Nenda kwa yaliyomo

Bayda'

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Al-Bayda')
Makala hii inazungumzia eneo linalojulikana kwa jina la Bayda'. Ili kujua kuhusiana na kuangamia jeshi la Sufiyani katika eneo hili, unaweza kuangalia makala ya Khasf al-Bayda'.

Al-Bayda' au Dhat al-Jaysh (Kiarabu: البيداء ) ni eneo ambalo kijiografia lipo baina ya Makka na Madina (nchini Saudi Arabia) ambapo jeshi la Sufiyani litaangamia katika eneo hilo mwisho wa zama (Akher Zaman). Kwa mujibu wa riwaya na hadithi mbalimbali ni kwamba, jeshi la Sufiyani litafunga safari na kuelekea huko Makka kwa ajili ya kwenda kupigana vita na Imam Mahdi (a.t.f.s) na litakapofika katika eneo hilo kutatokea muujiza ambapo litamezwa na ardhi hiyo ya eneo hilo.

Wanazuoni wa Fiqhi wa Kishia wanasema kuwa, ni makuruhu kuswali katika eneo hilo. Kadhalika kwa mtazamo wa wanazuoni hao ni kuwa, ni bora kwa Mahujaji wanaotoka Madina wakielekea Makka wakiwa katika kipando, wacheleweshe kutamka talbiya (kusema Labbaika Allahumma na Labbaika...) mpaka watakapopita katika eneo la al-Bayda'.

Lilipo Eneo la Bayda' na Umuhimu wa Kadhia

Bayda' katika hadithi linaashiriwa eneo ambalo lipo baina ya miji mitakatifu ya Makka na Madina.[1]Ibn Idriss Hilli anasema: Umbali wake mpaka Dhul-Hulayfa (Miqati ya watu wa Madina) ni farsakh tatu.[2] Bayda' kilugha ina maana ya jangwa ambalo ndani yake hakuna maji wala majani.[3]

Istilahi hii imezungumziwa katika mlango wa alama za kudhihiri Imam Mahdi (a.t.f.s) wa vitabu vya hadithi[4] na katika milango ya Sala[5] na Hija[6] katika vitabu vya Fiq'h.

Khasf Bayda', Alama ya Kudhihiri Imam Mahdi (atfs)

Makala Asili: Khasf al-Bayda'

Kwa mujibu wa hadithi, Khasf Bayda' ni katika ishara na alama za kudhihiri Imam Mahdi (a.t.f.s).[7] Makusudio ya Khasf Bayda' ni kumezwa na kuangamia jeshi la Sufiyani katika ardhi ya Bayda', jeshi ambalo lilikuwa likielekea Makka kwa ajili ya kupigana vita na Imam Mahdi (a.t.f.s).[8] Ni kwa kuzingatia hilo ndio maana katika baadhi ya hadithi, ardhi ya Bayda' imetajwa pia kama Dhat al-Jaysh (mwenye jeshi).[9]

Imam Muhammad Baqir (a.s) amenukuliwa katika hadithi moja akisema: Mwisho wa zama wakati jeshi la Sufiyani litakapoingia katika eneo la Bayda', mwenye kunadi atanadi kutoka mbinguni na kusema: Ewe ardhi, iangamize kaumu hii! kisha ardhi italimeza jeshi la Sufiyani na kisha wote wataangamia isipokuwa watu watatu."[10]

Hukumu za Fiq'h

Katika vitabu vya fiq'h kumezungumziwa hukumu za kisheria kuhusiana na Bayda'.

  • Kuwa makuruhu kuswali Swala katika eneo hilo:[11] Kwa mujibu wa hadithi zilizonukuliwa katika vyanzo vya fikihi, inaelezwa kuwa, ni makuruhu kuswali Swala katika eneo la Bayda'.[12]
  • Kuchhelewwesha talibiya (kutamka Labbayka Alahumma Labbayka). Fatuwa ya baadhi ya wanazuoni wa fikihi inasema, ni vyema kwa hujaji anaelekea katika ibada ya Hija akitokea Madina asitamke talbiya mpaka atakapopita katika eneo la Bayda' ndio aanze kufanya hivyo.[13] Talbiya ni kutamka: (لَبَّیكَ الّلهُمَّ لَبَّیكَ، لَبَّیكَ لاشَریكَ لَكَ لَبَّیكَ، إنَّ الْحَمْدَ وَ النِّعْمَةَ لَكَ وَالْمُلكَ، لاشَریكَ لَكَ لَبَّیكَ) Hata hivyo baadhi yao wanasema kuwa, hukumu hii ni maalumu kwa hujaji ambaye anaenda Makka akiwa amepanda kipando.[14] Mwandishi wa kitabu cha Swahib al-Jawahir anasema: Wakati Hujaji aliyeko katika kipando anapofika katika eneo la Bayda' ni mustahabu atamke talibiya kwa sauti ya juu.[15]

Rejea

  1. Ibn Athīr, al-Nihāya, juz. 1, uk. 171; Yāqūt al-Ḥamawī, Muʿjam al-buldān, juz. 1, uk. 523.
  2. Ibnu Idriss, Al-sarāʾir, juz. 1, uk. 265.
  3. Ibn Athīr, al-Nihāya, juz. 1, uk. 171.
  4. Nuʿmanī, Al-ghayba, uk. 257, hadithi ya 15.
  5. Tazama; Ibn Idriss, Al-sarāʾir, juz. 1, uk. 265; Najafī, Jawāhir al-kalām, juz. 8, uk. 349.
  6. Najafī, Jawāhir al-kalām, juz. 18, uk. 278.
  7. Kulaynī, Al-Kāfī, juz. 8, uk. 310; Ṣadūq, Al-Khiṣāl, juz. 1, uk. 3.3, hadithi ya 82; Nuʿmanī, Al-ghayba, uk. 257, hadithi ya 15; Ṣanʿānī, Al-Muṣannaf, juz. 11, uk. 371, hadithi ya 20769.
  8. Suleimīyān, Farhangnāme mahdawīyyat, uk. 211.
  9. Kulaynī, al-Kāfī, juz. 3, uk. 90.
  10. Nuʿmanī, Al-ghayba, uk. 280, hadithi ya 67.
  11. Najafī, Jawāhir al-kalām, juz. 8, uk. 349.
  12. Ibnu Idriss, Al-sarāʾir, juz. 1, uk. 265.
  13. Ḥakīm, Mustamsak al-ʿUrwat al-wuthqā, juz. 11, uk. 411, Suala la 20.
  14. Najafī, Jawāhir al-kalām, juz. 18, uk. 278.
  15. Najafī, Jawāhir al-kalām, juz. 18, uk. 278.

Vyanzo

  • Ḥakīm, Muḥsin. Mustamsak al-ʿUrwat al-wuthqā. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d].
  • Ḥillī, Ibn Idrīs al-. Kitāb al-sarāʾir al-ḥāwī li taḥrīr al-fatāwī. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1410 AH.
  • Ibn Athīr, Majd al-Dīn Mubārak. Al-Nihāya fī gharīb al-ḥadīth wa al-athar. Mhariri: Ṭāhir Aḥmad Zāwī and Maḥmūd Muḥammad Ṭanāhī. Beirut: al-Maktabat al-Ilmīyya, 1979.
  • Kulaynī, Muḥammad bin Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad bin ʿAlī al-. Al-Khiṣāl. Mhariri: ʿAlī Akbar Ghaffārī. Qom: Jāmiʿat al-Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmiyya, 1362 Sh.
  • Najafī, Muḥammad Ḥassan al-. Jawāhir al-kalām fī sharḥ sharāʾiʿ al-Islām. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1362 Sh.
  • Nuʿmanī, Muḥammad bin Ibāḥīm al-. Kitāb al-ghayba. Tehran, Maktaba al-Saduq, 1397 AH.
  • Suleimīyān, Khudāmurād. Farhangnāma-ye mahdawīyyat. Tehran: Bunyād-i Farhangī-yi Haḍrat-i Mahdī-yi Mawʿūd, 1388 Sh.
  • Ṣanʿānī, ʿAbd al-Razzāq b. Humām. Al-Muṣannaf. Mhariri: Ḥabīb al-Raḥmān Aʿzamī. Beirut: 1403 AH.
  • Yāqūt al-Ḥamawī. Muʿjam al-buldān. Chapa ya pili. Beirut: Dār Ṣādir, 1995.