Ajjil Farajahum
Ajjil Farajahum (Kiarabu: عجل فرجهم) yenye maana ya «harakisha kudhihiri kwao» ni ibara na dhikri ambayo hutamkwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia baada ya kumswalia Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt (a.s) na wanaitambua hii kwamba, ni dua kwa ajili ya kuwarahisishia mambo Ahlul-Bayt (a.s) au kuharakisha kudhihiri Imamu Mahdi (a.t.f.s). Dhikri hii imekuja katika hadithi kwa ibara tofauti tofauti. Kwa mujibu wa hadithi, Mtume (s.a.w.w) na Imamu Ali bin Abi Twalib (a.s) walitumia dhikri ya ibara zinazofanana na hii. Katika hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebu ya Shia imeusia kutamka dhikri hii katika nyakati maalumu na zimetajwa sifa maalumu kama vile kukutana na Qaim Aal Muhammad (Imamu Mahdi) na kusalimika na mabalaa. Mafakihi kiujumla wanaona kuwa, inajuzu kutamka dhikri hii katika kusoma tashahudi; lakini baadhi wanaamini kwamba, haipaswi kuongeza dhikri hii kwa sura ya daima katika tashahudi.
Utambulisho
Ajjil Farajahum ni dhikri ambayo katika baadhi ya hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebu ya Shia husomwa baada ya Swalawaat (Allahumma Swali Alaa Muhammad Waali Muhammad)[1] na Waislamu wa madhehebu ya Shia huitumia na kuitaja dhikri hii baada ya kumswalia Mtume.[2] Kuambatanisha dua hii na kumswalia Mtume sababu yake ni kukaribia kwake kukubaliwa.[3]
Kwa maana kwamba, hua sababu ya dua kutakabaliwa. Kwa mujibu wa mlolongo wa mapokezi ya baadhi ya hadithi, ukongwe wa dhikri hii unarejea nyuma hadi kwa Imamu Ali (a.s).[4] Katika kitabu cha al-Balad al-Amin cha Ibrahim Kaf’ami (840-905H) kuna dua ambayo ndani yake kumekuja ibara ya: «عَجِّلْ اللّٰهُمَّ فَرَجَهُمْ»[5] Mapokezi ya hadithi hii yanarejea kwa Bwana Mtume (s.a.w.w).[6] Dhikri ya «عجل فرجهم» imeandikwa pamoja na ibara ya kumswalia Mtume kwa ajili ya kupamba baadhi ya maeneo ya kidini ya Mashia kama katika kuta za Msikiti Mkuu wa Isfahan, iran na Haram ya mtukufu Bibi Maasuma (a.s) Qom, Iran.[7]
Maana ya Faraj
Watafiti wanasema kuwa, dua’ Faraj wakati mwingine hutumika kwa maana ya kurahisisha na kusahilisha mambo ya Ahlul-Bayt na waumini na wakati mwingine huwa na maana ya kuomba kuharakishwa kudhihiri Imamu Mahdi (a.t.f.s).[8] Maana ya neno faraj (faraja) imetambuliwa kuwa ni kuwa mbali na ghamu na kuepushwa na matatizo.[9]
Katika matini ya baadhi ya dua, dhikri hii imekuja namna hii: «عَجِّلْ فَرَجَ مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ»[11] au «عَجِّلْ فَرَجَ أَوْلِیَائِکَ»[12] ; lakini katika matini ya Dua’ A’hd imekuja ibara ya «عجَّل فرَجه»[13] Kadhalika katika baadhi ya hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebu ya Shia ni kwamba, baada ya dhikri hii kumekuja ibara isemayo: «وَ أَهْلِکْ عَدُوَّهُمْ» yaani na ‘uwaangamize maadui zao’ na kumekuja pia ibara inayoshabihiana na hiyo.[14]
Sifa Maalumu za Swalawaat na Ajjil Farajahum
Katika hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebu ya Shia ni mustahabu kumswalia Mtume na kuambatanisha na «عَجِّل فرجهم» au «عجل فَرَجَ آل محمد» katika baadhi ya nyakati kama siku ya Ijumaa na baada ya adhuhuri ya siku ya Alkhamisi.[15] na kumetajwa faida na sifa maalumu ya jambo hilo. Katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) imenukuliwa ya kwamba, kila ambaye baada ya Sala ya alfajiri na adhuhuri atamswalia Mtume na kuambatanisha ibara ya «عجل فرجهم» basi atamuoma Qaim Aal Muhammad kabla ya kufa kwake.[16] Kuwa miongoni mwa masahaba wa Qaim,[17] kupata uombezi siku ya Kiyama,[18] kusalimika roho[19] na kuwa mbali na hatari ya wanyama ni miongoni mwa sifa zingine za dhikri hii pamoja na baadhi ya masharti na adabu zilizobainishwa kuhusiana na hili.[20]
Kutamka Ajjil Farajahum katika Swala
Kwa mujibu wa Fat’wa iliyotolewa na baadhi mafaikihi wa Kishia ni kwamba, inajuzu kutamka ibara ya Ajjil Farajahum baada ya Swalawaat ya Tashahudi katika hali yoyote ile. Ayatullah Tabrizi na Sistani[21] wamesema kuwa, inajuzu kuileta dhikri hii baada ya Swalawaat ya Tashahudi. Kwa mtazamo wa Ayatullah Bahjat na Fadhil Lankarani ni kwamba, hakuna tatizo kama nia itakuwa ni dua. Kwa mtazamo wa Ayatullah Khamenei, Safi Golpaygani[22] na Noori Hamedani[23] ni kwamba, kama itakuwa sio kwa nia ya amali na kitendo ambacho Mwenyezi Mungu amekiamrisha basi hakuna tatizo; lakini Ayatullah Makarim Shirazi[24] anasema kuwa, mtu anayeswali hapaswi kuitia na kuiongezea kwa sura ya daima dhikri hii katika kisomo cha Tashahudi na kwa tahadhari (ihtiyat) hapaswi kufanya hilo.[25]
Rejea
- ↑ Sheikh Bahai, Miftah al-Falah, uk. 87; Nuri, Mustadrak al-Wasail, juz. 5, uk. 74; Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 87, uk. 215.
- ↑ Ferestane Shalawat Ba 'Ajjil Farajahum, Tovuti.tibyan.net.
- ↑ Ilahi Nejad, «Barresi wa Tahlil Naqshe Du'a Dar Ta'jil Bakhshe Zuhur», uk. 10.
- ↑ Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 95, uk. 127.
- ↑ Kaf'ami, Balad al-Amin, juz. 1, uk. 96.
- ↑ Kaf'ami, Balad al-Amin, juz. 1, uk. 91.
- ↑ Kuchani, «Khat Bana-i Mu'aqqali, Tajalli Ali (a.s) Bar Khatt Kufi Bana-i», uk. 91; Sutudeh, «Kuteib-haye Astaneh Muqaddas Qom», uk. 33.
- ↑ Ilahi Nejad, «Barresi wa Tahlil Naqshe Du'a Dar Ta'jil Bakhshe Dhuhur», uk. 10; Yazdi Nejad, «Chande Nukteh Dar Ma'anae Hadith Amr Be Du'a Faraj», uk. 263-264.
- ↑ Dehkhuda, Lugat-nameh (Kamusi), Chini ya neno Faraj (فرج).
- ↑ Riwayati Az Saqakhaneh-i Waqfi Be Qadamat 3 Qarn, Tovuti farsnews.ir.
- ↑ Sheikh Bahai, Miftah al-Falah, uk. 87.
- ↑ Kaf'ami, Balad al-Amin, juz. 1, uk. 244.
- ↑ Nuri, Mustadrak al-Wasail, juz. 5, uk. 74.
- ↑ Sheikh Tusi, Misbah al-Mutahajjid, juz. 1, uk. 265; Kaf'ami, Balad al-Amin, juz. 1, uk. 71.
- ↑ Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 87, uk. 215.
- ↑ Nuri, Mustadrak al-Wasail, juz. 5, uk. 96.
- ↑ Nuri, Mustadrak al-Wasail, juz. 5, uk. 98.
- ↑ Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 86, uk. 353.
- ↑ Nuri, Mustadrak al-Wasail, juz. 6, uk. 97-98.
- ↑ Tabrasi, Makarim al-Akhlak, uk. 291.
- ↑ Sistani, Pursesh wa Pasukh: Tashahhud, Tovuti sistani.org.
- ↑ Shafi Gulpeighani, Jami'u al-Ahkam, juz. 1, uk. 73.
- ↑ Nuri Hamedani, Hezar wa Yek Mas'aleh Fiqhi, juz. 2, uk. 59.
- ↑ Makarim Shirazi, Istiftaat Jadid, 1427 AH, juz. 2, uk. 107, Suala ka 263.
- ↑ Wahid Pasukhgui Be Sualat Jamiat Zahra (a.s), «Dastaneha: Fiqh wa Zindeqi», uk. 55.
Vyanzo
- Dehkhuda, Ali Akbar, Lugat Nameh, Tehran, Daneshgah Tehran, 1377 S.
- Ilahi NeJad, Hussein, Barresi wa Tahlil Naqsh Du'a Dar Ta'jil Bakhshe Dhuhur, Majalah Pazuheshha-e Mahdavi, juz. 20, Bahar 1396 S.
- Kaf'ami, Ibrahim bin Ali, al-Balad al-Amin.
- Kuchani, Abdullah, Khat Bana-i Mu'aqqali, Tajalli Ali (a.s) Bar Khatt-e Kufi Bana-i, Majalah Kitab Mahe Hunar, juz. 31 & 32 Farvardin & Urdibehest, 1380 S.
- Majlisi, Muhammad Baqir bin Muhammad Taqi, Bihar al-Anwar, Beirut, Dar Ihya al-Turath al-Arabi, 1368 S/1403 HS.
- Makarim Shirazi, Nashir, Istifta'at Jadid, Qom, Madrasah al-Imam Ali bin Abi Talib (a.s), 1427 HS.
- Markaz Pasukhgui Be Sualat Jamiat Zahra (a.s), Dastaneha, Fiqh wa Zindeqi,, Mutala'at Qur'ani Nameh Jameeh, juz. 51, Dey 1387 S.
- Nuri Hamedani, Hussein, Hezar wa Yek Mas-aleh Fiqhi, Qom, Mahdi Mau'ud (a.j.f.s), 1388 S.
- Nuri, Hussein Muhammad Taqi, Mustadrak al-Wasail, Beirut, Muasase Āhlul-bait li Ihya al-Turath 1408-1429 HS/1987-2008 M.
- Safi Golpeighani, Luthfullah, Jami' al-Ahkam, Qom, Daftar Tandhim wa Nashr Athar Ayatullah Safi Golpeighani, 1385 S.
- Sistani, Sayyid Ali, Pursesy wa Pasukh: Tashahhud, Tovuti sistani.org. Tarikh Bazdid: 10 Dey 1402 S.
- Tovuti farsnews.ir. Riwayati Az Saqakhaneh-i Waqfi be Qadamat 3 Qarn. Tarikh Bazdid: 10 Bahman 1402 S.
- Tovuti farsnews.ir. [https://farsnews.ir/isfahan/news/14021108001019/%D8%B1%D9%88%D8%A7%DB%8C%D8%AA%DB%8C-%D8%A7%D8%B2-%D8%B3%D9%82%D8%A7%D8%AE%D8%A7%D9%86%D9%87%E2%80%8C%D8%A7%DB%8C-%D9%88%D9%82%D9%81%DB%8C-%D8%A8%D9%87-%D9%82%D8%AF%D9%85%D8%AA-3-%D9%82%D8%B1%D9%86
- Tovuti masjid.ir. Ma'na-e Wa 'Ajjil Farajahum Cist. Tarikh Darj Matalib: 8 Khurdad 1397 S, Tarikh Bazdid: 10 Dey 1402 S.
- Tovuti article.tibyan.net . Ahammiyat Ferestan Salawat Ba 'Ajjil Farajahum, Tarikh Darj Matalib: 28 Azar 1390 S, Tarikh Bazdid: 10 Dey 1402 S.
- Sutudeh Manuchahr, «Kitibehaye Astaneh Muqaddas Qom», Ma'arif-e Islami (Sazman Auqaf), juz. 16, Bahar, 1353 S.
- Sheikh Bahai, Muhammad bin Hussein, Miftah al-Falah fi 'Amal al-Yaum wa al-lailah min al-Wajibat wa al-Mustahabbat, Dar al-Kutub al-Islami.
- Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan, Mishbah al-Mutahajjid, Beirut: Muasase Fiqh al-Shiah, 1411 HS/1991 M.
- Tabrasi, Hassan bin Fadhl, Makarim al-Akhlak, Sharif Radhi, 1370 S.
- Yazdi, Abdu-Rasul, «Chande Nukteh Dar Ma'nae Hadith Amr Be Du'a-e Faraj», Imamat Pazuhi, juz. 12, Satan, 1392 S.