Tawhidi Katika Ngazi ya Dhati
Tawhidi Katika Ngazi ya Dhati (Kiarabu: التوحيد الذاتي) ni mojawapo ya aina za tawhidi, inayomaanisha imani juu ya umoja asili, au upweke wa Mwenye Ezi Mungu katika ngazi ya dhati yake. Tawhidi Katika Ngazi ya Dhati katika istilahi za wanazuoni wa fani ya teolojia, humaanisha kwamba; Mwenye Ezi Mungu hana mshirika wala anayefanana naye; lakini kwa mujibu wa wanazuoni wengine, pia inamaanisha kuwa Dhati ya Mungu haikujengeka kwa vipengele vya aina yoyote ile, wala haiwezi kugawanyika kwa namna yoyote ile.
Aya kama vile «وَ لَم یَکُن لَه کُفواً أحَد» (Wala hakuna yeyote yule anayefanana naye.) Na «لیس کَمِثلِه شَیء» (Hakuna kitu kinacho fafana naye.) Hutafsiriwa kwa maana ya kukanusha uwepo wa kifani au mshirika. Aya isemayo: «قُلْ هُوَ اللّٰهُ أَحَد» (Sema: Yeye ni Mungu Mmoja.) Inachukuliwa kuwa na maana ya kukanusha uwepo wa mchanganyiko au sehemu yoyote ile ndani ya asili (Dhati) ya Mwenye Ezi Mungu.
Imamu Ali (a.s), katika barua yake kwa Imamu Hassan (a.s), alitoa hoja kuhusiana na kutokuwepo kwa mshirika wa Mwenye Ezi Mungu amesema: Kama Mwenye Ezi Mungu angekuwa na mshirika, basi bila shaka manabii wa mshirika wake wangekufikieni, na mngeliweza kuona athari za mamlaka na utawala wa mshirika huyo, na bila mngelipata welewe kuhusiana na kazi zake. Ila ni wazi kwamba manabii wote wamekuja wakihubiri kuhusiana na Mungu Mmoja tu.
Pia, kuna hoja kadhaa za kiakili zilizo wasilishwa katika vitabu vya elimu ya kalamu, ili kuthibitisha maana zote mbili husika za Tawhidi Katika Ngazi Dhati.
Nafasi
Tawhidi Katika Ngazi ya Dhati, ni mojawapo ya ngazi na aina za Tawhidi Nadharia [1] (ambayo ni kinyume cha Tawhidi Amali), [Maelezo 1] na inahisabiwa kuwa ndiyo msingi muhimu wa welewe wa dhaza mbali mbali za Kiislamu. Hii ni fikra inayotambulika kama ni moja ya dhana (fikra) za juu kabisa za binadamu pamoja na Uislamu kwa jumla. Kulingana na maelezo ya Murtadha Mutahhari, dhana hii imeshamiri na kunawiri mno ndani madhehebu ya Kishia. [2] Katika elimu ya falsafa ya Kiislamu, Tawhidi Katika Ngazi ya Dhati pia inajulikana kama ni "Tawhidi au Upwekesha Katika Ngazi ya Wajibu Al-Wujuud' (Mwepo Awajibikaye Kuwepo). [3] Baadhi ya watafiti wanaamini kwamba kadri mtu anavyopata welewa wa Tawhidi Katika Ngazi ya Dhati, ndivyo anavyoweza kuielewa vyema Tawhidi Katika Ngazi ya Matendo (Tawhid fi Al-af’al) na Tawhidi Katika Ngazi ya Matendo (Tawhid fi Al-Sifati). Haiwezekani kwa mcha-Mungu mwenye kufungamana na Mola wake, aweze kuifikia Tawhidi Katika Ngazi ya Matendo kabla ya kuielewa Tawhidi Katika Ngazi Dhati. Bila shaka yule anayefikia daraja ya Tawhidi Katika Ngazi ya Matendo (Tawhid fi Al-af’al) huwa tayari amepata mabadiliko ndani ya dhati yake, bila hata ya yeye mwenyewe kujijua, hali ambayo humwezesha kupata ufahamu wa Tawhidi Katika Ngazi ya Dhati kwa kiwango fulani. [4]
Semantiki (Tafiti za Kilugha)
Tawhidi Katika Ngazi ya ki-kiini au Dhati ya Mungu, kama inavyotumiwa na wataalamu wa fani ya theolojia, inamaanisha kwamba; Mwenye Ezi Mungu ni mmoja, Halingana na mwengine wala hakuna chochote kile kanachofanana Naye, wala hana mshirika. [5] Murtadha Mutahhari anasema kwamba; Tawhidi Katika Ngazi ya ki-kiini au Dhati ya Mungu, hali maalumu ya kuwa na ufahamu pamoja na kuwa na imani juu ya upweke wa Dhaati ya Mwenye Ezi Mungu. [6] Kinyume cha Tawhidi Katika Ngazi ya ki-kiini (Dhati ya Mungu) ni shirk katika ngazi ya ki-kiini (Dati ta Mwenye Ezi mungu), imani ambayo hupelekea mtu kutoka katika dini ya Uislamu na hatimae kuandamwa na vifungu vya sheria vyenye kuhusiana na masuala ya shirki. [7]
Maana Nyingine za Tawhidi Katika Ngazi ya Dhati
Mara nyingine Tawhidi Katika Ngazi ya Dhati hutumika kwa maana pana zaidi, ambapo ibara hii yenye maana ya; kukosa mwenza na mfano, pia hujumuisha mchujuko wa Dhati ya Mungu, yaani, kufutilia mbali aina zote za mchanganyiko au nyongeza fulani ndani ya Dhati ya Mwenye Ezi Mungu. Kulingana na maana hii, Tawhidi Katika Ngazi ya Dhati, itakuwa imegawika katika maana mbili zifuatazo:
- Mwenye Ezi Mungu ni mmoja na wa kipekee, hana mshirika wala kinacho fanana Naye; maana hii hujulikana kwa jina la "Tawhidi au upwekeshaji wa Dhati ya Mungu kwa kuichuja na Dhati hiyo kutokana na aina yoyote ila ya idadi."
- Mungu ni mmoja na wa kipekee, na amepwekeka kwa aina zote za upweke; yaani, hana vigao wala hana mchanganyiko wa vipengele vya nje (vya kimaada) wala vya akili vifikirikavyo. Ngazi hii upwekesheaji, inajulikana kwa jina la Tawhidi Ahadiyyun, yaani Tawhidi ichujayo kila kinachoweza fikiraka na kuhisika, iwe kwa njia ya kiakili au kupitia hisia za kimwili. [8] Abdullah Jawadi Amuli, mwanafalsafa na mfasiri wa Qur’ani wa upande wa madhehebu ya Shia, anasema kwamba; Mwenye Ezi Mungu ni mmoja na wa kipekee. Tunaposema ni Mmoja, tunamaanisha kwamaba, Yeye hana mshirika wala mfano, na tunaposema ni wa kipekee tunamaanisha kwamba Yeye ni mpweke asiye na aina yoyote ile ya vigao. [9] Katika istilahi ya wanatheolojia, umoja huu unajulikana kama ni Wahdatu Haqq, kwa maana ya umoja wa haki na wa kweli" wenye maana ya kwamba; Yeye hana mwingiliano au mchanganyiko wa aina yoyote ile. [10]
Imeelezwa ya kwamba; Aya isemayo: «وَ لَم یَکُن لَه کُفواً أحَد» Na wala hakuna yeyote anayefanana Naye pamoja na Aya isemayo: «لیس کَمِثلِه شَیء» Hakuna kitu kinachofanana Naye”, zinaashiria maana ya kwanza ya Tawhidi Katika Ngazi ya Dhati, yaani zinaashiria kukataa mfano na mshirika. Na Aya isemayo: «قُلْ هُوَ اللّٰهُ أَحَد» Sema, Yeye ni Mungu mmoja tu", inahusiana na maana ya pili ya Tawhidi, yaani, inakataa kuwepo kwa aina yoyote ile ya vigao na mchanganyiko ndani ya Dhati Yake. [13]
Sababu Juu ya Upweke wa Dhati
Wanatheojia na wanafalsafa wa Kiislamu wamekuwa na mitazamo madhubuti katika kukataa dhana ya kuwepo kwa mwenza wa Mungu, na pia kukataa wazo lolote linalohusisha muundo au sehemu fulani fulani katika uwepo wa Mungu. [14] Hoja kuu zipingazo dhana hizo ni kama ifuatavyo:
Sababu za Kutokuwa na Mfano au Mshirika kwa Mungu
Wanazuoni wa Kiislamu wamethibitisha suala la Mungu kutokuwa na mfano wala mshirika kupitia hoja ya uhitaji wa kuwepo Mwepo Awajibikaye Kuwepo (Wajibu Al-wujud). Wakisimamisha hoja hii wamesema: Ikiwa kuna Mwepo Awajibikaye Kuwepo mwingine zaidi ya Mwenye Ezi Mungu, basi wawepo wawili hawa, ama wanatakuwa na tofauti au hawatakuwa na tofauti. Ikiwa hawatakuwa na tofauti yoyote kati yao, basi hapatakuwa na maana ya uwili kati yao, na natija yake ikatakuwa ni kimoja, na haitawezekana kujenga dhana ya kuwepo kwa waungu wawili, jambo ambalo litapelekea kuthibitisha kwamba; Mungu ni Mmoja tu na hana mshirika; lakini ikiwa kutakuwa na tofauti kati yao, basi hiyo itasababisha kutengeneza muundo au sehemu mbali mbali, jambo ambalo linapingana na dhana ya kutangulia kwa Mwepo Awajibikaye Kuwepo kabla ya kuja kwa kitu chengine (viumbe). Kwani muundo wa kupitia vitu mbali mbali unahusiana tu na viumbe vilivyopo ndani ya ulimwengu wa uwezekano wa kuwepo (kuumbwa), ambavyo havina sifa ya Mwepo Awajibikaye Kuwepo. Hii ni kwa kuwa tayari kiakili imeshathibitika kwamba Mwepo Awajibikaye Kuwepo, hawezi kuwa amejengeka kupitia sehemu au vigao tofauti. Kwa sababu iwapo atakuwa amejengeka kupitia vigao au sehemu tofauti, bado tutakuwa na swali la kuuliza kwamba; Je, ni nani kati ya sehemu au vigao hivyo kilichotangulia kuwepo au chenye kumhitajia mwengine katika uwepo wake. [15]
Katika barua kwa Imamu Hassan (a.s), Imamu Ali (a.s) akitoa hoja kuhusiana na umoja (upweke) wa Mwenye Ezi Mungu, alisema kwamba; Kama Mungu angekuwa na mshirika, basi bila shaka mitume wa washirika wake wangeonekana wangelikufikieni na kukuleteeni ujumbe wao, pia mgeliweza kushuhudia uwezo na nguvu za utawala wa washirika (Miungu) hao, na bila shaka mgeliweza kuelewa baadhi ya matendo pamoja na baadhi ya sifa zao. [16] Akitoa ufafanuzi juu ya hoja hii, mwanachuoni na mfasiri wa Kishia Nasir Makarim Shirazi anaeleza akisema kwamba; Kama Mwenye Ezi Mungu angelikuwa na mshirika, basi bila shaka mshirika huyo, angelikuwa na hekima maalumu, hekima ambayo ingelimpelekea yeye kuwajulisha waja wake kuhusiana na uwepo wake, na bila shaka angetoa maagizo yake kupitia mitume maalumu. Ila lililo wazi ni kwamba, mitume wote wamekuwa wakiwalingania wanadamu kumwabudu Mungu mmoja pekee. Aidha, kama kungelikuwa na Mungu mwengine, basi dalili za nguvu na utawala wake zingelidhihiri ulimwenguni. Lakini, lililo dhahiri ulimwenguni humu, ni kule ulimwengu huu kuwa na mfumo mmoja thabiti, jambo ambalo linaashiria umoja wa Mungu, na kwamba Yeye hana mshirika. [17]
Muhammad-Taqi Misbah-Yazdi, akinukuu hoja za wanafalsafa wa Kiislamu, naye pia amethibitisha dhana ya umoja (upweke) wa Dhati ya Mwenye Ezi Mungu, kupitia hoja ijulikanayo kwa jina la (Al-Burhan al-Siddiqin). Yeye ameitambua hoja hii kuwa ndiyo hoja makini ya hali ya juu kabisa, na yenye uthibitisho kamili zaidi wa umoja wa Dhati ya Mwenye Ezi Mungu. [18]
Hoja ya Kukanusha Uwepo wa Muungano au Ziada Ndani ya Uungu wa Mungu
Hoja ya kukataa uwepo wa muungano au ongezeko kinyume na uhalisia wa Dhati ya Mungu, imeelezewa kama ifwatavyo: Kila kitu chenye muungano huwa na sifa ya uhitaji juu ya sehemu zilizo ungana nacho, na kila sehemu kati ya sehemu hizo, ni tofauti na uhalisia wa kitu kizima kinachoundwa kupitia sehemu hizo. Zaidi ya hayo, kutegemea kitu kingine ni sifa ya viumbe vyenye sifa ya uwepo kwa njia ya uwezekano (sio kwanjia kama ile ya Mwepo Awajibikaye Kuwepo), hali ya kwamba Mungu halisi ni yule Mwepo Awajibikaye Kuwepo. Kwa hivyo, aina yoyote ya muungano -iwe wa nje (kimwili) au wa dhana (kidhahania)- haiwezi kuwa ni sifa ya Mwenye Ezi Mungu asiye na dosari. [19]
Maelezo
- ↑ Tawhidi ya ki-nadharia inahusiana na uwanja wa maarifa na imani, yenye ya kumtaka mwanadamu kuamini upweke wa Mwenye Ezi Mungu. Kinyume chake, ni tawhidi ya kimatendo (Tauhidi Amali), ifanyayo kazi katika uwanja wa matendo ya mwanadamu. (Mutahhari, Majmue Aathar, Mwaka 2011, Juz. 26, Uk. 97.)