Yanbu'

Kutoka wikishia

Yanbu' (Kiarabu: يَنبُع) ni mji ulioko magharibi mwa Madina, ambao ni maarufu kwa chemchemi zake nyingi na mlima wa Radhwi unapatikana ndani yake. Mji huu ulitekwa na Waislamu katika mwaka wa pili wa Hijria.

Yanbu' ilikabidhiwa kwa Imam Ali (a.s) baada ya baadhi ya matukio, na kwa kuboresha kilimo, akaligeuza eneo hilo kuwa wakfu kwa Alawi (kizazi cha Alawi), na watoto wa Imamu Hassan (a.s) pia waliishi katika eneo hilo.

Imam Sajjad (a.s) alitoa hifadhi kwa familia ya Marwan bin Hakam wakati wa tukio la Harra na kujificha Nafsi Zakiyah (Muhammad bin Hassan bin Abdallah) katika eneo hilo ni moja ya matukio ya kihistoria katika eneo hilo.

Mahali Lilipo na Kuitwa Kwake kwa Jina Hilo

Yanbu' ni mji ulioko katika pwani ya Bahari Nyekundu [1] katiika viunga vya Hijaz [2] na eneo hilo linahesabiwa kuwa ni sehemu ya mji wa Madina [3] ambalo magharibi yake [4] iko umbali wa nyumba saba [5] au tisa [6] ]. Mji huu uko umbali wa kilomita 225 kutoka Madina. [7]

Hapo awali, eneo hilo lilikuwa na mashamba ya mitende, kilimo [8] na chemchemi nyingi [9], ambapo kutokana na kuwa na ongezeko la chemchemi kutoka ardhini [10] likapewa jina la Yanbu'.

Yanbu' ilikuwa kwenye njia ya misafara ya Hija iliyokuwa ikitoka Misri [11] na Syria [12] kwenda Madina na Makka. Mlima wa Radhwi unapatikana hapo ukiwa na umbali wa tofauti ya nyumba moja. [13] Nafs Zakiyah alijificha katika Mlima wa Radhwi kwa muda wakati wa utawala wa Mansour. [14]

Wakfu za Ali (a.s)

Mji wa Yanbu' uliangukia mikononi mwa Waislamu bila ya vita katika vita vya pili vya Mtume (s.a.w.w) [15] vilivyojulikana kwa jina la Dhu al-Ashirah katika Mwaka wa Pili Hijria. Mtume (s.a.w.w) alilikabidhi eneo hilo kwa baadhi ya Waislamu. [17] Imam Ali (a.s) alinunua kutoka kwao na akalima na kuchimba maji hapo. [18] Hata hivyo baadhi wanaamini kuwa, eneo hili alipatiwa Imamu Ali na Mtume (s.a.w.w) [19] au Omar.

Katika vyanzo, kumetajwa kuhusu wakfu nyingi za Amirul-Muuminin Ali (a.s) katika eneo hilo. [21] Imamu Hussein (a.s) alitoa faida ya bidhaa za eneo hili kwa Abdullah bin Jafar bin Abi Talib, naye baada ya muda alimpa pia Muawiyah bin Abi Sufiyan [22] mahali hapo. Wakati wa tukio la Harra, Imam Sajjad (a.s) alikwenda Yanbu' [23] na kwa mujibu wa simulizi, pia aliichukua familia ya Marwan pamoja na familia yake hadi Yanbu'. [24]

Abdullah bin Hassan al-Muthanna alijaribu kuichukua kutoka kwa khalifa wakati wa utawala wa Safah [25] na ikapelekea kuibuka mabishano baina ya watoto wa Ali (a.s.) juu ya wakfu wa Yanbu' [26] na hatimaye eneo hilo likakabidhiwa na Mahdi Abbasi kwa Alawi. [27].

Wakazi Wake

Katika vyanzo vingi, wakazi wa Yanbu' wanachukuliwa kuwa Ansar, [28] Hasanian, [29] na Zaidiyyah [30] na vilevile kabila la Jahniyah [31]. Mmoja wa watu mashuhuri wa eneo hilo ni Hassan bin Qasim bin Muhammad, ambaye alikwenda Morocco kutoka Yanbu' mnamo mwaka wa 664 AH [32]. Alikuwa babu wa wakuu wa Alawi wa Morocco, ambao waliunda serikali katika eneo hilo. [33]

Rejea

Vyanzo