Nenda kwa yaliyomo

Asma bin Khaarjah al-Fazari

Kutoka wikishia

Asma bin Khaarjah al-Fazari (aliyefariki mwaka wa 82 Hijria) alikuwa kiongozi mashuhuri na aliyekuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa katika mji wa Kufa, hasa katika kipindi cha matukio yaliyopelekea maafa ya tukio la Karbala. Asma alishiriki katika vita vya Siffin akiwa katika jeshi la Imam Ali (a.s). Hata hivyo, baada ya vita hivyo, alihamia Kufa na kuwa karibu na watawala wa Bani Umayya, akihudumu mara kwa mara katika mji mkuu wa utawala wao. Asma pia alikuwa ni mshauri muhimu wa kisiasa wa wakati huo, na ushawishi wake uliongezeka zaidi kupitia binti yake, ambaye alikuwa ni mke wa watawala watatu wa Kufa: Ubaidullah bin Ziyad, Bushar bin Marwan, na Hajjaj bin Yusuf al-Thaqafi.

Asma bin Khaarjah al-Fazari alishirikiana na Ibn Ziyad katika kumkamata Hani bin Urwah na kumhudhurisha kwenye kasri ya utawala, naye pia alihusika tena katika mauaji ya Muslim bin Aqil. Hata hivyo, katika tukio la Karbala, Asma alimwokoa Hassan al-Muthanna kutokana na uhusiano wa kifamilia waliokuwa nayo.

Pia, Asma bin Khaarjah al-Fazari ndiye aliye watambulisha baadhi ya waasi dhidi ya Othman bin Affan, pia akawatambilisha wafuasi mashuhuri wenye mrengo wa Kishia kama vile Kumayl bin Ziyad kwa Hajjaj bin Yusuf al-Thaqafi.


Nafasi ya Asma bin Khaarjah katika Matukio ya Mwanzoni mwa Uislamu

Asma bin Kharjeh al-Fazari alikuwa ni miongoni mwa viongozi maarufu wa Kufa na mmoja wa wafuasi (miongoni mwa matabi’ina) wa Masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w). [1] Asilia yake inatokana na kabila la Banu Fazara, [2] naye alikuwa na nafasi muhimu katika matukio ya mwanzoni mwa Uislamu, hususan katika siasa na vita vya zama hizo.

Hind, binti wa Asma, aliolewa na viongozi watatu maarufu wa mji mkuu wa Kufa, ambao ni; Ubaidullah bin Ziyad, [3] Bushar bin Marwan bin Hakam, na Hajjaj bin Yusuf al-Thaqafi. [4] Hata hivyo, ndoa yake na Hajjaj ilivunjika baada ya kugundulika kwamba Hind alionyesha hisia kwa mume wake wa zamani, Ubaidullah bin Ziyad. [5] Asma bin Kharjah, pia alikuwa akijulikana kwa majina ya; Abu Hassaan, [6] Abu Muhammad [7] na Abu Hind, [8] majina alipewa kwa kulingana na majina ya watoto wake.

Asma pia alikuwa ni miongoni mwa wanazuoni maarufu wa Hadithi (muhaddithun). [9] Miongoni watu walionukuu Hadithi kutoka kwa Asma ni pamoja na; mwanawe (Malik) na Ali bin Rabiah [10] ambao ni miongoni wa wapokezi wa Hadithi wa wakati huo. Kuna khitilafu za kimitazamo kusiana na tarehe halisi ya kifo cha Asma. Orodha ya mitazomo tofauti kuhusiana na kifo chake ni; mwaka 60, [11] 65, [12] 66, [13] na mwaka 82 Hijiria. [14] Ibn Hajar al-Asqalani, mtaalamu maarufu wa rikodi za wapokezi wa Hadithi, anasema kwamba; Asma alikufa akiwa na umri wa miaka 80, na kwa msingi huo yeye anasema kwamba; alizaliwa mnamo mwaka wa 60 Hijiria, kabla ya Tukio la Mab’ath (kuanza kupokea wahyi kwa bwana Mtume). [15]


Ushuhuda Dhidi ya Hujr bin Adiy

Asma bin Khaarjah, aliyewahi kushiriki katika jeshi la Imam Ali (a.s.) wakati wa Vita vya Siffin,  [16] baadae alikuja husika katika kutoa ushahidi dhidi ya Hujr bin Adiy, mmoja wa masahaba waaminifu wa Imam Ali (a.s). [17] Ushahidi huu ulitolewa kwa kupitia matakwa ya Ziyad bin Abihi yaliyokumtaka yeye kusimamisha ushahidi huo. Kutokana na ushahidi huo, Hujr alikamatwa na hatimae kuuawa shahidi mwaka wa 51 Hijria. [18] Baadhi ya vyanzo vinasema kuwa Asma baadaye alijutia matendo yake ya kushiriki katika suala hilo. [19]


Nafasi ya Asma bin Khaarjah Katika Tukio la Karbala

Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, Asma bin Khaarjah alikuwa na nafasi ya kipekee katika matukio yanayohusiana na Tukio la Karbala. Miongoni mwa matendo yake kuhusiana na tukio hilo ni:

1. Kusambaratisha Wafuasi wa Muslim bin Aqil

Wakati Ubaidullah bin Ziyad alipochukua nafasi ya uongozi wa mji Kufa mwaka 60 Hijiria, Asma alichukuwa uamuzi wa kumwozesha binti yake Ibn Ziyad. [20] Na Baadae ya hapo mwenyewe alikuja kuwa ni miongoni wa watumishi wa serikali ya Ibn Ziyad. [20] Asma akiwa katika nafasi hiyo alihusika katika kutekeleza mpango wa kuwatisha wakazi wa Kufa ili waache kumuunga mkono Muslim bin Aqil, balozi wa Imam Hussein (a.s). [22] Ibn Ziyad aliwaagiza Asma na watu wake wengine, kama vile Kathir bin Shihab Harithi, kueneza hofu na kuwashawishi watu kutotii harakati za Muslim bin Aqil, alifanya hivyo ili kuzuia hatari ya kupoteza nafasi ya serikali yao kupiti harakati zilizotarajiwa kutokea baada ya kuwasili Imamu Hussein (a.s) katika mji hou. [23]

2. Ushirikiano Wake Katika Kumnasa Hani bin Urwah

Wakati Ubaidullah bin Ziyad alipokuwa na nia ya kumhudhurisha Hani bin Urwah kwenye kasri la utawala wake (Dar al-Khilafah), ili kumtaka amkabidhi Muslim bin Aqil, au, kama atakataa amuue, alimtuma Asma bin Kharjeh na Muhammad bin Ash’ath kumfuata Hani alia je katika hilo na kupokea amri hizo. [24] Katika baadhi ya vyanzo, kuna majina ya watu wengine waliohusika na tukio hili, miongoni mwao ni; Amr bin Hajjaj al-Zubaidi na Hassan,ambaye ni mwana wa Asma. [25]

Ibn Qutayba na Tabari wakiripoti tukio hili wanasema kwamba; Pale Asma bin Khaarjah alipoamua kutekezela matakwa ya uongozi wa serikali hiyo, yeye hakuwa na habari kuhusu nia ya Ubaidullah bin Ziyad katika suala hilo. [26] Mwanzoni mwa tukio hilo, yeye alijaribu kumtafutia Hani dhamana kutoka kwa Ubaidullah, [27] lakini baada ya kushuhudia Hani akipigwa, kutukanwa na kuwekwa kizuizini, alichukuwa maamuzi ya kumkosoa Ubaidullah, jambo ambalo lilipelekea yeye mwenyewe kutiwa kizuizini. [28] Hata hivyo, baadhi ya wanahistoria kama vile Namazi Shahrudi wanaamini kuwa; mtu ambaye hakuwa na habari na aliyempinga Ubaidullah katika tukio hilo hakuwa Asma, bali alikuwa ni Hassan, ambaye ni mwana wa Asma. [29]


3. Kumuokoa Hasan al-Muthanna Katika Karbala

Kwa mujibu wa mtazamo wa Sheikh Mufid na Muhammad Taqi Shoshtari; Asma hakuwa miongoni mwa waliojiunga na jeshi la Umar bin Sa’ad katika vita dhidi ya Imamu Hussein (a.s). Ila baada ya kumalizika kwa vita, Asma alikuja kumwokoa Hassan al-Muthanna, ambaye alikuwa amejeruhiwa vibaya vitaniu humo, uokozi wake huo unatokana na uhusiano wa kikabila uliopo baina ya Hassan al-Muthanna na mama wa Asma. [30]

4. Kuorodheshwa Katika Malengo ya Kisasi ya Mukhtar

Wakati Ubaidullah bin Ziyad alipomweka gerezani Mukhtar bin Abi Ubaid al-Thaqafi na kuapa kwamba atamuua, Asma bin Khaarjah akiwa pamoja na Urwa bin Mughira walimtembelea Mukhtar akiwa gerezani. Katika ziara yao hiyo walimtaka aachane  na vitendo vyovyote vile vya uchochezi dhidi ya Ubaidullah. [31] Hata hivyo, baada ya Mukhtar kushika funguo za mamlaka ya mji wa Kufa, na kuwadia zama za kulipiza kisasi dhidi ya wahusika wa tukio la Karbala, alimtaja Asma kwa lugha ya hasira hukuaakittoa lugha za vitisho dhidi yake. Kwa kuhofia usalama wake, Asma alilazimika kuukimbia mji wa Kufa [32] na hakuweza kurejea hadi Mukhtar alipopinduliwa. [33] Katika harakati zake, Mukhtar aliamuru nyumba ya Asma na zile za binamu zake zivunjwe, ishara ya kulipiza kisasi kwa wale waliodhaniwa kuwa ni wapinzani wa malengo yake. [34]

Ushirikiano na Watawala wa Kufa na Kufichua Wafuasi wa Kishia

Baada ya kuanza kwa utawala wa Hajjaj bin Yusuf al-Thaqafi katika mji wa Kufa mwaka wa 75 Hijria, Asma bin Kharjeh alijikuta na nafasi ya kipekee kwenye kasri la kiongozi huyu, akiwa ni baba mkwe wa mtawala mpya. [35] Hii ilimpa fursa ya kupita na kupituka mara kwa mara katika jengo la Dar al-Khilafa (ikulu ya utawala), nafasi hii hii ilimfanya yeye kuwa ni mshirika muhimu wa kisiasa. [36]

Wakati wa utawala wa Abdullah bin Mutii, ambaye aliteuliwa kuwa ni mtawala wa mji wa Kufa kupitia Abdullah bin Zubair (aliyefariki mwaka wa 73 Hijria), Asma aliendelea kushirikiana na watawala wa zama hizo. Mara nyingi alikuwa akihudhuria mikutano ya Dar al-Khilafa na kutumiwa kama ni mshauri wa kisiasa na mtawala wa wakati huo. [37]

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Tabari, ni kwamba; Wakati Hajjaj bin Yusuf alipoendesha msako dhidi ya waasi waliompinga Othman bin Affan na wafuasi wa Kishia wa Imam Ali (a.s), Asma bin Kharjeh alikuwa ni miongoni mwa waliohusika kwa karibu zaidi katika operesheni hizo. Asma ndiye anayesemekana kuwafichua baadhi ya waasi na wafuasi mashuhuri wa Kishia mbele ya Hajjaj, akiwemo Kamil bin Ziyad aliyefichuliwa kupitia operesheni hiyo. [38]

Aidha, katika kipindi cha ukhalifa wa Abdul Malik bin Marwan (66-86 Hijria), na wakati ambapo ndugu yake Abdul Malik, yaani Bushar bin Marwan, alipokuwa mtawala wa Kufa, Asma alichukua maamuzi ya kumwoza binti yake kwa Bushar. [39] Naye pia alihusika katika uteuzi wa Muhalab bin Abi Safra akiwa kama ni mshauri katika kumteua Muhalab kwa ajili ya kuongoza vita dhidi ya Makhawarij wa Azraqiyya. [40]


Ukoo wa Asma bin Khaarjah

Baadhi ya wajukuu wa Asma bin Khaarjah ni miongoni mwa wanazuoni waliohusika katika kazi ya kunukuu Hadithi. Miongoni mwao ni Muhammad, mwana wa Ummu Habib binti Asma bin Kharjah, [41] Ibrahim bin Muhammad bin Harith bin Asma bin Khaarjah, anayejulikana kwa jina la Abu Ishaq al-Fazari, [42] na Abu Abdullah Marwan bin Muawiyah bin Harith bin Asma, [43]  ambaye ni binamu wa Ibrahim, ambao wote walikuwa ni miongoni mwa wanazuoni wa Hadithi wa upande wa Kisunni.

Aidha, mama wa Muhammad Dhul-Shamah, ambaye aliwahi kuteuliwa kuwa ni mtawala wa Kufa kupitia Maslama bin Abdul Malik mwaka wa 102 Hijria, naye pia alikuwa mmoja wa mabinti wa Asma bin Khaarjah. [44]