Al-Wilayatu al-Takwiiniyyah

Kutoka wikishia

Al-Wilayatu al-Takwiiniyyah (Kiarabu: الولاية التكوينية) au Mamlaka juu ya ulimwengu wa kimaada: Ni uwezo ulio furutu ada ulioko nje ya ulimwengu wa hisia (ulimwengu wa kimaada), nao ni uwezo wenye mamlaka ya kuusarifu ulimwengu hisia (ulimwengu wa kimaada) na vilivyomo ndani yake. Mamlaka ya Mungu juu ya ulimwengu wa kimaada humaanisha uwezo wake, uwendeshaji wake pamoja na utawala wake juu ya viumbe wote (kila kilichomo) ulimwenguni. Suala la mamlaka juu ya ulimwengu wa kimaada ndani ya madhehebu ya Shia, pia limehusishwa kwa Mtume (s.a.w.w) na Maimamu wa Kishia (a.s) na ni miongoni mwa mada ya maudhui zinazojadiliwa katika fani ya Irfani ya Kiislamu (tasawwuf). Katika tamaduni za lugha ya kiuandishi, suala la mamlaka ya Mtume na Maimamu (a.s) juu ya ulimwengu wa kimaada, ni suala lililozoeleka na wala sio suala la kutia kimeme wala wahaka mbele ya mila za waandishi na wanazuoni wa madhehebu ya Shia. Ni wazi kwamba; asili ya uwepo wa mamlaka juu ya ulimwengu wa kimaada kwa Mtume na Maimamu (a.s), ni suala lisilo na mjadala katika jamvi la mila za kielemu za wanazuoni wa Kishia. Ila kinachoingia katika mjadala ni upeo na mipaka ya mamlaka hayo. Kuna nadharia mbili tofauti juu ya upeo na mipaka yake, nazo kama ifuatavyo:

 • Kulingana na nadharia ya mwanzo ni kwamba; Mamlaka ya Mtume na Maimamu (a.s) juu ya ulimwengu wa kimaada sio mamlaka huria, bali mamlaka yenye mikapa maalumu. Nadhiria inafinya na kunahusisha mamlaka hayo katika sekta maalumu kama vile; kuwa na nguvu na uwezo wa kujua yaliyomo ndani ya nafsi na nyoyo za wanadamu, na uwezo kuingilia kati mambo ya kimaumbile na wakipenda kubadili nyenendo za mambo hayo kwa uwezo wa Mungu Subhanahu Wataala.
 • Nadharia ya pili inaamini kwamba; Mtume na Maimamu (a.s) wana mamalaka makubwa zaidi katika kuingilia kati au kuendesha mambo mbali mbali ya kiulimwengu. Kwa lugha nyingine ni kwamba; wao wana mamalaka ya kila kitu kilichomo katika ulimwengu wa kimaada, na hata suala la kufa na kukufuka kwa viumbe hai limo mikononi mwao, na Mwenye Ezi Mungu anafadhili na kutunukia viumbe wake kupitia mikononi mwao.

Ufafanuzi na maana ya al-Wilayatu al-Takwiiniyyah

al-Wilayatu al-Takwiiniyyah (Mamlaka juu ya ulimwengu wa kimaada); ni uwezo ulio furutu ada katika utawala juu ulimwengu wa kimaada pamoja na vilivyomo ndani yake. Hii ina maana ya kwamba; Mwenyezi Mungu ni mwenye uwezo wa kutawala kila kitu na kusimamia mambo ya viumbe vyote vya ulimwenguni.[1] Au pia mwanadamu ambaye amepata ukamilifu wa kiroho, kwa idhini ya Mola wake, anaweza kufanya mabadiliko ya ajabu ulimwenguni humu.[2]

Baadhi ya mifano ya mamlaka ya utawala wa kiumbe juu ya ulimwengu huu wa kimaada ni pamoja na: Miujiza na karama za Manabii na Maimamu, kazi za ajabu kama vile kusafiri ardhini kwa kufumba na kufumbua bila ya kipando,[3] kutembea juu ya maji,[4] kujua siri za wengine, [5] kuzungumza na wanyama,[6] kuivua roho yake kutoka katika mwili wake (kujifisha na kujifufua kwa hiari),[7] na kuleta mabadilko ya kimaumbile ulimwenguni kupitia nguvu za kiroho walizo nazo.[8]

Nini hasa maana halisi ya al-Wilayatu al-Takwiiniyyah

Mara nyingi ndani ya vyanzo vya Kiislamu, linapozungumzwa suala la al-Wilayatu al-Takwiiniyyah (mamlaka juu ya ulimwengu wa kimaada) linapo jadiliwa, huwa linalenga zaidi juu ya mamlaka waliyo nayo baadhi ya wanadamu na sio viumbe wengine (kama vile malaika). Swali halisi hapa ni kwamba; je, mwanadamu anaweza kuwa na mamlaka juu ya ulimwengu wa kimaada au la, na ikiwa ndio, basi upeo wake utakuwa ni wa kiasi gani?.[9]

Hapa hapakusudiwi ule ukaribu wa mja mbele ya Mola wake, ambapo dua zake hutakabali papo hapo na Mwenye Ezi Mugu huleta miujiza kupitia maombi yake au humtimizia matilaba yake bila ya pingamizi,[10] bali ni kwamba mwanadamu, kutokana utiifu wake mbele ya Mungu wake, hupata nguvu ya kiroho ambayo kwayo anaweza kuleta baadhi ya mabadiliko kwenye ulimwengu wa kimaumbile. Bila shaka, mabadiliko hufanyika kwa idhini ya Mwenye Ezi Mungu mwenyewe.[11]

Asili na chimbuko la suala la al-Wilayatu al-Takwiiniyyah

Kulingana na mwongozo wa Sayyid Murteza Motahari (aliye zaliwa mwaka 1298 na kufariki 1358 Shamsia), ni kwamba; suala la al-Wilayatu al-Takwiiniyyah ni suala la kiirfani (Kisufi na kiuchamungu) na la kiroho, na pia kwa mtazamo wa madhehebu ya Shia, ni suala la kidini. Lakini ushahidi wa kihistoria unaonesha kwamba; Irfani ya Kiislamu (Usufi) imelichukua kutoka kwenye vyanzo vya sheria za Uislamu.[12]

Kuna Hadithi zilizo pokewa kutoka kwa Maimamu wa Shia, ambazo zinazungumza juu ya "Tafwidhu" (uwakili huria) wa Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.s) waliopewa na Mungu katika uendeshaji na uhimili wa ulimwengu wa kimaada. Katika baadhi ya hadithi hizi, suala Tafwidhu “uwakili huo huria” linalowapa wao mamalaka juu ya ulimwengu wa kimaada limesisisitizwa ndani yake,[13] ila katika baadhi ya Hadithi limekanushwa.[14]

Kwa mujibu wa moja ya tafiti ni kwamba; suala la mamlaka juu ya ulimwengu wa kimaada (Wilayatu Takwiniyyah) liliibuliwa kwa mara ya kwanza kabisa mnamo karne ya tatu Hijiria kwenye elimu ya irfani ya kiislamu (tasawwuf au usufi) chini ya jina la "Wilayah". Baada ya hapo, neno hilo likaendelea kutumika katika elimu irfani ya Kiislamu, hadi kufikia zama za Ibn Arabi (aliye zaliwa mwaka 560 na kufariki 638 Hijiria) ambaye alikuja kuielezea kwa kina kabisa na kuifafanua.[15] Uchunguzi huo huo unasema kwamba mchanganyo wa maneno mawili "al-Wilayatu + al-Takwiiniyyha" uliibuka kwa mara ya kwanza kabisa katika karne za hivi karibuni na katika fasihi ya wanazuoni wa Shia.[16]

Al-Wilayatu al-Takwiiniyyah kwa bwana Mtume na Maimamu (a.s)

Wanazuoni wa Kishia wanaamini ya kwamba; Mtume Muhammad na Maimamu (a.s) wanamiliki al-Wilayatu al-Takwiiniyyah, yaaani wana mamlaka juu ya uendeshaji na uhimili wa ulimwengu na vilivyomo ndani yake. Ila kuhusiana na mipaka ya mamlaka hayo na upeo wake, kuna khitilafu ndani yake:

Kundi moja la wanazuoni linaamini ya kwamba; Maasumina wana uwezo wa kutia mkono wao kwenye ulimwengu wa kimaada na kuleta mabadiliko ndani yake. Ila kwa mtazamo wao, mamlaka hayo yana mipaka maalumu ndani yake, kwa maana wao hawana mamlaka huria ya moja kwa moja katika jambo hili. Miongoni mwa wanaounga mkono nadharia hii ni; Murtadha Mutahhari, Safi Gulpegani na Ja’afar Subhani.[17] Kwa mtazamo wao; “al-Wilayatu al-Takwiiniyyah” haimaanishi kwa wao wapewa “uwakili huria” na mamlaka ya kuingilia kila jambo, au kwamba wamepewa mamlaka yote wa uendeshaji wa ulimwengu, kiasi ya kwamba iweze kusemwa kuwa wao wanaumba na kufisha kwa niaba ya Mwenye Ezi Mungu.[18] Kwa mtazamo wa Sheikh Mufidu na Sheikh Saduq ni kwamba; Imani ya “uwakili huria” juu ya mamlaka ya viumbe, ni itikadi ya Maghulati.[19]

Kwa upande mwingine kuna la pili la wanazuoni kama vile; Muhammad Hussein Gharawi Isfahani (maarufu kwa jina la kampani) na Sayyid Muhammad Husseini Tehrani (maarufu kwa jina la Allamah Tehrani), wao wanaamini ya kwamba; Mtume na Maimamu (a.s) wana mamlaka kamili juu ya ulimwengu wa kimaada. Wanaamini pia; Mtume na Maimamu (a.s) ndio ukingo upitao mchirizi wa Mwenye Ezi Mungu katika kuwafadhili na kuwaneemesha waja wake.[20]

Bibliografia (Orodha au seti ya Vyanzo Msingi)

Baadhi ya vitabu kuhusu al-Wilayatu al-Takwiiniyyah ni pamoja na:

 1. Wilayate Takwiiniy, cha Hassan Hassanzadeh Aamuli
 2. Al-Wilayatu al-Takwiiniyyah wa al-Tashrii’iyyah, cha Sayyid Jafar Mortadha al-‘Aamiliy
 3. Al-Wilaayatu wa waliyyu al-Maasum (a.s) cha Muhammad Muumin Qommiy
 4. Ithabatu al-Wilayati al-‘Aammati Lilnabiyyi wa al- Aimmati (a.s), cha Sayyid Ali Husseini Milani
 5. Al-Wilayatu al-Takwiiniyyah Baina al-Kitabi wa a-lSunnati, cha Hisham Sharafiy al- ‘Aamiliy
 6. Al-Wilayatu al-Takwiiniyyah Baina al-Qur'ani wa al-Burhani, cha Dhiyaau al-Sayyid Adnan al-Khabbaaz al-Qatifiy
 7. Al-Wilaayatani al-Takwiiniyyah wa al-Tashrii’iyyah ‘Inda al-Shi’ati wa Ahli al-Sunnati, cha Muhammad Ali Hulwu.

Mada zinazo husiana

Rejea

 1. Allamah Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān, juz. 6, uk. 12.
 2. Subḥānī, Wilāyat-i takwīnī wa tashrīʿī az dīdgāh-i ʿilm wa falsafa, uk. 26.
 3. Raḥīmī, "Barrasī-yi taṭawwur-i tārīkhī-yi wilāyat-i takwīnī az Ḥākim Tirmidhī tā Ibn ʿArabī dar mutūn-i manthūr-i ʿirfānī", uk. 82.
 4. Raḥīmī, "Barrasī-yi taṭawwur-i tārīkhī-yi wilāyat-i takwīnī az Ḥākim Tirmidhī tā Ibn ʿArabī dar mutūn-i manthūr-i ʿirfānī", uk. 82.
 5. Muṭahharī, Majmūʿa-yi āthār, juz. 3, uk. 285-286.
 6. Raḥīmī, "Barrasī-yi taṭawwur-i tārīkhī-yi wilāyat-i takwīnī az Ḥākim Tirmidhī tā Ibn ʿArabī dar mutūn-i manthūr-i ʿirfānī", uk. 82.
 7. Subḥānī, Wilāyat-i takwīnī wa tashrīʿī az dīdgāh-i ʿilm wa falsafa, uk. 49-50.
 8. Subḥānī, Wilāyat-i takwīnī wa tashrīʿī az dīdgāh-i ʿilm wa falsafa, uk. 49-50.
 9. Tazama: Muṭahharī, Majmūʿa-yi āthār, juz. 3, uk. 285-286; Ṣāfī Gulpāyigānī, Wilāyat-i takwīnī wa wilāyat-i tashrīʿī, uk. 82, 99, 100; Subḥānī, Wilāyat-i takwīnī wa tashrīʿī az dīdgāh-i ʿilm wa falsafa, uk. 26.
 10. Ṣāfī Gulpāyigānī, Silsila mabāḥith-i imāmat wa mahdawīyyat, juz. 1, uk. 43.
 11. Tazama: Muṭahharī, Majmūʿa-yi āthār, juz. 3, uk. 285; Subḥānī, Wilāyat-i takwīnī wa tashrīʿī az dīdgāh-i ʿilm wa falsafa, uk. 26.
 12. Muṭahharī, Majmūʿa-yi āthār, juz. 3, uk. 289.
 13. Rabbānī Gulpaygānī, "Naqsh-i fāʿilī-yi Imām dar niẓām-i āfarīnish", uk. 20-25.
 14. Ṣadūq, al-Iʿtiqādāt, juz. 1, uk. 100.
 15. Raḥīmī, "Barrasī-yi taṭawwur-i tārīkhī-yi wilāyat-i takwīnī az Ḥākim Tirmidhī tā Ibn ʿArabī dar mutūn-i manthūr-i ʿirfānī", uk. 75.
 16. Raḥīmī, "Barrasī-yi taṭawwur-i tārīkhī-yi wilāyat-i takwīnī az Ḥākim Tirmidhī tā Ibn ʿArabī dar mutūn-i manthūr-i ʿirfānī", uk. 73.
 17. Muṭahharī, Majmūʿa-yi āthār, juz. 3, uk. 285-286; Ṣāfī Gulpāyigānī, Wilāyat-i takwīnī wa wilāyat-i tashrīʿī, uk. 99-100; Subḥānī, Wilāyat-i takwīnī wa tashrīʿī az dīdgāh-i ʿilm wa falsafa, uk. 51.
 18. Muṭahharī, Majmūʿa-yi āthār, juz. 3, uk. 286; Ṣāfī Gulpāyigānī, Wilāyat-i takwīnī wa wilāyat-i tashrīʿī, uk. 98; Subḥānī, Wilāyat-i takwīnī wa tashrīʿī az dīdgāh-i ʿilm wa falsafa, uk. 51.
 19. Ṣadūq, al-Iʿtiqādāt, juz. 1, uk. 97-100; Mufīd, Silsilat muʾallifāt al-Shaykh al-Mufīd, juz. 5, uk. 134.
 20. Gharawī Iṣfahānī, Ḥāshiyat al-Makāsib, juz. 2, uk. 379; Ḥusaynī Tihrānī, Imām shināsī, juz. 5, uk. 114.

Vyanzo

 • Gharawī Iṣfahānī, Muḥammad Ḥusayn. Ḥāshiyat al-Makāsib. Qom: Nashr-i Dhawi al-Qurbā, 1427 AH.
 • Ḥusaynī Tihrānī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn. Imām shināsī. Mashhad: Allāma Ṭabāṭabāʾī, 1426 AH.
 • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Silsilat muʾallifāt al-Shaykh al-Mufīd. Beirut: Dār al-Mufīd, 1414 AH.
 • Muṭahharī, Murtaḍā. Majmūʿa-yi āthār. Tehran: Intishārāt-i Ṣadrā, 1375 Sh.
 • Rabbānī Gulpaygānī, ʿAlī. "Naqsh-i fāʿilī-yi Imām dar niẓām-i āfarīnish". Intiẓār-i mawʿūd 29". (1388 Sh)
 • Raḥīmī, Ja'far. "Barrasī-yi taṭawwur-i tārīkhī-yi Wilāyat-i takwīnī az Ḥākim Tirmidhī tā Ibn ʿArabī dar mutūn-i manthūr-i ʿirfānī". Muṭāliʿāt-i ʿirfānī 20. (1393 Sh)
 • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Iʿtiqādāt. Second edition. Qom: Kungira-yi Jahānī Hizāra-yi Shaykh Mufīd, 1414 AH.
 • Ṣāfī Gulpāyigānī, Luṭf Allāh. Silsila mabāḥith-i imāmat wa mahdawīyyat. Qom: Daftar-i Nashr-i āthār-i Āyat Allāh Ṣāfī Gulpāyigānī, 1391 Sh.
 • Ṣāfī Gulpāyigānī, Luṭf Allāh. Wilāyat-i takwīnī wa Wilāyat-i tashrīʿī. Qom: Daftar-i Nashr-i āthār-i Āyat Allāh Ṣāfī Gulpāyigānī, 1393 Sh.
 • Subḥānī, Jaʿfar. Wilāyat-i takwīnī wa tashrīʿī az dīdgāh-i ʿilm wa falsafa. Qom: Muʾassisat al-Imām al-Ṣādiq, 1385 Sh.
 • Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1417 AH.