Sariyya

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na vita ambavyo Mtume (s.a.w.w) hakushiriki. Kwa maana kwamba, vita ambavyo Mtume hakushiriki vinajulikana kwa jina la Sariyya. Ili kujua kuhusiana na vita vyote vya Mtume angalia makala ya vita vya Mtume (s.a.w.w).

Sariyya au Ba’ath (Kiarabu: السرية أو البَعْث) ni vita vilivyopiganwa na Waislamu katika zama za uhai wa Bwana Mtume (s.a.w.w) bila ya Mtume kushiriki katika vita hivyo. Bali vilipiganwa kwa uongozi na ukamanda wa mmoja wa masahaba wa Mtume (s.a.w.w). Lengo kuu la Sariyya lilikuwa ni kutangaza utayari na nguvu za Waislamu. Malengo mengine ya kando na yasio malengo makuu ya vita hivyo yalikuwa ni kama vile tablighi, kujihami, kushambulia na kukusanya taarifa za adui.

Katika hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Hadi (a.s) idadi ya Sariyya (vita vilivyopiganwa bila ya Mtume kushiriki) zimetajwa kuwa ni 55. Pamoja na hayo, katika vitabu vya historia, idadi ya vita hivyo imetajwa kuwa ni 35, 48 na 66. Kwa mujibu wa Sheikh Ja’far Sobhani, baadhi ya vita hivyo havijahesabiwa na kujumuishwa kutokana na idadi ndogo ya watu. Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana, kumejitokeza hitilafu katika kuhesabu na kuorodhesha idadi ya vita hivyo.

Sariyya ya Hamza bin Abdul-Muttalib katika pwani ya Bahari Nyekundu, Sariyya ya Ubaydah bin Harith katika jangwa la Rabigh na Sariyya ya Sa’d bin Abi Waqqas kuelekea Kharrar zimeripotiwa kuwa Sariyya za mwanzo. Idadi ya wapiganaji wa Kiislamu wa Sariyya hizi ilikuwa ikilingana na nguvu na idadi ya vikosi vya adui na vilevile kwa kuzingatia majukumu tofauti na wakati mwingine kulikuwa kukitumwa watu kadhaa kwa ajili ya vita fulani na baadhi ya wakati kulikuwa kukitumwa zaidi ya watu 1,000.

Maana na Sababu Kuitwa Jina Hilo

Katika vitabu vya historia ya Uislamu vita vya Mtume vinagawanywa katika makundi makundi mawili vya Ghaz’wa na Sariyya. [1] Katika vita ambavyo Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akishiriki na kuwa kamanda na kiongozi wa vita hivyo moja kwa moja vinatambulika kwa jina la “Ghaz’wa” na vile vita ambavyo Mtume hakushiriki na badaka yake alimteua mmoja wa masahaba zake kuwa kamanda na kiongozi na kisha kuwatuma sehemu fulani kupigana vita, vinafahamika kwa jina la «Sariyya» au «Ba’ath». [2] Pamoja na hayo, baadhi ya wahakiki wanaamini kuwa, fasili na maana illiyotolewa kwa ajili ya Ghaz’wa na Sariyya sio makini; bali Ghaz’wa ni vita vya Mtume ambavyo vilifanyika kwa uwazi vikiwa na wapiganaji wengi; lakini vita vya Mtume vilivyofanyika kwa sura ya kujificha vikiwa na wapiganaji wachache vinafahamika kwa jina la «Sariyya». [3] Fasili na maana hizi mbili hazina tofauti katika misdaqi na kielelezo cha Ghaz’wa na Sariyya; kwani kwa mujibu wa maana ya pili, Mtume hakuwa akishiriki katika operesheni za kivita ambazo zilikuwa zikifanyika kwa kushirikisha kundi ndogo la wapiganaji zikiwa na lengo kama la kukusanya taarifa. [4] Ibn Athir, mwandishi wa kitabu cha al-Nihayah Fi Gharib al-Hadith Wal-Athar, vita hivi vimeitwa Sariyya kwa kuzingatia kwamba, waliokuwa wakienda katika vita hivi walikuwa ni wale tu walioteuliwa; kwa sababu neno «sariy» maana yake ni bora au yenye thamani. [5]

Malengo ya Sariyya

Inaelezwa kuwa lengo kuu la Sariyya lilikuwa ni kuonyesha utayarifu na nguvu za Waislamu. [6] Sayyid Ja’far Murtadha al-Amili mwandishin wa kitabu cha al-Sahih min sirat al-nabiy al-A’dham anasema kuwa, vita vya Sariyya vya Mtume vilikuwa vikifanyika kwa sababu mbili tu:

  1. Kufikisha ujumbe wa Uislamu.
  2. Kuvuruga mkusanyiko wa wanaotaka kufanya fitina na ambao walikuwa wakipanga kuwashambulia Waislamu. [7]

Pamoja na hayo baadhi ya wahakiki wamegawanya Sarriya za Mtume katika makundi manne: [8]

  1. Sariyya za kufanya tablighi, kama Sariyya ya Raji’i [9] ambayo ilikuwa ikifanyika kwa siri au kwa dhahiri kwa kuzingatia mazingira; [10]
  2. Sariyya za kujihami ambazo zilifanyika kwa lengo la kulinda na kuhami maslahi ya Waislamu au kwa ajili ya kukabiliana na baadhi ya hujuma na mashambulio ya adui. [11]
  3. Sariyya za kushambulia, kama Sariyya ya Hamza bin Abdul-Muttalib [12] ambayo ilifanyika kwa kuchukua hatua kabla ya adui na kikawaida hilo lilikuwa likifanyika katika ardhi zilizo mbali. [13]
  4. Sariyya ya kukusanya taarifa, kama Sariyya ya Abdallah bin Jahsh [14] ambayo ilikuwa ikifanyika kwa sura ya siri na lengo lake ni kukusanya taarifa za watu au eneo alipo adui. [15]

Mtume (s.a.w.w) alikuwa ametoa amri kwamba, katika kila Sarriya (vita vilivyopiganwa bila ya Mtume kuweko) endapo Waislamu watapata ushindi basi wasimsake na kumfuatilia adui. [16] Mchakato wa maamuzi na namna ya kufanyika na kutekelezwa vita hivyo (Sarriya) ulikuwa chini ya uangalizi na usimamizi wa Mtume na masahaba zake wa karibu. [17] Mtume (s.a.w.w) akiwa na lengo la kumchagua kamanda wa kuongoza Sariyya alikuwa akizingatia na kutoa umuhimu kwa sifa kama ushujaa na kuwa na weledi wa mbinu za kijeshi. [18]

Takwimu

Makala asili: Orodha ya vita vya Mtume (s.a.w.w)

Kwa mujibu wa riwaya iliyonukuliwa katika kitabu cha Tadhkirat al-Khwawas kutoka kwa Imamu Hadi (a.s), majimui ya Sariyya (vita vilivyopiganwa pasi na ya Mtume kuhudhuria) ni 55. [19] Waandishi wa historia wamenukuu idadi tofauti tofauti kuhusiana na Sariyya hizi: Muhammad Ibrahim Ayati amesema katika kitabu chake cha «Tarikh Payambar Islam» kwamba, idadi ya vita hivyo ilikuwa 82. [20] Ali bin Hussein Mas’oudi katika kitabu chake cha Muruj al-Dhahabi amenukuu kwamba, baadhi ya wanahistioria wamesema Sariyya hizo zilikuwa 35, amenukuu kutoka kwa Muhammab bin Jarir Tabari kwamba, vita hivyo vilikuwa 48 na amenukuu kutoka kwa baadhi ya wanahistoria wengine kwamba, vita hivyo vilikuwa 66. [21] Fadhl bin Hassan Tabarsi anaandika katika kitabu cha I’lam al-Wara kwamba, zilikuwa Sariyya 36. [22] Sheikh Ja’far Sobhani mwandishi wa kitabu cha «Forogh Abadiyat» anasema kuwa, baadhi ya Sariyya kutokana na kuwa na idadi ndogo ya watu hazijahesabiwa, na ni kutokana na sababu hiyo ndio maana kumejitokeza tofauti katika idadi. [23] Kwa mujibu wa Muhammad bin Omar Waqidi, mwandishi wa historia wa karne ya pili Hijria, Sariyya za Hamza bin Abdul-Muttalib na Ubaydah bin Harith na Sariyya ya Sa’ad bin Abi Waqqas ni Sariyya za kwanza kabisa zilizotokea katika mwaka wa kwanza Hijria. [24]

Idadi ya wapiganaji katika Sariyya ilikuwa ikitofautiana kulingana na nguvu na idadi ya wapiganaji wa adui na vilevile kwa kuzingatia aina ya majukumu ambapo katika baadhi ya Sariyya walikuwa wakitumwa watu kadhaa na baadhi ya zingine wapiganaji 3,000 kama katika Sariyya ya Osamah bin Zayd. [25] Watar mwandishi wa kitabu cha «Fann al-Harb al-Islami Fi A’had al-Rasul» (s.a.w.w) anasema: Hasara lilizopata jeshi la Uislamu katika vita ambavyo Mtume hakushiriki (Sariyya) ni kubwa zaidi ya vita vingine. [26] Sababu ya hilo ni kutokuwa na tahadhari baadhi ya makamanda, adui kuwa na nguvu na kutofanikiwa asili ya kushtukiza. [27] Kadhalika katika baadhi ya Sariyya ambazo zilifanyika kwa lengo la kulingania Uislamu, kutokana na kutochukuliwa tahadhari zilipelekea kupatikana hasara kubwa; kiasi kwamba, katika baadhi ya vita hivyo, wapiganaji wote wa jeshi la Uislamu waliuawa. [28] Akthari ya Sariyya zilitokea katika miaka ya awali ya Hijria jirani na mji wa Madina. [29].


Tarehe Jina Idadi ya Waislamu Kamanda Idadi ya maadui Kamanda Mahali Matokeo
2/624 Ramadhan Hamza bin 'Abd al-Muttalib 30 kutoka kwa Muhajirin Hamza bin 'Abd al-Muttalib Wapiganaji wenye farasi 300 Abu Jahl bin Hisham 'Is Hakukuwa na vita
2/624 Shawwal 'Ubayda bin Harith bin 'Abd al-Muttalib 60 au 80 kutoka kwa Muhajirin 'Ubayda bin Harith Wapiganaji wenye farasi 200 & watembea kwa miguu 'Ikrama bin Abi Jahl Thaniyya al-mara Mshale mmoja tu ulirushwa na Sa'd b. Abi Waqqas
2/624 Dhu l-Qa'da Sa'd bin Abi Waqqas 8 kutoka kwa Muhajirin Sa'd b. Waqqas Kharrar Kurejea.
2/624 Rajab 'Abd Allah bin Jahsh 8 au 11 kutoka kwa Muhajirin 'Abd Allah b. Jahsh 4 'Amr bin al-Hadrami Nakhla 'Amr bin al-Hadrami aliuwawa and wawili wengine walikamatwa mateka na baadhi ya vitu kukamatwa kama ngawira.
2/624 Ramadhan 'Umayr bin 'Adi 1 'Asma' bint. Marwan 'Asma' bt. Marwan aliuwawa.
2/624 Shawwal Salim bin 'Umayr 1 Abu 'Afak Abu 'Afak aliuwawa.
3/624 Rabi' I Muhammad bin Maslama 4 Muhammad bin Muslima Ka'b bin Ashraf Ka'b bin Ashraf aliuwawa.
3/624 Jumada II Zayd bin Haritha Wapiganaji 100 wenye farasi Zayd bin Haritha Msafara wa kivita wa Maquraysh Haijulikani Qarada Dirham 100,000 zilikamatwa kama ngawira and Furat bin Hayyan alikamatwa.
4/625 Muharram Abu Salama 150 Abu Salama Tulayha & Salama Qatan Mateka watatu na baadhi ya kondoo na ngamia kama ngawira.
4/625 Muharram 'Abd Allah bin Unays 1 Sufyan bin Khalid b. Nubayh al-Hudhali Nakhla Sufyan bin Khalid bin Nubayh al-Hudhali aliuwawa.
4/625 Safar Raji' 6 au 10 Marthad bin Abi Marthad 'Adal & Qara Raji' Marthad na wafuasi wake waliuwawa.
4/625 Safar Bi'r Ma'una 40 au 70 Mundhir bin 'Amr Khazraji Kbila la 'Usayya & Ri'l & Dhakwan 'Amir bin Tufayl Bi'r Ma'una Waislamu wote waliuwawa isipokuwa 'Amr b. Umayya.
4/625 'Amr bin Umayya Damri 2 'Amr b. Umayya Damri Abu Sufyan Makka Baadhi ya washirikina na mtumwa mmoja waliuwawa.
5/627 Dhu l-Qa'da Abu 'Ubayda bin Jarrah Fihri Abu 'Ubayda bin Jarrah Fihri Sayf al-Bahr
6/627 Muharram Muhammad bin Maslama Wapiganaji 30 wenye farasi Muhammad bin Maslama Kabila la Qurata' Bakarat Baadhi ya washirikina waliuwawa, ngamia 150 na kondoo 3,000 zilichukuliwa kama ngawira.
6/627 Rabi' I 'Ukasha Wapiganaji 40 wanao tembea kwa miguu 'Ukasha bin Muhsin Bani Asad Haijulikani Ghamr Bani Asad walitoroka na ngamia 200 zilikamatwa kama ngawira.
6/627 Rabi' II Muhammad bin Maslama 10 Muhammad bin Maslama Bani Tha'laba & Bani 'Uwal Haijulikani Dhu l-Qassa Waislamu wote waliuwawa.
6/627 Rabi' II Abu 'Ubayd bin Jarrah 40 Abu 'Ubayd bin Jarrah Bani Tha'laba & Bani 'Uwal Haijulikani Dhu l-Qassa Baadhi ya ngamia na kondoo kama ngawira.
6/627 Rabi' II Zayd bin Haritha 40 Zayd bin Haritha Bani Sulaym Haijulikani Jamum Washirikina walitoroka na kondoo walikamatwa kama ngawira.
6/627 Jumada I Abu Bakr Wapiganaji 10 wanao tembea kwa miguu Quraysh Ghamim Kurejea
6/627 Jumada I 'Umar bin al-Khattab Qara Washirikina walitoroka.
6/627 Jumada I Hilal bin Harith Muzani Bani Malik bin Fihr Washirikina walitoroka.
6/627 Jumada I Bishr bin Suwaid Juhani Bani Harith bin Kinani
6/627 Jumada II Zayd bin Haritha Wapiganaji 170 wenye farasi Zayd bin Haritha Msafara wa kivita wa Maquraysh Haijulikani Msafara wote na baadhi yao akiwemo Abu l-'As b. Rabi' walikamatwa mateka.
6/627 Jumada II Zayd bin Haritha 15 Zayd bin Haritha Bani Sa'laba Taraf Ngamia 20 kama ngawira.
6/627 Jumada II Zayd bin Haritha 500 Zayd bin Haritha Judham Hunayd na mtoto wake waliuwawa.
6/627 Rajab Zayd bin Haritha Bani Fazara Wadi l-Qura Baadhi ya waislamu waliuwawa.
Zayd bin Haritha Madyan Baadhi ya watumwa
6/627 Sha'ban 'Abd al-Rahman bin 'Awf 'Abd al-Rahman bin 'Awf Bani Kalb Asbagh bin 'Amr Kalbi Dawmat al-jandal Bani Kalb waliukubali uislamu.
6/627 Sha'ban 'Ali bin Abi Talib 100 'Ali bin Abi Talib Bani Sa'd bin Bakr Fadak Bani Sa'd walitoroka na ngamia 500 & kondoo2,000 walikamatwa kama ngawira.
6/628 Ramadhan Zayd bin Haritha Zayd bin Haritha Kabila la Badr Umm Qarnad Wadi l-Qura Baadhi walikamatwa mateka.
6/628 Ramadan 'Abd Allah bin Rawaha 3 'Abd Allah bin Rawaha Khiybar Khiybar Operesheni ya kiuchunguzi.
6/628 Shawwal 'Abd Allah bin Rawaha 30 'Abd Allah bin Rawaha Kbila la Yusayr bin Rizam Mayahudi waliuwawa.
6/628 Shawwal Kurz bin Jabir Fihri 20 Kurz bin Jabir Fihri 8 kutoka kabila la Bajila Jamma' Wote 8 waliuwawa.
7/628 Sha'ban Turaba 30 'Umar bin al-Khattab Kbila la Hawzan 'Abla' Hawzan alitoroka na Waislamu walirejea bila vita.
7/628 Sha'ban Najd Abu Bakr Bani Kilab bin Rabi'a Dariyya Washirkina 7 waliuwawa na mmoja alikamatwa mateka.
7/628 Sha'ban Bashir bin Sa'd 30 Bashir bin Sa'd Bani Murra Fadak Waislamu waliuwawa isipokuwa Bashir bin Sa'd.
Zubayr bin 'Awam 200 Zubayr bin 'Awam au Ghalib b. 'Abd Allah Bani Murra
7/629 Ramadan Ghalib bin 'Abd Allah 130 Ghalib bin 'Abd Allah Bani 'Uwal & Bani 'Abd bin Tha'laba Mayfa'a Baadhi ya washirikina waliuwawa na baadhi ya ngamia na kondoo walikamatwa kama ngawira.
7/629 Shawwal Bashir bin Sa'd Ansari 300 Bashir bin Sa'd Ansari Kbila la Ghatfan Yumn & Jubar Kukamatwa kwa watumwa wawili na wanyama wengi kama ngawira.
7/629 Dhu l-Hijja Ibn Abi l-'Awja' 50 Ibn Abi l-'Awja' Bani Sulaym Kwa sababu ya baadhi ya majasusi Waislamu wote waliuawa isipokuwa Ibn Abi l-'Awja'.
7/629 Dhu l-Hijja 'Abd Allah bin Abi Hadrad 3 'Abd Allah bin Abi Hadrad many Rifa'a bin Zayd Jushami Ghaba Rifa'a bin Zayd Jushami aliuawa and baadhi ya ngamia na kondoo walikamatwa kama ngawira.
7/629 Dhu l-Hijja Muhayyisa bin Mas'ud Fadak
7/629 Dhu l-Hijja 'Abd Allah bin Abi Hadrad Idam
8/629 Safar Ghalib bin 'Abd Allah Ghalib bin 'Abd Allah Bani Malawwah Kadid Baadhi ya washirikina waliuwawa na baadhi ya wanyama walikamatwa kama ngawira.
8/629 Safar Ghalib bin 'Abd Allah 200 Ghalib bin 'Abd Allah Bani Murra Fadak Baadhi ya washirikina waliuwawa na baadhi ya wanyama walikamatwa kama ngawira.
8/629 Rabi' I Ka'b bin 'Umayr Ghifari 15 Dhat Atlah Waislamu wote waliuwawa isipokuwa mmoja.
8/629 Rabi' I Shuja' bin Wahb 24 Shuja' bin Wahb Hawzan Siyy Wanyama wengi walikamatwa kama ngawira.
Qutba b.'Amir 20 Qutba bin'Amir Khath'am Tabala Baadhi ya wanyama walikamatwa kama ngawira.
8/629 Jumada I Muta 3,000 Zayd bin Haritha Waroma na Waarabu Heraclius Balqa' Waislamu 17 wakiwemo Ja'far b. Abi Talib & Zayd bin Haritha & 'Abd Allah b. Rawaha waliuwawa. Baadhi ya maadui waliuwawa.
8/629 Jumada II Dhat al-Salsal 500 'Amr bin 'As Quda'a Eneo la Baliyy & 'Udhra & Balqayn Kuwashinda washirikina.
8/629 Rajab Abu 'Ubayd bin Jarrah 300 Abu 'Ubayd bin Jarrah Juhayna Qabaliyya Bila vita yoyote
8/629 Sha'ban Abu Qatada bin Rib'i 15 Abu Qatada bin Rib'i Bani Ghatafan Baadhi ya washirikina waliuwawa, ngamia 200 na kondoo 2,000 walichukuliwa kama ngawira.
8/629-30 Ramadhan Abu Qatada bin Rib'i 8 Abu Qatada bin Rib'i Batn Idam
8/629-30 Ramadhan Khalid bin Walid Wapiganaji 30 wenye farasi Khalid bin Walid Nakhla Yamaniyya Masanamu wa 'Uzza waliteketezwa.
8/629-30 Ramadhan 'Amr bin 'As Ruhat Masanamu wa Suwa' waliteketezwa.
8/629-30 Ramadhan Sa'd bin Zayd Ashhali Wapiganaji 20 wenye farasi Sa'd bin Zayd Ashhali Mushallal Masanamu wa Manat waliteketezwa.
8/629-30 Ramadhan Khalid bin Sa'id bin 'As 300 Khalid bin Sa'id b. 'As 'Urna
8/629-30 Ramadhan Hisham bin 'AS 200 Hisham bin 'As Yalamlam
8/630 Ghalib bin 'Abd Allah Bani Mudlij
8/630 'Amr bin Umayya Damri Bani Dayl
8/630 'Abd Allah bin Suhayl 500 'Abd Allah b. Suhayl Bani Ma'is & Muharib bin Fihr Waliukubali uislamu.
8/630 Numayla bin 'Abd Allah Laythi Bani Damra
8/630 Shawwal Khalid bin Walid 350 Khalid bin Walid Bani Jadhima Ghumaysa' Khalid, kinyume na amri ya Mtume, aliwaua baadhi yao.
8/630 Shawwal Abu 'Amir Ash'ari Hawzan Awtas Abu 'Amir aliuwawa and wanafiki waliuwawa.
8/630 Shawwal Tufayl bin 'Amr Dawsi Masanamu ya Dhi l-Kaffayn yaliharibiwa.
8/630 Abu Sufyan Ta'if
8/630 'Ali bin Abi Talib (a.s) Khash'am Ta'if 'Ali bin Abi Talib (a.s) aliyaharibu masanamu yote.
9/630 Muharram 'Uyayna bin Hisn Fizazi Wapiganaji 50 wenye farasi 'Uyayna bin Hisn Fizazi Bani l-'Anbar Suqya 52 mateka.
9/630 Rabi' I Dahhak bin Sufyan Kilabi Qurata' Washirikina waliuwawa.
Thumama bin Uthal Hanafi alikamatwa.
9/630 Rabi' II 'Alqama bin Mujazzaz Mudliji 300 'Alqama bin Mujazzaz Baadhi ya watu wa Habash Bila vita yoyote
9/630 Rabi' II 'Ali bin Abi Talib (a.s) 150 'Ali bin Abi Talib (a.s) Fols Eneo la kabila la Tayy Masanamu yaliteketezwa, baadhi ya watu walishikwa mateka na baadhi ngamia na kondoo walikamatwa kama ngawira.
9/630 Rabi' II 'Ukkasha bin Mihsan 'Udhra & Baliyy Jinab

Vyanzo

  • The material for this article is mainly taken from سریه in Farsi WikiShia.
  • Ayati, Muhammad Ibrahim. Tarikh-i payambar-i Islam. Tehran: Tehran Universiy, 1378
  • Halabi, 'Ali b. Ibrahim al-. Al-Sira al-halabiyya.
  • Ibn Athir, Mubarak b. Muhammad. Al-Nihaya fi gharib al-hadith wa l-athar. Qom: Isma'iliyan, 1376
  • Ibn Ishaq. Sirat al-nabiyy. Mustafa al-Halabi, 1355
  • Mas'udi, 'Ali b. Husayn al-. Al-Tanbih wa l-Ishraf. Tehran: Intishart-i 'Ilmi Farhangi, 1356
  • Miqrizi, Ahamd b. 'Ali al-. Imta' al-asma' . Beirut: Dar al-Kutub al-'Ilmiyya
  • Tabrisi, al-Fadl b. al-Hasan al-. I'lam al-wara bi a'lam al-huda. Beirut: Dar al-Ma'rifa, 1399