Umra ya mufrad

Kutoka wikishia

Al-Umra al-Mufrada (Kiarabu: العمرة المفردة) ni katika aina za Umra na mjumuiko wa amali (matendo) ambayo hufanywa kwa ajili ya kuzuru al-Kaaba (nyumba ya Mwenyezi Mungu). Umra al-Mufrada sio sehemu ya amali (matendo) ya Hija na ni kwa namna hiyo ndio maana iko mkabala (kinyume) na Umra al-Tamatui ambayo ni sehemu ya Hajj al-Tamatui.

Umra

Makala asili: Umra

Umra ni mkusanyiko wa matendo (amali) ya kisheria kama kuvaa ihram, tawafu na [[kufanya sa'ayi baina ya swafa na marwa][1] ambayo hufanywa kwa lengo la kuzuru nyumba ya Mwenyezi Mungu.[2] Kuna aina mbili za Umra: Umra al-Tamatui na Umra al-Mufrada.[3] Umra al-Tamatui hufanywa pamoja na Hajj al-Tamatui na ni sehemu yake (ni sehemu ya Hajj al-Tamatui).[4] Umra al-Mufrada inajitegemea peke yake. Kwa maana kwamba, iko kando na Hajj al-Tamatui[5] Mafakihi wanasema, kutekeleza Umra kama ilivyo Hija ni wajibu kwa muislamu mara moja katika umri wake kwa yule aliyetimiza masharti[6] na kufanya zaidi ya mara moja ni mustahabu.[7]

Kupewa jina na vigawanyo vyake

Umra al-Mufrada imeitwa mufrada kutokana na kuwa siyo sehemu ya Hija na hufanywa peke yake.[8] Umra Qiraan na Ifraad ni katika vigawanyo vya Umra Mufrada. Umra Qiraan ni Umra ambayo ni ya mtu ambaye anapaswa kutekeleza Hajj Qiraan.[9] Umra ifrad ni Umra ya mtu ambaye anapaswa kutekeleza Hajj Ifrad (ni makhsusi kwa wakazi wa Makka).[10]

Amaali (matendo) ya Umra al-Mufrada ni

Umra al-Mufrada ina amali (matendo saba), ambayo ni kama ifuatavyo:

  1. Ihram
  2. Kufanya tawafu
  3. Sala ya tawafu
  4. Sa'ayi
  5. Kupunguza au kunyoa nywele
  6. Tawafu ya Nisaa
  7. Sala ya tawafu ya Nisaa.[11]

Kwa mujibu wa hadithi na kauli za mafakihi, Umra al-Mufrada inayofanyika katika mwezi wa Rajab ina fadhila kubwa sana kuliko Umra al-Mufrada inayofanyika katika miezi mingine.

Tofauti baina ya Umra Mufrada na tamatui

Umra Mufrada na Umra al-Tamatui zinatofautiana katika mambo kadhaa yafuatayo:

Umra yenye fadhila zaidi

Kwa mujibu wa vitabu vya fiqh, Umra katika mwezi wa Rajab ina fadhila na thawabu nyingi zaidi ikilinganishwa na miezi mingine.[14] Jambo hili limebainishwa pia katika hadithi mbalimbali. Katika kitabu cha Wasail al-Shiah kuna hadithi zimenukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) na Imam Swadiq (a.s) ambazo zinabainisha kwamba, kufanya Umra katika mwezi wa Rajab ni Umra Mufrada yenye fadhila nyingi zaidi.[15][Maelezo 1]

Maelezo

  1. یادداشت

Rejea

  1. Muhaqqiq Hilli, Shara'i al-Islam, juz. 1, uk. 275
  2. Sheikh Tusi, al-Mabsut, juz. 1, uk. 296; Najafi, Jawahir al-Kalam, juz. 2, uk. 441
  3. Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhang Fiqh,juz. 5, uk. 479
  4. Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhang Fiqh,juz. 5, uk. 481
  5. Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhang Fiqh,juz. 5, uk. 485
  6. Tazama: Muhaqqiq Hilli, Shara'i al-Islam, juz. 1, uk. 274; Najafi, Jawahir al-Kalam, juz. 2, huk. 441
  7. Sheikh Tusi, al-Mabsut, juz. 1, uk. 297; Tim peneliti Bi'tsah Aytullah Khomenei, Muntakhab Manasik Haj, uk. 59
  8. Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhang Fiqh, juz. 5, uk. 485
  9. Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhang Fiqh, juz. 5, uk. 485
  10. Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhang Fiqh, juz. 5, uk. 485
  11. Muhaqiq Hili، Shara'i al-islam، 1408 H، juz. 1، uk. 275.
  12. Muhaqiq Hili، Shara'i al-islam، 1408 H، juz. 1، uk. 275-276.
  13. Muassasah Dairah al-Ma'arif fiqh Islami, Farhang Fiqh, juz. 5, uk. 488
  14. Tazama: al-Durus al-Shariiya, 1417 H, ju. 1, uk. 337; Muhaqqiq Hilli, Shar'i al-Islam, 1408 H, juz. 1, uk. 276.
  15. Hur Amuli, Wasail al-Shiah, juz. 14, uk. 302

Vyanzo

  • Hur Amuli, Muhammad bin Hassan, Tafshil Wasail al-Shi'ah ila Tahshil Masail al-Shari'ah, Qom: Muassasah Al Al-Bait, cet. I, 1409 H.
  • Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqhi Islami, Farhang Fiqh Muthabeqe Mazhab Ahlibait (a.s), Qom: Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqhi Islami, cet. I, 1392 HS.
  • Muhaqqiq Hilli, Ja'far bin Hassan, Sharayi' al-Islam fi Masail al-Halal wa al-Haram, Diteliti dan direvisi oleh: Abdul Hussein Muhammad Ali Baqqal. Qom: Ismailiyan, cet. II, 1408 H.
  • Najafi, Muhammad Hassan, Jawahir al-Kalam fi Sharh Sharayi' al-Islam. Beirut: Dar Ihya al-Turats al-Arabi, cet. VII, 1404 H.
  • Shahid Awal, Muhammad bin Makki al-Amuli. Al-Durus al-Shar'iyah fi al-Fiqh al-Imamiyah, Qom: Penerbit Islami, cet. II, 1417 H.
  • Sheikh Tusi, Muhamamd bin Hassan. Al-Mabsuth fi al-Fiqh al-Imamiyah, Diteliti dan direvisi oleh Sayyied Muhammad Taqi Kashfi. Teheran: al-Maktabah al-Murtadhawiyah li Ihya' al-Athar al-Ja'fariyah, cet. III, 1387 HS.
  • Tim peneliti Bi'tsah Ayatullah Khomenei. Muntakhab Manasik Hajj. Pnerbit Mash'ar, cet. II, 1426 H.