Shawdhab Mawla Shakir

Kutoka wikishia

Shawdhab Mawla Shakir ni mmoja wa mashahidi wa Karbala na mpelekaji barua (mesenja) za Muslim bin Aqil kwa Imamu Hussein (a.s). Yeye alikuja Karbala pamoja na msafara wa Imamu Hussein (a.s) akitokea Makka. Aliuawa shahidi siku ya Ashura baada ya Handhala bin As’ad al-Shibami. Jina lake limekuja katika ziyara za Rajabiyah za Imam Hussein (a.s) na Ziyarat al-Shuhadaa ambamo ndani yake mashahidi wa Karbala wanatolewa salamu.

Kiapo na agano la kabila la Shakir

Katika vyanzo vya historia na vya hadithi, Shawdhab ametajwa kwa neno Mawla Shakir.[1] Kwa mujibu wa Muhaddith Nouri, Shakir ni kaumu ya Yemen kutoka kabila la Hamdan, ambalo nasaba yake ilikuwa ikiishia kwa Shakir bin Rabi'a bin Malik. Shawdhab Mauwal alikuwa amekula kiapo na agano na kabila la Abis halikuwa mtumwa wa Abis.[2] Pamoja na hayo, Muhammad Mahdi Shamsuddin katika Ansar al-Hussein[3] amemchukulia kuwa mtumwa wa Shakir bin Abi Shabibi Shakir. Muhaddith Qumi anasema katika kitabu chake cha Nafs al-Mahmum kwamba pengine nafasi ya Shawdhab ni ya juu zaidi kuliko nafasi ya Abis kwa sababu walisema haki kuhusiana na yeye. Shawdhab alikuwa mstari wa mbele katika shule na maktaba ya Ushia.[4] Kwa mujibu wa Muhammad bin Tahir Samawi: Alikuwa mmoja wa Mashia wakubwa na mmoja wa wahifadhi wa hadithi, na alikuwa akinukuu hadith kutoka kwa Imamu Ali (a.s).[5]

Kuuawa shahidi katika tukio la Karbala

Shawdhab, akifuatana na Abis bin Abi Shabib Shakiri, alileta barua ya Muslim bin Aqeel kutoka Kufa hadi Makka na kuifikisha kwa Imamu Hussein (a.s) na akatoka Makka pamoja na Imam hadi Karbala.[6] Aliuawa shahidi siku ya Ashura baada ya Handhala bin As’ad al-Shibami.[7] Katika vyanzo, kumenukuliwa mazungumzo baina yake na Abis, ambayo yanahusu kwenda kwake katika uwanja wa vita kabla ya Abis na yanaashiria utetezi na himaya yake kwa Imamu Hussein (a.s).[8]

Katika Zirayarat Rajabiyya ya Imamu Hussein (a.s), ambamo ndani yake wametajwa mashahidi wa Karbala, Shawdhab anasalimiwa kwa ibara isemayo: ((السَّلَامُ عَلَی سُوَیدٍ مَوْلَی شَاکر ))[9]Kadhalika katika Ziyarat al-Shuhadaa ambamo ndani yake mashahidi wa Karbala wametolewa salamu, anatajwa kwa jina la Shawdhab Maulma Shakir.[10]

Rejea

  1. Tazama: Tabari, Tarikh al-umam wal-muluk, 1387 H, juz. 5, uk.443; Sheikh Mufid, Al-irshad, 1413 H, juz. 2, uk. 105; Tusi, Rijalu al-tusi, 1373 s, uk. 101.
  2. Nury, Luuluu wa marjan, 1388 S, uk. 222.
  3. Shams al-Dīn, Anṣār al-Ḥusayn (a.s), uk. 79.
  4. Qummi, Nafsi al-mahmum, Al-nashr: Maktaba al-haydaria, uk 574.
  5. Samāwī, Ibṣār al-ʿayn, uk. 117.
  6. Samāwī, Ibṣār al-ʿayn, uk. 117.
  7. Mufīd, al-Irshād, juz. 2, uk. 105; Ṭabrisī, Iʿlām al-warā, uk. 246; Ibn Athīr, al-Kāmil, juz. 4, uk. 73.
  8. Tabari, Tarikh al-umam wal-muluk, 1387 H, uk. 443-444.
  9. Ibnu Tausi, Iqbal al-amal, 1376 S, juz. 3, uk. 346.
  10. Ibnu Tausi, Iqbal al-amal, 1376 S, juz. 3, uk. 79.

Vyanzo

  • Ibn Ṭāwūs, ʿAlī b. Mūsā. Iqbāl al-aʿmāl. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1367 Sh.
  • Ibn al-Athīr al-Jazarī, ʿAlī b. Abī l-Karam. Al-Kāmil fī l-tārīkh. Beirut: Dār Ṣādir, 1385 AH-1965.
  • Khwārizmī, Muwaffaq b. Aḥmad al-. Maqtal al-Ḥusayn. Edited by Shaykh Muḥammad al-Samāwī. Qom: Maktabat al-Mufīd, [n.d].
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: Muʾassisa al-Wafaʾ, 1404 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿalā l-ʿibād. Qom: Kungira-yi Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Nūrī, Mīrzā Ḥusayn al-. Luʾ Luʾ wa marjān dar sharṭ pilla-yi awwal wa duwwum-i minbar-i rawḍakhānān. Tehran: Nashr-i Āfāq, 1388 sh.
  • Samāwī, Muḥammad b. Ṭāhir al-. Ibṣār al-ʿayn fī anṣār al-Ḥusayn (a). Edited by Muḥammad Jaʿfar Ṭabasī. [n.p]. Markaz al-Dirāsāt al-Islāmīyya li Ḥars al-Thawra, 1377 Sh/1419 AH.
  • Shams al-Dīn, Muḥammad Mahdī. Anṣār al-Ḥusayn (a). Tehran: Muʾassisa-yi al-Biʿtha, 1407 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥaasn al-. Al-Rijāl. Qom: Jamāʿa-yi Mudarrisīn, 1415 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Iʿlām al-warā bi-aʿlām al-hudā. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, [n.d].
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-Ṭabarī. Edited by Muḥammad Abu l-faḍl Ibrāhīm. Beirut: Dar al-Turāth, 1387 AH.