Nenda kwa yaliyomo

Aya ya Ilai

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Aya ya Ilai (aina ya kiapo))
Makala hii inahusiana na Aya ya 226 katika Surat al-Baqarah ambayo ni mashuhuri kwa jina la Aya ya Ilai. Ili kujua kuhusiana na mafuhumu (maana) ya kifikihi ya Ilai, angali makala ya Ilai.
Aya ya Ilai

Aya ya Ilai (Kiarabu: آية الإِيلَاء) (Baqarah: 226) inazungumzia Ilai na hukumu zake. Ilai ni katika ada zilizokuwako enzi za Ujahilia na maana yake ni mwanaume kula kiapo cha kuacha kuwa na mahusiano ya tendo la ndoa na mkewe ambapo katika Uislamu ni haramu na jambo hilo limetengewa na kuainishiwa adhabu ya kafara. Lengo la hatua hii katika zama za ujahilia lilikuwa ni kumtesa na kumuudhi mke, kumuacha anatangatanga na kumzuia asiolewe tena. Katika Aya hii Mwenyezi Mungu anabainishha hukumu za Ilai na njia za kufungua hilo.

Kwa mujibu wa Aya hii, endapo mwanaume atafanya kiapo cha Ilai, mke anaweza kwenda kushtaki kwa Mtawala wa Sheria au mahakamani. Mtawala wa sheria atampa mume muda wa miezi minne kumrejea mke wake ghairi ya hivyo atamlazimisha ampe talaka mkewe huyo.

Utambulisho na Sababu

Aya ya 226 ya surat al-Baqara inatambuliwa kwa jina la Aya ya Ilai. [1] Katika Aya hii Mwenyezi Mungu anaipinga ada na tabia hii ya kijahilia ya Ilai na anabainisha njia za kufungua tatizo hili [2] na inatoa hukumu ya kuhuisha haki za wanawake. [3] Ilai ni ada iliyokuwa imezoeleka katika zama za ujahilia. [4] Ilikuwa kwa namna hii, katika zama za ujahilia, ikitokea kwamba, mwanaume amemchukia mkewe, basi alikuwa akiapa kwamba, hatakutana naye kimwili [5] wala kumpa talaka [6] kwa mwaka au miaka kadhaa [7] au mpaka mwisho wa umri wake. [7] Inaelezwa kuwa, lengo la hatua hii [8] katika zama za ujahilia lilikuwa ni kumtesa na kumuudhi mke, kumuacha anatangatanga na kumzuia asiolewe tena. [9]

لِلَّذِينَ يُؤْلُونَ مِنْ نِسَائِهِمْ تَرَبُّصُ أَرْبَعَةِ أَشْهُرٍ فَإِنْ فَاءُوا فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ


Kwa wanao apa kuwa watajitenga na wake zao, wangojee miezi mine. Wakirejea basi Mwenyezi Mungu hakika ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.



(Qur'an: 2: 226)


Matumizi ya Kifikihi

Makala Kuu: Ilai
  • Kuharamishwa Ilai: Ilai kwa mtazamo wa kifikihi ni haramu na sababu ya hilo ni kuharamishwa katika Uislamu kuacha kukutana kimwili na mke kwa zaidi ya miezi mine. [10] Baadhi wamechukua kuharamishwa Ilai kutoka katika Aya ya 226 ya Surat al-Baqara. [11] Hata hivyo kwa mujibu wa Ayatullah Makarim Shirazi ni kuwa, Qur'an haijabatilisha kabisa hukumu ya Ilai, lakini imeondoa athari zake mbaya; kwani hairuhusu mwanamke kuteswa na kuudhiwa na mumewe na kufanywa mtu wa kutangatanga. [12]
  • Kwa mujibu wa Aya ya Ilai mafakihi wanaamini kwamba, Mafakihi wanaamini kuwa, kama mwanaume atakula kiapo cha Ilai, mke anaweza kwenda kushtaki kwa Mtawala wa Sheria. Mtawala wa sheria atampa mume muda wa miezi minne kumrejea mke wake na baada ya kukutana naye kimwili atoe kafara ya kuvunja kiapo. [13] Kama mwanaume katika kipindi na muda huu aliopatiwa na mtawala wa Sheria hatafanya hivyo, mtawala wa sheria atampa hiari baina ya kumrejea mke na kutoa talaka na kama atakataa kufanya lolote kati ya mawili hayo atamlazimisha kuchagua baina ya hukumu ya kufungwa na kubinywa katika kupewa chakula. [14] Baadhi ya mafakihi wanaamini kwamba, katika hali hii mtawala wa sheria anaweza kumpa talaka mwanamke huyo. [15]
  • Masharti ya Ilai: Ili Iilai itimie kuna masharti ambayo yametajwa na kubainishhwa; [16] miongoni mwayo ni kuwa: Kuapa kunapaswa kuwa kwa kutumia moja ya majina ya Mwenyezi Mungu, [17] kabla ya kula kiapo cha Ilai mke na mume wanapaswa kuwa hapo kabla waliwahi kukutana kimwili [18], msukumo na sababu ya mfanya Ilai (yaani mume) inapaswa kuwa ni kwa ajili ya kumuudhi mkewe. [19]
  • Mafakihi wanaamini kwamba, makusudii ya فى‌ء yaani kurejea katika Aya hiii ni kukutana kimwili au kuonyesha kutaka hilo wakati kunapokuwa na vizuizi vya kisheria au maradhi. [20]

Rejea

Vyanzo

  • Ālūsī, Maḥmūd b. ʿAbd Allāh al-. Rūḥ al-maʿānī fī tafsīr al-Qurʾān al-ʿaẓīm. Edited by ʿAlī ʿAbd al-Bārī al-ʿAṭīyya. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1415 AH.
  • Abū l-Futūḥ al-Rāzī, Ḥusayn b. 'Alī. Rawḍ al-Jinān wa Rawḥ al-Janān fī Tafsīr al-Qurʾān. Mashhad: Āstān-i Quds-i Raḍawī, 1408 AH.
  • ʿAyyāshī, Muḥammad b. Masʿūd al-. Tafsīr al-ʿAyyāshī. Edited by Rasūlī Maḥallātī. Tehran: al-Maktaba al-ʿIlmīyya, 1380 Sh.
  • Abū Ḥayyān Andulusī, Muḥammad b. Yusuf. Al-Baḥr al-muḥīṭ fī al-tafsīr. Beirut: Dār al-Fikr, 1420 AH.
  • Bayḍāwi, ʿAbd Allāh b. ʿUmar. Anwār al-tanzīl wa asrār al-taʾwīl. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1418 AH.
  • Dīnawarī, ʿAbd Allāh b. Muḥammad. Al-Wāḍiḥ fī tafsīr al-Qurʾān al-karīm. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1424 AH.
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-. Al-Tafsīr al-Kabīr. 3rd edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
  • Fayḍ al-Kāshānī, Muḥammad b. al-Murtaḍā al-. Tafsīr al-Ṣāfī. Edited by Ḥusayn Aʿlamī. 2nd edition. Tehran: Maktabat al-Ṣadr, 1415 AH.
  • Ibn ʿArabī, Muḥammad b. ʿAbd Allah. Aḥkām al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Jayl, 1408 AH.
  • Jurjānī, ʿAbd al-Qāhir b. ʿAbd al-Raḥmān. Darj al-durar fī tafsīr al-Qurʾān al-ʿaẓīm. Jordan: Amman: Dār al-Fikr, 1430 AH.
  • Jaʿfarī, Yaʿqub. Tafsīr kawthar. Qom: Muʾassisat Intishārāt-i Hijrat, 1376 Sh.
  • Mughnīya, Muḥammad Jawād al-. Tafsīr al-Kāshif, Qom: Dār al-Kitāb al-Islāmī, 1424 AH.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. 10th edition. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1371 Sh.
  • Qummī, ʿAlī b. Ibrāhīm al-. Tafsīr al-Qummī. 3rd edition. Qom: Dār al-Kitāb, 1363 Sh.
  • Sulṭān ʿAlīshāh, Muḥammad b. Ḥaydar. Matn wa tarjuma-yi fārsī-yi bayān al-saʿāda fī maqāmāt al-ʿibāda. Tehran: Sirr al-Asrār, 1372 Sh.
  • Thaʿlabī, Aḥmad b. Muḥammad al-. Al-Kashf wa l-bayān ʿan tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1422 AH.
  • Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. 2nd edition. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1490 AH.
  • Ṭaliqānī, Maḥmūd. Partuwī az Qurʾān. 4th edition. Tehran: Shirkat-i Sahāmī-yi Intishār, 1362 Sh.
  • Ṭabarānī, Sulaymān b. Aḥmad. Tafsīr al-kabīr: tafsīr al-Qurʾān al-ʿazīm. Irbid, Jordan: Dār al-Kitāb Thiqāfī, 2008.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Tafsīr-i jawāmiʾ al-jāmiʾ. 1st Edition. Qom: Markaz-i Mudīrīyat-i Ḥawza-yi Ilmīya-yi Qom, 1412 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Tehran: Naṣir Khusru, 1372 Sh.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Tibyān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d].
  • Zamakhsharī, Maḥmūd b. ʿUmar al-. Al-Kashshāf ʿan ḥaqāʾiq ghawāmiḍ al-tanzīl wa ʿuyūn al-aqāwīl fī wujūh al-tʾawīl. 3rd edition. Beirut: Dār al-Kitāb al-ʿArabī, 1407 AH.