Dua ya Sita ya Sahifa Sajjadiyya
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Abdullah Yazdi, iliyoandikwa katika Sha'ban 1102 AH. | |
Mtoaji / Mwandishi | Imamu Sajjad (a.s) |
---|---|
Lugha | Kiarabu |
Msimulizi / Mpokezi | Mutawakkil ibn Harun |
Mada | Dua imejikita katika kuelezea neema mbali mbali za Mwenye Ezi Mungu, ikiwemo neema ya uumbaji wa usiku na mchana, pamoja na mpangilio wake kamili na manufaa yake kwa maisha ya binadamu. |
Chanzo | Sahifa Sajjadiyah |
Tafsiri kwa Lugha ya | Kifarsi |
Dua ya Sita ya Sahifa Sajjadiyya (Kiarabu: الدعاء السادس من الصحيفة السجادية ) ni miongoni mwa dua maarufu zilizonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s) ambayo husomwa kila asubuhi na jioni, ikiwa ni sehemu ya ibada na nyiradi za kila siku. Imamu Sajjad (a.s) katika dua yake hii, ameashiria suala la uumbaji wa mchana na usiku, na jinsi gani mabadiliko haya yanavyo athiri maisha ya mwanadamu. Pia, ndani yake anasisitiza wajibu wa waumini ndani ya usiku na mchana, na namna ambavyo mwanadamu hutahiniwa na kupitia majaribio mbali mbali ndani ya vipindi viwili hivyo. Imam Sajjad (a.s) katika dua hii anaonesha ni jinsi gani viumbe wanavyotekeleza harakati zao kupitia uwezo wa Allah. Hivyo basi ametumia dua hii akimuomba Mungu Amuwafikishe katika kutenda amali njema, na kupata taufiki ya kumshukuru Mola wake. Aidha, duani mwake humu anathibitisha utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) huku akimuomba Allah ampe msamaha.
Dua hii imechambuliwa kwa mapana kabisa undani ya vitabu mbali mbali vya tafsiri ya Sahifatu Sajjadiyya, miongoni mwa vitabu hivyo ni pamoja na; Diyare Ashaqan cha Hussein Ansarian, kilichoandikwa kwa lugha ya Persia, na Riyadhu as-Salikin cha Sayyid Ali Khan Madani, kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu.
Mafuzo ya Sita
Muqtadha halisi wa Dua ya Sita kutoka katika Sahifa Sajadiyya, isomwayo kila asubuhi na jioni, umejikita katika kuelezea neema mbali mbali za Mwenye Ezi Mungu, ikiwemo neema ya uumbaji wa usiku na mchana, pamoja na mpangilio wake kamili na manufaa yake kwa maisha ya binadamu. Pia dua hii Inazungumzia majukumu na wajibu wa muumini katika kipindi cha siku nzima (usiku na mchana). Mengine yaliomo ndani ya dua hii, ni maombi ya Imamu Sajjad (a.s) ya kuomba kupata ufanisi wa kuwa na shukurani mbele ya Mwenye Ezi Mungu, pamoja na kumtakia rehema na amani Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Aali zake.[1] Vipengele vya Mafuzo ya dua hii ni kama ifuatavyo:
- Kuumbwa kwa usiku na mchana kwa uwezo wa Kimungu na maelezo juu ya mpangilio wa vipindi viwili hivi.
- Usiku ni chanzo cha utulivu, faraja, na fursa ya kupumzika na kurejesha nguvu, na ni moja ya nyakati muhimu ya kustarehe.
- Mchana ni chanzo cha mwanga kwa waja wa Mwenye Ezi Mungu ili waweze kujipatia neema, riziki, na njia ya kufikia fadhila za milele za Akhera.
- Majaribio kwa waja wa Mungu kupitia usiku na mchana.
- Kumshukuru Mwenye Ezi Mungu kwa kutupa neema ya usiku na mchana.
- Harakati za viumbe vyote chini ya uwezo na mipango ya Kiungu.
- Hakuna kheri isipokuwa ila ile itokayo kwa Mwenye Ezi Mungu.
- Ushuhuda wa mchana juu ya matendo ya wanadamu, dua kwa ajili ya kupata mchana mwema, na dua ya kutumia vizuri kila saa ya mchana huo.
- Malaika ni waandishi (na mashahidi) wa matendo ya wanadamu.
- Ombi la kuomba uongofu na upendo wa Mwenye Ezi Mungu.
- Dua ya kuepushwa na maasi ya Mwenye Ezi Mungu.
- Dua ya kuomba taufiki ya kutenda matendo mema, kuepukana na maovu, kuamrisha mema na kukataza maovu, kuutetea Uislamu, kumwongoza aliyepotea, kusaidia wanyonge, na kuwapa himaya wenye maamivu na huzuni.
- Kuridhika na hukumu (maamuzi) ya Kiungu na kushuhudia juu ya upweke na uadilifu wa Mwenye Ezi Mungu.
- Kushuhudia juu ya Utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na upendo wake katika kuutakia kheri umma wake, na ombi la kumtaka Mwenye Ezi Mungu kumpa bwana Mtume (s.a.w.w) malipo adhimu.
- Kuomba msamaha wa Mwenye Ezi Mungu.[2]
Tafsiri ya Dua ya Sita ya Sahifatu Sajjadiyya
Kuna tafsiri kadhaa za Dua ya sita, zinayopatikana katika vitabu vya tafsiri ya kitabu Sahifatu Sajjadiyya. Miongoni mwa vikitabu vilivyofasiri dua hii ni pamoja na; Diyaare Ashaqaan cha Hussein Ansarian,[3] Shuhud wa Shenakht cha Muhammad Hassan Mamdouhi Kermanshahi,[4] na Tafsiri wa Tarjume Sahife Sajadiyyye cha Sayyid Ahmad Fahri.[5] Maelezo ya dua hii yamechambuliwa kwa lugha ya Kifarsi.
Pia kwa upande wa pili, kuna vitabu vya Kiarabu vilivyokuja kufasiri dua hii, navyo ni pamoja na; Riyadhu al-Saalikina cha Sayyid Ali Khan Madani,[6] Fi Dhilali Al-sahifati Al-sajjaadiyya, cha Muhammad Jawad Mughniyya,[7] Riadhu Al-arifina, cha Muhammad bin Muhammad Daarabiy[8] na Afaqi al-Ruh cha Sayyid Muhammad-Hussein Fadhlullah.[9] Pia tafsiri ya msamiati wa maneno yake umefafanuliwa kwa umakini na Faydh Kashani, katika kitabu chake kiitwacho Taaliiqaat Alaa Al-sahifati Al-sajjadiyya.[10]
Matini ya Dua na Tafsiri yake
وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ عِنْدَ الصَّبَاحِ وَ الْمَسَاءِ
الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي خَلَقَ اللَّيْلَ وَ النَّهَارَ بِقُوَّتِهِ، وَ مَيَّزَ بَيْنَهُمَا بِقُدْرَتِهِ، وَ جَعَلَ لِكُلِّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا حَدّاً مَحْدُوداً، وَ أَمَداً مَمْدُوداً.
يُولِجُ كُلَّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا فِي صَاحِبِهِ، وَ يُولِجُ صَاحِبَهُ فِيهِ بِتَقْدِيرٍ مِنْهُ لِلْعِبَادِ فِيما يَغْذُوهُمْ بِهِ، وَ يُنْشِئُهُمْ عَلَيْهِ
فَخَلَقَ لَهُمُ اللَّيْلَ لِيَسْكُنُوا فِيهِ مِنْ حَرَكَاتِ التَّعَبِ وَ نَهَضَاتِ النَّصَبِ، وَ جَعَلَهُ لِبَاساً لِيَلْبَسُوا مِنْ رَاحَتِهِ وَ مَنَامِهِ، فَيَكُونَ ذَلِكَ لَهُمْ جَمَاماً وَ قُوَّةً، وَ لِيَنَالُوا بِهِ لَذَّةً وَ شَهْوَةً
وَ خَلَقَ لَهُمُ النَّهَارَ مُبْصِراً لِيَبْتَغُوا فِيهِ مِنْ فَضْلِهِ، وَ لِيَتَسَبَّبُوا إِلَى رِزْقِهِ، وَ يَسْرَحُوا فِي أَرْضِهِ، طَلَباً لِمَا فِيهِ نَيْلُ الْعَاجِلِ مِنْ دُنْيَاهُمْ، وَ دَرَكُ الآْجِلِ فِي أُخْرَاهُمْ
بِكُلِّ ذَلِكَ يُصْلِحُ شَأْنَهُمْ، وَ يَبْلُو أَخْبَارَهُمْ، وَ يَنْظُرُ كَيْفَ هُمْ فِي أَوْقَاتِ طَاعَتِهِ، وَ مَنَازِلِ فُرُوضِهِ، وَ مَوَاقِعِ أَحْكَامِهِ، لِيَجْزِيَ الَّذِينَ أَسَاؤُوا بِمَا عَمِلُوا، وَ يَجْزِيَ الَّذِينَ أَحْسَنُوا بِالْحُسْنَى.
اللَّهُمَّ فَلَكَ الْحَمْدُ عَلَى مَا فَلَقْتَ لَنَا مِنَ الْإِصْبَاحِ، وَ مَتَّعْتَنَا بِهِ مِنْ ضَوْءِ النَّهَارِ، وَ بَصَّرْتَنَا مِنْ مَطَالِبِ الْأَقْوَاتِ، وَ وَقَيْتَنَا فِيهِ مِنْ طَوَارِقِ الآْفَاتِ.
أَصْبَحْنَا وَ أَصْبَحَتِ الْأَشْيَاءُ كُلُّهَا بِجُمْلَتِهَا لَكَ سَمَاؤُهَا وَ أَرْضُهَا، وَ مَا بَثَثْتَ فِي كُلِّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا، سَاكِنُهُ وَ مُتَحَرِّكُهُ، وَ مُقِيمُهُ وَ شَاخِصُهُ وَ مَا عَلَا فِي الْهَوَاءِ، وَ مَا كَنَّ تَحْتَ الثَّري
أَصْبَحْنَا فِي قَبْضَتِكَ يَحْوِينَا مُلْكُكَ وَ سُلْطَانُكَ، وَ تَضُمُّنَا مَشِيَّتُكَ، وَ نَتَصَرَّفُ عَنْ أَمْرِكَ، وَ نَتَقَلَّبُ فِي تَدْبيِرِكَ.
لَيْسَ لَنَا مِنَ الْأَمْرِ إِلَّا مَا قَضَيْتَ، وَ لَا مِنَ الْخَيْرِ إِلَّا مَا أَعْطَيْتَ.
وَ هَذَا يَوْمٌ حَادِثٌ جَدِيدٌ، وَ هُوَ عَلَيْنَا شَاهِدٌ عَتِيدٌ، إِنْ أَحْسَنَّا وَدَّعَنَا بِحَمْدٍ، وَ إِنْ أَسَأْنَا فَارَقَنَا بِذَمٍّ.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ ارْزُقْنَا حُسْنَ مُصَاحَبَتِهِ، وَ اعْصِمْنَا مِنْ سُوءِ مُفَارَقَتِهِ بِارْتِكَابِ جَرِيرَةٍ، أَوِ اقْتِرَافِ صَغِيرَةٍ أَوْ كَبِيرَةٍ، وَ أَجْزِلْ لَنَا فِيهِ مِنَ الْحَسَنَاتِ، وَ أَخْلِنَا فِيهِ مِنَ السَّيِّئَاتِ، وَ امْلَأْ لَنَا مَا بَيْنَ طَرَفَيْهِ حَمْداً وَ شُكْراً وَ أَجْراً وَ ذُخْراً وَ فَضْلًا وَ إِحْسَاناً.
اللَّهُمَّ اجْعَلْ لَنَا فِي كُلِّ سَاعَةٍ مِنْ سَاعَاتِهِ حَظّاً مِنْ عِبَادِكَ، وَ نَصِيباً مِنْ شُكْرِكَ وَ شَاهِدَ صِدْقٍ مِنْ مَلَائِكَتِكَ.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ احْفَظْنَا مِنْ بَيْنِ أَيْدِينَا وَ مِنْ خَلْفِنَا وَ عَنْ أَيْمَانِنَا وَ عَنْ شَمَائِلِنَا وَ مِنْ جَمِيعِ نَوَاحِينَا، حِفْظاً عَاصِماً مِنْ مَعْصِيَتِكَ، هَادِياً إِلَى طَاعَتِكَ، مُسْتَعْمِلاً لِمَحَبَّتِكَ.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ وَفِّقْنَا فِي يَوْمِنَا هَذَا وَ لَيْلَتِنَا هَذِهِ وَ فِي جَمِيعِ أَيَّامِنَا لِاسْتِعْمَالِ الْخَيْرِ، وَ هِجْرَانِ الشَّرِّ، وَ شُكْرِ النِّعَمِ، وَ اتِّبَاعِ السُّنَنِ، وَ مُجَانَبَةِ الْبِدَعِ، وَ الْأَمْرِ بِالْمَعْرُوفِ، وَ النَّهْيِ عَنِ الْمُنْكَرِ، وَ حِيَاطَةِ الْإِسْلَامِ، وَ انْتِقَاصِ الْبَاطِلِ وَ إِذْلَالِهِ، وَ نُصْرَةِ الْحَقِّ وَ إِعْزَازِهِ، وَ إِرْشَادِ الضَّالِّ، وَ مُعَاوَنَةِ الضَّعيِفِ، وَ اِدْرَاكِ اللّهيِفِ.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اجْعَلْهُ أَيْمَنَ يَوْمٍ عَهِدْنَاهُ، وَ أَفْضَلَ صَاحِبٍ صَحِبْنَاهُ، وَ خَيْرَ وَقْتٍ ظَلِلْنَا فِيهِ
وَ اجْعَلْنَا مِنْ أَرْضَى مَنْ مَرَّ عَلَيْهِ اللَّيْلُ وَ النَّهَارُ مِنْ جُمْلَةِ خَلْقِكَ، أَشْكَرَهُمْ لِمَا أَوْلَيْتَ مِنْ نِعَمِكَ، وَ أَقْوَمَهُمْ بِمَا شَرَعْتَ مِنْ شرَائِعِكَ، وَ أَوْقَفَهُمْ عَمَّا حَذَّرْتَ مِنْ نَهْيِكَ.
اللَّهُمَّ إِنِّي أُشْهِدُكَ وَ كَفَى بِكَ شَهِيداً، وَ أُشْهِدُ سَمَاءَكَ وَ أَرْضَكَ وَ مَنْ أَسْكَنْتَهُمَا مِنْ مَلائِكَتِكَ وَ سَائِرِ خَلْقِكَ فِي يَوْمِي هَذَا وَ سَاعَتِي هَذِهِ وَ لَيْلَتِي هَذِهِ وَ مُسْتَقَرِّي هَذَا، أَنِّي أَشْهَدُ أَنَّكَ أَنْتَ اللَّهُ الَّذِي لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، قَائِمٌ بِالْقِسْطِ، عَدْلٌ فِي الْحُكْمِ، رَؤُوفٌ بِالْعِبَادِ، مَالِكُ الْمُلْكِ، رَحيِمٌ بِالْخَلْقِ.
وَ أَنَّ مُحَمَّداً عَبْدُكَ وَ رَسُولُكَ و خِيَرَتُكَ مِنْ خَلْقِكَ، حَمَّلْتَهُ رِسَالَتَكَ فَأَدَّاهَا، وَ أَمَرْتَهُ بِالنُّصْحِ لِأُمَّتِهِ فَنَصَحَ لَهَا
اللَّهُمَّ فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، أَكْثَرَ مَا صَلَّيْتَ عَلَى أَحَدٍ مِنْ خَلْقِكَ، وَ آتِهِ عَنَّا أَفْضَلَ مَا آتَيْتَ أَحَداً مِنْ عِبَادِكَ، وَ اجْزِهِ عَنَّا أَفْضَلَ وَ أَكْرَمَ مَا جَزَيْتَ أَحَداً مِنْ أَنْبِيَائِكَ عَنْ أُمَّتِهِ
إِنَّكَ أَنْتَ الْمَنَّانُ بِالْجَسِيمِ، الْغَافِرُ لِلْعَظِيمِ، وَ أَنْتَ أَرْحَمُ مِنْ كُلِّ رَحِيمٍ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ الطَّيِّبِينَ الطَّاهِرِينَ الْاَخْيَارِ الْاَنْجَبيِنَ.
Na ilikuwa miongoni mwa dua zake zilizokuwa zikiombwa na Imamu Sajjad (a.s), asubuhi na jioni. Ni ile dua isemayo:
Shukurani zote ni za Mwenye Ezi Mungu aliyeumba usiku na mchana kwa uwezo Wake, akazipambanua nyakati mbili hizo kwa nguvu Zake, na akaweka mpaka pambanuzi wa kila moja kati yake, kisha kila mmoja akaurefusha kwa kiwango chake maalumu.
Kila mmoja kati yao (kati ya usiki na mchana) huuingiza kwenye mwenza wake, na (yule aliyeingizwa kwa mwenzke) naye huwaingiza mwenzake (anayefuata baada yake). Yote hayo hutendeka kwa mipango na takwimu maalumu, kwa ajili ya ile lishe anayowalisha nayo, na ule ukuwaji wao anaowakuza nao.
Kwa hiyo (Mwenye Ezi Mungu) aliwaumba usiku ili wapumzike ndani yake kutokana machofu ya harakati (za mchana) na juhudi (zao mbali mbali), kisha akaufanya (usiku huo) kuwa ni vazi ili wauvae utulivu uliomo ndani yake, na kufaidika na usingizi wake, nao uwe ni ujazo na nguvu (utakaowapa nguvu mpya), na ili waweze kufikia starehe na ladha (za kindoa).
Na akawaumbia mchana wenye nuru, ili (waja Wake) waweze kutafuta fadhili za Mola wao ndani yake na wautumia mchana huo kama ni njia ya kuzifikia rizki za Mola wao. Kisha wasambae katika ardhi Yake kwa lengo la kupata kipato cha kidunia kwa ajili ya dunia yao. Kisha wachume chumo la Akhera yao ndani yake.
Mwenye Ezi Mungu hutumia mambo haya yote, kwa ajili ya kuwarekebishia wanadamu mambo yao, humurika na kutahini nyenendo zao, na huangalia jinsi ya hali zao zilivyo katika ndani ya nyakati za ibada Yake, na walivyo katika (kutekeleza na kuthamini) daraja mbali mbali za wajibu Wake, na namna wanavyoamilia na nyanja mbali mbali za hukumu Zake; (yote hayo) ili aje kuwaadhibu wale waliotenda maovu kutokana na matendo yao hayo, na awatuze kwa tunzo njema wale waliotenda mema.
Ee Mola! Ni Wewe tu unayestahiki kushukuriwa kwa neema hii ya kutupasulia (kutupambazulia) giza la usiku na ukatudhihirishia nuru ya asubuhi, na ukatuneemesha kwa mwangaza wa mchana (baada ya giza hilo), na ukatuelekeza jinsi ya kujitafutia riziki, na ukatulinda dhidi ya majanga yazukayo ndani ya zaman a nyakati mbali mbali.
Tumeamka katika uwanja wa milki Yako. Na vyote vilivyomo mbinguni na ardhini vimeingiliwa na asubuhi (Yako), hali vikiwa vimemilikiwa na mamlaka ya Ufalme Wako. Kwa baraka ya amri Yako tunatenda mambo, na chini ya mpango Wako tunabadilika.
Tumeingiwa na asubuhi hali tukiwa tumo katika udhibiti wako, tumezungukwa na utawala wako, na tumekumbatiwa na (mbweleko wa) mapenzi Yako, na kila tulitendalo twalitenda uwezo wako (kwa maamuzi yako), na tunazunguka (huku na kule) kwa mipango yako.
Hakuna lolote tunalolimudu mikononi mwetu, isipokuwa lile ulilolipitisha, wala hakuna chochote kile chenye kheri kwetu isipokuwa kile ulichotupatia.
Na ni siku hii ya leo ni tukio jipya, nayo kwetu ni shuhuda imara kwetu, iwapo tutafanya mema ndani yake, basi tutaagana nayo huku tukihimidiwa, na iwapo tutatenda maovu basi tuachana nayo kwa lawama (huku tukilaumiwa).
Ewe Mola, mbariki Muhammad na Aali zake, na utujalie kuwa na uhusiano bora naye, na tuepushe na kuwa uhusiano mbaya dhidi yake kupitia utendaji wa dhambi, au kwa njia ya kuchuma dhambi ndogo au kubwa. Na tutunuku wingi wa kheri ndani yake, na utuepushe na mabaya ndani yake, na ujazie baina ya upande zake mbili (mwanzo wa siku na mwisho wake) shukuruni, sifa njema, thawabu, hazina (ustawi), fadhila, pamoja na hisani.
Ewe Mola wetu, tunakuomba utujalie kuwa na sehemu (nafasi na wasaa maalumu) kwa ajili ya ibada Yako, na (uturuzuku) sehemu ya muda fulani kwa ajili shukrani zako, na utuwekee shuhuda (mlinzi) wa ukweli (wa imani na amali zetu) miongoni kwa malaika wako.
Ewe Mola, mbariki Muhammad na Aali zake, na utuwekee ulinzi mbele kwetu, nyuma yetu, kuliani kwetu, kushotoni kwetu, pamoja na kila pembe iliyotuzunguka. Tupe ulinzi utakaotuepesha na maasi yako, ambao utatuongoza na kutuweka kwenye njia ya taa (umtiifu) Yako, ulinzi ambao utafanya kazi yake kupitia upendo Wako (kwetu).
Ewe Mola, mbariki Muhammad na Aali zake, na utuwafikishe kufanya mema ndani ya mchana wetu huu, na usiku wake, pamoja na masiku mengine yote yaliyomo maisha mwetu. Tupe uwezo wa kuepuka mabaya, kushukuru neema Zako, kufuata Sunna sahihi, kuepuka bida’a, kuamrisha mema, na kukataza mabaya, kuulinda Uislamu, kudhahalilisha batili, kuiiunga mkono haki kuisaidia, kumwongoza aliyepotea, kumsaidia mnyonge na kumpa himaya aliyegubikwa na matatizo.
Ewe Mola, mbariki Muhammad na Aali zake, na ufanye siku yetu hii ya leo kuwa ndiyo siku bora zaidi maishani mwetu, na uijaalie kuwa ni rafiki bora zaidi tuliyesahibiana naye, na wakati (uwe ndio wakati) mzuri zaidi tuliokaa ndani yake.
Na tufanye tuwe ndio walioridhika zaidi miongoni mwa wale waliopitiwa na usiku na mchana miongoni mwa waja Wako, na tuwe ndiwo wenye kushukurani zaidi miongoni wale uliowaneemesha kwa neema Zako, na utujaalie tuwe ndiwo imara na mashupavu zaidi juu ya sheria na amana Zako za kisheria, na tuwe ndiwo wenye msimamo makini zaidi katika kuepuka yale yote uliyoyaonya kwa makatazo Yako.
Ewe Mola wangu! Hakika mimi ninakushuhudisha, na wewe unatosha kuwa ni shahidi. Na ninaishuhudisha mbingu Yako, ardhi yako, na Malaika Wako miongoni mwa wale uliowawekwa ndani mbingu na ardhi Yako, pamoja na viumbe wako wote walioko katika mchana wangu huu wa leo, saa yangu hii, usiku wangu huu, na mahali pangu hapa, kwamba mimi ninashuhudia kwamba wewe ndiye Mungu (wa haki), ambaye hakuna mungu mwingine yeyote yule ila wewe tu, umesimamia (umejidhatiti) kwa uadilifu (haki), Mwadilifu katika hukumu Zako, na ni mwenye huruma kwa waja wako, mfalme wa ufalme (utawala), na mwenye rehema kwa viumbe Wako.
Na kwamba Muhammad ni mja Wako na mjumbe Wako, na ndiye bora zaidi miongoni mwa viumbe wako. Ulimwisha dhamana ya ujumbe wako naye akaifikisha ipaswavyo, na ulimwamuru kuusia umma wake, naye akauusia ipaswavyo.
Ewe Mola, mbariki Muhammad na Aali zake, kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko unavyombariki mwengine yeyote yule miongoni mwa viumbe wako. Na umpe ujira bora zaidi (kutokana na kheri alizotufanyia), ujira ambao uwe ni mkubwa zaidi kuliko malipo ya wengine wote miongoni mwa waja wako. Mlipe malipo makubwa mno yenye ukarimu wa hali ya juu kabisa, kuliko malipo anayopata nabii wako yeyote yule (kutokana na kazi yake katika) umma wake.
Hakika wewe ni Mtoaji anayetoa neema isiyo na kifani, Msamehevu wa makosa makubwa, na Wewe ndiye Mrehemevu zaidi kuliko warehemevu wengine wote. Basi, mbariki Muhammad na Aali zake wema na watoharifu, walio bora, na wlioteuliwa kwa uteule maalumu.
Rejea
- ↑ Mamduhi, Shuhud wa Shanakhte, 1388, juz. 1, uk. 357.
- ↑ Ansarian, Diyar Ashiqan, 1371, juz. 4, uk. 15-101.
- ↑ Ansarian, Diyar Ashiqan, 1371, juz. 4, uk. 15-101.
- ↑ Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shanakhte, 1388 S, juz. 1, uk. 357-420.
- ↑ Fihri, Sharh wa Tafsir Sahifa Sajjadiyah, 1388 S, juz. 1, uk. 319-390.
- ↑ Madani Shirazi, Riadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 2, uk. 175-300.
- ↑ Mughniyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 19–134.
- ↑ Darabi, Riadh al-Arifin, 1379 AH, uk. 103–118.
- ↑ Fadhlulallah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 1, uk. 133-184.
- ↑ Faidh Kashani, Taaliqat Ala al-Sahaifa al-Sajadiyeh, 1407 AH, uk. 30-33.
Vyanzo
- Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
- Khalji, Muhammad Taqi, Asrar al-Khamushan, Qom, Parto Khorshid, 1383 S.
- Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
- Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
- Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
- Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
- Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
- Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
- Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.