Al-Wilayatu al-Tashrii’iyyah

Kutoka wikishia

Al-Wilayatu al-Tashrii’iyyah (Kiarabu: الولاية التشريعية) au Mamlaka ya utungaji wa sheria: Ni haki ya kutunga sheria au kutunga kanuni maalumu katika nyanja za kidini. Mamlaka ya utungaji sheria humaanisha kwamba; Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.s) wamepewa mamlaka ya kutunga sheria za kidini na Mungu wao na kwa niaba yake yeye mwenyewe.

Suala la “Al-Wilayatu al-Tashrii’iyyah / mamlaka ya utungaji wa sheria” ni suala lenye khitilafu miongoni mwa wanazuoni wa Shia: Wapo wanaamini juu ya suala hilo, na pia kuna wengine wanao amini kwamba; haki ya kutunga sheria ni haki pekee ya Mungu. Pia kuna tafsiri nyingine ya Al-Wilayatu al-Tashrii’iyyah, ambayo ni yenye kukubaliwa na wanazuoni na wanaamini wote wa madhehebu ya Shia. Kulingana na tafsiri hii ni kwamba; Mwenye Ezi Mungu amempa Bwana Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Imamu (a.s) mamlaka kamili juu ya roho na mali za watu, na chochote wakisemacho ni lazima kifuatwe.

Al-Wilayatu al-Tashrii’iyyah yenye maana ya tafsiri ya kwanza, inaonekana kuwepo katika vyanzo vya Hadithi, ambapo ndani yake mmeelezewa suala la mamalaka ya Kitheokrasia (kiungu) aliyo nayo bwana Mtume na Maimamu (a.s), na kwamba wao wamepewa (tafwidhu kamili) “uwakili huria” juu ya mambo.

Maana mbili tofauti za Al-Wilayatu al-Tashrii’yyah

Katika fasihi ya wanachuoni wa Kishia, mamlaka ya kisheria ina maana mbili:

  • Maana ya kwanza ni mamlaka na haki ya kisheria juu ya roho na mali za watu. “Al-Wilayatu al-Tashrii’iyyah / mamlaka huria ya kisheria”, kwa maana hii, yanapo nasibishwa kwa bwana Mtume(s.a.w.w) na Maimamu (a.s), huwa na maana ya kwamba; Wao wana mamlaka kamili na huria ya kisheria juu ya roho na mali za watu, na wana haki ya kuviamili viwili hivyo kwa njia waitakayo. Kwa mfano; Wao wanaweza kuuza mali za watu hao, na katika hali hiyo watu hao wanapaswa kuwatii.[1] Wanachuoni wa Shia wanakubali maana ya kwanza ya Al-Wilayatu al-Tashrii’iyyah kuhusu Mtume na maimamu; Yaani kila wanaamini kuwa Mtume na maimamu wana mamlaka juu ya maisha na mali za watu na mambo yote ya dini na ulimwengu wa watu yako chini ya uongozi wao na lazima watiiwe juu ya hayo.[2]
  • Maana ya pili ya Al-Wilayatu al-Tashrii’iyyah “mamlaka ya kitheokrasia na kisheria”; Ni haki ya kutunga sheria katika uwanja wa dini; yaani, kutunga sheria za ibada, kiuchumi, kisiasa, mahakama na kadhalika.[3] Kwa maneno mengine ni kwamba; inamaanisha kuwa wao wana haki ya kutoa hukumu ya kisheria kwa mada fulani na kupitisha uhalali au uharamu wa jambo fulani.[4]Maana hii ya mamlaka ya kisheria pia inajulikana kama ni “tafwidhu” "uwakili huria” wa Mwenye Ezi Mungu kwa Mtume na Maimamu (a.s)".[5]

Khitilafu za kinadharia juu ya suala la al-Wilayatu al-Tashrii’iyyah

Mada ya mamlaka huru au uwakili huria kwa maimamu juu ya kutunga kisheria, ni suala la mjadala kati ya wanazuoni wa Shia. Swali moja muhimu hapa ni kwamba; Je, Mtume na Maimamu (a.s) wana mamlaka huria kutunga sheria, badala ya Mwenyezi Mungu mwenyewe. Kwa maneno mengine, je, Mwenye Ezi Mungu huwapa au kuwapa haki na uwakili huria wa kutunga sheria?[6]

Kundi moja la wanazuoni, akiwemo Ja’afar Subhani na Lutfullahi Saafi-Gulpaygani, wanatetea kwa nguvu kwamba haki ya kutunga sheria katika Uislamu ni ya Mwenyezi Mungu tu na sio ya mwanadamu yeyote. Kulingana na mtazamo wao, hakuna mtu yeyote anayeweza kudai mamlaka ya kutunga sheria kwa niaba ya Mwenye Ezi Mungu, Kwani Mwenye Ezi Mungu hajampa mtu yeyote yule uwakili huria wa kutunga sheria kwa niaba yake.[7] Wao wakubaliana na hilo kwenye baadhi tu ya vipengele vya sheria, ambapo Hadithi zinaonyesha kwamba Mtume (s.a.w.w) alipewa ruhusa ya kutunga sheria juu ya vipengele hivyo.[8] Kwa upande mwingine, kuna watetezi kama vile; Gharawi Isfahani, Sayyid Ja’afar Murtadha Al-'Aamiliy, na Husseini Tehrani, ambao wanaamini kabisa kwamba Mtume na Maimamu wana mamlaka kamili na huria ya kutunga sheria katika mambo yote ya kidini.[9]

Hoja na vielelezo vya Wapinzani

Wanachuoni wanaopinga mamlaka huria ya Mtume na Maimamu (a.s) juu ya utunzi wa sheria, wanatumia vielelezo kadhaa kutoka kwa Qur'an na Hadithi kuunga mkono hoja zao, baadhi yake ni:

  • Aya ya Qur’an isemayo: “إِنِ الْحُکْمُ إِلَّا لِلَّـهِ” (Utoaji wa hukumu ni haki ya Mwenye Ezi Mungu tu).[10]
  • Aya ya Qur’an isemayo: “وَمَنْ لَمْ يَحْكُمْ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ” (Na wasio hukumu kupitia yale yalio teremshwa na Mwenye Ezi Mungu, basi hao ndiwo makafiri).[11]
  • Aya ya Qur’an isemayo: “فَاحْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ” (Basi hukumu baina yao kwa mujibu wa yale aliyo yashusha Mwenye Ezi Mungu).[12]
  • Hadithi ya Imamu Baqir (a.s) isemayo: “((الحكم حكمان، حكم الله وحكم الجاهلية، وقد قال الله عز وجل: ((وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ” ; “Kuna hukumu za aina mbili; hukumu za Mungu na hukumu za kijahili”[13][14]

Kundi hili la wanazuoni wa Shia linasisitiza kwamba; masimulizi Hadithi yanayounga mkono mamlaka huria ya Mtume na Maimamu (a.s) katika kutunga sheria, yanawasilisha ujumbe wa kwamba Mwenye Ezi Mungu ndiye mwanzilishi wa sheria kisha huziwasilisha kwa Mtume (s.a.w.w) kupitia Wahyi. Hata hivyo, Mtume (s.a.w.w) amepewa wadhifa na ruhusa ya kutoa ufafanuzi na ufumbuzi fulani juu ya baadhi ya vipengele vya sheria hizo, kupitia mwongozo wa Allah.[15] Kwa mfano, katika moja ya Hadithi inasemekana kwamba; Mwenyezi Mungu alifaradhisha rakaa mbili tu katika kila sala za kila siku, lakini Mtume aliongeza rakaa mbili kwenye sala ya Adhuhuri na Alasiri katika sala za mchana. Na kwa upande was ala za usiku, aliongeza rakaa moja kwenye sala ya magharibi na rakaa mbili kwenye sala ya Isha, na Mwenyezi Mungu akayapitisha maamuzi yake.[16]

Hoja na vielelezo vya wanao wafiki nadharia ya Mamlaka Huria ya Mtume na Maimamu (a.s)

Wakubaliaji nadharia ya ewepo wa mamlaka huria ya kutunga sheria kwa Mtume na Maimamu (a.s) wametegemea zile Hadithi ambazo zinasisitiza utoaji wa Mwenye Ezi Mungu wa mamlaka huria ya kutunga sheria za dini kwa Mtume na Maimamu (a.s). Sayyid Ja'afar Murtadha al-'Aamili amesema kwamba; Hadithi hizo ni Hadithi mutawatiru.[17] Katika baadhi ya vyanzo vya Hadithi, kuna milango maalumu inayo zungumzia mada ya utoaji mamlaka ya utunzi wa sheria za dini kwa Mtume na Maimamu (a.s). Kati yake ni; kitabu cha al-Kafi kilichoandikwa na Sheikh Kulayni, ambacho katika mlango uliopewa jina la "Utoaji wa mamlaka ya mambo ya kidini kwa Mtume na Maimamu (a.s)". Katika kitabu hichi mmetajwa Hadithi kumi kuhusiana na jambo hilo.[18] Pia katika kitabu Basaair al-Darajaat, kilicho andikwa na Saffaar, ndani yake mna sehemu maalumu inayo elezea mada hii.[19] Baadhi ya wanazuoni wakitegemea baadhi ya Hadithi, wamesema kwamba; Maana ya Mtume na Maimamu (a.s) kukabidhiwa mamlaka huria (tafwidhu) juu ya kutunga sheria za mambo ya kidini, inamaanisha kuwa wao wana haki ya kutunga sheria juu ya hukumu za kidini.[20] Baadhi ya Hadithi hizo ni:

  • Hadithi ya Imamu Ja'afar al-Sadiq (a.s), isemayo: “Mwenyezi Mungu Mtukufu alimlea Mtume wake kwa kumwelekeza kwenye upendo wake (kumpenda Mungu), kisha akamwambia: "Kwa hakika wewe ni mwenye tabia bora mno." Kisha akampa mamlaka (tafwidhu)... na akasema: "Yeyote anayemtii Mtume wa Mwenyezi Mungu, atakuwa amemtii Mwenyezi Mungu. Mtume wa Mwenyezi Mungu akamkabidhi mamlaka hayo Ali na akamtambua kuwa ni mtu mwaminifu... Sisi ndio kivuko kati yenu na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mwenyezi Mungu hajaweka kheri yoyote kwa yeyote yule anayepinga amri zetu."[21]
  • Imamu Ja'afar al-Sadiq amesema: "Mwenyezi Mungu Mtukufu alimlea Mtume wake, na bila shaka amlea malezi mema mno, na alipomkamilisha kiadabu, akasema: Hakika wewe una tabia njema za hali ya juu. Hapo ndipo alipomkabidhi kazi ya dini na umma ili awaongoze waja wake."[22][23]

Rejea

  1. Ḥusseinī Mīlānī, al-Wilāya al-tashrīʿīyya, uk. 49.
  2. Ḥusseinī Mīlānī, al-Wilāya al-tashrīʿīyya, uk. 49 ; Ṣāfī Gulpāyigānī, Silsila mabāḥith-i imāmat wa mahdawīyyat, 1391 S, juz. 1, uk. 105-107.
  3. Ṣāfī Gulpāyigānī, Silsila mabāḥith-i imāmat wa mahdawīyyat, juz. 1, uk. 97.
  4. Subḥānī, Wilāyat-i takwīnī wa tashrīʿī az dīdgāh-i ʿilm wa falsafa, uk. 19.
  5. Tazama: Majlisī, Biḥār al-anwār, juz. 25, uk. 348; ʿĀmilī, al-Wilāya al-takwīnīyya wa al-tashrīʿīyya, uk. 60-63.
  6. Tazama: Majlisī, Biḥār al-anwār, juz. 25, uk. 348; Subḥānī, Mafāhīm al-Qurʾān, juz. 1, uk. 610; Ṣāfī Gulpāyigānī, Silsila mabāḥith-i imāmat wa mahdawīyyat, juz. 1, uk. 99, 100; Gharawī Iṣfahānī, Ḥāshiyat al-Makāsib, juz. 2, uk. 379; ʿĀmilī, al-Wilāya al-takwīnīyya wa al-tashrīʿīyya, uk. 60-63.
  7. Subḥānī, Mafāhīm al-Qurʾān, juz. 1, uk. 610; Ṣāfī Gulpāyigānī, Silsila mabāḥith-i imāmat wa mahdawīyyat, juz. 1, uk. 99, 101.
  8. Subḥānī, Wilāyat-i takwīnī wa tashrīʿī az dīdgāh-i ʿilm wa falsafa, uk. 20-21; Ṣāfī Gulpāyigānī, Silsila mabāḥith-i imāmat wa mahdawīyyat, juz. 1, uk. 101-102.
  9. Gharawī Iṣfahānī, Ḥāshiyat al-Makāsib, juz. 2, uk. 379; ʿĀmilī, al-Wilāya al-takwīnīyya wa al-tashrīʿīyya, uk. 60-63; Ḥusaynī Tihrānī, Imām shināsī, juz. 5, uk. 114, 179.
  10. Qur'an 12:40, 67; Qur'an 6:57.
  11. Qur'an 5:44.
  12. Qur'an 5:48.
  13. Kulaynī, al-Kāfī, juz. 6, uk. 407.
  14. Subḥānī, Mafāhīm al-Qurʾān, juz. 1, uk. 606-612.
  15. Majlisi, Biharu al-anwar, 1403 H, juz. 25, uk. 348
  16. Subḥānī, Wilāyat-i takwīnī wa tashrīʿī az dīdgāh-i ʿilm wa falsafa, uk. 21.
  17. ʿĀmilī, al-Wilāya al-takwīnīyya wa al-tashrīʿīyya, uk. 61.
  18. Kulaynī, al-Kāfī, juz. 1, uk. 265-268.
  19. Ṣaffār, Baṣāʾir al-darajāt, uk. 378, 383.
  20. ʿĀmilī, al-Wilāya al-takwīnīyya wa al-tashrīʿīyya, uk. 60-63.
  21. Kulaynī, al-Kāfī, juz. 1, uk. 265-268.
  22. Kulaynī, al-Kāfī, juz. 1, uk. 266
  23. ʿĀmilī, al-Wilāya al-takwīnīyya wa al-tashrīʿīyya, uk. 62

Vyanzo

  • ʿĀmilī, al-Sayyid Jaʿfar al-Murtaḍā al-. Al-Wilāya al-takwīnīyya wa al-tashrīʿīyya. Second edition. Beirut: al-Markaz al-Islāmī li-l-Dirāsāt, 1428 AH.
  • Gharawī Iṣfahānī, Muḥammad Ḥusayn. Ḥāshiyat al-Makāsib. Qom: Dhawi l-Qurbā, 1427 AH.
  • Ḥusaynī Mīlānī, ʿAlī. Al-Wilāya al-tashrīʿīyya. Qom: Al-Ḥaqāʾiq, 1432 AH.
  • Ḥusaynī Tihrānī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn. Imām shināsī. Mashhad: Allāma Ṭabāṭabāʾī, 1418 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār al-jāmiʿa li-durar akhbār al-aʾimmat al-aṭhār. Third edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Ṣaffār, Muḥammad b. Ḥasan. Baṣāʾir al-darajāt fī faḍāʾil Āl Muḥammad. Edited by Muḥsin Kūchabāghī. Qom: Kitābkhāna-yi Āyat Allāh al-Marʿashī, 1404 AH.
  • Ṣāfī Gulpāyigānī, Luṭf Allāh. Silsila mabāḥith-i imāmat wa mahdawīyyat. Qom: Daftar-i Nashr-i āthār-i Āyat Allāh Ṣāfī Gulpāyigānī, 1391 Sh.
  • Subḥānī, Jaʿfar. Mafāhīm al-Qurʾān. Qom: Muʾassisat Imām al-Ṣādiq (a), 1421 AH.
  • Subḥānī, Jaʿfar. Wilāyat-i takwīnī wa tashrīʿī az dīdgāh-i ʿilm wa falsafa. Qom: Muʾassisat al-Imām al-Ṣādiq, 1385 Sh.