Nenda kwa yaliyomo

Tawhid Al-Sifaat

Kutoka wikishia

Tawhid Al-Sifaat (Kiarabu: التوحيد الصفاتي) ni aina ya Tawhidi katika ngazi ya Sifa, ikimaanisha imani ya umoja uliopo baina ya Sifa za Mwenyezi Mungu zenyewe kwa zenyewe, pamoja umoja wa Sifa hizo na Dhati yake (uwepo wake). Kwa mujibu wa nadharia ya Tawhid Al-Sifsati, ni kwamba; Sifa za Mwenyezi Mungu haziakisi zaidi ya kitu kimoja tu (Dhati ya Mwenyezi Mungu), na kwamba utofauti uliopo baina yake, ni utofauti wa welewa wa dhana za kila moja kati yake tu. Mtazamo huu, unaojulikana kama ni mtazamo wa «Sifat ‘Ainu Al-dhat» (uwepo pweke kati ya Dhati na Sifa), ni mtazamo wa wanafalsafa na wanatheolojia wote wa upande wa madhehebu ya Shia Imamiyyah pamoja na baadhi ya makundi ya Ahlu-Sunna. Kwa upande mwingine, Ashaira na Maturidiyya, kutoka upande wa madhehebu ya kitheolojia ya Ahlu-Sunna, wanaamini kwamba Sifa na Dhati za Mwenyezi Mungu ni vitu viwili tofauti, na kwamba Sifa hizo ni za tangu kwa jinsi ya utangu wa Mungu ulivyo.

Imani katika utofauti wa Sifa na Dhati imetambuliwa kama ni «Shirk Al-Sifati», yaani shirki katika ngazi ya Sifa za Mungu; lakini wanazuoni wamesemwa kwamba; shirki katika ngazi hii si jambo hatari sana bali ni Shirki Khafiyy (shirki iliyo jificha). Hii ni kuwa Tawhid Sifati ni suala tete linalohitaji umakini wa hali ya juu kabisa katika welewa wa dhana yake, na kwamba dhana hiyo si dhana idirikiwayo kila mtu, bali hudirikiwa na kutafitiwa na wanazuoni wa theolojia. Hivyo Shirk katika ngazi ya Sifa haiwezi kumtoa mtu katika Uislamu.

Wanatheolojia wa Kishia wametumia hoja mbali mbali za vitabuni (maandiko) pamoja na kiakili katika kuthibitisha Tawhid Sifati. Kwa mujibu wa maelezo ya Jafar Subhani, mtaalamu wa teolojia wa Kishia, ni kwamba; hoja ya kuthibitisha ukweli huu inaweza kufikiwa kwa kuelewa ya kwamba: kujiepusha na imani uwili kati ya Sifa na Dhati ni moja ya njia ya kuepuka imani ya kumfanya Mungu kuwa ni mhitaji wa mwengine au kitu chengine, na kiuhalisia hakuna mwengine au chengine baada yake ila huwa ni kiumbe chake, na ni wazi kwamba Mungu haihitaji chochote kutoka kwa viumbe wake. Pia, Miongoni mwa hoja za maandiko, ni maneno ya Imamu Ali (a.s) katika hotuba ya kwanza ya Nahjul Balagha, ambapo kukanusha uwili kati ya Sifa na Dhati yake Allah, nakasema kwamba; kumvua Mungu kutokana na Sifa mbali mbali ndiyo ukamilifu wa kumpwekesha Mwenye Ezi Mungu Mtukufu.

Nafasi na Uchambuzi Wake

Tawhidi katika ngazi ya Sifa: Ni miongoni mwa misingi mikuu ya mafunzo ya Kiislamu, na ni moja ya dhana muhiumu zaidi katika nyanja za tafakuri za wanadamu. Dhana hii imeonekana kukuwa na kunawiri kwa kasi kubwa mno miongoni mwa madhehebu mbali mbali, hasa katika madhehebu ya Shia. [1] Tawhidi katika ngazi ya Sifa za Mwenye Ezi Mungu, inahusiana na imani ya kwamba; kakuna uwili wala wingi kati ya Sifa za Dhati za Mwenye Ezi Mungu na kiini cha Dhati yake (Mungu mwenyewe), na pia Sifa zote hizo ni moja tu, zisizo na wingi au muundo wowote ule mwenza katika kiini au Dhati ya Mungu mwenyewe. [2] Kwa msingi huu, Sifa za Mungu hazina mifano au miundo mwenza inayotofautiana na Dhati ya Mungu mwenyewe; bali zote dhana tofauti zinazoeleweka kwa maana mbali mbali katika akili ya mwanadamu, huwa ni zenye uhalisia mmoja tu usio na uwili wala mchambuko ndani yake, nao ni ile Dhati ya Mwenye Ezi Mungu. [3] Kwa mujibu wa mtazamo huu, Sifa zote zinazohusishwa na Mwenye Ezi Mungu kama vile; elimu, nguvu na uhai, ni sawa na Dhati ya Mungu mweneyewe, haidhuru kila moja huwa inatofautiana na nyengine kidhana na namna welewa wake katika akili ya mwanadamu. [4]

Kwa mujibu wa mtazamo wa Abdullah Jawadi Amuli, mwanafalsafa na faqihi wa Shia, ni kwamba; maana kuto kuwa na uwili wala mchambuko wowote ule kati ya Sifa na Dhati ya Mwenye Ezi Mungu ni kwamba; ukamilifu wa Dhati ya Mungu ni pweke, yaani hakijajumuishwa na kitu chochote kile ndani yake. hii ina maana ya kwamba, Sifa zote kamilifu zipo kwenye Dhati yake bila ya kuwepo ongezeko lolote lile ndani ya Dhati yake Alla Subhanahu wa Ta’ala. Jambo ambalo ni tofauti kwa upande wa viumbe, kwani Sifa zao huwa ni nyongeza iyongezekayo kwenye dahati zao, na zinaweza kuvuliwa na kutenganishwa na zao hizo. [5]

Ali Rabani Gulpayegani, mtafiti wa elimu ya kalam (akida), anasema kwamba; mada asili ijadiliwayo katika Tawhidi (upwekeshaji) katika ngazi ya Sifa, ni vile jinsi ya Sifa asilia -za Mungu- zinavyohusiana na Dhati ya Mwenye Ezi Mungu mwenyewe. Akitoa ufafanuzi juu ya hili, anasema kwamba; Imani ya kuamini kuwa Sifa ni sawa na Dhati ya Mungu ndiyo Tawhidi (upwekeshaji) sahihi katika ngazi ya Sifa, na imani ya Sifa Zake kuwa ni tofauti na Dhati Yake, ni moja ya aina za shirki kwenye ngazi ya Sifa. [6]

Mitazamo ya madhehebu Mbalimbali Kuhusiana na Tawhidi Katika Ngazi ya Sifa

Wanafalsafa wote wa Kiislamu pamoja na wanatheolojia wa madhehebu ya Shia Ithnaasharia [7] wakiwemo baadhi ya wafuasi wa madhehebu ya Kisunni, [8] wana imani juu ya umoja (kutowepo uwili) kati ya Sifa na Dhati ya Mwenye Ezi Mungu. Kwa upande wa pili, waumini wa Kiashairiyya [9] na Matuuridiyya [10] ambao ni miongoni mwa wafuasi wa madhehebu ya Kisunni, wanaamini ya kwamba; Sifa za Allah zinatofautiana na Dhati yake katika namna ya uwepo wake, ila wanasema kwamba, Sifa hizo ni za tangu kwa utangu wa Dhati yake Subhanahu wa Ta’ala. Kuna khitilafu za kimitazamo kuhusiana na imani khasa ya kundi (madhehebu) la Mu’utazila. Shahidi Murtadhaa Mutahhari na Jawadi Amuli wanasema kwamba; Mu’utazila wanamtakasa Mungu kutokana na Sifa mbali mbali, [11] yaani wanakataa kuwepo kwa Sifa za Mwenye Ezi Mungu. Ila Ali Rabbani Gulpeigani, ambaye ni mtafiti wa fani ya Tawhidi (akida), anasema kwamba; Mu’utazila ni sawa na Shia Ithnaasharia, wao pia wanaamini juu ya umoja kati ya Sifa na Dhati ya Mwenye Ezi Mungu. [12]

Jawad Amuli akitoa maoni yake juu ya mada hii anasema kwamba; Kwa kuwa suala la upwekeshaji wa Mwenye Ezi Mungu katika ngazi ya Sifa ni miongoni mwa mwa masuala nyeti yanayohitaji umakini ndani yake, na si mada ielewekayo kiundani na watu wkawaida, bali ni moja ya dhana maalumu ijadiliwayo na wataalamu fani ya theolojia, basi si tatizo kwa watu wa kawaida kuwa na aina fulani ya mitelezo ndani ya imani hii. Hivyo basi mitelezo inayohusiana na upwekeshaji Mungu katika ngazi ya Sifa, ni mitelezo ya shirki zilizo kifichoni, ambazo hazimfanyi mtu awe nje ya Uislamu kutokana na kule yeye kuto kuwa makini katika upwekesha wake Mungu katika ngazi hii. [13]

Hoja

Wanazuoni wa Shia wametoa hoja na vielelezo kadhaa vya kuthibitisha Tawhidi na upweke wa Mwenye Ezi Mungu alionao katika ngazi ya Sifa zake, hoja ambazo zinathibitisha moja kwa moja ya kwamba; hakuna wingi wala uwili kati ya Sifa na Dhati ya Mwenye Ezi Mungu Subhanahu wa Ta’ala. Baadhi ya hoja zilizotolewa na wanazuoni wa Kishia, ni hoja za kiakili huku nyengine zikiwa ni ithibathi za maandiko yatokayo katika vyanzo vya Hadithi. Miongoni mwa hoja zao ni kama ifuatavyo:

Hoja za Kiakili

Ja'afar Subhani, mtaalamu wa fani ya theolojia ya Kishia, akielezea moja ya hoja za kiakili za Tawhidi kwenye ngazi ya Sifa anasema: Upweke wa ngazi ya sifa, ambao ni upweke wa Mungu ulioko baina ya Dhati na Sifa zake, una nia ya kumpwekesha na kumtakasa Mwenye Ezi Mungu, kwa maana ya kwamba; Yeye hahitajii kitu chengine chochote kile katika ngazi ya Sifa zake. Lakini, kinyume chake, ile imani ya kuamini kwamba; Sifa si sawa na Dhati ya Yake! Humaanisha kwamba; Mungu ni mhitaji wa vitu vyengine tofauti ambavyo ni vyenza vijengavo uwili au wingi kati yao na Dhati yake. Katika hali hiyo, ile imani ya kwamba Mungu ana elimu au uwezo, itathibiti kupitia kitengo maalumu cha msaada wa maarifa na uwezo ambavyo si kiini cha Dhati yake. Kwa hiyo, kwa kuwa Mwenye Ezi Mungu ni mkwasi mwenye kujitosheleza ambaye hana haja ya kitu chengine, bila shaka Sifa zake haziwezi kuwa ni nyongeza zilizopo katika Dhati yake, bali Sifa zake ndiyo kiini cha Dhati yake. [14]

Maelezo ya Muhammad-Taqi Misbah-Yazdi na Abdullah Jawadi Amuli kuhusiana na dhana hii ni kwamba: Ikiwa kila moja kati ya sifa za Mungu itakuwa na dhihiriko tofauti, basi haiwezi kuwa nje ya hali mbili: Ima uwepo dhihiriko la kila moja utakuwa ndani ya Dhati ya Mungu, ambapo hii itamaanisha kwamba Dhati ya Mungu imeundwa kupitia sehemu tofauti. Bila shaka hii itakuwa inapingana na umoja wa Dhati ya Allah. Au uwepo wao utakuwa upo nje ya Dhati ya Mungu. Katika hali hii, ima sifa hizo zichukuliwe kuwa ni za lazima na zisizohitaji muumba, jambo ambalo litamaanisha kuwepo kwa Dhati kadhaa, jambao ambali litaishia katika ushirikina, au zichukuliwe kuwa ni Sifa yumkinifu ila si za lazima ambazo zimeumbwa na Mungu mwenyewe. Matokeo ya hili ni kwamba asili ya Mungu, ambayo kwa mujibu wa nadharia yetu kwanza ilikuwa haina Sifa hizo, itaonesha kwa Dhati ya Mungu imeziumba Sifa hizo kisha kujipamba nazo. Hali hii pia haiwezekani; kwa sababu haiwezekani muumba asilia awe haina ukamilifu unaopatikana ndani ya viumbe vyake, ambavyo yeye ndiye sababu wao kuwa na sifa hizo kamilifu. Kwa kukanusha na kubatilika kwa nadharia zote hizi, ndiko kunakozaa na kuthibitisha nadharia ya umoja kati ya Sifa na Dhati ya Mungu. [15]

Hoja Kutoka Kwenye Maandiko ya Hadithi

Kwa mujibu wa Muhammad-Taqi Mesbah-Yazdi, mwanafalsafa na mfasiri wa Kishia, ni kwamba; umoja upwekesha katika ngazi ya Sifa umewasilishwa na Hadithi kwa maana «kumtakasa Mungu tokana Sifa mbali mbali». Katika hotuba ya kwanza ya Nahj al-Balagha, imenukuliwa kutoka kwa Imamu Ali (a.s), akisema: «Na ukamilifu wa upwekesha Allah, ni kumtakasa, na ukamilifu wa kumtakasa ni kukana na kumvua sifa zote (zilizo nje ya Dhati)». Ayatullah Subhani ameihisbu kauli hii kuwa ni uthibitisho kamili wa umoja kati ya Sifa na Dhati yake Subhanahu wa Ta’ala. [18]

Allamah Majlisi amesema kwamba; Hadithi nyingi zinazozungumzia Sifa za Mungu zinadokeza juu ya kukana ziada ya Sifa juu ya Dhati; hata hivyo, hazitoi maelezo ya kina kuhusiana na umoja wa Sifa na Dhati ya Mwenye Ezi Mungu. [19] Allamah Tabatabai ameihisabu kauli hii kuwa ya kushangaza, na akasema kwamba; bali Hadithi hizo zinaonyesha wazi umoja wa Sifa na Dahti ya Mungu. [20]

Rejea

Vyanzo