Mkopo:Dua ya hamsini na tatu ya kitabu cha Sahifa Sajjadiya
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Abdullah Yazdi, iliyoandikwa mnamo Sha'ban 1102 AH. | |
| Mada | Dua ya iliyokuwa ikitumiwa na Imam Sajjad (a.s) katika nyakati zake za kunyenyekea na kujidogosha mbele ya Mwenye Ezi Mungu. |
|---|---|
| Ina Mapokezi au Haina Mapokezi | Ina Mapokezi |
| Imenukuliwa Kutoka kwa | Imamu Sajjad (a.s) |
| Mpokezi | Mutawakkil ibn Harun |
| Vyanzo vya Kishia | Sahifa Sajjadiyah |
| Dua ya Tawassuli • Dua ya Kumaili • Dua ya Nudba • Dua ya Samati • Dua ya Faraji • Dua ya Abu Hamza Thumali • Ziara ya Ashura • Ziara ya Jamiat Kabira • Ziara ya Warith • Ziara ya Aminu-Llah • Ziara ya Arobaini | |
Dua ya Hamsini na Tatu ya Sahifa Sajjadiya (Kiarabu: الدعاء الثالث والخمسون من الصحيفة السجادية) ni moja ya dua zilizonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s). Hii ni maalumu aliyokuwa ikisomwa na Imamu Sajjad (a.s) wakati wa kujidogosha (kujishuha) pamoja na kudhihirisha unyenyekevu mbele ya Mola wake. Katika dua hii, Imamu Sajjad (a.s) anazungumzia namna ya madhara ya dhambi yanavyo athiri moj kwa moja mwenendo mzima wa maisha ya mwanadamu, duniani pamoja na Akhera. Hivyo basi anawahimiza waja wa mwenye Ezi Mungu kuamka kutoka usingizi wa mghafala wa dunia kabla ya kifo. Dua hii imejikita zaidi katika kuomba msamaha wa makosa na kutafuta utulivu wa siku ya hukumu.
Dua ya tatu na hamsini imetafsiriwa na kufafanuliwa kitaalamu kupitia lugha na vitabu mbali mbali vilivyofanya kazi ya kufasiri dua zilizomo ndani ya kitabu cha Sahifa Sajjadiya. Miongoni vya lugha ya Kiajemi vilivyotoa uchambuzi wa dua ya hamsini na tatu sambamba na dua nyengine za Sahifa Sajjadiyya ni pamoja na; Shuhud wa Shenakht kilichoandikwa na mwanachuoni ajulikanaye kwa jina la Hassan Mamduhi Kermanshahi. Aidha miongoni mwa vitabu maarufu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiarabu, katika juhudi za kueneza mafunzo ya dua hamsini na tatu pamoja na dua nyengine za Sahifa Sajjadiyya, ni kile kitabu kiitwacho Riadhu al-Salikin kilichoandikwa na bwana Sayyid Ali Khan Madani.
Mafunzo yaliyomo Ndani ya Dua ya Hamsini na Tatu
Dua ya hamsini na tatu ni miongoni mwa dua za Sahifa Sajjadiyya iliyokuwa ikitumiwa na Imam Zain al-Abidin katika nyakati zake za kunyenyekea na kujidogosha mbele ya Mwenye Ezi Mungu. Kulingana na maelezo ya Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah katika ufafanuzi wa dua hii, ni kwamba; tendo la kuonesha unyenyekevu mbele ya Mungu kwa njia ya ulimi sambamba na kudhihirisha unyenyekevu huo kupitia viungo vingine vya mwili, ni moja mambo muhimu yanamfanya mja apate daraja maalumu za roho pamoja na kumpa taufiki ya kupata ukuruba wa kumkaribia Mwenye Ezi Mungu.[1] Aidha, Hasan Mamduhi Kermanshahi anaeleza kwamba; nafsi ya mja ni kinyume kabisa na nafasi ya Mwenye Ezi Mungu, ambayo ni yenye utukufu, hadhi isiyo na mipaka. Sifa ambazo zinadhihirika kupitia sifa ya kujitosheleza. Hivyo basi, sifa kamili anayotakiwa kuwa nayo mja fulani pale anapokuwa mbele ya Mola wake, ni ile sifa ya kujinyongesha na kuwa na unyenyekevu. Uhalisia huo alionao mwanadamu, ndiwo unaomfanya Imamu Maasumu aliyefika hatua za juu kabisa za maarifa, kuwa na unyenyekevu mkubwa zaidi kuliko wengine mbele ya Mwenye Ezi Mungu.[2] Mafunzo ya dua ya hamsini na tatu yamekuja kama ifuatavyo:
- Athari za dhambi siku ya Kiyama: Kutoweza kusema, kuchanganyikiwa na kufikwa na majuto, kuona haya na kudhalilika.
- Mwanadamu ni mateka wa matendo yake na mfungwa wa nafsi yake mwenyewe
- Udhalili na unyonge utokanao na matendo ya dhambi.
- Kupuuza maonyo ya adhabu za Mwenye Ezi Mungu kwa njia ya kufanya dhambi.
- Ujasiri na ukiukaji wa heshima za Mungu kwa kutenda dhambi
- Kukiri makosa mbele ya Mwenye Ezi Mungu
- Kutangaza utayari wa kupokea adhabu mbele ya Mwenye Ezi Mungu kupitia ujasiri wa kufanya dhambi.
- Umuhimu wa kuamka kutoka kwenye usingizi wa ujinga kabla ya kifo.
- Ombi la kuomba taufiki ya kupata rehema za Mwenye Ezi Mungu baada ya kifo.
- Ombi la kuomba kuhurumiwa wakati wa kuoza kwa miili
- Ombi la kuomba usalama na amani ndani ya uwanja wa rehema za Mwenye Ezi Mungu
- Ombi la kuomba kuwa pamoja na marafiki wa Mwenye Ezi Mungu siku ya Kiyama
- Ombi la kuomba msamaha wa dhambi kwa uvumilivu na bila kuwa na haraka.[3]
Tafsiri Chambuzi za Dua ya Hamsini na Tatu
Dua ya hamsini na tatu imefafanuliwa kupitia lugha na vitabu mbali mbali vilivyofasiri na kutoa maelezo ya dua za kitabu cha Sahifa Sajjadiya. Miongoni mwa vitabu vilivyofanya kazi yake kwa lugha ya Kiajemi ni pamoja na; Diare Ashiqan kilichoandikwa na Hussein Ansarian,[4] Shuhud wa Shenakht kazi ya na Muhammad Hassan Mamduhi Kermanshahi,[5] pamoja na Sharh wa Tarjuma Sahifa Sajjadiyyeh kilichoandikwa na Sayyid Ahmad Fahri.[6]
Halikadhika, dua hii ya hamsini na tatu ya Sahifa Sajjadiyya imefafanuliwa kwa lugha ya Kiarabu katika vitabu mbalimbali, ikiambatanishwa na chambuzi za dua nyengine za Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa kazi muhimu za Kiarabu zilizohudumia watumizi wa lugha hii ni pamoja na; kitabu kiitwacho Riadh al-Salikin kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani,[7] Fi Dhilali al-Sahifa al-Sajjadiyya cha Muhammad Jawad Mughniyya,[8] Riadhu al-Arifina kilichoandikwa na Muhammad bin Muhammad Darabi,[9] na Afaqi al-Ruh cha Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah.[10] Zaidi ya hayo, pia kuna jitihada maalumu zilizofanywa na baadhi ya wanazuoni kuhusiana na ucvhambuzi wa maana ya msamiati na maneno yaliyotumika ndani ya ya dua hii sambamba na dua nyengine za Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa matunda ya jitihada hizo ni pamoja na kitabu kiitwacho Ta'aliqat ala al-Sahifa al-Sajjadiyya cha Faidhu Kashani[11] pamoja na Sharhu al-Sahifa al-Sajjadiyya cha Izzu al-Din Jaza’iri.[12]
Matini ya Kiarabu ya Dua ya Hamsini na Tatu Pamoja na Maelezo Yake kwa Kiswahili
وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي التَّذَلُّلِ لِلَّهِ عَزَّ وَ جَلَّ
رَبِّ أَفْحَمَتْنِي ذُنُوبِي، وَ انْقَطَعَتْ مَقَالَتِي، فَلَا حُجَّةَ لِي، فَأَنَا الْأَسِيرُ بِبَلِيَّتِي، الْمُرْتَهَنُ بِعَمَلِي، الْمُتَرَدِّدُ فِي خَطِيئَتِي، الْمُتَحَيِّرُ عَنْ قَصْدِي، الْمُنْقَطَعُ بِي. قَدْ أَوْقَفْتُ نَفْسِي مَوْقِفَ الْأَذِلَّاءِ الْمُذْنِبِينَ، مَوْقِفَ الْأَشْقِيَاءِ الْمُتَجَرِّينَ عَلَيْكَ، الْمُسْتَخِفِّينَ بِوَعْدِكَ
سُبْحَانَكَ! أَيَّ جُرْأَةٍ اجْتَرَأْتُ عَلَيْكَ، وَ أَيَّ تَغْرِيرٍ غَرَّرْتُ بِنَفْسِي!
مَوْلَايَ ارْحَمْ كَبْوَتِي لِحُرِّ وَجْهِي وَ زَلَّةَ قَدَمِي، وَ عُدْ بِحِلْمِكَ عَلَى جَهْلِي وَ بِإِحْسَانِكَ عَلَى إِسَاءَتِي، فَأَنَا الْمُقِرُّ بِذَنْبِي، الْمُعْتَرِفُ بِخَطِيئَتِي، وَ هَذِهِ يَدِي وَ نَاصِيَتِي، أَسْتَكِينُ بِالْقَوَدِ مِنْ نَفْسِي، ارْحَمْ شَيْبَتِي، وَ نَفَادَ أَيَّامِي، وَ اقْتِرَابَ أَجَلِي وَ ضَعْفِي وَ مَسْكَنَتِي وَ قِلَّةَ حِيلَتِي.
مَوْلَايَ وَ ارْحَمْنِي إِذَا انْقَطَعَ مِنَ الدُّنْيَا أَثَرِي، وَ امَّحَى مِنَ الْمَخْلُوقِينَ ذِكْرِي، وَ كُنْتُ مِنَ الْمَنْسِيِّينَ كَمَنْ قَدْ نُسِيَ
مَوْلَايَ وَ ارْحَمْنِي عِنْدَ تَغَيُّرِ صُورَتِي وَ حَالِي إِذَا بَلِيَ جِسْمِي، وَ تَفَرَّقَتْ أَعْضَائِي، وَ تَقَطَّعَتْ أَوْصَالِي، يَا غَفْلَتِي عَمَّا يُرَادُ بِي.
مَوْلَايَ وَ ارْحَمْنِي فِي حَشْرِي وَ نَشْرِي، وَ اجْعَلْ فِي ذَلِكَ الْيَوْمِ مَعَ أَوْلِيَائِكَ مَوْقِفِي، وَ فِي أَحِبَّائِكَ مَصْدَرِي، وَ فِي جِوَارِكَ مَسْكَنِي، يَا رَبَّ الْعَالَمِينَ.
Bila shaka mimi ni mwenye kukiri dhambi zangu, na ni mwenye kukubali makosa yangu. Mikono yangu (mkono wa kuumeni kwangu) na nywele za usoni kwango viko mbele Yako, (tayari nipo mikononi mwako nikisubiri maamuzi Yako, kwa lugha nyengine ni kwamba; mimi ni mateka Wako nimeshajisalimisha kwako na ninasubiri maamuzi Yako), najinyenyekeza (na kujileta mbele Yako nikiwa dhalili kabisa) kwa ajili ya kisasi cha nafsi yangu (kwa ajili ya kulipizwa kisasi cha makosa yangu).
(Ninakuom) uuhurumie uzee wangu, na uhurumie upungukaji wa siku zangu, (na uhurumie) ukaribiaji wa mauti yangu, (na uhurumie) udhaifu, unyonge wangu, na kwa uchache wa uwezo wangu wa kujinusuru.Na (ifuatayo) ilikuwa ni miongoni mwa dua zake (amani iwe juu yake) aliyokuwa akiitumia kwa ajili ya kudhihirisha unyenyekevu mblele ya Mwenye Ezi Mungu aliye Mueza na Mtukufu.
Ewe Mola wangu, dhambi zangu zimezizima kauli zangu (zimeufunga mdomo wangu), na maneno yangu yamekatika (wala sin a la kusema); sina hoja ya kujitetea (mbele Yako). Hivyo basi nimekuwa ni mateka wa balaa langu mwenyewe (mimi ni matekawa dhambi zangu), na ukombozi wangu upo chini ya dhamana ya matendo yangu, ninayumbayumba katika makosa yangu, nimechanganyikiwa na lengo langu, na nimekatikiwa na njia yangu. Hivyo basi nimeisimamisha nafsi yangu mbele zako kwa kisimamo cha wanyonge wenye dhambi, na kwa kisimamo cha waasi waliokosa haya mbele ya utukufu wako (waliothubutu na waliokuwa na ujasiri wa kutenda dhambi mbele utukufu wako), wanaodharau ahadi zako (wanaodharau ahadi Zako kuhusiana na malipo ya amali zao).
(Ewe Mola wangu) umetakasika (kwa utakaso ulioje)! Ni ujasiri wa aina gani niliothubutu kukufanyia, na ni udanganyifu wa namna gani nilioufanyia (niliojifanyia) nafsi yangu!
Ewe Mola wangu, nihurumie kutokana na muanguko wangu wa kuangukia uso wangu (muanguko wangu kifudifudi), na (nakuomba unihurumie) kutokana na mtelezo wa miguu yangu (wa kutelezea makosani). Na (Ewe Mola wangu nakuomba) unirudie kwa uvumilivu Wako juu ya ujinga wangu, na (nakuomba unirudi) kwa hisani Zako juu ya maovu yangu. Bila shaka mimi ni mwenye kukiri dhambi zangu, na ni mwenye kukubali makosa yangu. Mikono yangu (mkono wa kuumeni kwangu) na nywele za usoni kwango viko mbele Yako, (tayari nipo mikononi mwako nikisubiri maamuzi Yako, kwa lugha nyengine ni kwamba; mimi ni mateka Wako nimeshajisalimisha kwako na ninasubiri maamuzi Yako), najinyenyekeza (na kujileta mbele Yako nikiwa dhalili kabisa) kwa ajili ya kisasi cha nafsi yangu (kwa ajili ya kulipizwa kisasi cha makosa yangu). (Ninakuom) uuhurumie uzee wangu, na uhurumie upungukaji wa siku zangu, (na uhurumie) ukaribiaji wa mauti yangu, (na uhurumie) udhaifu, unyonge wangu, na kwa uchache wa uwezo wangu wa kujinusuru.
Ewe Mola wangu, na ninakuomba unihurumie pale athari yangu nitakapokuwa imeshakatika duniani humu, na pale kumbukumbu yangu itakapokuwa imeshafutika ndani ya kumbukumbu za miongoni mwa viumbe (Wako), wakati ambapo nitakuwa ni miongoni mwa walisahauliwa kama vile walivyosahaulika wale waliokwisha sahaulika.
Ewe Mola (bwana) wangu, nihurumie wakati sura na hali yangu zitakapobadilika, na pale mwili wangu utakapooza, na viungo vyangu vitakapotawanyika, na mifupa yangu (ilioshikana) itakapoachana. Ni mgafala (uzembe) mkubwa ulioje wa kutojua kinachoningojea!
Ewe Mola wangu, nihurumie katika siku ya kutolewa kaburini kwamgu na kufufuliwa kwangu (wakati wa kurejeshwa roho yangu ndani ya mwili wangu). Na unijaalie ndani ya siku hiyo niwe pamoja na wapenzi Wako (niwe kwenye safu ya wapenzi Wako), na niwe ni miongoni mwa marafiki zako (miongoni mwa walio karibu Nawe), na Ee Mola wa walimwengu wote, (ninakuomba uyafanye) makazi yangu yawe ni jirani Nawe.
Rejea
- ↑ Fadhlullah, Afaq al-Rouh, 1420 AH, juz. 2, uk. 626-627.
- ↑ Mamduhi Kermanshahi, Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 365.
- ↑ Mamduhi Kermanshahi, Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 365-376.
- ↑ Ansarian, Diyar Asheqan, 1373, juz. 7, uk. 623-629.
- ↑ Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 3, uk. 363-376.
- ↑ Fahri, Sherh wa Tafsir Sahifa Sajjadih, 1388, juz. 3, uk. 571-572.
- ↑ Madani Shirazi, Riyadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 6, uk. 395-412.
- ↑ Mughniyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 657-660.
- ↑ Darabi, Riyadh al-Arifin, 1379 AH, uk. 725-730.
- ↑ Fadhlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 2, uk. 630-635.
- ↑ Faydh Kashani, Ta'baqat al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1407 AH, uk. 103.
- ↑ Jazairi, Sharh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1402 AH, uk. 296-298.
Vyanzo
- Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
- Jazairi, Izu-Din, Sherh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Beirut, Dar al-Taaruf Lil-Matbuat, 1402 AH.
- Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
- Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
- Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
- Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
- Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
- Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
- Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.