Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s)
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) likiwa na akronimi ya ABNA lina mfungamano na Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) na lilizinduliwa rasmi Machi 2005 na linaakisi kwa lugha mbalimbali habari zinaohusiana na Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Shirika hili la habari linaendesha shughuli zake kwa lugha 26 na limefanikiwa kupata tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo bora ya Shirika la Habari katika Maonyesho ya Kimataifa ya Magazeti ya Iran.
Umuhimu na malengo
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (ABNA) liliasisiwa kwa ajili ya kueneza habari zinazohusiana na madhehebu ya Shia na matukio ya Mashia ambapo limekuwa na nafasi muhimu katika hilo. [1]
Shirika hili kwa kutangaza na kuakisi habari ya kupigwa marufuku harakati za Mashia nchini Gambia liliandaa uwanja wa kuweko mazungumzo baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Gambia kwa ajili ya kuikinaisha serikali ya Banjul ili itambue rasmi harakati za Mashia katika nchi hiyo ya Kiafrika. [2] Mnamo mwaka 2023, Shirika la Habari la ABNA liliamua kuunda Muungano wa Kimataifa wa Wanaharakati wa vyombo vya habari na waandishi wa habari kwa mhimili wa Ahlul-Bayt (a.s). [3]
Mtandao wa ABNA ulichujwa nchini Saudi Arabia na Bahrain kufuatia mwamko wa Kiislamu katika nchi za Kiarabu mwaka wa 2010. [4]
Kurasa za habari za kiutamaduni
Shirika la Habari la ABNA lina kurasa za habari za kidini na kiutamaduni. Anuani ya baadhi ya kurasa hizo ni: Masuala ya Qur’an, hadithi, maisha ya Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt (a.s), hatua kwa hatua na al-Wilaya na itikadi juu ya Imamu Mahdi, hijabu, uwahabi, kuijua dini na maktaba zingine…nk. [5]
Historia fupi ya lugha
Awali Shirika la Habari la ABNA lilikuwa na anuani ya “Shia News” na lilianza shughuli zake 14 Machi 2005. Lilipoanza lilikuwa na lugha tatu za Kifarsi, Kiarabu na Kiingereza. Miaka mitatu baadaye, shirika hili la habari lilibadilishwa jina na kuwa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) na lilizunduliwa na aliyekuwa Rais wa wakati huo wa Iran. [6]
Lugha
Mwaka 1393 Hijria Shamsia Shirika la Habari Ahlul-Bayt (ABNA) likawa likifanya shughuli zake kwa lugha 19 za Kiingereza, Kiarabu, Kifaransa, Kifarsi, Kihispania, Kirusi, Kituruki Istanbuli, Kituruki Azari, Kiurdu, Kibangali, Kimalayo, Kihindi, Kiindonesia, Kiswahili, Kimyanmar, Kibosnia na Kihausa. [7] Katika miaka iliyofuata wigo wa lugha uliponuka na kufikia lugha 26. [8]
Tuzo
Shirika la Habari la ABNA limeshiriki katika maonyesho na matamasha mbalimbali ya kimataifa, kitaifa na kieneo na kufanikiwa kutunukiwa tuzo tofauti na baadhi yazo ni:
- Shirika bora la habari mwaka 2012 katika Maonyesho ya Kimataifa ya Magazeti na Mashirika ya Habari Novemba 2012. [9]
- Shirika bora la Habari katika Kongamano la kwanza la kimataifa la filamu la Ishraq Juni 2012. [10]
- Kupata tuzo katika Kongamano la 6 la Kimataifa la Vyombo vya Habari vya Dijitali Januari 2013. [11]
- Shirika bora la Habari katika Kongamnao la Kitaifa la Filamu la Ishraq Novemba 2013. [12]
Vyanzo
- Nyenzo za makala hii zimechukuliwa kutoka About ABNA, AhlulBayt News Agency.