Nenda kwa yaliyomo

Ayn al-Warda

Kutoka wikishia
Ayn al-Warda

Ayn al-Warda (Kiarabu: عين الوردة ) ni eneo lilililopo katika kisiwa (eneo lililopo baina ya Mto Tigris na Mto Furat) [1] ambapo palitokea harakati ya Tawwabin. [2] Tawwabin ni kundi la watu wa Kufa ambalo lilikuwa likiongozwa na kamanda Sulayman bin Sudar Khuzai na lilianzisha harakati kwa ajili ya kulipiza kisasi cha damu ya Imamu Hussein (a.s) na kwa ajili ya kufidia kuzembea kwao katika kumsaidia na kumnusuru Imamu Hussein (a.s). Kundi hili lilianzisha harakati dhidi ya utawala wa Bani Abbas na liliuawa shahidi katika eneo hilo. [3]

Inaelezwa kuwa, Ayn al-Wardah ni moja ya mashukio baina ya Kufa na Damascus. [4] Eneo hili linajulikana pia kwa jina la Ra’as al-Ayn. [5] Ra’as al-Ayn ni eneo lililopo katika mkoa wa Hasakah kaskazini mashariki mwa Syria. [6]

Rejea

Vyanzo