Amakinu Takhyir
Msemo wa “Amakinu Takhyir /اماکن تخییر” au “Amakinu Arba’a / اماکن اربعه” unarejelea maeneo ambayo msafiri ana haki ya kuchagua kati ya kusali sala zake kwa ukamilifu au kwa kupuza rakaa za sala za kwa mujibu wa shria za fiq-hi. Kulingana na mtazamo maarufu miongoni mwa mafaqihi wa Kishia, maeneo haya ni: Makka, Madina, Msikiti wa Kufa, na Harem la Imam Hussein (a.s). Hata hivyo, baadhi ya mafaqihi wanasema kwamba hukumu ya takhyir haihusiani wala haifanyi kazi kwenye msikiti yote ya Makka wala msikiti yote ya Madina, bali inahusiana na Msikiti wa Mtume (s.a.w.w) na Msikiti mkuu wa Haram peke yake. Aidha, baadhi ya mafaqihi wanaeleza kwamba hukumu ya takhyir inafanya kazi ndani ya mipaka ya zamani ya misikiti hiyo, yaani haiingizo maeneo yaliyo jumuishwa baada ya upanuzi wa misiki hiyo.
Sababu ya Jina Amakinu Takhyir: ni maeneo maalumu ambayo msafiri aliyemo nandi yake, huwa ana haki ya kuchagua jinsi ya kusali sala zake, ima asali kamili au asali sala ya safari. Hii ni kwa kuwa msafiri ana uhuru wa kuchagua kati ya kusali sala zake kiukamilifu au kupunguza rakaa za sala hizo kulingana na ufafanuzi wa sheria za fiq-h. Aidha, maeneo huitwa “Amakinu Al-Arba’a”, jina ambalo kutokana na idadi ya maeneo hayo. [1] Maeneo-Lengwa Kwa mujibu wa maoni maarufu ya mafaqihi wa madhehebu ya Shia, miji ya Makka na Madina, [2] pamoja na Msikiti wa Kufa na Haram ya Imamu Hussein (a.s), ndiyo maeneo-lengwa ya Amakinu Takhyir. [3] Sheikh Tusi ameeleza kwamba; kulingana na baadhi ya Hadithi, hukumu ya Amakinu Takhyir pia inajumuisha mji wa Kufa [4] na Najaf. [5] Pia kuna baadhi ya mafaqihi wanaomini kwamba; mji wa Kufa ni moja sehemu ya maeneo ya Amakinu Takhyir. [6] Kuhusiana na Makka na Madina, kuna mafaqihi wasemao kwamba; makusudio yake ni msikiti mkuu wa Makka na msikiti wa Madina wa bwana Mtume (s.a.w.w) ndiyo iliyomo katika hukumu hiyo. [7] Kuna kauli inayodaiwa kuwa ni ya Sayyid Murtadha na Ibn Junayd [8] ya kwamba; wanaamini kwamba ni sunna kufuata hukumu ya Amakinu Takhyir, ila pia wanaamini kuwa ni mustahabbu kusali sala kamili katika maeneo ya Haramu za Maimamu (a.s). [9] Hata hivyo, mwandishi wa Jawahir anaamini kwamba maoni haya hayana msingi thabiti. [10]
Hukumu za Kifiq-hi Mafaqihi wa madhehebu ya Shia Ithnaashariyya wamejadili kwa kina hukumu zinazohusiana na sala [11] pamoja na ibada za niaba (istiijari), katika maeneo ya Takhyir. Kulingana na maoni maarufu kati yao, msafiri katika maeneo haya ana haki ya kusali sala safari au kusali sala kamili, ingawa inashauriwa zaidi kusali kwa kamili. [13] Hukumu za ziada kuhusiana na maeneo ya Takhyir ni: • Hukumu za maeneo ya Takhyir inahusiana na sala peke yake na haiwezi kutumiki wala kufanya kazi katika mambo ya saumu. [14] • Wengi wa mafaqihi wanasema kuwa; iwapo msafiri aliyekwenda maeneo hayo atapitwa na baadhi ya sala zake akiwa kstika maeneo hayo, basi ni bora kuzilipa sala hizo kwa mtindo wa sala ya safari. [15] • Kulingana na fatwa za baadhi ya mafaqihi, mtu aliyeko katika maeneo ya Takhyir anaweza kubadilisha nia yake kutoka sala fupi ya safari hadi sala kamili au kinyume chake hali akiwa ndani ya sala hizo. Yaani mtu anaweza kutia nia ya sala ya safari, kisha katika ya sala yake akabadili nia yake na kuamua kusali kamili, au anaweza kutia nia ya kusali kamili kisa akabadili nia yake huku akiwa salani mwake na kuamua kusali safari. [16] • Baadhi ya mafaqihi wanaamini kuwa hukumu ya Takhyir inatumika tu katika mipaka ya zamani ya maeneo haya. Hii inamaanisha mwamba maeneo yote yalioingizwa kama ni sehemu ya maeneo hayo baada ya utanuzi wa maeneo hayo, hayatakuwa na nafasi ya kuingia katika hukumu za maeneo ya Takhyir. [17] Mada zinazohusiana: Sala ya safari