Nenda kwa yaliyomo

Al-Hajjaj bin Zayd al-Tamimi al-Sa'di

Kutoka wikishia

Al-Hajjaj bin Zayd al-Tamimi al-Sa'di (Kiarabu: الحَجّاج بن زيد تَمیمی سعدی) ni miongoni mwa mashahidi wa tukio la Karbala na mmoja wa wafikishaji wa barua za tukio la Karbala.

Kwa mujibu wa Muhammad Samawi katika Ibsar al-Ain, Hajjaj bin Badr alitoka katika ukoo wa Bani Sa'd wa kabila la Bani Tamim. [1] Baada ya barua ya Imam Hussein (a.s) kwa wakuu wa Basra, ambao aliwaalika kwake, Masoud. bin Amr Azdi alikuwa mmoja wa watano waliohutubiwa katika barua ya Imam Hussein (a.s) ambapo aliandika barua ya kuonyesha himaya na uungaji mkono wake na wa kabila lake kwa Hussein bin Ali na kuikabidhi kwa Hajjaj bin Zayd. Hajjaj alipeleka barua kwa Imamu Hussein (a.s) na alibakia pamoja naye na aliuawa shahidi siku ya Ashura katika shambulio la kwanza la Jeshi la Omar bin Sa’d.[2]

Baba yake Hajjaj, Zayd, alikuwa mmoja wa makhatibu na watoa waadhi katika zama zake na mmoja wa masahaba wa Imamu Ali (a.s) katika Vita vya Siffin. [3] Baada ya kuuawa shahidi Imamu Ali (a.s), Muawiya alimteua kuwa mkuu wa polisi, lakini alikataa uteuzi huo. [4]

Katika ziara ya mashahidi anatolewa salamu kwa maneno:«اَلسَّلَامُ عَلَی الْحَجَّاجِ بْنِ زَیدٍ السَّعْدِی ; Amani iwe juu ya al-Hajjaj bin Zayd al-Sa'di».[5] Katika ziara ya Rajabbiya ya Imamu Hussein (a.s) anasalimiwa kwa ibara ya: «السَّلَامُ عَلَی حَجَّاجِ بْنِ یزِیدَ ; Amani iwe juu ya Hajjah bin Yazid». [6] Sayyid Mohsen Amin pia amemtaja kama ni Hajjaj bin Badr Tamimi katika kitabu chake cha A'yan al-Shia.[7]

Rejea

Vyanzo