Nenda kwa yaliyomo

Sala ya Tawafu

Kutoka wikishia
Mahujaji wakiswali nyuma ya Maqam Ibrahim

Sala ya Tawafu (Kiarabu: صلاة الطواف) ni moja kati ya mambo ya wajibu katika ibada ya Hija na Umra. Sala hii ina rakaa mbili kama ilivyo Sala ya Alfajiri na baada ya kumaliza kufanya tawafu (kuzunguka Kaaba), Sala hii huswaliwa nyuma ya Maqam Ibrahim (jiwe lililoko kando ya Kaaba) . Sala ya Tawafu Nisaa inatofuatiana katika nia yake tu na Sala hii ya tawafu.


Historia

Kuifanya Maqam kuwa sehemu ya kuelekea ni hatua ambayo ina historia tangu zama za Ibrahim na Ismail mpaka katika zama za Mtume Muhammad (s.a.w.w)[1] na Qur’an tukufu pia imewatolea mwito Waislamu wa kuswali mahali hapo. Aya hiyo inasema: Na alipokuwa akisimama Ibrahim pafanyeni pawe pa kusalia.[2]


Namna ya kusali Sala ya Tawafu

Kila baada ya kukamilisha kufanya tawafu (kuzunguka Kaaba) ya wajibu, ni lazima kusali rakaa mbili za Sala ya tawafu kama ilivyo Sala ya Alfajiri na sio lazima kutoa sauti wakati wa kusoma alhamdu na sura.

Nia ya Sala hii inahusiana na tawafu: Baada ya kukamilisha Tawafu ya ziara nia ya Sala hii itakuwa Sala ya tawafu ya ziyara na baada ya kukamilisha Tawafu Nisaa, nia ya Sala hii itakuwa Sala ya tawafu Nisaa. Haipasi kuweko pengo na ucheleweshaji baina ya tawafu na Sala ya tawafu. Kwa maana kwamba, mara tu baada ya kukamilisha tawafu inapasa kusali Sala ya tawafu.[3]

Mahali pa kuisali Sala ya Tawafu

Sala ya Tawafu ya wajibu inapasa kusaliwa nyuma ya Maqam Ibrahim na karibu na eneo hilo takatifu bila ya kuwasumbua watu wengine.[4]


Kuhusiana na watu ambao kutokana na udhuru wanalazimika kufanya tawafu katika ghorofa ya pili lakini wanaweza kusali katika uwanja (eneo) wa Masjid al-Haram na nyuma ya Maqama Ibrahim, kuna hitilafu za kifat’wa baina ya wanazuoni.[5]

Sala ya tawafu ya mustahabu inaweza kuswaliwa sehemu yoyote ile katika Masjid al-Haram.[6]

Rejea

  1. Tabrasi, Majmam al-Bayan, 1379 H, juz. 1, uk. 203.
  2. Surat al-Baqarah, aya ya 125
  3. Manasik al-hajj, Mas'ale 790
  4. Manasik al-hajj, Mas'ale 796
  5. Manasik al-hajj, Mas'ale 2/800
  6. Al-wadhihu fi sharh al-uruwat al-uthqah, juz. 4, uk. 286

Vyanzo

  • Qur'an Kareem
  • Mahmoudy, Muhammad Ridhaa, Manasik al-hajj mutabiq fatawa'a Imam Khomeini wa marajii muudham taqlid, Tehran, Markaz tahqiq hajj baathe maqam muudham rahbary nashr mash'ar, chapa ya nne,1387 S.
  • Tabrasi, Fadhli bin Hassan, Majmau al-bayan, Beirut, Dar ihyau turath al-arabi, 1379 H.
  • Jawahir, Muhammad, Al-wadhihu fi sharh al-urwat al-uthqah, Qom, Al-arif lilmat'buat, 1436 H.