Nenda kwa yaliyomo

Umra ya Tamatui

Kutoka wikishia

Umra al-Tamatui ni katika aina za Umra ambayo hutekelezwa pamoja na Hajj al-Tamatui. Ibada ya Umra al-Tamatui ni mkabala wa Umra ya mufrad ambayo hutekelezwa kando (ikiwa pekee) na Hajj al-Tamatui. Umra al-Tamatui inaundwa na amali tano ambazo kwa utaratibu na mpangilio ni: Ihram, tawafu, sala ya tawafu, kufanya sa'ayi' baina ya swafa na mar'wa na taqsir (kupunguza nywele au kucha).

Umra

Makala asili: Umra

Umra ni mkusanyiko wa matendo ya kisheria kama Ihram, tawafu, kufanya sa'ayi baina ya swafa na marwa [1] ambayo hutekelezwa wakati wa kuzuru nyumba ya Mwenyezi Mungu. [2] Umra inagawanywa katika sehemu mbili: Umra al-Tamatui na Umra ya mufrad. [3] Umra al-Tamatui ni sehemu ya Hajj al-Tamatui na hufanywa pamoja nayo. [4] Umra al-Mufrada ni ibada ya kujitegemea na haifanywi pamoja na Hajj al-Tamatui. [5] Kwa mujibu wa fat'wa za mafakihi, kufanya Umra kama ilivyo Hija endapo masharti yatatimia ni wajibu mara moja katika kipindi cha umri wa mwanadamu [6] na kufanya zaidi ya mara moja ni mustahabu. ]7] Kwa maana kwamba, wajibu ni mara moja tu.

Matendo (Amali) ya Umra al-Tamatui

Umra al-Tamatui inaundwa na amali tano ambazo kwa utaratibu na mpangilio ni:

  1. Kufunga ihram miqati (moja ya maeneo matano ambapo hapo anayekwenda kuhiji anapaswa kufunga ihram hapo). [8] na iwe ni katika miezi ya Hija, [9] kwa namna ambayo amali za Umra hukamilika kabla ya adhuhuri ya siku ya Arafa. [10]
  2. Kufanya tawafu (kuzunguka Kaaba).
  3. Sala ya tawafu.
  4. Kufanya sa'ayi' baina ya swafa na mar'wa na taqsir (kupunguza nywele au kucha).
  5. Taqsir (kupunguza sehemu ya nywele au kucha). [11]

Tofauti yake na Umra al-Mufrada

Amali za Umra al-Tamatui zina tofauti na Umra ya mufrad. Tofauti hizi ni:

  • Katika Umra al-Tamatui kinyume na Umra al-Mufrada, hakuna amali za tawafu Nisaa na swala ya tawafu Nisaa.
  • Ihram ya Umra al-Tamatui inapaswa kuvaliwa katika miezi makhsusi ya Hija (Shawwal, Dhul-Qaadah na Dhul-Hija, yaani Mfunguo Mosi, Pili na Tatu); lakini ihram ya Umra al-Mufrada haina sharti hili.
  • Katika Umra al-Tamatui baada ya kumaliza kufanya sa'ayi baina swafa na mar'wa ni lazima kufanya taqsir (kupunguza kiwango fulani cha nywele au kucha); lakini katika Umra al-Mufradah kuna hiari baina ya kupunguza na kunyoa (kunyoa kipara). [12]
  • Katika Umra al-Tamatui ihram inapaswa kuvaliwa katika moja ya maeneo matano yanayojulikana kama mawaqit (vituo); lakini katika Umra al-Mufrada, jambo hili sio lazima, bali ihram inaweza kuvaliwa katika eneo la karibu zaidi nje ya haram. [13]

Vyanzo

  • Markaz-i Taḥqīqāt-i Ḥajj. Adʿīya wa ādāb al-ḥaramayn fī l-ʿumra al-mufrada. Tehran: Mashʿar, 1383 Sh.
  • Fāḍil Lankarānī, Muḥammad. Aḥkām-i ʿumra-yi mufrada. Eleventh edition. Qom: Intishārāt-i Amīr-i Qalam, 1426 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Fourth edition. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.