Sirdabu takatifu

Kutoka wikishia
Sirdabu takatifu

Sirdabu takatifu au Sardabu ya Ghaiba (Kiarabu: سرداب الغيبة أو سرداب المقدسة) ilioko chini ya nyumba ya Imamu Hassan Askari (a.s), iko kaskazini magharibi mwa Haram ya Askariyyaini huko Samarra, Iraq. Utakatifu wa mahali hapa unaoaminiwa na Waislamu wa madhehebu ya Mashia, unatokana na ukweli wa kwamba; Eneo hilo lilikuwa ndio makazi ya Imamu Hadi (a.s), Imamu Askari (a.s), na Imamu wa Zama (Mahdi) (a.j.f.s).

Baadhi ya waandishi wa Sunni wanawatuhumu Mashia kwa kuamini kwamba; Sirdabu ya Ghaiba ndio mahali anapoishi Imamu Mahdi (a.j.f.s) katika kipidi chake cha ghaiba (maisha ya mafichoni), na pia itakuwa ndio mahali pa kudhihirika kwake katika kipindi cha kudhihiri kwake. Hata hivyo, katika vyanzo vya Shia hakuna kitu kama hicho, bali Shia wanaamini kwamba Imamu wa Zama (Mahdi) (a.j.f.s), atadhihirika huko Makka.

Jengo la kwanza lililojengwa kama ni Sardabu linarudi katika kipindi cha utawala wa Bani Abbas, na baada ya hapo likakarabatiwa na kutengenezwa upya mara kadhaa pamoja na majengo ya makaburi ya ya Askariyyain katika vipindi tofauti.

Hadhi na Umuhimu Wake

Sirdabu, ambayo ni basement (tabaka ya chini kabisa) ya nyumba ya Imam Askari (a.s) ilikuwapo huko mjini Samarra. [1] Utakatifu wa mahali hapa unatokana na uhusiano wake na Maimamu watoharifu wa Kishia; [2] kwa sababu ilikuwa ni mahali pa kuishi kwa Imamu Hadi (a.s), Imamu Askari (a.s), na Imamu Mahdi (a.j.f.s). [3] Sirdabu iko takriban mita 15 kutoka makaburi ya Maimamu wawili waitwao -kiumaarufu- Askariyyain (a.s) [4] na iko katika upande wa kaskazini-magharibi mwa makaburi ya Askariyyain (a.s). [5]

Kulingana na Sheikh Abbas Qummi, mwanahistoria wa Shia (aliyefariki 1359 Hijiria), kupewa mahali hapa jina la Sirdabu ya Ghaibah, kunahusiana na kipindi kilicho fuata baadaye na siyo kipindi cha uwepo wa Imamu Mahdi (a.j.f.s), na sababu yake haijafafanuliwa katika vitabu vilivyoandikwa kuhusina Imamu Mahdi (a.j.f.s). [6]

Je, Imamu Mahdi (a.s) Atadhihiri Akitokea Handakini (Sirdabu)?

Kuba la Masjid al-Sahib (a.j.f.s) ambao umejengwa juu ya pango takatifu.

Baadhi ya waandishi wa Sunni, ikiwa ni pamoja na Yaqut al-Hamawi katika Mu’ujam al-Buldani na Ibnu Hajar al-Haitamiy katika kitabu cha Al-Sawa’iq al-Muhriqah, wamedai kwamba; Mashia wanaamini kuwa Imamu Mahdi (a.j.f.s) amejificha katika Sirdabu (basement), na atadhihiri tena kutoka katika Sirdabu hiyo. [7] Pia waandishi hawa, wamezungumzia kuhusu kikundi cha Mashia ambacho hunasimama karibu na Sirdabu hiyo na kuomba Imamu Mahdi (a.j.f.s) adhihiri hali wakiwa wamesimama katika eneo hilo. [8]

Kulingana na Zabihullah Mahallati, mwandishi wa Shia wa karne ya 15 Hijria katika Ma’athiru al-Kubra fi Tarikh Samarra, ameandika akisema kuwa; madai hayo si sahihi, kwa sababu wanazuoni wa Shia wanakubaliana na wana mawafikiano ya kwamba, Imamu Mahdi (a.j.f.s) atadhihiri kutokea Makka. [9] Vilevile, kulingana na maelezo ya Lutfullah Safi Gulpaigani, mmoja wa mafaqihi na mujitahid wa Shia, ni kwamba; taarifa hizo zimetengenezwa kwa nia ya kujnga uadui dhidi ya Shia, kuwakingiusha watu kutoka kwenye mwelekeo wa Ahlul-Bait na kuwaelekeza kwenye mwelekeo wa Bani Umayya na maadui wa familia ya Utume (s.a.w.w). [10] Kulingana na maeleo ya Safi Gulpaigani, ni kwamba; hakuna hata mtu mmoja kutoka upande wa Shia aliyedai kwamba Imamu amejificha katika Sirdabu ya Samarra, bali vitabu na hadithi za Shia zinakanusha madai hayo. [11]

Sayyid Sadruddin Sadru, mmoja wa mafaqihi wa Shia (aliyefariki mwaka 1373 Huijiria), alieleza kwamba; Matamshi kama hayo kutoka kwa Ibnu Hajar Haithami yanatokana na kule yeye kuto kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusiana na Iraq pamoja na Shia wa eneo hilo; kwa sababu, kulingana na maelezo ya Sayyid Sadruddin Sadru, Ibn Hajar hakuwahi kutoka katika mji wa Hijazi, wala hajawahi kuiona kwa macho yake Samarra. [12] Katika muktadha huo huo, Muhaddith Nouri, [13] Sayyid Muhsin Amin, [14] Sayyid Murtadha Askari, [15] Sayyid Hadi Khosroshahi, [16] na Ibrahim Amini, [17] pia wamekanusha kwamba; Imamu Mahdi (a.j.f.s) amejificha katika Sirdabu takatifu, na kwamba atadhihiri tena kupitia mahali hapo.

Handaki au Shimo la Maficho

Katika Sirdabu (basement), kuna shimo kinachojulikana kama «Handaki au Shimo la Ghaiba» [18] ambalo, kulingana na Sheikh Abbas Qummi, baadhi ya wafanya ziara wanao zuru Sirdabu hiyo, walikuwa na tabia ya kuchota udongo kutoka kwenye hodhi lililokuwa ni sehemu ya wudhuu ya Imamu Askari na Imamu Hadi kwa nia ya kupata baraka (kutabaruku) kupitia udongo huo, mwishowe tabia hiyo ikapelekea eneo hilo kujulikana kama ni handaki la Ghaiba. [19]

Pia Sheikh Abbas Qumi amenukuu kutoka kwa Muhaqqiq Nouri akisema kwamba; baadhi ya watumishi wanaoshughulikia Sirdabu (Handaki Takatifu) hulitambulisha hisho na handaki hilo kama ni handaki la Imamu Mahdi (a.j.f.s). Watumishi hao hufanya hivyo kutokana na tamaa ya kujipatia ya kidunia. Wao walikuwa na kawaida ya kuchota udongo wa mahali hapo na kuwapatia wafanyaji ziara wanao tembelea aeneo hilo na kuchukua kiasi fulani cha fedha kutoka kwo, nao wakawa wanbeba udongo huo na kwenda nao makwao kwa nia ya kujipatia baraka kutokana na udongo huo mtakatifu! Sheikh al-Iraqiyyina (mkuu wa Waarabu wa Iraq) alijaribu kuzuia kitendo hicho kwa kujaza dongo kwenye handaki au shimo hilo na kufunga mlango wa kungilia shimoni humo, lakini baadaye watumishi hao walilifungua tena. [20]

Ramani na Tarehe Kujengwa Kwake

Hitilafu kutengeneza picha ndogo:
Kuingia kwa Sardabu kabla ya uharibifu wa Haram ya Askariyein

Sirdabu imeungwa ikiwa na chumba kimoja cha pembe sita na vyumba viwili vya mraba, kimo kikubwa na kingine kidogo, ambavyo vinaunganishwa na koridoo moja refu. [21] Chumba cha mraba kikubwa kinajulikana kama ni sehemu ya ibada ya wanaume, na chumba cha mraba kidogo kinajulikana kama ni sehemu ya ibada ya wanawake. [22] Njia ya kuingia na kutoka kwenye Sirdabu ni kupitia ngazi zinazoishia kwenye chumba cha pembe sita. 23] Pia, juu ya Sirdabu kuna msikiti uliojengwa zamani unaojulikana kama ni Masjidwa Sahib (a.f) ambao una kuba lililopambwa kwa tiles. [24]

Hali ya Sardabu takatifu baada ya kujengwa upya

Kulingana na maelezo ya Muhadith Nouri (aliyefariki mwaka 1320 Hijria), ni kwamba; Al-Nasir li-Dini Llahi, mmoja wa Makhalifa wa Banu Abbas, alijenga Sirdabu hiyo mnamo mwaka wa 606 Hijria, na aliandika kwenye jiwe la msingi la ujenzi huo majina ya watu watakatifu kumi na wanne, yaani Maimamu 12, bwana Mtume (s.a.w.w) pamoja na bibi Fatima (a.s). [25] Hata hivyo, inasemekana kwamba kabla ya hapo, Nasir al-Dawlah kutoka familia ya Hamdanian alikuwa ndiye wa kwanza aliye jenga nyumba ya Imamu Hadi (a.s) mwaka wa 333 Hijria, na manmo mwaka wa 337 Hijria, Mu’ayyadu al-Dawlah kutoka familia ya Buwahi akaja kukamilisha ujenzi huo. [26]

Jengo la Sirdabu pamoja na Haram ya Imamu Hadi na Imamu Askari (a.s), yote kwa pamoja yalikarabatiwa na kujengwa upya katika vipindi tofauti; [27] kwa mfano, mwaka wa 1202 Hijiria, Ahmad Khan Denbali alipofanya matengenezo na ukarabati wa Haram ya Imamu Hadi na Imamu Askari (a.s), alijenga uwanja maalumu kwa ajili ya Sirdabu na alitengeneza njia mpya ya kuelekea katika Sirdabu hiyo. [28] Ndani ya Sirdabu kuna athari za sanaa za usanifu wa mbao, kazi za sanaa ya usanifu wa tiles, na sanaa nyingine za usanifu mwenge mbali mbali. [29]

Sirdabu (basement) hii pia iliharibiwa na kukarabatiwa tena baada ya uharibifu uliofanya katika Haramu za Imamu Hadi na Imamu Askari (a.s), kupitia milipuko wa mabomu ya kigaidi ya Mawahabi mnamo tarehe 3 Esfand mwaka 1384 Shamsia na 23 Khordad 1386 Shamsia. [30]

Maudhui zinazo fungamana