Nenda kwa yaliyomo

Fat’wa ya Shurayh al-Qadhi

Kutoka wikishia

Fat’wa ya Shurayh al-Qadhi (Kiarabu: فتوى شريح القاضي) ni fat’wa inayonasibishwa na Shurayh bin Harith al-Kindi Kadhi wa Kufa katika zama za kutokea tukio la Karbala ambayo madhumuni yake yalikuwa ni kuidhidhisha kuuawa Imamu Hussein (a.s). Fat’wa hii haijaja katika vyanzo vya kale na baadhi ya Maulamaa na watafiti wanasema kuwa, fat’wa hiyo haina msingi na ni bandia.

Umuhimu na nafasi

Kwa mujibu wa Sayyid Muhammad Ali Qazi Tabatabai katika kitabu chake cha utafiti juu ya Arbaeen ya kwanza wa Sayyid al-Shohada, wasomaji wengi wa mashairi ya maombolezo ya Imamu Husseini wananukuu maneno yanayonasibishwa na Shurayh al-Qadhi na kuyataja kuwa moja ya sababu za kutokea tukio la Karbala na wanayakikiri maneno hayo. [2] Shurayh bin Harith al-Kindi, anayejulikana kama Shurayh al-Qadhi alikuwa hakimu na kadhi wa mji wa Kufa tangu wakati wa Omar bin Khattab Khalifa wa pili hadi mwaka wa 78 Hijiria. [3]

Andiko linalonasibishwa na Shurayh

Kwa mujibu wa kile ambacho kimekuja katika sehemu ya ufafanuzi wa tarjuma ya kitabu cha al-Fain, matini (andiko) ya fat’wa inayonasibishwa kwa Shurayh al-Qadhi ni:

Kwa hakika Husein bin Ali amesababisha mgawanyiko baina ya Waislamu na amempinga Amirul-Muuminina (Yazid) na ametoka katika dini. Jambo hili kwangu limethibiti. Kwa msingi huo, nimetoa hukumu kuuawa kwake ili kuhifadhi Sheria ya Mtume (s.a.w.w). [4]

Vyanzo vilivyonukuu fat’wa hii

Kwa mujibu wa Muhammad Sihhati Sardurudi, mtafiti wa Kishia wa tukio la Ashura ni kuwa, fat’wa ya Shurayh imenukuliwa ikiwa na tofauti kidogo katika vitabu kama Jawahir al-Kalal Fi Sawanih al-Ayyam kilichoandikwa na Hassan Ash’raf al-Waidhin katika karne ya 14 Hijria na Tarjumat al-Alfain kilichoandikwa katika karne ya 15 Hijria. [5] Qadhi Tabatai ameileta pia fat’wa hii katika kitabu chake cha Thamarat al-Anwar wa Mazamir al-Awliya alichoakiandika katika karne ya 14 Hijria. [6] Kwa mujibu wa kitabu cha Tarikh Jami’ Sayyid al-Shuhadaa pia kadhia ya fat’wa ya Shurayh imeandikwa na kunukuliwa katika vitabu kama Tadhkirat al-Shuhadaa kjilichoandikwa na Mulla Habibullah Kashani cha karne ya 14 Hijiria. [7] Kisa hiki kimenukuliwa pia kutoka kwa Abdul-Nabi Iraqi Najafi (aliaga dunia 1344 Hijria Shamsia) ambapoo yeye pia aliishi katika karne ya 14 Hijria. [8]

Wanaokana kutolewa fat’wa kama hii

Kwa mujibu wa Muhammad Sihhati Sardurudi, katika matini ya kitabu cha Al-Alfain kilichoandikwa na Allama Hilli hakuna kitu kama hicho na yale aliyoyatoa mfasiri katika sehemu ya maelezo hayajatajwa katika kitabu chochote kilichotangulia. [9] Sihhati pia anataja vitabu 31 vya awali ambamo ndani yake hakujaashiriwa fat’wa ya Shurayh. [10] Qadhi Tabatabai pia katika kitabu chake cha Tahqiq Dar Baroye Arbain (Uhakiki Kuhusu Arubaini) anatambua vyanzo vya fat’wa hii kwamba, havina msingi. [11] Mwandishi wa kitabu cha Tharallah pia anasema kuwa, fat’wa ya Shurayh ni tetesi na uvumi. Kwa mujibu wake, jina la Shurayh limekuja sehemu mbili tu katika Maqatil (simulizi za mauaji ya shakhsia muhimu) na sehemu zote mbili hizo zinahusiana na kutiwa mbaroni Hani bin Ur’wah. [12] Kadhalika inaelezwa kuwa, kitabu cha Mash’huraat Bi I’tibar (kilichoandikwa 1398 Hijiria Shamsia), hatua ya Mukhtar al-Thaqafi ya kumpa wadhifa Shurayh ni ithbati ya kuwa bandia fat’wa hii. Mwandishi wa kitabu hiki anasema: Uteuzi huu kama tutajaalia fat’wa hiyo ilitolewa na Shurayh, hauendani na mbinu na mkakati wa Mukhtar wa kulipiza kisasi kwa wahusika wa tukio la Karbala. [13]

Katika kamusi ya Dekhoda pia imekuja chini ya Shurayh kwamba: Kisa hiki hakijanukuliwa katika vyanzo vyenye itibari. [14] Waandishi wa kitabu cha Tarikh Jami’ Sayyid al-Shuhadaa pia wanaitambua Fat’wa ya Shurayh kwamba, haina sanadi na mapokezi ya kuaminika na wameandika, madai haya yanapatikana tu katika vyanzo vya karne ya 14 Hijiria. [15]

Rejea

Vyanzo

  • ʿAndalīb, Ḥusayn. Thār Allāh. Qom: Intishārāt-i dar rāh-i ḥaq, 1376 Sh.
  • Group of authors. Tārīkh-i qīyām wa maqtal-i jāmiʿ-i Sayyid al-Shuhadāʾ. Qom: Muʾassisa-yi Āmūzishī wa Pazhūhishī-yi Imām Khomeiniī, 1392 Sh.
  • Khudāyī, Sayyid Alī Akbar. Shurayḥ-i Qāḍī Zindigīnāma wa ʿamalkard. Tārīkh-i Islām Journal, No. 7, Fall 1380 Sh.
  • Qāḍī Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad ʿAlī. Taḥqīq darbāra-yi awwal arbaʿīn-i ḥaḍrat-i sayyid al-shuhadāʾ.Third edition. Qom: Nashr-i bunyād-i ʿilmī wa farhangī-yi shahīd Āyat Allāh Qāḍī Ṭabāṭabāʾī, 1368 Sh.
  • Ṣiḥḥatī Sardrūdī, Muḥammad. Taḥrīf-shināsī-yi ʿashūrā wa tārīkh-i Imām Ḥusayn. Tehran: Chāp wa Nashr-i Bayn al-Milal, 1394 Sh.
  • Sulaymānī, Mahdī. Mashhūrāt-i bī iʿtibār dar tārīkh wa ḥadīth. First edition. Qom: Kitāb-i Ṭāhā, 1398 Sh.
  • Wijdānī, Jaʿfar. Tarjuma-yi al-Alfayn. Second edition. Qom: Intishārāt-i Hijrat, 1409 AH.