Dua ya thelathini na moja ya Sahifa Sajjadiya
Dua ya thelathini na moja ya Sahifa Sajjadiya: ni moja ya dua zilizonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s). Katika dua hii Imamu Sajjad (a.s) anaelekeza maombi yake kwa Mola wake, akimwomba taufiki ya kutubia toba ya kweli. Miongoni mwa mambo muhimu yanayoangaziwa ndani ya dua hii, ni pamoja na; masharti ya toba ya kweli, hali na sifa za mwobaji wa toba ya kweli na njia za kukombolewa kutokana na dhambini. Kulingana na maudhui ya dua hii, mabadiliko ya ndani ya binadamu ndiyo sharti hasa la toba ya kweli, na upendo wa Mwenye Ezi Mungu ndiyo ngome pekee inayomkinga mja na dhambi mbai mbali. Kama asemavyo mtukufu Imamu Zainul-Aabidiin (a.s), dhambi huanza mwandama mwanadamu kuanzia hapa duniani hadi kesho Akhera. Aidha kiasiali, moto wa Jahanamu ndiyo matokeo yanayotarajiwa kumwandama mtenda madhambi. Hivyo basi, ni lazima manadamu awe ni mwenye kumwomba Mola wake taufiki ya kutubu kutokana na makosa yake mbali mbali. Miongoni mwa mafundisho mengine muhimu yaliyomo ndani ya dua hii, kuomba shufaa ya Muhammad (s.a.w.w) pamoma na Aali zake (a.s), kwa ajili ya kupata uokozi wa kuepukana na ujinga na upotofu wa nafsi zetu. Kitabu “Atre Ma’rifat: Golvajegan az Golistan Maarifat Tawbe” cha Sayyid Muhammad Zia’abadi, ni moja ya vitabu maarufu vilivyofasiri na kuchambua dua ya 31 kwa lugha ya Kiajemi. Aidha, dua hii imefasiria kiuchambuzi kupitia vitabu vyengine kadhaa vya Kiajemi pamoja na Kiarabu, vilivyofasiri dua zilizomop ndani ya kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Mafundisho Yaliyomo Ndani ya Dua ya Tahalathini na Moja
Mada kuu ya dua ya thelathini na moja ya Sahifa Sajjadiya, ni kuomba toba kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu. Dua ya hii mahususi ya Toba, imesifiwa kuwa ni miongoni mwa dua angavu (zenye mwanga) zaidi, kati ya dua za Sahifa Sajjadiya. [1] Imam Sajjad (a.s) ametufunza mambo kadhaa kupitia dua hii, yakiwemo; aina za dhambi, hali na sifa za mwenye kutubu, pamoja na masharti ya toba ya kweli. [2] Mafundisho ya dua hii yamekuja katika miktadha ifuatayo:
• Mwenye Ezi Mungu yuko juu ya maelezo ya kila mwelezaji; na wala hakuna awezaye kumfafanua kikamilifu. • Kiasili, Jahannamu ni dhihirisko la madhambi zetu. • Mungu ndiye tumaini la mwisho la wenye matumaini. • Mungu hapotezi malipo ya watendao mema. • Hofu na khushuu ya waja mbele ya Mungu. • Mungu ndiye kilele cha khofu ya waabudio (wacha-Mungu). • Uhai wa binadamu uko mikononi mwa uwezo wa Mungu. • Kukiri makosa na dhambi mbele ya Mwenye Ezi Mungu. • Mabadiliko ya ndani ya nafsi, ndio sharti la toba ya kweli. • Dhambi humwandama mwanadamu kuanzia duniani hadi Akhera. • Kutengana na upofu wa moyo ndio utangulizi wa kuingia kwenye toba (starehe ya dhambi ni kuzuizi cha toba). • Tumaini la msamaha wa Mwenye Ezi Mungu huharakisha toba. • Ujinga wa kutouelewa uweza wa Mungu na kukataa fadhila na ihsani Zake ni matokeo ya kutawaliwa na Shetani. • Hali na sifa za mtubiaji wa kweli: unyenyekevu na khushuu mbele ya Mwenye Ezi Mungu; macho yaliojaa machozi; kuomba kwa ikhlasi na kuwa na majuto kwa umri uliopotea. • Msamaha wa madhambi makubwa uko mikononi mwa Mwenye Ezi Mungu. • Mungu ameahidi kujibu dua za waja Wake. • Mungu haharakishi kuwaadhibu waja wake kwa dhambi zao. • Njia za kuokoka na dhambi: uthabiti wa kubaki katika utiifu na ibada; kujiepusha na maeneo yenye mitelezo ya dhambi; kukimbilia na kuomba stara ya Mwenye Ezi Mungu, pamoja na kuutakasa moyo na uchafu wa dhambi. • Mapenzi ya Mungu kwa watubiao. • Masharti ya toba ya kweli: kutubu kutokana na dhambi dhahiri pamoja na dhambi za batini, kutubia kutokana na makosa ya zamani pamoja na ya sasa, kuweka ahadi na Mwenye Ezi Mungu ya kutorudia makosa yaliopita, pamoja na kutakasa moyo kwa kujutia dhambi zilizopita. • Toba ya kweli hufanywa kwa kutegemea na kutamania fadhila za Mungu. • Toba ya kweli: Ni kutokuwa na matarajio kwa asiye Mungu na kutoogopa yeyote yule isipokuwa Mwenye Ezi Mungu peke yake. • Ombi la kumwomba Mwenye Ezi Mungu taufiki ya kutenda yale yanayompendeza. • Upendo wa Mungu ndiyo ngome thabiti inayozuia dhambi. • Ombi la kuomba uthabiti katika nia ya utumishi wa kumwbudu Mungu. • Kuingia ahadi na Mwenye Ezi Mungu ya kutorudia yale asiyoyapenda. • Kuweka dhamana ya kutokutenda yale yaliyokemewa na Mungu. • Kumuahidi Mungu ya kwamba uko tayari kuepuka kila dhambi. • Kudumu katika njia ya toba hutokana tu na fadhila na ulinzi wa Mungu. • Kuomba toba inayosafisha madhambi ya kale pamoja na kuilinda nafsi na dhambi za baadae. • Kuomba toba inayomlinda mwanadamu na adhabu ya Mungu. • Kuomba toba yenye taufiki ya kukaa mbali na kila lililo kinyume na irada na mapenzi ya Mungu. • Kumwomba Mungu aamiliana na yule mtumishi mnyenyekevu kwa muamala wa heshima, huku akimwomba Mola wake kwa unyenyekevu na kilio. • Kukiri majuto, kuacha dhambi, na kuomba msamaha katika kuthibitisha toba. • Dua ya kufidia haki za watu zilizosahauliwa. • Kutafuta kinga ya Mungu dhidi ya kurejea tena kwenye dhambi. • Kuomba msamaha mbele ya Mungu tokana na ujinga. • Kutubu kutokana na matendo yanayomtoa mtu kwenye upendo wa Mungu. • Kuomba shafaa (uombezi) ingawa hatustahili kupa shufaa hiyo. • Kuomba shafaa kupitia ukarimu na ukuu wa Mwenye Ezi Mungu. • Hakuna wa kumlinda mtu dhidi ya adhabu ya Mungu. • Mbingu na ardhi ni miongoni mwa vyenye kushuhudia toba. • Kuwasilisha hoja kwa njia iliyo bora mbele ya Mungu, ili kuifanya dua ya mwombaji ikubaliwe. • Ukombozi wa watu wa kuepukana na ujinga na upotofu kupitia njia ya Muhammad na Ahlul‑Bait (a.s). [3] Tafsiri Chambuzi za Dua ya Thalathini na Moja Miongoni mwa tafsiri chambuzi kuhusiana na dua ya Thalathini na moja zilizoandikwa kwa lugha ya Kifarsi, ni ile tafsiri inayoatikana katika kitabu kiitwacho “Atar Ma’rifat: Golwajegane az Golestan Ma’arifat Tawbe”, kazi ya Sayyid Muhammad Zia’abadi. Kitabu hichi Kilichapishwa na Taasisi ya Bunyade Khairiyye al-Zahra (s.a) mjini Tehran mwaka 1393 SHamsia. [4] Pia Dua hii imeshughulikiwa kwa fasiriwa na vitabu mbali mbali ilivyofasiri matini za kitabu Sahifa al Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu hivyo vilivyoshughukikia dua hii pamoja na dua nyengi za Sahifa Sajjadiyya, ni pamoja na; Diyare Ashiqan, kazi iliyofanya na Hussein Ansarian, [5] Shuhud wa Shenakht kazi ya Mohammad Hasan Mamduhī Kermanshah, [6] na Sharhe wa Tarjomeye Sahife Sajjadiyya, kazi ya Sayyid Ahmad Fahri. [7] Tafsiri zote hizi zimeandikwa katika lugha ya Kifarsi. Waandishi wa lugha ya Kiarabu nao hawakuonekana kukaa nyuma katika jitihada za kufasiri dua za kitabu Sahifa Sajjadiyya, ikiwemo dua ya thalathini na moja ya kitabu hicho. Baadhi ya vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiarabu katika ufafanuzi wa kitabu hicho adhimu ni pamoja na; Riadhu al-Salikina, kitabu cha Sayyid Ali Khan Madani, [8] Fi Dhalali al-Sahifa al-Sajjadiyya, cha Muhammad Jawad Mughniyya, [9] Riadhu al-Arifina, cha Muhammad bin Muhammad Darabi, [10] na Afaqi al-Ruh, cha Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah. [11] Vilevile, msamiati wa dua hii umechambuliw na kufasiri katika kazi maalimu za kiisimu. Miongoni mwazo kama vile; Ta ‘aliqat ala al-Sahifa al-Sajjadiyya, kazi ya Faidhu Kashani [12] pamoja na Sharhu al-Sahifa al-Sajjadiyya, kazi ya Izzu al-Din al-Jaza’iri. [13] Matini ya Dua Kwa Kiarabu Pamoja na Maelezo ya Kiswahili وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي ذِكْرِ التَّوْبَةِ وَ طَلَبِهَا Na (ifuatayo ilikuwa ni) miongoni mwa dua zake (amani iwe juu yake), pale alipoizungumzia toba na kuitafuta toba hiyo (mbele ya Mola Wake). Matini ya hii imekuja kwa mtiririko usemao: اللَّهُمَّ يَا مَنْ لَا يَصِفُهُ نَعْتُ الْوَاصِفِينَ
Ewe Mwenye Ezi Mungu, Ewe ambaye hakuna sifa hata moja ya wasifu za (wale) wenye kukusifu yenye uwezo wa kukufafanua. وَ يَا مَنْ لَا يُجَاوِزُهُ رَجَاءُ الرَّاجِينَ
Na Ewe ambaye hapitwi na tumaini la wenye kutumaini. وَ يَا مَنْ لَا يَضِيعُ لَدَيْهِ أَجْرُ الُْمحْسِنِينَ
Na ewe ambaye kwake yeye hakupotea ujira wa watenda wema. وَ يَا مَنْ هُوَ مُنْتَهَى خَوْفِ الْعَابِدِينَ.
Na Ewe ambaye yeye ndiye kikomo cha khofu za wacha-Mungu وَ يَا مَنْ هُوَ غَايَةُ خَشْيَةِ الْمُتَّقِينَ
Na Ewe ambaye yeye ndiye kilele cha tahadhari za wachaji.
هَذَا مَقَامُ مَنْ تَدَاوَلَتْهُ أَيْدِي الذُّنُوبِ، وَ قَادَتْهُ أَزِمَّةُ الْخَطَايَا، وَ اسْتَحْوَذَ عَلَيْهِ الشَّيْطَانُ، فَقَصَّرَ عَمَّا أَمَرْتَ بِهِ تَفْرِيطاً، وَ تَعَاطَى مَا نَهَيْتَ عَنْهُ تَغْرِيراً.
Hii ni kadhia (ndiyo hali) ya yule ambaye ameyumbishwa na (kugeuzwa huku nakule) kwa mikono ya maasi (kwa nguvu za upepo wa maasi), na kuendeshwa na hatamu za dhambi, na Ibilisi akapata udhibiti dhidi yake. Hivyo basi, alidhihirisha mapungufu katika utekelezaji wa amri Zako (kwa kutelekeza wajibu wake), na akajihusisha na yale uliyoharamisha kwa msukumo wa mghafala wake (kwa msukumo wa kuhadalika kwake). كَالْجَاهِلِ بِقُدْرَتِكَ عَلَيْهِ، أَوْ كَالْمُنْكِرِ فَضْلَ إِحْسَانِكَ إِلَيْهِ حَتَّى إِذَا انْفَتَحَ لَهُ بَصَرُ الْهُدَى، وَ تَقَشَّعَتْ عَنْهُ سَحَائِبُ الْعَمَى، أَحْصَى مَا ظَلَمَ بِهِ نَفْسَهُ، وَ فَكَّرَ فِيما خَالَفَ بِهِ رَبَّهُ، فَرَأَى كَبِيرَ عِصْيَانِهِ كَبِيراً وَ جَلِيلَ مُخَالَفَتِهِ جَلِيلًا.
Kama vile yeye ni mjinga asiyejua uwezo wako juu yake, au kama yule anayekanusha fadhila za wema wako kwake, hadi pale jicho la uongofu lilipomfungukia, na mawingu ya upofu yakampambazukia. Ndipo (alipogutuka na) kutathmini yale aliyofanyia nafsi yake, na akatafakari na akataamali namna alivyomkhalifu Mola wake, na hivyo akatambua ukubwa wa uasi wake, na kuuhisabu kuwa ni mkubwa, kisha (akatathmini) uzito wa upinzani wake na kuuona kuwa ni mzito.
فَأَقْبَلَ نَحْوَكَ مُؤَمِّلًا لَكَ مُسْتَحْيِياً مِنْكَ، وَ وَجَّهَ رَغْبَتَهُ إِلَيْكَ ثِقَةً بِكَ، فَأَمَّكَ بِطَمَعِهِ يَقِيناً، وَ قَصَدَكَ بِخَوْفِهِ إِخْلَاصاً، قَدْ خَلَا طَمَعُهُ مِنْ كُلِّ مَطْمُوعٍ فِيهِ غَيْرِكَ، وَ أَفْرَخَ رَوْعُهُ مِنْ كُلِّ مَحْذُورٍ مِنْهُ سِوَاكَ.
Hivyo basi, (mja huyu) ameelekea kwako akiwa na matumaini kutoka wako, huku uso wake ukiwa na kutokana na utukufu wa dhati yako. Kwa kigezo cha uhakika wa kiimani aliokuwa nao, ameelekeza shauku yake kwenye mamlaka yako adhimu. Na kwa yakini yake isiyo na shaka, amekuelekea wewe kwa kilele cha shaku yake; na kwa msingi wa usafi wa nia (ikhlasi) yake, amejiwasilisha kwako huku khofu yake ikiwa ndiyo rasilimali katika safari yake hii ya kiroho. Bila shaka (amekuelekea Wewe), huku akiwa aiepusha tamaa yake na kila kinachotumainiwa, isipokuwa wewe; na ikaihamisha khofu yake kutoka kwa kila chanzo cha tishio, isipokuwa kwako wewe tu.
فَمَثَلَ بَيْنَ يَدَيْكَ مُتَضَرِّعاً، وَ غَمَّضَ بَصَرَهُ إِلَى الْأَرْضِ مُتَخَشِّعاً، وَ طَأْطَأَ رَأْسَهُ لِعِزَّتِكَ مُتَذَلِّلا، وَ أَبَثَّكَ مِنْ سِرِّهِ مَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنْهُ خُضُوعاً، وَ عَدَّدَ مِنْ ذُنُوبِهِ مَا أَنْتَ أَحْصَى لَهَا خُشُوعاً، وَ اسْتَغَاثَ بِكَ مِنْ عَظِيمِ مَا وَقَعَ بِهِ فِي عِلْمِكَ وَ قَبِيحِ مَا فَضَحَهُ فِي حُكْمِكَ مِنْ ذُنُوبٍ أَدْبَرَتْ لَذَّاتُهَا فََذَهَبَتْ، وَ أَقَامَتْ تَبِعَاتُهَا فَلَزِمَتْ.
Basi, akasimama mbele yako akiomba kwa unyenyekevu, na akayainamisha chini macho yake, na kuyaelekeza ardhini kwa heshima (Yako). Akakiinamisha kichwa chake kwa ajili kujidhalilisha (mbele Yako). Akakufunulia siri zake (mble Yako), hali ya kwamba wewe ni mjuzi zaidi wa siri hizo kuliko yeye mwenye, na akazihisabu (akakuhisabia) dhambi zake, akiwa katika hali unyenyekevu, hali ya kwamba wewe ni mjuzi wa zaidi wa idadi ya dhambi zake. Na ameomba msaada kwako, kutokana na uzito wa yale makubwa yaliyompata, miongoni mwa yale yalioko katika elimu yako, na ubaya wa yale (madhambi) yaliyomfedhehesha katika hukumu zako; madhambi ambayo ladha zake zimetaguli na kuondoka, na yakabaki madhara yake yakimwandama. لَا يُنْكِرُ يَا إِلَهِي عَدْلَكَ إِنْ عَاقَبْتَهُ، وَ لَا يَسْتَعْظِمُ عَفْوَكَ إِنْ عَفَوْتَ عَنْهُ وَ رَحِمْتَهُ، لِأَنَّكَ الرَّبُّ الْكَرِيمُ الَّذِي لَا يَتَعَاظَمُهُ غُفْرَانُ الذَّنْبِ الْعَظِيمِ Ewe Mungu wangu, iwapo utamuashidu, (katu mja huyu) hatanushi uadilifu (kutokana na hukumu hiyo), wala yeye hauoni msamaha wako kuwa ni jambo kubwa mno (lisilowezekana), iwapo utaamua kumsamehe na kumrehemu; kwa sababu Wewe ndiye Bwana Mkarimu ambaye hawezi kuelemewa na mzigo wa kusamehe dhambi kubwa (za waja wake).
اللَّهُمَّ فَهَا أَنَا ذَا قَدْ جِئْتُكَ مُطِيعاً لِأَمْرِكَ فِيما أَمَرْتَ بِهِ مِنَ الدُّعَاءِ، مُتَنَجِّزاً وَعْدَكَ فِيما وَعَدْتَ بِهِ مِنَ الْإِجَابَةِ، إِذْ تَقُولُ ﴿ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ﴾. Ee Mwenye Ezi Mungu, mimi ndiye huyu, nimekujia nikiwa mtiifu kwenye amri Zako juu ya yale uliyoamrisha kuhusiana na dua, (nimekuja) nikiutafuta utimilifu wa ahadi Yako katika ulivyoahidi kuhusiana na kuitikia (dua za waja wako), kwa sababu Wewe mwenyewe ulisema: “Niombeni, nami nitakujibuni”.
اللَّهُمَّ فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ الْقَنِي بِمَغْفِرَتِكَ كَمَا لَقِيتُكَ بِإِقْرَارِي، وَ ارْفَعْنِي عَنْ مَصَارِعِ الذُّنُوبِ كَمَا وَضَعْتُ لَكَ نَفْسِي، وَ اسْتُرْنِي بِسِتْرِكَ كَمَا تَأَنَّيْتَنِي عَنِ الِانْتِقَامِ مِنِّي.
Ee Mungu, mbariki basi Muhammad pamoja na Aali zake; unikabili (uniamili) kwa Maghfirah Yako kama vile mimi nilivyokukabili kwa kukiri kwangu (juu ya dhambi zangu); na uniweke mbali na uwanja wa mieleka ya dhambi, kama vile mimi nilivyoiweka nafsi yangu Kwako (mikononi kwako); na unistiri kwa stara Yako kama ulivyoakhirisha (ulivyoghairisha) kisasi cha dhidi yangu. اللَّهُمَّ وَ ثَبِّتْ فِي طَاعَتِكَ نِيَّتِي، وَ أَحْكِمْ فِي عِبَادَتِكَ بَصِيرَتِي، وَ وَفِّقْنِي مِنَ الْأَعْمَالِ لِمَا تَغْسِلُ بِهِ دَنَسَ الْخَطَايَا عَنِّي، وَ تَوَفَّنِي عَلَى مِلَّتِكَ وَ مِلَّةِ نَبِيِّكَ مُحَمَّدٍ عَلَيْهِ السَّلَامُ إِذَا تَوَفَّيْتَنِي.
Ee Mwenyezi Mungu, na ithibitishe nia yangu katika (njia ya) utiifu Wako, na imarisha basira yangu (welewa wangu) katika ibada Yako, na unijalie ufanisi katika matendo ambayo utayatumia katika kunitakasa kutokana na unajisi wa dhambi zangu; na wakati wa kufa kwangu, nifishe nikiwa katika itikadi ya dini Yako na dini ya Nabii Wako Muhammad (s.a.w.w). اللَّهُمَّ إِنِّي أَتُوبُ إِلَيْكَ فِي مَقَامِي هَذَا مِنْ كَبَائِرِ ذُنُوبِي وَ صَغَائِرِهَا، وَ بَوَاطِنِ سَيِّئَاتِي وَ ظَوَاهِرِهَا، وَ سَوَالِفِ زَلَّاتِي وَ حَوَادِثِهَا، تَوْبَةَ مَنْ لَا يُحَدِّثُ نَفْسَهُ بِمَعْصِيَةٍ، وَ لَا يُضْمِرُ أَنْ يَعُودَ فِي خَطِيئَةٍ
Ewe Mwenye Ezi Mungu, hakika mimi ninatubia kwako katika hali yangu hii (katika kisimamo changu hichi), kutokana na madhambi yangu makubwa na madogo, na maovu yangu ya siri na ya dhahiri, na makosa yangu yaliyopita na yajayo. Ninatubu toba ya mtu ambaye hatawazia katu uasi, na wala haweki nia ya kurudia tena kwenye kosa lolote lile.
وَ قَدْ قُلْتَ يَا إِلَهِي فِي مُحْكَمِ كِتَابِكَ إِنَّكَ تَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِكَ، وَ تَعْفُو عَنِ السَّيِّئَاتِ، وَ تُحِبُّ التَّوَّابِينَ، فَاقْبَلْ تَوْبَتِي كَمَا وَعَدْتَ، وَ اعْفُ عَنْ سَيِّئَاتِي كَمَا ضَمِنْتَ، وَ أَوْجِبْ لِي مَحَبَّتَكَ كَمَا شَرَطْتَ
Na bila shaka, Ewe Mungu wangu, Wewe mwenyewe umesema katika Kitabu chako chenye hukumu thabiti ukituambia kwamba; Wewe ni mwenye kukubali toba kutoka kwa waja wako, na ni mwenye kusamehe maovu yao, na ni mwenye kuwapenda wale wenye kutubia. Basi, ikubali toba yangu kama ulivyoahidi, na usayamehe maovu yangu kama ulivyodhamini, na uniwajibishie upendo wako kama ulivyosharitisha (kama ulivyojiwajibishia). وَ لَكَ يَا رَبِّ شَرْطِي أَلَّا أَعُودَ فِي مَكْرُوهِكَ، وَ ضَمَانِي أَنْ لَا أَرْجِعَ فِي مَذْمُومِكَ، وَ عَهْدِي أَنْ أَهْجُرَ جَمِيعَ مَعَاصِيكَ.
Na Kwako, Ewe Mola Mkuu, ninaweka sharti langu la kutojihusisha tena na vitendo vichukivu Kwako, hakikisho langu la kutorejelea mienendo yenye kulaumika, na agano langu la kuachana kikamilifu na ukiukaji wote wa amri Zako. اللَّهُمَّ إِنَّكَ أَعْلَمُ بِمَا عَمِلْتُ فَاغْفِرْ لِي مَا عَلِمْتَ، وَ اصْرِفْنِي بِقُدْرَتِكَ إِلَى مَا أَحْبَبْتَ.
Ewe Mwenyezi Mungu, hakika Wewe ni mjuzi kamili wa niliyoyatenda, basi nisamehe yale unayoyajua, na nielekeze kwenye yale unayoyapenda kwa uwezo wako.
اللَّهُمَّ وَ عَلَيَّ تَبِعَاتٌ قَدْ حَفِظْتُهُنَّ، وَ تَبِعَاتٌ قَدْ نَسِيتُهُنَّ، وَ كُلُّهُنَّ بِعَيْنِكَ الَّتِي لَا تَنَامُ، وَ عِلْمِكَ الَّذِي لَا يَنْسَى، فَعَوِّضْ مِنْهَا أَهْلَهَا، وَ احْطُطْ عَنِّي وِزْرَهَا، وَ خَفِّفْ عَنِّي ثِقْلَهَا، وَ اعْصِمْنِي مِنْ أَنْ أُقَارِفَ مِثْلَهَا.
Ewe Mwenye Ezi Mungu, nami nina dhima zilizomo ndani ya kumbukumbu yangu, na pi dhima nilizozisahau ambazo sina kumbukumbu nazo. Na zote hizo ziko chini ya uangalizi wa jicho Lako lisizolala, na ndani ya maarifa Yako yasiyokumbwa na ushau. Hivyo basi, wafidie wahusika wake (wanaohusika na dhima hizo), na unitue mzigo wa dhambi zake, nipunguza elemeo lake, na uniepushe (unilinde) na utendaji wa makosa yanayofanana nayo. اللَّهُمَّ وَ إِنَّهُ لَا وَفَاءَ لِي بِالتَّوْبَةِ إِلَّا بِعِصْمَتِكَ، وَ لَا اسْتِمْسَاكَ بِي عَنِ الْخَطَايَا إِلَّا عَنْ قُوَّتِكَ، فَقَوِّنِي بِقُوَّةٍ كَافِيَةٍ، وَ تَوَلَّنِي بِعِصْمَةٍ مَانِعَةٍ.
Ewe Mwenyezi Mungu, na hakika siwezi kutimiza (kudumisha ahadi ya) toba yangu isipokuwa kwa hifadhi yako, na wala siwezi kujizuia na makosa isipokuwa kwa nguvu zako. Basi, nipe nguvu za kutosha, na uniweke chini ya ulinzi wako uzuiao. اللَّهُمَّ أَيُّمَا عَبْدٍ تَابَ إِلَيْكَ وَ هُوَ فِي عِلْمِ الْغَيْبِ عِنْدَكَ فَاسِخٌ لِتَوْبَتِهِ، وَ عَائِدٌ فِي ذَنْبِهِ وَ خَطِيئَتِهِ، فَإِنِّي أَعُوذُ بِكَ أَنْ أَكُونَ كَذَلِكَ، فَاجْعَلْ تَوْبَتِي هَذِهِ تَوْبَةً لَا أَحْتَاجُ بَعْدَهَا إِلَى تَوْبَةٍ. تَوْبَةً مُوجِبَةً لَِمحْوِ مَا سَلَفَ، وَ السَّلَامَةِ فِيمَا بَقِيَ.
Ee Mola Mkuu, endapo mtumishi yeyote atatubu Kwako, huku elimu Yako ikijuwa wazi kuwa yeye atatangua toba yake na kurejea kwenye dhambi zake na makosa yake, basi mimi najilinda Kwako dhidi ya kuwa na hadhi kama hiyo. Hivyo, ifanye toba yangu hii kuwa toba isiyohitaji kufuatiwa na toba nyengine; toba inatakayopelekea kufutwa kwa yaliyotangulia na kudhamini usalama katika kipind cha maisha kilichosalia. اللَّهُمَّ إِنِّي أَعْتَذِرُ إِلَيْكَ مِنْ جَهْلِي، وَ أَسْتَوْهِبُكَ سُوءَ فِعْلِي، فَاضْمُمْنِي إِلَى كَنَفِ رَحْمَتِكَ تَطَوُّلًا، وَ اسْتُرْنِي بِسِتْرِ عَافِيَتِكَ تَفَضُّلًا.
Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninaomba radhi kwako kutokana na ujinga wangu, na nakuomba unipe msamaha (wako) kutokana na matendo yangu mabaya. Basi niingize katika hifadhi ya rehema zako kwa ukarimu wako, na unisitiri kupitia stara ya msamaha wako kwa fadhila zako. اللَّهُمَّ وَ إِنِّي أَتُوبُ إِلَيْكَ مِنْ كُلِّ مَا خَالَفَ إِرَادَتَكَ، أَوْ زَالَ عَنْ مَحَبَّتِكَ مِنْ خَطَرَاتِ قَلْبِي، وَ لَحَظَاتِ عَيْنِي، وَ حِكَايَاتِ لِسَانِي، تَوْبَةً تَسْلَمُ بِهَا كُلُّ جَارِحَةٍ عَلَى حِيَالِهَا مِنْ تَبِعَاتِكَ، وَ تَأْمَنُ مِمَا يَخَافُ الْمُعْتَدُونَ مِنْ أَلِيمِ سَطَوَاتِكَ.
Ewe Mwenyezi Mungu, kwa hakika mimi ninatubu kwako kutokana na kila jambo lililokwenda kinyume na matakwa yako, au kutoka nje ya upendo wako, kuanzia mawazo ya moyo wangu, mitupo ya jicho langu, pamoja na maneno yanayotiririka katika ulimi wangu. Ninatubia toba itakayokiepishia kila kiungo madhara ya adhabu yako kutokana na dhambi hizo, na kupata amani dhidi ya yale wanayoyaogopa warukao mipaka miongoni mwa adhabu zako kali ziumizazo. اللَّهُمَّ فَارْحَمْ وَحْدَتِي بَيْنَ يَدَيْكَ، وَ وَجِيبَ قَلْبِي مِنْ خَشْيَتِكَ، وَ اضْطِرَابَ أَرْكَانِي مِنْ هَيْبَتِكَ، فَقَدْ أَقَامَتْنِي يَا رَبِّ ذُنُوبِي مَقَامَ الْخِزْيِ بِفِنَائِكَ، فَإِنْ سَكَتُّ لَمْ يَنْطِقْ عَنِّي أَحَدٌ، وَ إِنْ شَفَعْتُ فَلَسْتُ بِأَهْلِ الشَّفَاعَةِ.
Ewe Mwenyezi Mungu, basi urehemu upweke wangu mbele ya mikono Yako, na mapigo wa moyo wangu kutokana na hofu Yako, na mtetemeko wa viungo vyangu kutokana na utukufu Wako. Kwani, Ewe Bwana, dhambi zangu zimeniweke katika hali ya kuona haya mbele Yako. Hivyo basi nikinyamaza, hakuna atakayesema kwa niaba yangu, na kama nitajitetea, basi mimi mwenye kustahili maombezi. اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ شَفِّعْ فِي خَطَايَايَ كَرَمَكَ، وَ عُدْ عَلَى سَيِّئَاتِي بِعَفْوِكَ، وَ لَا تَجْزِنِي جَزَائِي مِنْ عُقُوبَتِكَ، وَ ابْسُطْ عَلَيَّ طَوْلَكَ، وَ جَلِّلْنِي بِسِتْرِكَ، وَ افْعَلْ بِي فِعْلَ عَزِيزٍ تَضَرَّعَ إِلَيْهِ عَبْدٌ ذَلِيلٌ فَرَحِمَهُ، أَوْ غَنِيٍّ تَعَرَّضَ لَهُ عَبْدٌ فَقِيرٌ فَنَعَشَهُ. Ewe Mwenye Ezi Mungu, mrehema Muhammad na Aali zake, na ujaalie ukarimu wako uwe ni mwombezi wa makosa yangu, na yarejelee (yaandame) maovu yangu kwa msamaha wako. Wala usinilipe kwa adhabu yako kama ninavyostahili. Na unikunjulie fadhila zako, na nifunike kwa stara yako. Na uniamiali muamala wa Mwenye Nguvu ambaye mja dhalili amemnyenyekea naye akamrehemu, au Tajiri ambaye mja masikini amemwendea naye akamneemesha. اللَّهُمَّ لَا خَفِيرَ لِي مِنْكَ فَلْيَخْفُرْنِي عِزُّكَ، وَ لَا شَفِيعَ لِي إِلَيْكَ فَلْيَشْفَعْ لِي فَضْلُكَ، وَ قَدْ أَوْجَلَتْنِي خَطَايَايَ فَلْيُؤْمِنِّي عَفْوُكَ.
Ee Mola Mkuu, sina wa kinikinga Nawe, basi aha utukuwa Wako uweni ni wenye kunihami. Wala sina muombezi mbele Yako, basi acha hisani Yako iwe muombezi wangu. Na kwa hakika, makosa yangu yamenisababishia hofu, basi acha niwe chi ya dhamana ya msamaha Wako.
فَمَا كُلُّ مَا نَطَقْتُ بِهِ عَنْ جَهْلٍ مِنِّي بِسُوءِ أَثَرِي، وَ لَا نِسْيَانٍ لِمَا سَبَقَ مِنْ ذَمِيمِ فِعْلِي، لَكِنْ لِتَسْمَعَ سَمَاؤُكَ وَ مَنْ فِيهَا وَ أَرْضُكَ وَ مَنْ عَلَيْهَا مَا أَظْهَرْتُ لَكَ مِنَ النَّدَمِ، وَ لَجَأْتُ إِلَيْكَ فِيهِ مِنَ التَّوْبَةِ.
Basi, yote niliyoyanena hayatokani na ujahili wangu juu ya shari ya matendo yangu, wala kusahau kwangu amali zangu mbovu zilizotangulia. Bali (nimeyanena hayo) ili zisikie mbingu Zako pamoja na wakaao ndani yake, na ardhi Yako pamoja na wakaao juu yake, ile nadama niliyoiweka wazi mbele Yako, na (waiskie ile) toba niliyoitumia kama ni nyenzo ya kukimbilia ulinzi Wako. فَلَعَلَّ بَعْضَهُمْ بِرَحْمَتِكَ يَرْحَمُنِي لِسُوءِ مَوْقِفِي، أَوْ تُدْرِكُهُ الرِّقَّةُ عَلَيَّ لِسُوءِ حَالِي فَيَنَالَنِي مِنْهُ بِدَعْوَةٍ هِيَ أَسْمَعُ لَدَيْكَ مِنْ دُعَائِي، أَوْ شَفَاعَةٍ أَوْكَدُ عِنْدَكَ مِنْ شَفَاعَتِي تَكُونُ بِهَا نَجَاتِي مِنْ غَضَبِكَ وَ فَوْزَتِي بِرِضَاكَ. Yawezekana kwamba baadhi yao (miongoni wale liomo mbinguni na ardhini mwaka), watanihurumia kwa kudra ya rehema Zako, kutokana na uduni wa hadhi yangu, au watapatwa na hisia za huruma kwa ajili ya unyonge wa hali yangu, hali itakayopelekea kuniombea dua yenye usikivu mkubwa zaidi mbele Yako kuliko dua yangu mimi, au shufaa yenye madhubuti zaidi Kwako kuliko shafaa yangu mimi mwenyewe, na hivyo ikawa ndio njia ya kunusurika kwangu na ghadhabu Zako na kufaulu kwangu katika kupata ridhaa Yako.
اللَّهُمَّ إِنْ يَكُنِ النَّدَمُ تَوْبَةً إِلَيْكَ فَأَنَا أَنْدَمُ النَّادِمِينَ، وَ إِنْ يَكُنِ التَّرْكُ لِمَعْصِيَتِكَ إِنَابَةً فَأَنَا أَوَّلُ الْمُنِيبِينَ، وَ إِنْ يَكُنِ الِاسْتِغْفَارُ حِطَّةً لِلذُّنُوبِ فَإِنِّي لَكَ مِنَ الْمُسْتَغْفِرِينَ.
Ee Mwenye Ezi Mungu, ikiwa nadama hufasiriwa kuwa ni toba mbele Yako, basi mimi ndiye mkuu wa wenye nadama. Na endapo kuachana na uasi wako ni inaba (urejeo), basi mimi ni wa kwanza wa wenye kurejea (Kwako). Na endapo istighfari ni kifuto cha dhambi, basi hakika mimi ni miongoni mwa waombaji msamaha Kwako. اللَّهُمَّ فَكَمَا أَمَرْتَ بِالتَّوْبَةِ، وَ ضَمِنْتَ الْقَبُولَ، وَ حَثَثْتَ عَلَى الدُّعَاءِ، وَ وَعَدْتَ الْإِجَابَةَ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اقْبَلْ تَوْبَتِي، وَ لَا تَرْجِعْنِي مَرْجِعَ الْخَيْبَةِ مِنْ رَحْمَتِكَ، إِنَّكَ أَنْتَ التَّوَّابُ عَلَى الْمُذْنِبِينَ، وَ الرَّحِيمُ لِلْخَاطِئِينَ الْمُنِيبِينَ.
Ewe Mwenye Ezi Mungu, basi kama ulivyoamuru toba, na ukadhamini kuikubali, na ukahimiza kuomba dua, na ukaahidi kujibu, basi mswalie Muhammad na Aali zake, na ikubali toba yangu, na usinirejeshe katika hali ya kukata tamaa kutokana na rehema Zako. Hakika Wewe ndiye Mpokeaji wa toba kwa wenye dhambi, na Mwenye kuwarehemu wakosaji wanaorejea Kwako. اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، كَمَا هَدَيْتَنَا بِهِ، وَ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، كَمَا اسْتَنْقَذْتَنَا بِهِ، وَ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، صَلَاةً تَشْفَعُ لَنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَ يَوْمَ الْفَاقَةِ إِلَيْكَ، إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، وَ هُوَ عَلَيْكَ يَسيِرٌ.
Ewe Mwenye Ezi Mungu, mrehemu Muhammad na Aali zake, kwa kadiri ya hidaya uliyotujaalia kupitia yeye. Na msalie Muhammad na Aali zake, kama ulivyotuokoa kupitia muongozo wake. Na msalie Muhammad na Aali zake, sala itakayotuombea Siku ya Kiyama na siku ya uhitaji wetu Kwako. Hakika Wewe ni Muweza wa kila kitu, na hilo kwako ni jepesi.