Murtadd Fitri

Kutoka wikishia

Murtadd Fitri (Kiarabu: المرتد الفطري) ni mtu ambaye baba na mama yake au mmoja kati yao alikuwa muislamu wakati yeye anazaliwa na kisha baada ya kubaleghe akaritadi na kutoka katika Uislamu. Adhabu ya Murtaddi Fitri ni kuuawa, lakini kama ni mwanamke anatiwa jela mpaka atakapotubu au aage dunia. Kwa mujibu wa fat'wa ya akthari ya mafakihi wa Kishia ni kwamba, toba ya murtadd Fitri haikubaliwi. Pamoja na hayo Ayatullah Khui mmoja wa Marajii Taqlidi wa Kishia wa karne ya 14 Hijria anaamini kuwa, toba yake haipelekei kuondolewa hukumu ya kuuawa, kubatilishwa ndoa na kugawanywa mali yake baina ya warithi, lakini huwa sababu ya kuwa muislamu na kusamehewa dhambi zake.

Utambuzi wa maana

Makala asili: Al-Irtidâd (Kuritadi)

Murtadd Fitri ni mtu ambaye baba na mama yake au mmoja kati yao ni muislamu na kisha baada ya yeye kubaleghe akaritadi na kutoka katika dini ya uislamu. [1] Kwa mujibu wa kauli mashuhuri, kigezo cha Uislamu wa baba na mama yake ni katika kipindi cha kutunga mimba yake. [2] pamoja na hayo, Sahib al-Jawahir amenukuu nadharia ya ajabu kutoka katika kitabu cha "Rasail al-Jazairi" ya kwamba, baba au mama yake au wote wawili wakati wa kuzaliwa kwake wawe ni waislamu. [3] Mkabala na Murtadd Fitri kuna Murtaddi Milli ambaye huyu ni mtu ambaye wakati wa kutunga mimba yake baba na mama yake hawakuwa waislamu, lakini baada ya kubaleghe akasilimu na kuingia katika Uislamu na kisha baadaye akaritadi na kuwa kafiri. [4]

Adhabu

Kwa mujibu rai mashuhuri ya mafakihi wa Kishia, adhabu ya Murtadd Fitri ni kuuawa. [5] Kadhalika kwa mujibu wa mafakihi, mali ya Murtadd Fitri inagawanywa baina ya warithi na ndoa yake inavunjwa. [6] Kama ambavyo hawezi kumrithi muislamu. [7] Kama mwanamke atakuwa ni Murtadd Fitri, kwa mujibu wa raia ya mafakihi wa Kishia hauliwi; [8] hata hivyo anatiwa jela mpaka atakapotubu au afe. [9] Kadhalika ndoa yake inavunjwa. [10] Kwa mujibu wa baadhi ya mafakihi, kama mwanamke Murtadd Fitri atakariri kuritadi kwake huko mara nne, adhabu yake itakuwa ni kuuawa. [11] Hata hivyo, Ayatullah Khui anaamini kwamba, hata kama mwanamke atakariri kuritadi kwake na akawa ni Mutadd Fitri hilo halipelekei auawe. [12]

Kutubu

Kwa mujibu wa Ayatullah Khui ni kwamba, lililo mashuhuri baina ya mafakihi ni kwamba, toba ya mwanaume ambaye ni Murtadd Fitri (aliyezaliwa na baba na na mama waislamu au mmoja wao na kisha yeye baada ya kubaleghe akaritadi) haikubaliwi. [13] Hata hivyo raia ya Ibn Junayd Askafi, mmoja wa mafakihi wa Kishia wa karne ya 4 ni kwamba, kama Murtadd Fitri atatubu, hukumu ya kuuawa kwake inaondolewa, mali yake inarejeshwa na anaweza kumrejea mke wake bila ya kufunga ndoa upya. [14] Hata hivyo Ayatullah Khui anaamini kuwa, Murtadd Fitri ambaye atatubu hukumu yake ni muislamu licha ya kuwa hukumu zingine kama kuuawa kwake na kugawanywa mali yake haziondolewi. [15] Ayatullah Khui anaamini kwamba, kutubu kwa maana ya kuonyesha kujutia ukafiri na kuonyesha majuto, hilo halipelekei kuondolewa adhabu za kivitendo kama kuuawa. [16]

Rejea

Vyanzo

  • Khui, Abu al-Qasim. Al-Tanqih fi Sharh al-'Urwah al-Wuthqa. Catatan: Mirza Ali Garawi. Qom: Dar al-Hadi, 1413 H.
  • Khui, Abu al-Qasim. Mabani Takmilah al-Minhaj. Qom: Muasasah Ihya' Atsar al-Imam Khui, 1413 H.
  • Musawi Ardibili, Sayyied Abdul Karim. Fiqh al-Hudud wa al-Ta'zirat. Qom: Jamiah al-Mufid, 1429 H.
  • Najafi, Muhammad Muhsin. Jawahir al-Kalam. Riset: Ibrahim Sulthani. Beirut: Dar Ihya' al-Turats al-Arabi, 1362 H.
  • Shahid Awwal, Muhammad bin Makki. Al-Durus al-Shari'ah fi Fiqh al-Imamiyah. Qom: Jamiah al-Mudarrisin, 1404 H.
  • Shahid Thani, Zainuddin bin Ali. Masalik al-Afham ila Tanqih Syarai' al-Islam. Qom: Muasasah al-Ma'arif al-Islamiyah, 1413 H.