Muwalat

Kutoka wikishia

Muwālāt / mfuatanisho (kiarabu: الموالاة) ni hali ya kuweko mfuatanisho au hali ya kufuatanisha baina ya kitu na kitu na kutokuweko pengo na hali ya kuchelewesha. Kuchunga muwālāt (hali ya kufuatanisha) katika udhu na Swala ni sharti la kusihi kwavyo. Hata hivyo katika Ghusli (kuoga) si wajibu kuzingatia hilo. Baadhi ya mafakihi (wanazuoni wa elimu ya fikihi) wanasema kuwa, ni lazima pia kuchunga mfuatanisho baina ya vipengee vya kauli ya kisheria ya mikataba yaani Ijab (pendekezo) na Qabul (kukubali pendekezo). Kigezo cha kuainisha mfuatanisho ni Urf (ada na mazoea).

Maana

Muwālāt ni kufanya vitu kwa kufuatanisha na bila kuchelewesha baina ya kitendo kimoja na kingine kinachofuata.[1] Katika istilahi ya fikihi inaelezwa kuwa ni kufanya kitendo kinachofuata bila ya kukichelewesha katika vipengee vya Ibada kama Swala, Udhu na kadhalika.[2] Wanazuoni wameliachia suala la kuainisha muwalaat (mfuatanisho) kwa ada na mazoea katika jamii.[3]

Maeneo ambayo ni wajibu

Kuchunga na kuzingatia muwālāt (mfuatanisho) ni moja ya masharti ya kusihi baadhi ya ibada kama vile:

  • Swala: Vipengee vya swala kama vile Qiraa (kisomo), Rukuu na Sujudu vinapaswa kutekelezwa kwa kufuatanisha na bila ya kuchelewesha. Kutochunga mfuatanisho kwa namna ambayo kwa mtazamo wa ada na mazoea katika jamii ielezwe kwamba, mhusika haswali, hilo linabatilisha swala.[4] Hata hivyo kurefusha rukuu na Sijda au kusoma sura ndefu katika swala hilo halivurugi hali ya mfuatanisho.[5]
  • Udhu: Wakati wa kutia udhu, haipaswi kuweko pengo baina ya kuosha na kupangusa viungo vya udhu, kwa namna ambayo wakati wa kuosha au kupangusa kiungo miongoni mwa viungo vya udhu, kiungo cha kabla yake kiwe kimekauka.[6]
  • Adhana na Iqama: Kwa mujibu wa Fatuwa za wanazuoni wa Fiqh wa Kishia ni kwamba, miongoni mwa masharti ya kusihi adhana (kuadhini) na iqama (kukimu Swala) ni kuchungwa na kuzingatiwa muwālāt (hali ya kufuatanisha) baina ya vipengee vyake.[7] Kwa maana kwamba, mwenye kuadhini au kukimu Swala anapaswa kusoma kipengee cha adhana au iqama kinachofuata mara tu baada ya kukamilisha kipengee cha kabla yake bila kuchelewa.
  • Mikataba ya Kidini (Uqud Shar’i): Kwa mujibu wa fatuwa za baadhi ya mafaqihi ni kuwa, ni jambo la lazima kuchunga na kuzingatia mfuatanisho baina ya vipengee vya mikataba ya kidini. Kama vile kuuza na kununua au ndoa na miamala ambayo ina vipengee viwili ambapo kuna kauli maalumu ambayo inapaswa kutamkwa baina ya wawili hao yaani mwenye kutangaza na mwenye kukubali ambavyo ni ijab (pendekezo) na Qabul (kukubali pendekezo).[8]

Muwālāt katika ghusl (josho)

Feidh Kashani anasema, kwa mujibu wa fatuwa za wanazuoni wa Shia Imamia, kuchunga na kuzingatia muwālāt (mfuatanisho) katika ghusl sio jambo la wajibu; [9], hata hivyo wametambua kuchunga hilo kuwa ni mustahabu. [10]

Rejea

  1. Ibn Manẓūr, Lisān al-ʿArab, juz. 15, uk. 412, chini ya neno "Wali"
  2. Baṣmajī, Muʿjam muṣṭalaḥāt al-fāz al-fiqh al-Islāmī, uk. 556.
  3. Kāshif al-Ghitāʾ, Suʾāl wa jawāb, p. 76; Banīhāshimī Khomeinī, Tawḍīḥ al-masāʾil-i marajiʿ, juz. 1, uk. 602, suala 1114.
  4. Banīhāshimī Khomeinī, Tawḍīḥ al-masāʾil-i marajiʿ, juz. 1, uk. 603, issue 1116.
  5. Banīhāshimī Khomeinī, Tawḍīḥ al-masāʾil-i marajiʿ, juz. 1, uk. 173, issue 283-284.
  6. Ṭabāṭabāʾī Yazdī, al-ʿUrwat al-wuthqā, juz. 2, uk. 425.
  7. Fayḍ al-Kāshānī, Muʿtaṣam al-shīʿa fī aḥkām al-sharīʿa, juz. 1, uk. 423.
  8. Sheikh Anṣārī, Kitāb Makāsib wa al-bayʿ wa al-khiyārāt, juz. 3, uk. 157-161.

Vyanzo

  • Baṣmajī, Sāʾir. Muʿjam muṣṭalaḥāt al-fāz al-fiqh al-Islāmī. Damascus: Ṣafaḥāt li-Dirasāt al-Nashr, 2009.
  • Banīhāshimī Khomeinī, Sayyid Muḥammad Ḥasan. Tawḍīḥ al-masāʾil-i marajiʿ. Tehran: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī affiliated to Jāmiʿa-yi Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmīyya-yi Qom, 1383 Sh.
  • Fayḍ al-Kāshānī, Mullā Muḥsin. Muʿtaṣam al-shīʿa fī aḥkām al-sharīʿa. Tehran: Madrasa Ālī Shahīd Muṭaharī, 1429 AH.
  • Ḥakīm, Muḥsin. Mustamsak al-ʿUrwat al-wuthqā. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d].
  • Ibn Manẓūr, Muḥammad b. Mukarram. Lisān al-ʿArab. Edited by Aḥmad Fāris. Beirut: Dār al-Fikr li-Ṭibāʿa, 1414 AH.
  • Kāshif al-Ghitāʾ, Muḥammad Ḥusayn. Suʾāl wa jawāb. Muʾassisa Kāshif al-Ghitāʾ, [n.d].
  • Mishkinī, ʿAlī. Muṣṭalaḥāt al-fiqh. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1428 AH.
  • Sheikh Anṣārī, Murtaḍā b. Muḥammad Amīn. Kitāb Makāsib wa al-bayʿ wa al-khiyārāt. Qom: Kungira-yi Jahānī Buzurgdāsht-i Sheikh Aʿzam Anṣārī, 1415 AH.
  • Yazdī, Sayyid Muḥammad Kāẓim al-. Al-ʿUrwat al-wuthqā. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1419 AH.