Bendera nyeusi

Kutoka wikishia

Bendera Nyeusi (Kiarabu: الرّايات السود) au al-Rāyāt al-sūd, ni ibara iliyokuja katika hadithi na inaashiria mapinduzi na harakati zitakazoanzishwa na kundi litalokuwa linamiliki au kubeba bendera nyeusi huko mashariki. Katika hadithi nyingi bendera nyeusi zimehusishwa na harakati ya Abu Muslim Khorasani na kuundwa dola ya Bani Abbasi. Baadhi ya hadithi miongoni mwazo pia zinaeleza kuwa, bendera nyeusi ni ishara ya kudhihiri mwokozi wa ulimwengu katika zama za mwisho (Akher zaman).

Watafiti wa masuala ya hadithi wanasema kuwa, hadithi hizi zimekuja zaidi katika vyanzo vya Kisuni na hadithi ambazo wapokezi wake wote ni shia zinaeleza kwamba, bendera nyeusi zinahusiana na harakati ya Abu Muslim Khorasani na ziko dhidi ya utawala wa Bani Umayya. Hata hivyo, mkabala wake baadhi ya watu pia wanaamini kwamba, bendera nyeusi ni ishara ya kudhihiri Imam Mahdi (a.t.f.s)

Utambuzi wa Maana (Conceptology)

Bendera nyeusi au al-Rāyāt al-sūd, ni ibara iliyokuja katika hadithi na inaashiria mapinduzi na harakati zitakazoanzishwa na kundi litakalokuwa na bendera nyeusi katika Khorasan. [1] Makusudio ya Khorasan katika hadithi hizi ni Khorasan ya kale ambayo ilikuwa ikujumuisha sehemu kubwa ya Iran, Afghanistan, Turkemanistan, Tajikistan na Uzbekistan. [2]

Vyanzo vya Hadithi za Bendera Nyeusi

Kwa mujibu wa waandishi wa tabu la maarifa kuhusu Imam Mahdi (Encyclopedia of Imam al-Mahdi), hadithi nyingi zinazohusiana na bendera nyeusi zinapatikana katika vitabu vya Ahlu-Sunna. Katika vyanzo vikuu vya hadithi vya Mashia, kuna hadithi chache kuhusiana na bendera nyeuzi zilizonukuliwa kutoka kwa Maimamu na akthari ya hadithi zilizonukuliwa katika uga huu zimenukuliwa kutoka kwa wapokezi wa hadithi wa Kisuni. [3]

Muhtawa (Maudhui) wa Hadithi

Katika baadhi ya hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebu ya Shia, bendera nyeusi zimeelezwa kuwa ni Alama za kudhihiri Imamu Mahdi (a.t.f.s). Kwa mfano katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imam Ali bin Abi Twalib (a.s), hitilafu baina ya watu wa Sham, bendera nyeusi na ukelele wa mbinguni katika mwezi wa Ramadhani zimetajwa kuwa ni katika ishara za kudhihiri mwokozi wa ulimwengu. Hata hivyo katika hadithi nyingine, bendera nyeusi zimehusishwa na kusambaratika utawala wa bani Umayya na harakati ya Abu Muslim Khorasani. Kwa mfano, katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imam Muhammad Baqir (a.s) kumeashiriwa suala la kusambaratika utawala wa Bani Umayya na Bani Abbas na kukazungumziwa suala la watu wa bendera nyeusi. [4] Kadhalika katika hadithi Abu Muslim Khorasani ametajwa wazi kabisa na bayana kwamba, ni mwenye bendera nyeusi. [5]

Mambo Yaliyozungumziwa pia katika Hadithi Zilizonukuliwa na Ahlu Sunna ni kama Ifuatavyo:

  1. Kusambaratika Bani Umayya baada ya mapinduzi na harakati ya bendera nyeusi. [6]
  2. Kulaumiwa watu ambao wataingia madarakani baada ya harakati ya bendera nyeusi. [7]
  3. Hitilafu miongoni mwa watu wa bendera nyeusi. [8]
  4. Kujitokeza Sufyani. [9]
  5. Ukamnada wa Shuaib bin Salih [10]
  6. Kudhihiri Imam Mahdi (a.t.f.s) katika mji wa Makka baada ya bendera nyeusi. [11]

Bendera Nyeusi ni Ishara ya Kudhihiri?

Baadhi ya wanazuoni na watafiti wa Kishia wanasema kuwa, makusudio ya bendera nyeusi ni harakati ya Abu Muslim Khorasani ambayo ilitokea dhidi ya utawala wa Bani Umayya na kupelekea kuasisiwa utawala wa Bani Abbasi. [12] Wanaamini kuwa, riwaya khalis (yaani hadithi ambazo wapokezi wake ni Mashia) hawajasimulia kwamba, hadithi za bendera nyeusi ni ishara za kudhihiri Imam Mahdi (a.t.f.s). Na lile kundi fulani la vyanzo vya Kishia ambavyo vimetambua kwamba, bendera nyeusi ni ishara ya kudhihiri Imam Mahdi (a.t.f.s) vimetegemea hadithi za Ahlu-Sunna. [13] Sayyid Muhammad Sadr ameandika, zimekuja hadithi mbalimbali kuhusiana na utawala wa Bani Abbasi ambapo akthari yake ni bandia na moja ya mbinu zilizoungwa mkono na Bani Abbas ni hizi hadithi ambazo zilitumiwa na utawala huo ambao ulinufaika nazo [14].

Pamoja na hayo yote, kuna watu wanaoamini kwamba, bendera nyeusi ni ishara ya kudhihiri Imam Mahdi (a.t.f.s) na zinaashiria harakati ambayo itatokea kabla ya kudhihiri kwake. [15] Mwandishi wa kitabu cha Asr al-Dhuhur amezitambua bendera nyeusi kuwa ni za Sayyid Khorasani ambapo kamanda wa jeshi lake ni Shuaib bin Salih na kutatokea vita baina ya jeshi lake na Sufyani na atamshinda Sufyani [16] na kisha kutoa baia na kiapo cha utii kwa Imam Mahdi (a.t.f.s). [17] Inaelezwa kuwa, katika kitabu cha Asr al-Dhuhur kwa ajili ya kuthibitisha jambo hili, kumetegemewa hadithi kutoka katika kitabu cha al-Fitan cha Ibn Hammad, hata hivyo kitabu tajwa hakina itibari kwa Mashia, kwani akthari ya hadithi zake hazijatoka kwa Maasumina (a.s). [18]

Daesh na Hadithi za Bendera Nyeusi

Baadhi ya wafuasi wa kundi la kigaidi la Daesh wamefasiri kwamba, hadithi zinazohusiana na bendera nyeusi zinalihusu kundi la Daesh ambalo linatumia bendera nyeusi kama alama yao. [19] Rasul Ja’fariyan mtafiti wa masuala ya kihistoria, sambamba na kuzitambua kuwa bandia hadithhi za bendera nyeusi anasema, baadhi ya Maulamaa wa Ahlu Sunna pia hawajakubali usahihi wa hadithi hizi na endapo zitakuwa sahihi, sio sahihi kuzitabikisha na kuzihusisha na kundi la Daesh.