Al-Hassan wa Al-Hussein Sayyidaa Shabaabi Ahlu al-Jannah

Kutoka wikishia

“Al-Hassan wa Al-Hussein Sayyidaa Shabaabi Ahlu al-Jannah اَلْحَسَنُ و اَلْحُسَینُ سَیِّدَا شَبَابِ أَهْلِ الْجَنَّة” ni Hadithi ya bwana Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na ubora na hadhi ya Imamu Hassan na Imamu Hussein (a.s) juu ya watu wa Peponi. Baadhi ya wanazuoni wa Kishia, waielewa na kuifasiri dhana ya Hadithi hii kwa maana ya kwamba; Maimamu wawili hawa pia ni bora zaidi kuliko watu wengine waliomo duniani humu na ni wajibu kwa umma kushikamana nao kuwafwata. Kulingana na baadhi ya wanazuoni wa Kisunni, wakizingatia Riwaya zinazosema kuwa watu wa Peponi wote ni vijana, wameifasiri hadithi hii kwa maana ya kwamba; Hassan na Hussein (a.s) ni mabwana wa watu wote wa Peponi; ingawaje ubora wao huo hautaweza kupindukia ubora wa Mtume (s.a.w.w) na Imam Ali (a.s). Hadithi hii inapatikana katika vyanzo kadhaa, kama vile Amali ya Sheikh Tusi, Man La Yahduruhu al-Faqih, na Sunan at-Tirmidhi. Pia imeripotiwa kutoka kwa watu 25 miongoni mwa Masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w) kama vile Imamu Ali (a.s), Abu Bakar, na Omar bin Khattab. Hidithi imepewa hadhi ya mutawaatir (yenye wingi wa mapokezi kupitia matabaka ya wapokezi tofauti) kutoka kwa wanazuoni wa madhehebu ya pande zote mbili za Sunni na Shia, na wakaihisabu Hadithi hiyo kuwa ni sahihi. Pia kuna Riwaya inayofanana na Hadithi hii kuotka katika baadhi ya vyanzo vya Sunni, ambayo imewatambulisha Abu Bakar na Omar kama vikongwe wa wazee wa Peponi; lakini baadhi ya wataalamu wa Hadithi wa upande wa Kisunni wanaihesabu Hadithi hii kuwa ni Hadithi dhaifu na bandia. Utambulisho na Hadhi Yake Hadithi ya Sayyidaa al-Shabab Ahlu al-Jannah: ni Riwaya maarufu kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w), [1] ambayo imekuwa ikitumiwa kama ni uthibitisho wa ubora wa Imamu Hassan na Imamu Hussein (a.s) juu ya watu wengine wa Peponi. [2] Katika kitabu cha Bihar al-Anwar kuna maelezo yasemayo kuwa; Katika tukio la Karbala, Imamu Hussein (a.s) alitumia hadithi hii kuitetea na kuthibitisha uhalali wake wa kustahiki nafasi ya Ukhalifa mbele ya maadui zake. [3] Matini na maelezo ya Hadithi hii ni kama ifuatavyo: “اَلْحَسَنُ وَ الْحُسَینُ سَیدَا شَبَابِ أَهْلِ الْجَنَّة؛” “Al-Hasan na Al-Hussein ni mabwana wa vijana wa watu wa Peponi”. [4] Pia Hadithi hii inapatikana vyanzo vya Hadithi vya Shia na Sunni kwa ibara nyengine isiokuwa hiyo, kama vile: «الْحَسَنُ وَ الْحُسَینُ سَیدَا شَبَابِ أَهْلِ الْجَنَّةِ وَ أَبُوهُمَا خَیرٌ مِنْهُمَا»؛. Ambayo maana yake ni kwamba; “Al-Hassan na Al-Hussein ni mabwana wa vijana wa watu wa Peponi, na baba yao ni mbora zaidi kuliko wao”. [5] Pia imekuja kwa ibara isemayo; “«الْحَسَنَ وَ الْحُسَینَ سَیدَا شَبَابِ أَهْلِ الْجَنَّةِ وَ أَنَّ فَاطِمَةَ سَیدَةُ نِسَاءِ أَهْلِ الْجَنَّة»؛. Yaani “Al-Hassan na Al-Hussein ni mabwana wa vijana wa watu wa Peponi, na Fatima ni mbora wa wanawake wa Peponi.” [6] Ubora wa Hassana na Hussein Juu ya Watu wa Peponi Katika baadhi ya Hadithi, imeelezwa ya kwamba; watu wote watakaoingia Peponi, wataingia humo hali wakiwa ni vijana. [7] Baadhi ya wanazuoni wa Kisunni wakitegemea Hadithi kama hizo wameeleza kuwa; neno la “vijana” lililoko katka Hadithi hiyo, ni neno la ziada lenye nia ya kutoa tafsiri na ufafanuzi [8] ya kwamba; Hassan na Hussein (a.s) ndio mabwana wa watu wote wa Peponi. [9] Hata hivyo, Mtume (s.a.w.w) na Imam Ali (a.s) wako nje ya hukumu hiyo kwani wao ni wabora zaidi kuliko Hassana na Hussein (a.s). [10] Katika hadithi nyingine imeelezwa kwamba; Bwana Mtume (s.a.w.w) alimvua Nabi Isa na Yahya katika orodha hiyo. [11] Lakini Muhammad Hasan Madhaffar, mwanazuoni wa Shia, amekataa maneno hayo, na ameona kuwa; kuna uwezekano wa kwamba Haidithi hii imetiwa mkono, na shaka yake ni kwamba; Iweje Nabi Isa na Yahya (a.s) wavuliwe kutoka katika orodha hiyo, hali ya kwamba kuna mitume wenye hadhi na daraja kubwa zaidi kuliko wao, ambao hawakuvuliwa kutoka katika orodha hiyo! Akiwemo Ibrahim na Musa (a.s), ambao ni bora kuliko Yahya, lakini hawakutajwa katika Hadithi hiyo. [12] Vielelezo vya Kuthibitishia Uimamu wa Hassan na Hussein (a.s)

Ali Baharani (aliye fariki mwaka 1340 Hijria) aliye kuwa mwanazuoni wa madhehebu ya Shia, anaamini na kusadiki kuwa; Hadithi inayothibitisha ubwana na utukufu wa Akhera, pia inathibitisha utukufu na ubora katika ulimwengu huu. [13] Hivyo basi yeye anaamini kwamba; kulingana na Hadithi isimayo Hassan na Hussein ni mabwana wa vijana wa Pepono, ni ithibati tosha ya haki ya Uimamu wa Hassan na Husain (a.s) dunianai humu, na kulingana na bora walionao ni lazima watiiwe kama ni viongozi. [14] Kwa kupitia msingi wa hoja hiyo, Hadithi hii inachukuliwa kuwa ni moja ya ushahidi wa Uimamu wa Maimamu hao wawili. [15]

Neno “Sayyid سَید” lililoko katika ibara ya Hadithi hiyo, kikawaida hutumiwa kwa ajili ya mtu aliye na cheo cha; uongozi, ukubwa, au heshima na hadhi maalumu. [16] Pia mtu bora na mkamilifu aliye kamilika kwa sifa zote njema kuliko wengine, naye huitwa Sayyid. [17] Hadithi Kuwa na Hadhi ya Mutawatiru Alamaah Mujlisi, ambaye mtaalamu wa Hadithi wa Shia; akizingatia hali ya mmiminiko wa nukuu juu ya Hadithi ya “Sayyidaa Shababu Ahlu al-Jannah”, ameichukulia Hadithi hiyo kuwa ni miongoni mwa Hadithi “mutawatiru” mbele ya wanazuoni wa pande zote mbili, Shia pamoja na Sunni. [18] Baadhi ya wanazuoni wa Ahl al-Sunna kama Suyuti na Nasir ad-Din al-Albani pia wamethibitisha “utawatiru” wa Hadithi hii. [19] Abu Nu’aim Isfahani, mtaalamu wa Hadithi wa Ahl as-Sunna, ametoa ishara fulani inayo ashiria uzito na usahihi wa nukuu ya Hadithi hii, akimnukuu Ahmad ibn Hanbal amesema kwamba: Ikiwa Riwaya hii atasomewa mwendawazimu, basi mwendawazimu ataondokewa na wendawazimu wake. [20] Nukuu mashuhuri za Hadithi zinapatikana kutoka kwa Sheikh Tusi ndani ya kitabu chake cha Amali [21] na kutoka kwa Sheikh Saduq katika kitabu chake cha Man La Yahduruhu al-Faqih. [22] Tirmidhi na Ibnu Abi Shaybah pia ni miongoni mwa wanazuoni wa Ahlu al-Sunna walioinukuu Riwaya hii. [23] Kulingana na baadhi ya watafiti, ni kwamba; Hadithi ya Sayyidaa Shabab Ahl al-Jannah - pamoja na Riwaya zinazofanana nayo - zimeripotiwa na watu 25 miongoni mwa Masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w), ikiwemo Imam Ali (a.s.), Abu Bakr, na Omar. [24] Uwekwaji wa Hadithi Bandia Juu ya Hadhi ya Omar na Abu Bakar Sambamba na Riwaya Hiyo Katika vyanzo vya Ahl al-Sunnah, kuna ripoti zinazoripoti Hadith zinazo fanana na Hadithi ya “Sayyidaa Shabab Ahl al-Jannah”, Hadithi ambazo zimenukuliwa kuhusiana na hadi ya Omar na Abu Bakar. Ndani ya ripoti ya Hadithi hizo, Omar na Abu Bakar wamesifiwa kuwa wao ni mabwana wa wazee wenye hadhi za kupindia juu ya watu wengine wa Peponi. [25] Mwandishi aitwaye Haythami akiambatana na Ibn Jawzi, ambao ni wanazuoni wa upande wa Ahl al-Sunna, wamezihisabu Riwaya hizo kuwa ni dhaifu na za uongo. [26]

Bwana Tabarsi amenukuu katika kitabu kiitwacho “Al-Ihtijaaj” ya kwamba; katika mjadala kati ya Yahya bin Aktham na Imamu Jawad (a.s), Yahya alimuuliza Imamu kuhusu Hadithi hiyo isemayo kwamba; “Abu Bakar na Omar ni viongozi au ni mambwana wa wazee wa Peponi.” Imamu akimjibu juu ya swali lake; alimwambia kuwa ni jambo geni na lisilowezekana kwamba maneno hayo yawe yametoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w), na akasema kamba, Hadithi hiyo ni Hadithi iliyo tungwa na Bani Umayya  dhidi ya ile Hadith isemayo kuwa ‘Hassan na Husayn ni mabwana wa watu wa Peponi.’ [26]