Tawwabin
- Makala hii inahusiana na kundi miongoni mwa Mashia ambalo lilianzisha harakati ya kulipiza kisasi damu ya Imamu Hussein (a.s). Ili kuangalia hatua na mambo waliyoyafanya soma makala ya Harakati ya Tawwabin.
Tawwabin (Kiarabu: التوّابون) (yenye maana ya wenye kutubia) ni kundi lililokuwa likiongozwa na Sulayman bin Sudar Khuzai ambalo mwaka 65 Hijiria lilianzisha harakati dhidi ya utawala wa Bani Umayyah kwa ajili ya kulipiza kisasi damu ya Imamu Hussein (a.s) na akthari yao waliuawa kishahidi katika eneo la Ayn al-Warda katika vita na jeshi la Ibn Ziyad. [1] Baadhi yao walituma barua hapo kabla walituma barua kwa Imamu Hussein (a.s) na kumualika aende Kufa na kwamba, watamhami, kumuunga mkono na kumsaidia; pamoja na hayo walimuacha Imamu Hussein peke yake na masahaba zake wachache katika tukio la Karbala. Kinyume na madai yao hawakumsaidia na kumnusuru Imamu Hussein (a.s). Baada ya tukio la Karbala walijutia hatua yao ya kumsaidia Imamu Hussein hivyo wakaamua kuanzisha harakati dhidi ya utawala wa Bani Umayyah kwa ajili ya kulipiza kisasi damu ya Imamu Hussein (a.s) na wakapata umaarufu kama Tawwabin. [2] Hii ilikuwa harakati ya kwanza ya Kishia baada ya tukio la Karbala. [3].
Inaelezwa kuwa, idadi ya kundi la Twwabin ilikuwa 4,000. Miongoni mwa waliokuwa viongozi wa Tawwabin ni Sulayman bin Surad, Rifa’ah bin Shaddad Bajali, Musayyib bin Najabah, Abdallah bin Sa’d Azadi na Abdallah bin Wal Taymi. Viongozi wote hao waliuawa shahidi katika harakati hiyo isipokuwa Rifa’ah. [5]