Hadithi ya Wanazuoni ni Warithi wa Manabii
Wanazuoni ni warithi wa manabii (Kifarisi: حديث العلماء ورثة الأنبياء) ni moja ya Hadithi zilizoripotiwa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) akimnukuu Mtume Muhammad (s.a.w.w). Lengo la Hadithi hii ni kutoa ilani ya kwamba; Wanazuoni wa dini ni warithi wa manabii. Muqtadha mkuu wa kijumla na tandavu wa maudhui ya Hadithi hii, unahusiana na nafasi na hadhi ya elimu pamoja na wanazuoni. Elimu inayokusudiwa katika Hadithi hii, ni ile elimu ya kidini yenye manufaa ya Akhera (elimu ya itikadi, maadili na fiqhi). Pia wanazuoni «علماء» wanaokusudiwa hapo ni wanazuoni wa masuala ya dini.
Vile vile, imeelezwa kwamba; maana ya warithi «وَرَثة» katika Hadithi hii ni wale warithi wenye urithi wa elimu na maarifa kutoka kwa «manabii» walio kuja na vitabu (waliokuja na sheria maalumu). Kwa mujibu wa mtazamo wa Muhammad Taqi Majlisi (aliyefariki mwaka 1071 Hijria), wanazuoni ni warithi wa manabii kwa upande wa masuala ya kidini ya unabii wao, ambapo jambo hili halipingani na ukweli wa kwamba manabii hawaachi urithi wa kielemu tu, bali pia wanaweza kuacha urithi wa mali. Baadhi ya wanazuoni wa fiqhi wametumia Hadithi hii katika kuthibitisha nadharia ya Wilayat al-Faqih. Hadithi hii inapatikana katika vyanzo tofauti vya kale vya Shia pamoja na Sunni. Miongoni mwa vitabu vyenye nukuu ya Hadithi hii kama vile; Basairu al-Darajat, Al-Kafi, Sunanu Ibnu Maja na Sunanu Abu Dawood.
Mashiko (Sanad) na Hadthi Yake
Hadithi isemayo: Wanazuoni ni warithi wa manabii (العُلماءُ وَرَثةُ الأنبِیاء) ni moja ya Hadithi zilizoripotiwa kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s) akimnukuu Mtume Muhammad (s.a.w.w). Hadithi hii imekuja kuwatambulisha wanazuoni wa dini kuwa warithi wa manabii. [1] Baadhi ya wanazuoni wa fiqhi kama vile Imamu Khomeini na Hussein-Ali Muntadhiri wametumia Hadithi hii katika kuthibitisha nadharia ya wilayat al- Faqih. [2] Kwa mawazo yao ni kwamba; Uongozi wa jamii ni miongoni mwa majukumu ya manabii yaliyo hamishiwa kwa wanazuoni, kwa mujibu wa nadharia hii, wanazuoni peke yao ndiwo wenye haki na mamlaka ya uongozi wa jamii. [3]
Hadithi hii imepokewa kutoka katika vyanzo kadhaa vya kale vya Shia pamoja na Sunni. [4] Miongoni mwa wanahadithi wa Kishia walio nukuu Hadithi hii, ni pamoja na; Saffaar Qomi (aliyefariki mwaka 290 Hijria) aliye inuku Hadithi hii katika kitabu chake Basair al-Darajat, [5] pia, Kulaini (aliyefariki mwaka 329 Hijria) katika kiitwacho Al-Kafi, [6] na Sheikh Saduq (aliyefariki mwaka 381 Hijria) katika chake kiitwacho Aamali. [7]
Kwa upande wa wapokezi wa Sunni, Hadithi hii inapatikana katika vitabu vya; Ibnu Majah (aliyefariki mwaka 273 Hijria), Abu Dawood (aliyefariki mwaka 275 Hijria), Tirmidhi (aliyefariki mwaka 279 Hijria), na Ibnu Hibban (aliyefariki mwaka 354 Hijria).
Nakala ya Hadith
Ibara inayowasifu wanazuoni kwa kuwataja kama ni warithi wa manabii, ni moja wapo ya ibara iliopo iliyo nukuliwa katika kitabu al-Kafi kupitia Hadithi yenye nukuu mbili tofauti; Ya kwanza ni nukuu ya Qaddaah [12] ambayo imeaminiwa (موثّق) kutokana na ithibati makini zinazo aminika. [13] Ya pili ni nukuu ya Abu al-Bakhtari [14], ambayo licha ya udhaifu wake [15] ila imeweza kukubaliwa na baadhi ya watu kutokana na muktadha wa maudhui yake. [16] Matini ya Hadithi ya Qadah iliyo simuliwa na Imamu al-Sadiq (a.s.), kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w.), ni kama ifuatavyo: [17]
(مَنْ سَلَکَ طَرِیقاً یَطْلُبُ فِیهِ عِلْماً سَلَکَ اللَّهُ بِهِ طَرِیقاً إِلَی الْجَنَّةِ وَ إِنَّ الْمَلَائِکَةَ لَتَضَعُ أَجْنِحَتَهَا لِطَالِبِ الْعِلْمِ رِضًا بِهِ وَ إِنَّهُ یَسْتَغْفِرُ لِطَالِبِ الْعِلْمِ مَنْ فِی السَّمَاءِ وَ مَنْ فِی الْأَرْضِ حَتَّی الْحُوتِ فِی الْبَحْرِ وَ فَضْلُ الْعَالِمِ عَلَی الْعَابِدِ کَفَضْلِ الْقَمَرِ عَلَی سَائِرِ النُّجُومِ لَیْلَةَ الْبَدْرِ وَ إِنَّ الْعُلَمَاءَ وَرَثَةُ الْأَنْبِیَاءَِ إِنَّ الْأَنْبِیَاء لَمْ یُوَرِّثُوا دِینَاراً وَ لَا دِرْهَماً وَ لَکِنْ وَرَّثُوا الْعِلْمَ فَمَنْ أَخَذَ مِنْهُ أَخَذَ بِحَظٍّ وَافِر). Tafsiri yake ni kwamba; (Yeyote yule atakaye shika njia ya kutafuta elimu, Mwenye Ezi Mungu atamnyoshea mtu huyo njiani ya kuelekea Peponi kupitia njia hiyo ya elimu aliyo ifuata, na hakia Malaika hutandaza mbawa zao kwa ajili mtafuta elimu, kutokana na wao kuridhika na mtu huyo, naye bila shaka huombewa msamaha na walio mbinguni pamoja na waazi wa ardhini, hata nyangumi walio baharini humuombea yeye msamaha. Na hadi ya mwenye elimu juu ya waja kama hadhi ya mwezi juu ya nyota nyengine pale ufikapo wakati wa mbaramwezi, na hakima wanazuoni ni warithi wa manabii (mitume), bila shaka manabii hawakurithisha pesa za dhahabu (Dinari) wala za fedha (Dirham), bali walirithisha elimu, yeyote basi atakaye chukuwa kutoka kwake (mtume), atakuwa amechukuwa kitu cha thamani mno).
Uchambuzi wa Baadhi ya Maneno katika Hadithi
Kuna chambuzi kadhaa kuhusiana na Hadithi isemayo: Wana elimu ni warithi wa manabii (العُلماء وَرَثةُ الأنبِیاء), iliyo wanataja wanazuoni kuwa ni warithi wa manabii. [18] Kwa maoni ya Mirza Naaini (aliyefariki mwaka 1315 Hijria) ni kwamba; Yawezeka neno wanazuoni «العلماء» lililomo ndani ya Hidithi hii likawa linamaanisha Maimamu Maasumina (a.s). [19] Hata hivyo, wengine wamesema kwamba wanazuoni waliokusudiwa Hadithini humo, ni wanazuoni wa elimu ya dini. [20] Kwa mtazamo wa Sayyid Muhammad Sadiq Ruhani (aliyefariki mwaka 1401 Hijria) ni kwamba, kutokana na muktadha wa maudhui ya Hadithi inayozungumzia thawabu za kujifunza, ni vigumu kudhani kwamba maana ya neno wanazuoni «العلماء» inahusiana na Maimamu peke yao. [21]
Watafiti wamesema kwamba; Maana ya neno manabii «انبیاء» lililomo katika ibara za Hadithi linamaanisha wale manabii walio shushiwa vitabu na Mola wao. [22] Manabii hawa ni pamoja na; Adam, Nuhu, Ibrahim, Musa, Isa na Muhammad (s.a.w.w). [23] Faidh Kashani (aliyefariki mnamo mwaka 1091 Hijria), ambaye ni mwanazuoni wa Fiqhi na mpokezi wa hadithi kutoka upande wa madhehebu ya Shia, aliwasifu wanazuoni kuwa ni watoto wa kiroho wa manabii, wanao rithi chakula cha kiroho ambacho ni elimu na maarifa kutoka kwa manabii yatokayo kwa manabii hao. [24]
Je, Manabii Hawachi Urithi wa Mali?
Katika sehemu inayofuata ya Hadithi ya "Wana elimu ni warithi wa manabii العلماء ورثة الانبیاء،", imeelezwa ya kwamba manabii hawaachi urithi wa mali kama mfano wa fedha au dhahabu, bali urithi wao ni elimu na maarifa, na hivyo, warithi wao ni wanazuoni. [25] Kwa mujibu wa maelezo ya Mulla Sadra (aliyefariki mwaka 1050 Hijria), ambaye ni mwanafalsafa wa upande wa madhehebu ya Shia, ni kwamba; maana ya kauli isemayo kuwa; manabii hawarithishi mali, inalenga upande na mrengo wa unabii wao, ambao ni upande wa kiroho uliobeba hazina ya elimu; na sio kwamba hawana urithi wa aina nyingine yoyote. [26]
Muhammad Taqi Majlisi (aliyefariki mwaka 1071 Hijria), mpokezi wa hadithi au mwanahadithi wa Kishia, pia naye anaamini kwamba; kitu kikubwa zaidi walicho nacho manabii duniani humu ni elimu na hekima. Huo basi ndiyo urithi nono unao achwa na manabii, na warithi wake ni wanazuoni. [27] Hivyo basi kwa maoni ya Majlisi, jambo hilo katu hailipingani na ukweli wa kwamba manabii pia wanaweza kuwa na urithi wa mali. Kwa hiyo, Ahlul-Bait (a.s) walikuwa ni warithi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika nyanja zote mbili za kiroho na kimwili. [28]
Ubora wa Elimu na Mwanazuoni
Kwa mujibu wa maelezo ya Imamu Khomeini, ni kwamba; Muktadha tandavu (wa kijumla) wa maudhui ya Hadithi isemayo: Wana elimu ni warithi wa manabii العلماء ورثة الانبیاء unahusiana na ubora na umuhimu na thamani ya elimu pamoja na wanazuoni. [29] Hata Kulani naye amitaja Hadithi hii pale alipokuwa akizungumzia ujira na malipo ya mkufunzi na mwanagenzi kitabu chake cha Al-Kafi, maelezo ambayo yanapatikana kwenye mlango uitwao "Thawabu ‘Alim wa Muta’allim (ثواب عالم و متعلّم) ulioko kitabuni humo. [30]
Imam Khomeini, katika kitabu chake kiitwacho Arba'in Hadith, ameigawa elimu kulingana na madhumuni yanayo kusudiwa katika kutafuta au kujifunza elimu hiyo. Yeye aliigawa elimu katika vigao viwili: Elimu ya kidunia na elimu ya Akhera. Akifafanu kuhusiana na vigao hivyo anasema; Ingawa kila aina ya elimu inalazimia na suala la kupatikana kwa ukamilifu na hadhi fulani, [31] ila maana ya elimu katika Hadithi hii ni elimu ya Akhera. [32] Imamu Khomeini kifafanua masuala ya elimu ya Kiakhera ameeleza ya kwamba; elimu ya Akhera inajumuisha mambo kadhaa ndani yake, nayo ni; maarifa ya kumwelewa Mwenye Ezi Mungu (elimu ya itikadi), kusafisha nafsi (elimu ya maadili), pamoja adabu, mila na desturi (elimu ya fiqhi na sheria). Naye amesisitiza ya kwamba; elimu hizi ndizo zinampelekea mtu kufuzu na kupata furaha ya akhera. [33]