Nenda kwa yaliyomo

Salim bin Amr

Kutoka wikishia

Salim bin Amr bin Abdallah (aliuawa shahidi mwaka 61 Hijria) ni miongoni mwa mashahidi wa tukio la Karbala. Alishiriki katika harakati ya Muslim bin Aqil na baada ya kuuawa shahidi Muslim, aliuangana na Imamu Hussein (a.s) na aliuawa shahidi katika siku ya Ashura (10 Muharram -Mfunguo Nne-).

Kuwa Pamoja na Muslim bin Aqil

Salim bin Amr bin Abdallah alikuwa mtumwa wa kabila la Banu al-Madinah Kalbi na mmoja wa Mashia wa Kufa. [1] Alishiriki katika harakati ya Muslim bin Aqil na baada ya kuuawa shahidi alitiwa mbaroni na Kathir bin Shahab. Baada ya muda fulani, alitoroka kutoka kwenye jela ya Ibn Ziyad na kujificha miongoni mwa kabila lake. [2]

Kuuawa Shahidi Karbala

Baada ya Imamu Hussein (a.s) kuwasili Karbala, Salim aliungana naye pamoja na baadhi ya watu kutoka Bani Kalb na aliuawa shahidi siku ya Ashura. [3] Katika kitabu Ibsar al-Ayn cha Muhammad Samawi (aliyefariki dunia 1370 Hijiria) ananukuu kutoka kwa Ibn Shahrashub na kumtambulisha Salim kuwa miongoni mwa mashahidi wa shambulio la kwanza katika siku ya Ashura, [4] ingawa mtafiti wa kitabu hajafikia matilaba hii. [5] Pia, katika baadhi ya nakala za Manaqib Ibn Shahrashub, jina lake halikujumuishwa miongoni mwa mashahidi wa shambulio la kwanza na wengineo. [6]

Shaka (Utata)

Muhammad Taqi Shushtari (1281-1374 Hijria Shamsia), mwanazuoni wa kidini wa Shia, ametilia shaka uwepo wa Salim bin Amr katika kitabu cha Kamus al-Rijal, [7] kwa sababu katika vyanzo vya kihiistoria na vya wasifu wa wapokezi wa hadithi vilivyotangulia vya Kishia, jina lake halijatajwa kuwa miongoni mwa mashahidi wa Karbala. [8] Pamoja na hayo, katika Ziyarat al-Shuhadaa anatolewa salamu namna hii:«السَّلَامُ عَلَى سَالِمٍ مَوْلَى بَنِي الْمَدَنِيَّةِ الْكَلْبِی». Na Hivyo kutajwa kuwa miongoni mashahidi wa Karbala. [9]

Rejea

Vyanzo