Aya ya Ilai
- Makala hii inahusiana na Aya ya 226 katika Surat al-Baqarah ambayo ni mashuhuri kwa jina la Aya ya Ilai. Ili kujua kuhusiana na mafuhumu (maana) ya kifikihi ya Ilai, angali makala ya Ilai.
Jina la Aya | Aya ya Ilai |
---|---|
Sura Husika | Baqara |
Namba ya Aya | 226 |
Juzuu | 2 |
Sababu ya Kushuka | Wanaume Kuwatenga Wake Zao |
Mahali pa Kushuka | Madina |
Mada Yake | Hukumu za Kifamilia |
Mengineyo | Hukumu za Kutengana Kati ya Mume na Mke |
Aya ya Ilai (Kiarabu: آية الإِيلَاء) (Baqarah: 226) inazungumzia Ilai na hukumu zake. Ilai ni katika ada zilizokuwako enzi za Ujahilia na maana yake ni mwanaume kula kiapo cha kuacha kuwa na mahusiano ya tendo la ndoa na mkewe ambapo katika Uislamu ni haramu na jambo hilo limetengewa na kuainishiwa adhabu ya kafara. Lengo la hatua hii katika zama za ujahilia lilikuwa ni kumtesa na kumuudhi mke, kumuacha anatangatanga na kumzuia asiolewe tena. Katika Aya hii Mwenyezi Mungu anabainishha hukumu za Ilai na njia za kufungua hilo.
Kwa mujibu wa Aya hii, endapo mwanaume atafanya kiapo cha Ilai, mke anaweza kwenda kushtaki kwa Mtawala wa Sheria au mahakamani. Mtawala wa sheria atampa mume muda wa miezi minne kumrejea mke wake ghairi ya hivyo atamlazimisha ampe talaka mkewe huyo.
Utambulisho na Sababu
Aya ya 226 ya surat al-Baqara inatambuliwa kwa jina la Aya ya Ilai. [1] Katika Aya hii Mwenyezi Mungu anaipinga ada na tabia hii ya kijahilia ya Ilai na anabainisha njia za kufungua tatizo hili [2] na inatoa hukumu ya kuhuisha haki za wanawake. [3] Ilai ni ada iliyokuwa imezoeleka katika zama za ujahilia. [4] Ilikuwa kwa namna hii, katika zama za ujahilia, ikitokea kwamba, mwanaume amemchukia mkewe, basi alikuwa akiapa kwamba, hatakutana naye kimwili [5] wala kumpa talaka [6] kwa mwaka au miaka kadhaa [7] au mpaka mwisho wa umri wake. [7] Inaelezwa kuwa, lengo la hatua hii [8] katika zama za ujahilia lilikuwa ni kumtesa na kumuudhi mke, kumuacha anatangatanga na kumzuia asiolewe tena. [9]
لِلَّذِينَ يُؤْلُونَ مِنْ نِسَائِهِمْ تَرَبُّصُ أَرْبَعَةِ أَشْهُرٍ فَإِنْ فَاءُوا فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ
Kwa wanao apa kuwa watajitenga na wake zao, wangojee miezi mine. Wakirejea basi Mwenyezi Mungu hakika ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.
(Qur'an: 2: 226)
Matumizi ya Kifikihi
- Makala Asili: Ilai
- Kuharamishwa Ilai: Ilai kwa mtazamo wa kifikihi ni haramu na sababu ya hilo ni kuharamishwa katika Uislamu kuacha kukutana kimwili na mke kwa zaidi ya miezi mine. [10] Baadhi wamechukua kuharamishwa Ilai kutoka katika Aya ya 226 ya Surat al-Baqara. [11] Hata hivyo kwa mujibu wa Ayatullah Makarim Shirazi ni kuwa, Qur'an haijabatilisha kabisa hukumu ya Ilai, lakini imeondoa athari zake mbaya; kwani hairuhusu mwanamke kuteswa na kuudhiwa na mumewe na kufanywa mtu wa kutangatanga. [12]
- Kwa mujibu wa Aya ya Ilai mafakihi wanaamini kwamba, Mafakihi wanaamini kuwa, kama mwanaume atakula kiapo cha Ilai, mke anaweza kwenda kushtaki kwa Mtawala wa Sheria. Mtawala wa sheria atampa mume muda wa miezi minne kumrejea mke wake na baada ya kukutana naye kimwili atoe kafara ya kuvunja kiapo. [13] Kama mwanaume katika kipindi na muda huu aliopatiwa na mtawala wa Sheria hatafanya hivyo, mtawala wa sheria atampa hiari baina ya kumrejea mke na kutoa talaka na kama atakataa kufanya lolote kati ya mawili hayo atamlazimisha kuchagua baina ya hukumu ya kufungwa na kubinywa katika kupewa chakula. [14] Baadhi ya mafakihi wanaamini kwamba, katika hali hii mtawala wa sheria anaweza kumpa talaka mwanamke huyo. [15]
- Masharti ya Ilai: Ili Iilai itimie kuna masharti ambayo yametajwa na kubainishhwa; [16] miongoni mwayo ni kuwa: Kuapa kunapaswa kuwa kwa kutumia moja ya majina ya Mwenyezi Mungu, [17] kabla ya kula kiapo cha Ilai mke na mume wanapaswa kuwa hapo kabla waliwahi kukutana kimwili [18], msukumo na sababu ya mfanya Ilai (yaani mume) inapaswa kuwa ni kwa ajili ya kumuudhi mkewe. [19]
- Mafakihi wanaamini kwamba, makusudii ya فىء yaani kurejea katika Aya hiii ni kukutana kimwili au kuonyesha kutaka hilo wakati kunapokuwa na vizuizi vya kisheria au maradhi. [20]