Ridha (Lakabu)

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka (lakabu) Ridha)

Ridha (Kiarabu: الرّضا) ni lakabu maarufu ya Imam Ali bin Musa al-Ridha (a.s)[1], - likimaanisha – au likiwa na maana ya kupendwa na kukubaliwa. Kuhusu kupewa cheo cha lakabu hiyo, inasemekana kwamba Ali bin Musa Ridha (a.s) alipokubali Taji la Ukhalifa baada ya Maamun. Maamun Abbasi [Maelezo 1] alimpa cheo cha Ridha[2] na kumwita Ridha Aali-Muhammad[3]. Katika kitabu U’yuwn Akhbar al-Ridha, kuna riwaya imenukuliwa kwamba Ahmad bin Abi Nasr Bizanti alimuuliza Imamu Jawadi (a.s). Inasemekana kwamba miongoni mwa wapinzani wenu wanaamini kuwa baba yako –Imam Ridha- Maamun amempa cheo cha Ridha kwa sababu amekubali Taji la Ukhalifa baada yake, Imam Jawad (a.s) akamjibu, hapana kwa hakika walimsingizia na wamekiri uwongo na wakafanya makosa. Mwenyezi Mungu alimwita Ali bin Musa (a.s) Ridha; Kwa sababu alikuwa radhi na Mwenyezi Mungu mbinguni na kumridhia Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na maimamu wengine duniani. Katika muendelezo wa riwaya hiyo, inasemekana kwamba Bizanti alimuuliza tena Imamu Jawad, Kwani wazazi wako wote waliopita (maimamu maasumu) walikuwa hawakuridhiwa na Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.w) na hawakuwa maimamu? Imamu akasema: ndio,[4]] Bizanti akasema: Kwa hivyo baba yako aliitwaje Ridha kati yao? Imamu (a.s) alisema: Kwa sababu maadui zake na wapinzani waliridhika naye pamoja na marafiki zake na wasaidizi wake, (Akikusudia aliridhiwa na marafiki na maadui zake wote) na hakuna hata mmoja katika baba zake aliyekuwa hivyo; Kwa hiyo, baba yangu aliitwa Ridha miongoni mwao.[5]

Rejea

  1. Amiyn, A’yan al-Shia, 1403 AH, juz. 2, uk. 13.
  2. Majlisiy, Bihar al-Anwar, 1363, juz. 49, uk. 146.
  3. Sabat bin Juwziy, Tazkirat Al-Khawas, 1418 AH, uk. 315.
  4. Saduwq, A’yuwn Akhbar al-Ridha, 1378 AH, juz. 1, uk. 13.
  5. A’ttardi, Musnad al-Imam al-Ridha (a.s), 1406 AH, uk. 10.

Maelezo

  1. Abu Abbas Abdullah bin Harun Abbasi (170-218 AH), anayejulikana kwa jina la Maamun Abbasi, khalifa wa saba kutoka ukoo wa Bani Abbas aliyetawala kuanzia mwaka 1980 hadi 218 Hijiria na alimpa sumu na kumuua shahidi Imam Ridha (a.s).

Vyanzo

  • Sheikh Saduq, Mohammad Bin Ali, A’yun Akhbar Al-Ridha, utafiti na marekebisho ya Mehdi Lajordi, Tehran, Jahan Publishing House, Chapa, 1378.
  • Sheikh Saduq, Muhammad Bin Ali, A’yun Akhbar al-Ridha, amani iwe juu yake, iliyotafsiriwa na Mohammad Taqi Aganjafi Esfahani, Tehran, Ilmia Islamic Publishing House, chapa ya kwanza, Beta.
  • Tabarsi, Ahmad bin Ali, Al-Ihtijaj Ali Ahl al-Jajj, imetafitiwa na kuhaririwa na Mohammad Baqer Khursan, Mashhad, Mortadha Publishing House, chapa ya kwanza, 1403 AH.
  • Kuleyni, Muhammad bin Yaqub, al-Kafi, iliyorekebishwa na Ali Akbar Ghafari na Muhammad Akhundi, Tehran, Darul Kitab al-Islamiya, 1407 AH.
  • Majlisi, Mohammad Baqir, Bihar al-Anwar al-Jamaa kiongozi Akhbar al-Imaa al-Athar, Beirut, Dar Ihya al-Turath al-Arabi, chapa ya pili, 1403 AH.