Sidanat al-Kaaba

Kutoka wikishia

Sidanat al-Kaaba (Kiarabu: سدانة الكعبة) ina maana ya kutoa huduma na kusimamia mambo yanayohusiana na Kaaba kama vile kuhifadh na kutunzai funguo, kufunga na kufungua Kaaba, kupokewa wafanyaziara wa nyumba ya Mwenyezi Mungu, kusafisha na kubadilisha kitambaa cha kufunika Kaaba na kadhalika. Kabla ya Uislamu ufunguo wa Kaaba ulikuwa ukishikiliwa na kutunzwa na Bani Shaiba. Baada ya Fat’h Makka, Mtume (s.a.w.w) aliacha mamlaka ya kushikilia ufunguo wa Kaaba kwa Othman bin Talha aliyekuwa akitunza funguo wakati huo na kwa amri ya Mtume jukumu hili likaachwa katika mamkala ya familia hiyo.

Kwa mujibu wa vyanzo, Abbas ami yake Mtume, aliona kuwa yeye ni mbora kuliko wengine kwa sababu ya jukumu la kutoa huduma ya maji kwa mahujaji. Familia ya Shaiba, nayo ambayo ilikuwa ikisimamia masuala yanayohusiana na Al-Kaaba, pia alijihesabu kuwa ni bora. Lakini Imam Ali (a.s) aliona kuwa yeye ni mbora wao kwa sababu aliamini kabla ya wengine na kisha akahama na kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa mujibu wa watafiti wa Kiislamu, baada ya tukio hili, Aya ya 19 ya Surat Tawba iliteremka na kuchukuliwa imani na jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni bora kuliko majukumu kuhusu Al-Kaaba. Kwa mujibu wa Tabari, mfasiri wa Kisunni, katika Qur’ani, Mwenyezi Mungu aliwakemea watu waliojisifu na kujifaharisha kutokana na kutoa huduma ya maji kwa Mahujaji na kusimamia masuala yanayohusiana na Kaaba na kuiona imani na jihadi kuwa ni bora kuliko majukumu ya kusimamia na kuendesha Kaaba.

Utambulisho

Sidanat al-Kaaba ina maana ya kutoa huduma na kusimamia mambo yanayohusiana na Kaaba [1] kama vile kuhifadhi ufunguo, kufunga na kufungua mlango wa Kaaba, [2] kupokewa wafanyaziara wa nyumba ya Mwenyezi Mungu, kusafisha na kubadilisha kitambaa cha kufunika Kaaba na kadhalika. [3]

Kufuli na funguo ya Kaaba

Jukumu la kuhifadhi ufunguo wa Kaaba pia liko mikononi mwa watu wanaosimamia masuala ya Kaaba. [4] Historia ya jukumu la kusimamia Kaaba inarejea nyuma huko kale ambapo baadhi wanasema kuwa, ilikuweko tangu katika zama za Nabii Ismail (a.s). [5] Baada ya kukombolewa Makka (Fat’h Makka), Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliidhinisha na kuthibitisha majukumu mawili tu na kuwaacha waliokuwa wakisimamia bila ya kuwabadilisha. Moja ni usimamuzi wa Kaaba na jingine ni kutoa huduma ya maji kwa mahujaji. [6]

Kuhifadhi ufunguo wa Kaaba; jukumu la familia ya Bani Shaiba

Kabla ya Uislamu jukumu la kuhifadhi ufunguo wa Kaaba lilikuwa mikononi mwa Bani shaiba. [7] Baada ya kukombolewa Makka (Fat’h Makka), Mtume (s.a.w.w) alichukua ufunguo wa Kaaba kutoka kwa Othman bin Talha, mshikaji na mhifadhi wa funguo ya Kaaba wakati huo, na akaingia kwenye Al-Kaaba. Kisha akamrudishia ufunguo na kusema kwamba, ufunguo wa Al-Kaaba ubaki mikononi mwa watu wa familia hii na hawatachukua ufunguo kutoka kwao isipokuwa watu madhalimu. [8] Ni kwa msinguo huo ndioa maana, jukumu la kushika funguo za Al-Kaaba likabakia kuwa mikononi mwa watu wa familia hii. [9]

Katika baadhi ya riwaya, imeelezwa kwamba, baada ya Mtume (s.a.w.w) kuchukua ufunguo kutoka kwa Othman bin Talha, alitaka kumpa ami yake Abbas, ambapo ikashuka Aya hii: Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. [10], hivyo Mtume akamrejeshea Othman bin Talha ufunguo huo wa Kaaba. [11]

Mnamo mwaka wa 1392 Hijria Shamsia, watu kutoka Bani Shaiba waliilalamikia serikali ya Saudi Arabia na kutangaza kwamba wamenyimwa na kuondolewa mambo mengi ambayo yalikuwa yakipewa familia hii katika historia kutokana na kusimamia Kaaba. [12]

Imani na jihadi ni bora kuliko kusimamia Kaaba

Kwa mujibu wa Tabari, mfasiri wa Kisunni, katika Qur’ani, Mwenyezi Mungu aliwakemea watu waliojisifu na kujifaharisha kutokana na kutoa huduma ya maji kwa Mahujaji na kusimamia masuala yanayohusiana na Kaaba na kuiona imani na jihadi kuwa ni bora kuliko majukumu ya Kaaba. [13]

Kwa mujibu wa vyanzo, siku moja Abbas, ami yake Mtume, aliona kuwa yeye ni bora kuliko wengine kwa sababu ya jukumu la kuwahudumia kwa maji mahujaji. Familia ya Shaiba, ambao ilikuwa na jukumu la kusimamia Kaaba (Sedanat al-Kaaba [14]), ikaijiona kuwa bora. Hamza akajihesabu kuwa mbora kwa sababu ya jukumu la ujenzi wa Al-Kaaba, na Ali (a.s.) pia akaona yeye ni mbora kuliko wao kwa sababu ya kuamini kabla ya wengine na kisha kuhama na kupigana jihadi. Aya ya kunywesha maji Mahujaji ikashusha:

أَجَعَلْتُمْ سِقَايَةَ الْحَاجِّ وَعِمَارَةَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ كَمَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ وَجَاهَدَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ لاَ يَسْتَوُونَ عِندَ اللَّهِ وَاللَّهُ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ
Je, mnafanya kuwanywesha maji Mahujaji na kuamirisha Msikiti Mtakatifu ni sawa na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.[15]

Inaelezwa kuwa baada ya tukio hilo la kila mtu kuona yeye ndiye bora kati ya tuliowataja, Mwenyezi Mungu akashusha Aya hii [16] na kuitaja imani na kupigana katika jihadi kuwa ni jambo kubwa na bora zaidi ya majukumu ya Kaaba. [17]

Katika baadhi ya nukuu Ali, Ja’afar na Hamza wametajwa kuwa watu ambao imani yao na kupigana kwao jihadi kuwa bora kuliko majukumu yanayohusiana na Kaaba. [18]