Umra

Kutoka wikishia

Umra (Kiarabu: العمرة) ni mjumuiko au mkusanyiko wa matendo fulani kama vile ibada za hija ambazo hutekelezwa wakatiwa kuzuru al-kaaba tukufu ya Mwenyezi Mungu. Kutekeleza ibada ya Umra pindi masharti yake yanapo timia ni wajibu mara moja katika umri wa mwanadamu, na zaidi ya mara moja ni mustahabu.Na kuna aina mbili za Umra: Umra ya tamatui na umrah mufradah. Na umrah tamatui ni sehemu ya ibada ya hija na hutekelezwa ndani ya miezi ya Dhul-hijja.

Ibada ya umra ni sawa na ibada ya hija, huzingatiwa kuwa ni sahihi na wajibu kwa kutimia masharti manne ambayo ni kuwa na akili timamu, kufikia balee, kuwa huru na (kutokuwa mtumwa), na kuwa na uwezo. Ihram, tawafu, swala ya Taawafu, sa'ayi kati ya swafa na mar'wah na kupunguza nywele au kunyoa ni miongoni mwa matendo ya ibada ya hija. Umrah mufradah na umrah Tammatui zinatofautina katika baadhi ya matendo.

Kwa msingi na kwa mujibu wa hadithi mbali mbali zinazo husiana na kuzungumzi umra ya mwezi wa rajabu ni kuwa umrah hii ina fadhila na ubora zaidi kuliko umra za miezi mingine.

Taarifa na utambulisho wa kifiqhi wa mgawanyo wake

Umrah ni matendo maalumu ya kisheria matendo ambayo hutekelezwa katika eneo la Makkah na katika Miiqaati (vituo vya kuingilia au kuanzia)[1] kwa lengo la kuzuru na kutembelea nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu.[2] na Umrah imegawanyika sehemu mbili, ya kwanza umra-tamatui, na pili umra mufradah.[3]

umrah tamatui ni umra ambayo hutekelezwa pamoja au sambamba na hija ya kiislaamu na huzingatiwa kuwa ni sehemu ya ibada ya hija.[4] Umrah mufradah pia ni Ibada ya umra ibada ambayo hutekelezwa kando ya ibada ya hija (hutekelezwa ikiwa peke yake kando na ibada ya hija).[5]

Hukumu za kifiqh

Kwa mujibu wa fat'wa za wanazuoni wa fiqhi ni kuwa kutekeleza matendo ya umrah ni sawa na hija, ni wajibu kwa kila muislamu aliye timiza masharti maalumu, na ni wajibu mara moja katika umri wa mtu.[6] Wajibu wa ibada ya umrah ni miongoni mwa ibada za wajibu wa haraka ambazo utekelezaji wake haijuzu kuuchelewesha.[7] Na kutekeleza Ibada ya umrah zaidi ya mara moja katika umri wa mtu ni jambo la mustahabu.[8]

Swahibul-jawahir (mtunzi wa kitabu Jawaahirul-kalaam) ameandika kwamba wanazuoni wa fiqh wamekubaliana na kufikia ijmai juu ya kwamba umrah ya hija ni wajibu.[9] na kwa mujibu wa maneno yake ni kwamba kuwa wajibu kwa ibada ya umrah ni suala lililo bainishwa na kufafanuliwa ndani ya hadithi na pia ndani ya Qur'an tukufu na miongoni mwa aya zilizo bainisha wajibu huo ni aya ya 196 ya Surat al-baqarah isemayo: (Na itimizeni hija na umra kwa ajili ya Mwenyeezi Mungu).[10]

Ni wajibu wa Mukallaf ambae atatekeleza ibada ya Hija tamatui pia kutekeleza pamoja nayo Umrah tamatui, na si wajibu kutekeleza Umrah mufradah.[11]

Masharti ya kuwa wajibu kwa umra

Masharti ya kuwa wajibu kwa umrah, ni sawa na masharti ya kuwa wajibu kwa hija,[12]kwa maana kwamba Umrah huwa wajibu pale mukallaf anapokuwa na akili timamu, awe amefikia balee na awe huru (asiwe mtumwa), pia awe na uwezo wa kimali (unao muwezesha kutekeleza Ibada hiyo)[13] na uwezo(istitwaa'ah) maana yake ni kuwa na uwezo wa kimwili na kimali, kuwa na muda wa kutosha na kutokuwepo vikwazo katika njia ya kutekelea ibada hiyo.[14]

Ibada ya umra

Umrah mufradah na Umrah tamatui zinashirikiana katika baadhi ya matendo na katika matendo mengine zinatofautiana. Na katika Umrah zote mbili ibada hizo hutekelezwa kwa utaratibu au matendo yake hutekelewa kwa utaratibu ufuatao: Ihram, tawaf, swala ya tawaf, sa'ayi kati ya swafa na mar'wah, kupunguza nywele.[15]tofauti ya matendo hayo ni kama ifuatavyo:

  • Katika ibada ya umratul mufradah baada ya kutekeleza matendo yaliyo tajwa hapo juu, pia ni unapaswa kutekeleza tawaf an-nisaa na swala ya tawaf an-nisaa.
  • Ihram katika umrah tamatui hufanyika tu katika miezi maalum ambayo ni (shawwal, dhul-qaadah, na dhul-hijjah) lakini katika umrah mufradah haifungiki na muda maalumu (ni wakati wote).
  • Katika umrah mufradah, mukallaf anaweza badala ya kupunguza kiasi fulani cha ya nywele au kucha pia anaweza kunyoa kipara, ama katika Umrah tamatui ni lazima kupunguza nywele tu na si vinginevyo.[16]
  • Miiqaat na vituo vya umratul tamatui ni kuwa ni lazima kuingia kwenye haram ya Makkah na kuanza ibada hiyo kupitia moja wapo kati ya mawaqiit na vituo vitano maalum, ama miiqaat na vituo vya umrah mufradah, pamoja na vituo na mawaqiit tano zilizo tajwa anaweza pia (kuanzia ibada yake sehemu ya karibu sana iliyo nje na haram au iliyokaribiana na haram). Na inawezekana kufanyika kuanzia sehemu ya karibu na haramu na iliyo nje na haram).[17]

Umra ya mwezi wa rajabu

Kwa mujibu wa maneno ya wanazuoni wa fiqhi ni kuwa, umrah ya mwezi wa rajabu ukiipima na kuilinganisha na umra za miezi mingine isiyokuwa rajab umrah hii ni yenye fadhila nyingi sana.[18] Riwaya mbali mbali pia zimenukuliwa kuhusiana na madhumuni haya ikiwemo kitabu wasaailus-shiah, ikinukuliwa kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) na imekuja kutoka kwa Imamu Swadiq(a.s) kwamba; miongoni mwa umrah zenye fadhila nyingi na kubwa ni umrah ya mwezi wa rajabu.[19]

Istilahi za umra

Umratul-islaam, Umratut-tahallul au Fawaat, Umratul- mabtuulah, umratul-qiraan na Umratul-ifraad hizi ni miongoni mwa istilihai na majina yaliyo tumika katika ibada ya Umrah na ufafanuzi wake utafuatia hivi punde:

  • Umratul-islaam: hii ni umrah ya mara ya kwanza ambayo huwa ni wajibu, umrah hii huitwa kwa jina la umratul-islaam. Na umrah hii ni muqabili wa umrah ya mustahabu na vile vile ni umrah inayo kuwa wajibu kwa sababu ya nadhiri na mfano wake, umra hii ni wajibu.Muassasatu daairatul-ma'aarifil-fiqhil-islaami, Farhang fiqhi, 1392 H, juz. 5, uk. 480.
  • Umratut-tahallul au Fawaat: Ni Umrah ambayo Al-haj baada ya kuvaa Ihram, hawezi kutimiza na kukamilisha hija yake kwa sababu yoyote ile. Kwa msingi huu, hana wajibu na ulazima wa kutekeleza matendo ya hija na wajibu wa kutekeleza matendo ya hija huondolewa kweke na sio wajibu kwake na nilazima kwa mukallaf anae tekeleza umrah kama hii kutoka na kuvua ihram yake.[20]
  • Umrah Mabtuulah: Ni jina lingine la Umratul- mufradah. Na ni kwa sababu kwamba Umrah mufradah iko kando na matendo ya hija, na ndio maana ikaitwa Mabtuulah (iliyo tenganishwa).[21]
  • Umratul-qiraan ni umrah ambayo wadhifa na jukumu la Mukallaf ni kutekeleza Hajji Qiraan.[22]
  • Umratul-ifraad ni Umrah ya mtu ambae anaitakidi na kuamini kuwa ni wajibu na lazima kwake kutekeleza Hajji Ifraad.[23]

Rejea

  1. Najafiy, Jawaahirul-kalaam, Beirut, juz. 20, uk. 441.
  2. Shekhe Tousiy, Al-mabsout, 1387 H, juz. 1, uk. 296; Najafiy, Jawaahirul-kalaam, Beirut, juz. 20, uk. 441.
  3. Muassasatu daairatul-ma'aarifil-fiqhil-islaami, Farhang fiqhi, 1392 H, juz. 5, uk. 479.
  4. Muassasatu daairatul-ma'aarifil-fiqhil-islaami, Farhang fiqhi, 1392 H, juz. 5, uk. 481.
  5. Muassasatu daairatul-ma'aarifil-fiqhil-islaami, Farhang fiqhi, 1392 H, jUZ. 5, uk. 485.
  6. Tazama: kitabu cha Muhaqqiq Hilli, Sharaaiul-islaam, cha mwaka 1408 H, juz. 1, uk. 274; Najafiy, Jawaahirul-kalaam, Beirut, juz. 20, uk. 441.
  7. Muhaqqiqu Hilli, Sharaaiul-islaam, 1408 H, juz. 1, uk. 277.
  8. Shekhe Tousiy, Al-mabsout, 1387 H, juz. 1, uk. 297, Kikundi cha utafiti cha Muadham Maqaamu Rahbariy, Muntakhab manaasikil-hajji, cha mwaka 1426 H, uk. 59.
  9. Najafiy, Jawaahirul-kalaam, Beirut, juz. 20, uk. 441.
  10. Najafiy, Jawaahirul-kalaam, Beirut, juz. 20, uk. 441
  11. Najafiy, Jawaahirul-kalaam, Beirut, juz. 20, uk. 449.
  12. Muhaqqiqu Hilli, Sharaaiul-islaam, 1408 H, juz. 1, uk. 274.
  13. Mahmuudiy, Manaasikul-hajji, 1387 S, uk. 20.
  14. Guruhe pazvesh baath Muadham Maqaamu Rahbariy, Muntakhab manaasikil-hajji, 1426 H, uk.21.
  15. Muhaqqiqu Hilli, Sharaaiul-islaam, 1408 H, juz. 1, uk. 275.
  16. Muhaqqiqu Hilli, Sharaaiul-islaam, 1408 H, juz. 1, uk. 275-276.
  17. Muassasatu daairatul-ma'aarifil-fiqhil-islaami, Farhang fiqhi, 1392 H, juz. 5, uk. 488.
  18. Tazama: Shahidul-awwal, Ad-durusus-shar'iyah, 1417 H, juz. 1, uk. 337; Muhaqqiqu Hilli, Sharaaiul-islaam, 1408 H, juz. 1, uk. 276.
  19. Hurrul-aamuli, Wasaailus-shiah, 1409 H, juz. 14, uk. 302.
  20. Muassasatu daairatul-ma'aarifil-fiqhil-islaami, Farhang fiqhi, 1392 H, juz. 5, uk. 480.
  21. Muassasatu daairatul-ma'aarifil-fiqhil-islaami, Farhang fiqhi, 1392 H, juz. 5, uk. 485.
  22. Muassasatu daairatul-ma'aarifil-fiqhil-islaami, Farhang fiqhi, 1392 H, juz. 5, uk. 485.
  23. Muassasatu daairatul-ma'aarifil-fiqhil-islaami, Farhang fiqhi, 1392 H, juz. 5, uk. 485.

Vyanzo

  • Hurrul-aamuliy, Muhammad bin Hassan, Tafswiilu wasaailus-shiah ilaa tahswiili masaailis-shariah, Qom, Muassasatu Aalul-baiti, Chapa ya kwanza, mwaka 1409 H.
  • Shahidul-awwal, Muhammad bin Makkiy Al-aamuli, Ad-duruusus-shar'iyah fil-fiqhi imaamiyah, Qom, Nashru islaamiy, chapa ya pili, mwaka 1417 H.
  • Sheikh Tousiy, Muhammad bin Hassan, Al-mabsout fil-fiqhil-imamiyah, kilicho hakikiwa na kusahihishwa na Sayyid Muhammad Taqiy Kashfiy, Tehran, Al-maktabatul-murtadhawiyah li ihyaail-aathaaril-jaafariyah, chapa ya tatu, mwaka 1387 H.
  • Guruhe pazvesh baath Muadham Maqaamu Rahbariy, Muntakhab manaasikil-hajji, Tehran, Nashru masha'ar, chapa ya pili, mwaka 1426 H.
  • Muhaqqiqu Hiliy, Jaafar bin Hasan, Sharaaiul-islaam fii masaailil-halali wal-haraam, kilicho hakikiwa na kusahihishwa na Abdulhusein Muhammad Aliy baqqal, Qom, Ismaailiyaan, chapa ya pili, mwaka 1408 H.
  • Mahmoudiy, Muhammad ridhwaa, Manaasikul-hajji mutwaabiqi boo fataawaa Imamu Khomeini wa maraaji'i muadham taqlidi, Tehran, Nashru Mash'ar, chapa ya nne, mwaka 1387 S.
  • Muassasatu daairatul-ma'aarif fiqhi islaam, Farhaang fiqhi mtwaabiqi Madhhab Ahlil-baiti Alaihimus-salaam, Qom, Muassasatu daairatul-ma'aarif fiqhi islaam, chapa ya kwanza, mwaka 1392 S.
  • Najafiy, Muhammad Hassan, Jawaahirul-kalaam fii sharhi sharaai'il-islaam, Beirut, Daru Ihyaait-turaathil-arabi, chapa ya saba, 1404 S.