Nenda kwa yaliyomo

Aya ya Harithu

Kutoka wikishia

Maelezo ya Aya Kigezo Maelezo Jina la Aya Aya ya Harith Mahala ilipo Suratu Al-Baqara Nambari ya Aya 223 Juzuu 2 Taarifa za Kimaudhui Sababu ya Uteremsho Kukataa imani ya Kiyahudi kuhusu vizuizi vya mahusiano ya ndoa. Mahali ilipoteremshwa Madina Mada Fiqhi , Kimaadili Ujumbe wake Hakuna vizuizi katika mahusiano ya ndoa. Aya ya Harithi Aya ya Harithu: ni sehemu ya Aya ya 223 ilioko katika Suratu Al-Baqara. Kiuhalisia Aya ni Aya yenye kuzungumzia mahusiano ya kindoa kati washirka wawili pamoja na masuala ya uzazi. Katika Aya hii, Mwenye Ezi Mungu anawalinganisha wanawake na mashamba ambayo wanaume hupanda mbegu zao ndani yake. Wanazuoni wa fiqhi wametumia Aya hii katika kuzungumizia masuala ya ndoa, hivyo basi katika vitabu vya fiqhi huzungumzia Aya kwenye mlango maalumu unaozungumzia masuala ya ndoa. Wengi wa wanazuoni wa fiqhi, wakitegemea kipengele kisemacho "An'naa shi'tum" (namna mpendavyo), kilichoko kwenye Aya hii, wametoa fatwa isemayo kwamba; ni halili kwa mume kumuingilia mkewe kwa njia ya nyuma katika mahusiano yao ya kindoa. Pia ili kuthibitisha mtazamo wao, wnazuoni hawa wamejaribu kutumia baadhi Hadithi zinazounga mkono mtazamo huo. Hata hivyo, baadhi ya wanafiqhi wengine wamelifsiri neno "An'naa" kwa maana ya “wakati”, yaani fanyeni tendo la ndoa "wakati wowote" mpendapo. Kutokana na Hadithi zinazokataza kitendo hicho, wanazuoni hawa wameamua kutoa fatwa ya kukataza tendo hilo, na kusema kwamba; tendo hili ni tendo la makruhu (halipendezi). Mwenye Ezi Mungu, katika sehemu ya mwisho ya Aya hiyo, anakumbusha umuhimu unaowataka wanadamu kutanguliza matendo mema huko waendako (Akhera), na kuwataka kumcha Mungu, na kutambua kwamba hatimae watakutana na Mola wao Siku ya Kiyama, ambapo matendo yao yote yatawekwa mezani yatahesabiwa. Sababu ya Kuitwa Hivyo Aya ya 223 ya Suratu Al-Baqara imepewa jina la "Aya ya Harithi" kwa sababu ya kule Aya hii kuzungumzia mahusiano ya ndoa pamoja na masuala ya uzazi. [1] Katika aya hii, Mwenye Ezi Mungu anawalinganisha wanawake na "harithi"—yaani, shamba au eneo la kilimo—ili kuonesha umuhimu wao katika uzalishaji na uendelezaji wa kizazi. [2] Matumizi ya lugha ya kimafumbo na sitiari katika Kurani, hasa katika masuala ya ndoa kama ilivyo katika aya hii, yanaonyesha mfumo mwema maadili ya Mwenyezi Mungu katika matumizi maneno. [3] Baadhi watafiti wanaona kwamba; matumizi ya sitiara ya neno “shamba” katika kumzungumzia mwanamke, ni mojawapo ya mifano bora zaidi ya ufasaha katika kuelezea na kutoa ufafanuzi wa kilugha katika kufikisha ujumbe kusudiwa. [4] Baadhi ya watafiti wamesema kwamba; ile lugha ya kumfananisha wanawake na shamba, inatokana na ukweli kwamba, mbegu ya mwanamume inayopandwa katika tumbo la mwanamke inafanana na mbegu (zipandwazo mashambani). [5] Aidha, kuna baadhi wanaona kwamba; matumizi ya lugha ya "shamba" katika Aya hii ni lugha ya mifano, huku wengine wakiona kuwa ni ligha ya sitiari, na wengine wakiona kuwa ni lugha ya ishara au mafumbo. [6]



Asili ya Kuteremshwa Kwake (Sababu Al-Nuzul) Kulingana na Riwaya iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Ridha (A.S.) kuhusiana na asili ya kuteremshwa wa Aya ya 223 ya Suratu al-Baqara, ni kwamba; Aya hii iliteremshwa ili kupinga baadhi ya itikadi za Kiyahudi juu ya masuala ya kujamiiana na wanawake. Kwa mujibu wa imani ya Kiyahudi, ni kwamba inaruhusiwa tu kujamiiana na wanawake kupitia upande wa mbele (uso kwa uso), na kwamba kujamiiana katika uke wa mwanamke kupitia nyuma kunaweza kusababisha mtoto kuzaliwa akiwa na makengeza. Kwa hiyo, Aya hii ilishuka kwa ajili kuruhusu kitendo hicho. [7] Hata hivyo, kuna asili nyingine za kuteremshwa kwa Aya hii zilizotajwa na wafasiri mbali mbali. [8] Utegemezi wa Aya ya Harithu Katika Mtindo wa Kujamiiana na Mwanamke Mafaqihi, ambao ni wanazuoni wa sheria za Kiislamu, wameitumia Aya hii katika masuala ya Watyi al-Mar'a Duburan (kwa Kiswahili: kujamiiana na mke kupitia tupu ya nyuma), huku wataalamu wa fani ya usuli fiqhi (wanazuoni wa fani ya misingi ya uzalishaji wa kanuni za kifiqh) wakiitumia katika suala la Al-Amru Aqiba al-Hadhar (kwa Kiswahili: amri baada ya katazo). [9] Mafaqihi wa upande wa madhebu ya Kishia wakiitumia Aya ya Harithu, wameonekana kutoa mitazamo tofauti juu ya hukumu za kifiqhi, kuhusiana na suala la kujamiiana na mwanamke kulingana na misingi ya kisheria. Wengi wao wamelifasiri neno "Anna" lililoko katika Aya husika, kwa maana ya "mahala popote", "kutoka upande wowote," "kwa namna yoyote", au "kwa mtindo wowote". Wanazuoni hawa wameiweka Aya ya Harithu sambamba na orodha ya ushahidi wa kisheria juu hukumu za kujamiiana na mwanamke kupitia dubur (tupu ya nyuma). [10] Kwa kuthibitisha maana hizo kupitia baadhi ya Riwaya, wamekihisabu kitendo hicho kuwa ni kitendo halali. [11] Kinyume na hao, baadhi ya wanazuoni wa Sheria za Kiislamu wamelifasiri neno "'Annaa" kwa maana ya "wakati wowote" na wakasema kwamba; Aya ya Harthu haikuwa na malengo ya kutoa ruhusa ya kufanya tendo la ndoa kwa kupitia njia ya makalio (sehemu ya nyuma). [12] Kutokana na utofauti wa masimulizi (Riwaya) kuhusiana na mada hii, [13] pamoja na wingi wa masimulizi yanayokataza kitendo hicho, pia uvumi mkumbwa wa fatwa zinazokabiliana na suala hili, hii imepelekea kutolewa fatwa za umakruhu wa hali ya juu katika kukabiliana kitendo hicho. Zaidi ya hayo, kuna wengine wanaohalalisha tendo hilo kwa masharti kuwepo kwa ridhaa kamili ya mwanamke katika kutenda tendo hilo. [14] Aidha, baadhi ya watafiti wameitumia ibara ya "Wa qaddimuu li-Anfusikum" (Kiswahili: "Na jitangulizieni mema") ilikoko katika Aya ya Harthu, kama ni ushahidi juu ya uharamu wa tendo hilio la ndoa kupitia njia ya makalioni. [15] Kwa mujibu wa maelezo yao, Aya ya Harthu inaruhusu lile tendo la ndoa lenye uwezekano wa kuzaa, na kwa kuwa tendo la ndoa kupitia makalioni, haliwezi kusababisha uzao, hivyo basi tendo hilo haliwezi kukubalika kisheria. [15] Kwa upande mwingine, kuna watafsiri wengine waliokuja na tafsiri tofauti kuhusiana na ibara isemayo "Wa qaddimuu li-Anfusukum". Kwa mtazamo wao ibara hii ni "sifa ya mtoto mwema", [16] wao wamefafanua kwa kusema kwamba; matendo mema ya mtoto fulani yanaweza kusababisha thawabu kwa wazazi wake. [17] Zaidi ya hayo, Tabatabai, mwandishi wa tafsiri ya Al-Mizan, amesisitiza kuwa agizo la "kumcha Mungu" lilitolewa katika Aya ya Harthu, linalenga kusisitiza haki na wajibu katika masuala yanayohusiana tendo la ndoa. [18]

Je, Aya ya Al-Harith Inamdhilifisha Mwanamke? Kuna baadhi ya watu wanaodhania kwamba; suala la kulinganisha mwanamke na shamba kama ilivyo katika Aya ya Al-Harith, ni moja njia ya kumshusha hadhi mwanamke. Na kwamba muji wa Aya hii, mwanamme ana haki kumuingilia mkewe kwa njia atako bila ya ridhaa ya mwanamke. [19] Ili kuunga mkono hoja hii, watoaji wa maoni haya wamejaribu kutaja baadhi ya Hadithi, kama ushahidi unaounga mkono maoni yao. [20] Ili kujibu hoja hii, watafiti wengine, wametumia Aya mbali mbali ziendazo kinyume na mawazo haya. Miongoni mwa zilizotumika katika kukabiliana na mawazo hayo, ni Aya ya 187 ya Sura Al-Baqarah na aya ya 13 ya Sura Al-Hujurat, ambazo zinasisitiza juu kuwepo kwa usawa kati ya mwanaume na mwanamke. Usawa huu uliozungumzwa na Aya hizi, ni ule usawa uliosimama juu ya misingi ya utu na hadhi ya kibinadamu. Katika kujibu hoja za kumdhalilisha mwanamke, watafiti hawa wanasema kwamba; Aya ya Al-Harithu imekuja kuzungumzia tofauti za kimaumbile na kifiziolojia kati ya mwanaume na mwanamke, zinazopelekea kufanikisha lengo la kudumisha kizazi. Wao wamefafanua wakisema kwamba; tofauti hizi haziwe kuleta uzito wowote ule kwa upande wa hadhi ya mwanamme wala hazisababishi kupunguka kwa hadhi ya mwanamke. [21] Pia, wamesisitiza kwamba; mfano huu haumaanishi kuwa vitu viwili hivi (shamba na mwanmke) ni vitu vyenye usawa wa moja kwa moja, bali unaonesha aina fulani ya mfanano unaoonekana kati yao. [22] Makarim Shirazi na Tabatabai, ambao ni wafasiri wa kutoka madhehebu ya Kishia, wanasema kwamba; Aya ya Harithu inalenga tu kuelezea umuhimu wa mwanamke katika jamii ya binadamu. Wakitoa maoni yao wamesema kwamba; mbegu kama mbegu haiwezi kuwa na thamani bila ya kuwepo shamba. Hivyo basi kama mbegu hizo zitakosa shamba la kuzipanda ndani yake, basi zitaharibika bila ya kupata faida kusudiwa ya uwepo wake. Hivyo basi kama hakuwa na wanawake, uhai na maisha ya binadamu yatakuwa hatarini. [23]

Kukutana na Mungu Katika sehemu ya mwisho ya Aya ya 223 ya Suratu Al-Baqara, Mwenye Ezi Mungu anasema: «وَ اتَّقُواْ اللَّهَ وَ اعْلَمُواْ أَنَّکُم مُّلَاقُوهُ وَ بَشِّرِ الْمُؤْمِنِین» (Na mcheni Mungu, na tambueni kuwa bila shaka mtamkutana Naye. Na wabashirie Waumini [kuhusu hilo]). [24] Kuna kauli mbili zilizotajwa na wanazuoni, kuhusiana na kile kinachorejelewa na kiwakilishi kilichoko katika neno «مُلاقُوه» (Naye) na jinsi au namna ya “kukutana” huko. [25] Kauli mbili hizi ni kama ifuatavyo: 1. Kirejeo cha kiwakilishi hicho ni Mungu Mwenyezi. Hii inamaanisha kuwa kukutana kunakozungumzwa hapo, ni kukutana kwao na Mungu Mwenye Ezi. Hivyo basi, Aya hii inawataka waja wamjali na wamtii Mola wao, na watambue kwamba, hatimae watamkutana Naye. [26] Kukutana huku na Mungu kutatokea Siku ya Kiyama. [27] Maana ya “kukutana” hapa siyo kumuona Mwenye Ezi Mungu kwa macho ya kimwili, bali ni hali maalumu ya kiroho wakati wa kukabiliana na uadilifu Wake. [28] Hapa Mwenye Ezi Mungu anawaonya watu ili wayape kipaumbele matendo mema, waogope dhambi, na wajue kwamba Siku ya Kiyama watakutana na Mola wao, na kila tendo lao litahukumiwa kwa uadilifu bila ya kupunjwa kitu chochote kile ndani yake. [29] 2. Kirejeo cha kiwakilishi hicho ni thawabu na adhabu ya matendo. Baadhi ya wafasiri wameeleza kwamba; neno “kukutana” lililotajwa ndani ya Aya hiyo, lina maana ya kuona matokeo ya matendo yao, thawabu kwa matendo mema na adhabu kwa matendo maovu. [30]