Haikuwa hisia nzuri, nilijihisi kwamba, kwamba, mimi ni mtu niliyekufa… kutembea bila ya mlinzi binafsi, kwenda kufanya manunuzi, kuonana na familia, kusafiri kwa ndege na yote haya ni mambo ambayo wakati huo hayakuwa yakiwezekana. [13]
Kuakisiwa
Hukumu ya kifo dhidi ya Salman Rushdie iliakisiwa pakubwa ndani na nje ya Iran:
Kuakisiwa ndani ya Iran
Baada ya kutolewa hukumu ya kifo dhidi ya Salman Rushdie, serikali ya wakati huo ya Iran, kwa mujibu wa amri ya Imam Khomeini, 15/02/1989 (26 Bahman 1367 Hijria Shamsia) nchini Iran kulitangazwa maombolezo ya nchi nzima. Wananchi wa Iran walifanya maandamano katika maeneo mbalimbali sambamba na kukusanyika katika misikiti na Husseiniya na kuonyesha hasira na chuki zao dhidi ya kuchapishwa kitabu cha Aya za Shetani na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa hukumu na fat’wa ya Imamu Khomeini. [14] Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu (Bunge la Iran) iliidhinisha kukatwa kabisa kwa uhusiano na Uingereza na wawakilishi 170 walitia saini barua ya kutaka mkutano wa kimataifa wa mabunge ushughulikie ipasavyo uchapishaji wa kitabu cha Aya za Shetani. [15] Mnamo 16/02/1989, Sheikh Hassan Sane’ei kiongozi wa Waqfu wa 15 Khordad, alitangaza zawadi ya toman milioni 20 kwa Muirani atakayemuua Salmana Rushdie na dola milioni 1 kwa asiyekuwa Muirani ambaye atamuua murtadi huyo. Zawadi hiyo imeongezwa mara kadhaa na mwaka 2012 dau hili lilifikia dola milioni 3.5. [16]
Kuakisiwa Kimataifa
Hukumu ya kifo iliyotolewa na Imamu Khomeini dhidi ya Murtadi Salman Rushie iliakisiwa pakubwa duniani. [17] Baada ya hukumu hiyo kuakisiwa pakubwa na ujumbe huo kutangazwa katika vyombo vya habari duniani, Salman Rushdie, waungaji mkono wake na wachapishaji wa kitabu chake walitishwa na kushambuliwa katika maeneo mbalimbali duniani. [18] Waislamu wa mataifa kama Uingereza, Malaysia, Italia, Ufaransa, Guinea, Uturuki, Sudan, Argentina, Australia, Hong Kong, Denmark, Canada, Uhispania, Finland, Jumuiya ya Waislamu nchini Marekani, Baraza la Maulamaa wa Jabal Amil, Baraza la Waislamu Sri Lanka, Baraza Kuuu la Waislamu Uganda na Baraza Kuu la Masuala ya Wailsamu Nigeria walitoa taarifa maalumu sambamba na kufanya mkusanyiko wakitangaza himaya na uungaji mkono wao kwa fatwa ya kuuawa Salman Rushdie. [19] Nchini Algeria kuliandika na kusambazwa kitabu kilichopewa jina la "Shetani wa Magharibi" kama jibu dhidi ya kitabu cha Aya za Shetani. Kitabu hiki sambamba na kuakisi hukumu ya kuuawa Salman Rushdie kilimsifia Imamu Khomeini. [20] Kitabu cha The Satanic Verses (Aya za Shetani) kimepigwa marufuku kuuzwa katika mataifa ya India, Afrika Kusini, Tanzania, Malaysia, Misri na Saudi Arabia. Shirika la Uchapishaji la Penguin ambalo lilichapisha kitabu cha Aya za Shetani nchini Uingereza lilijiimarishia na kujiongezea ulinzi. Kadhalika ofisi za baadhi ya wasambazaji wa kitabu hiki katika mataifa kama Marekani na Uingereza zilishambuliwa. [21] China nayo 19/08/1989 ilitangaza kupiga marufuku usambazwaji wa kitabu cha Aya za Shetani. [22] Kwa upande mwingine, Rais wa wakati huo wa Marekani George Bush 22/02/1989 alitangaza kumuunga mkono Salman Rushdie na kutangaza kuwa, tishio la kifo la Iran dhidi ya Salman Rushdie ni tishio dhidi ya maslahi ya Marekani. [23] Geoffrey Howe Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uingereza wakati huo, alizungumza kuhusu kuchapishwa kitabu hicho na athari za hukumu ya kifo ya Rushdie katika kubadilisha msimamo wa serikali ya Uingereza kuuheshimu Uislamu na kujitenga kwake na kitabu cha Aya za Shetani. [24] Nchi kumi na mbili wanachama wa Soko la Pamoja la Ulaya ziliwaita mabalozi au wakuu wa balozi zao kutoka Iran na kufuta mawasiliano na safari zozote za maafisa wa ngazi za juu kwenda Iran. [25] Serikali ya Marekani ilitoa mwito rasmi kwa Umoja wa Kisovieti kulaani hukumu ya Imamu Khomeini. Hata hivyo, Eduard Shevardnadze, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa wakati huo wa Umoja wa Kisovieti, alijibu kwa kusema kwamba nchi za Magharibi zinapaswa kuheshimu thamani na itikadi za Iran.[26] Mustafa Mazeh, kijana wa Kilebanon [27] na Ibrahim Atai [28] mwaka 1989 walikusudia kumuua Salman Rushdie lakini hawakufanikiwa baada ya kuuawa shahidi wa walinzi wa murtadi huyo. Tarehe 12 Agosti 2022 Salman Rushdie alishambuliwa mjini New York wakati anahutubia. Kijana mmoja mkaxzi wa New Jersey alimshambulia kwa kisu Salman Rushie na kumjeruhi. [29] Aliyemshambulia ni kijana aliyefahamika kwa jina la Hadi Matar (24). Murtadi Rushdie alipoteza jicho moja ambalo lilipofuka... Alipata majeraha makubwa matatu shingoni mwake. Mkono mmoja ulipooza kwa sababu mishipa kwenye mkono wake ilikatwa. [30
Rejea
Vyanzo