Murtaza Bhai
Al-haaj Murtaza Ramadhan Aliy jiyorajiya (1944-2021A.D) aliekuwa maarufu kwa jina la Murtaza Karbalaa, ni mwanaharakati wa kishia tanzania aliejishughulisha na mambo ya kitamaduni kiasi kwamba hadi pumzi ya mwisho ya maisha yake alikuwa akiutumikia Uislaam na waislaam. Kwa hakika bwana huyu alikuwa ni miongoni mwa waasisi na waanzilishi wa sunnah nzuri ya maadhimisho ya usiku wa Ashuraa mwaka 1969 A.D katika mji wa kigoma na maadhimisho hayo tangu wakati huo hadi sasa yamekuwa yakifanyika mfululizo bila kukatika na yamekuwa ni maadhimisho yenye kuleta hamasa kubwa. Al-haaj Murtaza, alijitolea na kusimamia na kutoa huduma nyingi na misaada mingi kwa jamii ya kishia wa khoja ithna asharia katika nchi ya Tanzania kiasi kwamba matokeo ya huduma yake kwa jamii hii na pia dauru yake katika kueneza maktab ya Ahlul-baiti (a.s) alipata bahati na fakhari ya kupokea Medali ya Abbasi kutoka kwa Raisi wa Federation ya Afrika ya watu wa jamii hii.
HOSTORIA YA MAISHA YAKE
Murtaza Bhai amezaliwa mnamo tarehe 03 mach mwaka 1944 A.D katika eneo la Ujiji kigoma katika nchi ya Tanzania, na alikuwa ni mtoto wa nne kwa mama na baba mzee Ramadhan Aliy Bhai na Maryam Bhai Jioraj baba ambae alikuwa na watoto kumi na mbili (12). Murtaza Bhai alipata masomo yake ya msingi katika mji wa kigoma na kumalizia masomo yake katika mji huo baada ya hapo mnamo mwaka 1964 A.D akahamia katika mji wa Dar-es-salaam kwa ajili ya kuendelea na masomo yake ya sekondari. Baada ya kuhitimu masomo yake ya sekondari mnamo mwaka 1967 A.D akajiunga na wizara ya vizazi na vifo na mnamo mwaka 1971 A,D akahamia katika mji wa mwanza na kuanzisha biashara yake ya kuuza spea za magari. Baada ya hapo mnamo kwama 1975 A.D akarejea na kurudi kwenye mji wa Dar-es-salaam, mahala ambapo yeye na kaka zake walifanikiwa kuanzisha kituo cha mambo ya picha na kamera kwa ufanisi mkubwa kiasi kwamba katika miaka yote hiyo kituo hicho kilipanuka na kujumuisha shirika la (Geo-Micro) lililo kuwa likijishughulisha na mambo ya picha na vifaa vinavyo husiana na mambo ya picha na Kamera.
HARAKATI ZA KITABLIGHI
Murtaza Karbalaa, alikuwa na shakhsiya yenye kupendeka, yenye mvuto na yenye kutoa matumaini. Kwa hakika huduma na harakati zake za kijamii alizianza katika ujana wake katika mji wa kigoma kwa anwani Huduma za kujitolea katika jamii ya khoja na kabla ya kuchaguliwa kwa anwani ya mkuu wa ushirikiano wa jamii ya khoja wa kigoma, alikuwa akishughulika katika kamati ya khoja (Jamaat Committee) katika mwaka 1967 A.D. Kwa hakika yeye alikuwa na dauru muhimu sana katika kuanza kwa maadhimisho ya usiku wa Ashuraa. Maadhimisho haya kwa mara ya kwanza yalifanyika katika mji wa kigoma mnamo mwaka 1969 A.D. sunna ambayo inaendelea hadi leo chini ya usimamizi wa taasisi ya (Bila Muslim Mission). Murtaza katika muda wote aliokuwa katika mji wa Mwanza alikuwa akitoa huduma kama mtu wa kujitolea na alikuwa ni mwanachama wa kamati ya club ya michezo ya Jaafar iliyo kuwa ikijulikana kwa jina la (Jaffery Sports Club).
Na mnamo mwaka 1975 A.D alijiunga na kikundi cha kujitolea cha umoja wa Ithnaa asharia chenye kujulikana kama Ithna-Asheri Union Volunteer (Ithna-Asheri Corps IUVC) katika mji wa Dar-es-salaam na kufanya harakati katika sehemu mbali mbali za jamii, vivyo hivyo alijiunga na umoja wa ithna ashari ulio julikana kwa jina la (Ithna-Ashari Union) na pia umoja wa Club za micheo (Union Sports Club) na kutoa huduma katika sehemu hiyo. Bwana Murtaza Bhai alishiriki na kuwa na haraka kubwa katika program mbalimbali za kikundi cha kujitolea cha umoja wa ithna ashariy (IUVC) na kushiriki kwenye harakati hizo. Program za umoja huu ni kama zifuatazo: Utoaji wa misaada kwa watu walio kumbwa na mafuriko ya Rufiji, mjumbe wa kamati maalum ya upangiliaji na usimamiaji wa maadhimisho ya Ashura, mnadhimu wa vikao na maadhimisho ya kila mwaka ya Bagamoyo, kusimamia maadhimisho ya siku ya Imam Husein (Husein Day) na sherehe za mazazi ya Mtume (s.a.w.w) katika mji wa Dar-es-salaam (Mji kubwa sana kati ya miji ya Tanzania).
Bwana Murtaza kuanzia miaka ya 1983-1986 A.D alikuwa ni mudiir na msimamizi mkuu wa kitengo cha vijana wa madrasa ya Huseiniy na kutoa huduma katika kitengo hicho na vilevile kuanzia mwaka 2004 hadi 2007 A.D alikuwa ni raisi wa taasia ya kitablighi ya Bilal Muslim Mission Tanzania. Bwana Murtaza Bhai mnamo mwaka 2007 A.D alichukua nafasi ya kitengo cha kumbukumbu (Archives) ya Fedration ya Afrika (AFED) (Afrika Federation) na kujiunga na (Baraza kuu la taasisi ya Bilal), na mnamo mwaka 2016 A.D alisimikwa kwa anwani ya raisi wa baraza hilo na hadi kifo chake alikuwa anashikilia nafasi hiyo. Kwa hakika bwana Murtaza alikuwa na mapenzi makubwa sana na historia ya jamaa wa kikhoja.
Pia bwana Murtaza Karbalaa alikuwa akimiliki albamu kubwa binafsi iliyo jawa picha nyingi za jamaa wa kikhoja, Misikiti mbali mbali, sehemu za histora ya maimamu (Imambargahs), pia picha za watu mbali mbali alizo zipata katika minasaba mbali mbali, picha ambazo alizipata na kuzikusanya na kuzihifadhi kutoka kwenye minasaba mbali mbali. Na alikuwa na plan ya kuanzisha maktaba na Galary ya picha katika ofisi mpya ya (AFED) katika mji wa Dar-es-salaam na mswaada kamili wa jambo hilo aliukabidhi na kuuweka wazi katika kikao cha 82 cha kamati kuu ya taasisai hiyo kilicho fanyika mwaka 2020 A.D.
HUDUMA ZAKE ZA KIFAHARI
Marehemu Murtaza Karbalaa kutokana na huduma za kifakhari na za kujitolea alizo fanya na kujitolea kwake kuihuduia jamii na wanadamu kwa ujumla na haswa jamaa wa khoja ithna ashariy aliweza kupokea Medali ya Abbasiy katika kikao cha 82 cha kamati kuu kilicho fanyika Dec mwaka 2020 A.D katika mji wa Dar-es-salaam, alipokuwa Medali hiyo ya Abbasiy kutoka kwenye mikono ya Shabiir Najafiy raisi wa Federation ya Afrika.
Bwana Murtaza Bhai katika miaka ya mwisho ya umri wake alikuwa akifanya juhudi kubwa za maandalizi ya program ya mazungumzo na mahojiano ya Federation ya Afrika iliyokuwa na anwani ya (Panjo Uganda), program ambayo kupitia kitengo cha kumbukumbu (Archives) kwa ushirikiano na kitengo cha mambo ya habari na vyombo vya habari vya Federation ya Afrika program ambayo ilipangwa kufanyika katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
KUAGA KWAKE DUNIA
Al-haaj Murtaza Ramadhanaliy Jiyoorj (Aliekuwa maarufu kwa jina la Murtadha Karbalaa) aliaga dunia siku ya Ijumaa 2 April mwaka 2021 A.D na kuzika katika mji wa Dar-es-salaam. Kwa hakika bwana huyu hadi pumzi yake ya mwisho alikuwa akitoa huduma katika njia ya Uislaam, mapenzi ya Ahlul-baiti (a.s) na maadhimisho ya msiba wa Imam Husein (a.s) na hivyo ndio vitu vilivyo bakia katika urithi wake.