Munjih bin Sahm

Kutoka wikishia
Makaburi ya Pamoja ya Mashahidi wa Karbala katika Haram ya Imamu Hussein (a.s)

Munjih bin Sahm (Kiarabu: مُنجِح بن سَهم) au Munhij (Kiarabu: منحج) mtumwa wa Imamu Sajjad (a.s), ambaye aliuawa shahidi katika tukio la Karbala. Mama yake Munjih alikuwa kanizi (binti au mwanamke asiye Muislamu aliyechukuliwa mateka katika vita baina ya Waislamu na makafiri) ambaye Imam Hussein (a.s) alimnunua kutoka kwa Nawfal bin Harith bin Abdul Muttalib. Aliolewa na mtumwa aliyeitwa Sahm na akazaliwa Munjih. Imamu Hussein (a.s) alimchukua Munjih na kumuweka katika utumishi wa Imam Sajjad (a.s). [1] Kwa mujibu wa baadhi ya ripoti, jina la mama yake Munjih ni Husniyyah (Hussainiyah). [2]

Baada ya Imamu Hussein (a.s) kuhama kutoka Madina kwenda Makka, Munjih pia aliondoka Madina pamoja na mama yake. [3] Hata hivyo baadhi wamemtambua kuwa mfuasi wa Imamu Hassan (a.s) ambapo akiwa na watoto wa Imamu Hassan aliondoka Madina pamoja na msafara wa Imam Hussein (a.s). [4]

Munjih aliuawa shahidi katika tukio la Karbala. [5] Hata hivyo tarehe hasa ya kuuawa kwake shahidi haijatajwa' lakini Ibn Shahrashub amesema, katika shambulio la kwanza, watumwa kumi wa Imamu Ali (a.s) na Imamu Hussein (a.s) waliuawa shahidi. [6] Muuaji wake ametajwa kuwa ni Hassan bin Bikr Handhali. [7] Samawi ananukuu kutoka katika kitabu cha al-Hadiqah al-Wardiyyah ya kwamba, muuaji wake ni Hassan bin Bikr na aliuawa shahidi wakati wa kuanza tu vita. [8] Jina la Munjih limetajwa katika Ziyarat al-Shuhada kwamba, ni mmoja wa mashahidi. Katika ziara hiyo anasalimiwa kwa ibara ya:

«اَلسَّلَامُ عَلَی مُنْجِحٍ مَوْلَی الْحُسَینِ بْنِ عَلِی(ع)»


Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya Munjih Maula al-Hussein bin Ali.[9]


Rejea

Vyanzo