Mali Zenye Shaka

Kutoka wikishia

Mali ya Shubha (Kiarabu: مال الشبهة) au Mali yenye utata ndani yake (Kiarabu:المال المشتبه), ni mali ambayo haifahamiki uharamu na uhalali wake. Mali yenye shubha ina tofauti na mali ambayo imechanganyika na haramu; kwa sababu katika mali ambayo imechanganyika na haramu kinyume na mali yenye shubha, mtu anafahamu wazi kwamba, katika mali yake kuna haramu ndani yake.

Wanazuoni wa fikihi wameitambua mali yenye shubha kwamba ni mali halali, na mali hii haina suala la kutolewa khumsi na mwenye kumiliki mali kama hii anaweza kuitumia kwa ajili ya kwenda kutekeleza ibada ya Hija.

Katika baadhi ya hadithi kumetolewa maagizo ya kuchukua tahadhari kuhusiana na mali ya shubha. Muhammad Taqi Majlisi kwa kuzingatia hadithi hizo anasema, ni bora mtu asiitumie mali yenye shubha na utata ndani yake. Mkabala, naye Imam Ruhullah Khomeini muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yeye amezifasiri hadithi hizi kama ni zenye kutoa muongozo na dira na hajakubaliana na makuruhu ya kifikihi ya kutumia mali yenye shubha na utata.

Utambuzi wa maana (Conceptology)

Mali yenye shubha katika mijadala na maudhui za kifikihi[1] na kihadithi[2] inaelezwa kuwa ni mali ambayo haifahamiki kuwa kwake halali au haramu.[3] Kwa maana kwamba, haifahamiki kama mali hii imepatikana kwa njia ya halali au ya haramu. Katika hadithi limetumika pia neno “Shubha au Shubhaat” [4]. Imekuja katika moja ya hadithi iliyopokewa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w): ((...حَلَالٌ بَيِّنٌ وَ حَرَامٌ بَيِّنٌ وَ شُبُهَاتٌ بَيْنَ ذَلِكَ; Halali iko wazi na bayana na haramu iko wazi na bayana na shubha ni baina ya viwili hivyo)). [5] Baadhi wamelitambua tonge au chakula chenye shubha na utata ndani yake kuwa ni katika mali zenye shubha, shaka na utata. [6]

Katika lugha neno shubha na utata huhusishwa na kitu ambacho kuna shaka kuhusiana na uhalali na uharamu wake. [7] Imekuja katika hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Ali ibn Abi Twalib(a.s) ya kwamba: ((سُمِّيَتِ الشُّبْهَةُ شُبْهَةً لأَنَّهَا تُشْبِه الْحَقَّ; Shubha imeitwa shubha kutokana na kuwa inashabihiana na haki)). [8]

Tofauti baina yake na mali iliyochanganyika na haramu

Mali ya shubha ina tofauti na mali iliyochanganyika na haramu; kwa sababu katika mali iliyochanganyika na haramu, kuna elimu na ufahamu kamili kuhusiana na kuweko haramu ndani yake, lakini katika mali ya shubha kuna shaka kwamba, ni ya haramu au la. [9]

Hukumu za fikihi

Kumetajwa hukumu kadhaa kuhusiana na mali ya shubha:

  • Kuwa kwake halali: Imeelezwa kuwa, mali ya shubha (utata) ni halali. [10] Hoja ya kuthibitisha hukumuu hii ni hadithi isemayo: ((کُلُ‏ شَیْءٍ هُوَ لَکَ حَلَالٌ‏ حَتَّی‏ تَعْلَمَ‏ أَنَّهُ‏ حَرَامٌ‏ بِعَیْنِهِ)); Kila kitu kwako ni halali mpaka utakapofahamu kwamba ni haramu katika uhalisi na dhati yake. [11] [12] Madhumuni ya hadithi hii kuashiria asili ya ruhusa ((اصالة الاباحة)). [13]
  • Kutokuwa na khumsi: Mali yenye shubha na utata haina khumsi; kwa maana kwamba, haitolewi khumsi; [14] kinyume na mali ambayo imechanganyika na haramu ambayo kutokana na kuchanganyika kwake na haramu ina khumsi yaani inatolewa khumsi. [15]
  • Kuhiji na mali ya shubha: Kwa mujibu wa nadharia na mtazamo wa mafuqahaa (wanazuoni wa elimu ya fiq’h), mtu anaweza kuhiji na mali ya shubha na hakuna tatizo kufanya hivyo. Kwa maana kwamba, ibada yake ya Hija inasihi kwa kuhiji na mali kama hii ambayo haifahamiki ni ya halali au ni ya haramu. [16] Hata hivyo kwa mujibu wa fat'wa ya Ayatullah Nasser Makarem Shirazi, kwa sharti kwamba, kidhahiri iwe imepatikana kwa njia ya halali. [17]

Tahadhari kuhusiana na kitu chenye shubha

Katika vitabu vikubwa na jumuishi vya hadithi kuna riwaya na hadithi zilizonukuliwa ambazo madhumuni yake yanaonyesha juu ya kuchukua tahadhari kuhusiana na kitu chenye shubha na utata ndani yake. Miongoni mwazo ni:

  • Acha kile ambacho kinakutia shaka, na chukua kile ambacho hakina shaka ndani yake: ((دَعْ مَا یُرِیبُكَ إِلَی مَا لَا یُرِیبُكَ‏)). [18]
  • Mwenye kuacha mambo yenye shubha ndani yake ameoko na mambo ya haramu na mwenye kuchukua yenye shubha ndani yake ametenda mambo ya dhambi: ((مَنْ تَرَكَ الشُّبُهَاتِ نَجَا مِنَ الْمُحَرَّمَاتِ وَ مَنْ أَخَذَ بِالشُّبُهَاتِ ارْتَکَبَ الْمُحَرَّمَات‏)). [19]
  • Kusimama katika jambo la shuba (na kutolifanyia kazi) ni bora kuliko kuangamia: ((الْوُقُوفُ عِنْدَ الشُّبْهَةِ خَیْرٌ مِنَ الِاقْتِحَامِ فِی الْهَلَکَةِ))[20]

Imam Ruhullah Khomeini amezijaalia hadithi hizi kuwa zina upande wa kutoa muongozo na dira kwa ajili ya kujiweka mbali na mambo ya haramu na hajakubaliana na suala la kuwa makuruhu kutumia mali yenye shubha kwa mujibu wa fikihi. [21]Muhammad Taqi Majlisi, mmoja wa Maulamaa wa madhehebu ya Shia wa karne ya 11 Hijria, anasema: Licha ya kuwa mali ya shubha ni halali kuitumia, lakini kwa mujibu wa hadithi ni bora kujitenga nayo mbali, ili isije ikapelekea kufanya mambo ya haramu. [22] Baadhi ya wanazuoni kwa kuzingatia hadithi zilizotangulia hapo juu wanasema kuwa, kuna haja ya kuepuka na kutoifanyia kazi mali ya shubha ili kupambana na mali ya shubha, na madhali haijapatikana yakini na uhakika kuhusiana na kuwa kwake ni mali ya halali, haipasi kutumia mali kama hiyo. [23]

Imeelezwa kuwa, kuacha mali na chakula chenye shubha na utata ni katika daraja za uchaji Mungu, ambayo ni maarufu kwa jina la hofu na uchaji Mungu wa waja wema. [24] Baadhi ya Maulamaa wamenukuliwa wakisema kuwa, walikuwa wakichukua tahadhari wanapokutana na tonge (riziki) la shubha na kama baadhi ya wakati ikitokea kwamba, wamekula chakula chenye shubha na utata ndani yake (kisichojulikana uhalali na uharamu wake) na kisha wakafahamu kwamba, kilikuwa chakula chenye shubha na utata, kama kulikuwa na uwezekano walikuwa wakikirejesha. [25]

Rejea

  1. Tazama: Shahid Thani, Masalik al-ifham, 1413 H, juz. 4 uk. 334
  2. Al-hadaiq al-nadhwira, 1405 H, juz. 21, uk. 197; Naraq, Awaid al-ayyam, 1417 H, uk. 144; Najafi, Jawahir al-kalam, Dar ihya turath al-arab, juz.26, uk. 328
  3. Tusi, Amali, 1414 H, uk. 381

Vyanzo

  • Imam Khomaini, Sayyied Rohullah. Al-Makasib al-Muharramah. Qom: Muassasah Tanzhim wa Nashr Athar Imam Khomaini, cet. I, 1415 H.
  • Bahrani, Yusuf bin Ahmad. Al-Hadaiq al-Nadhirah fi Ahkam al-'Itrah al-Thahirah. Qom: Daftar Intisharat-e Eslami, cet. I, 1405 H.
  • Hur Amili, Muhammad bin Yusuf. Wasail al-Shiah. Qom: Muassasah Āl al-Bait, cet. I, 1409 H.
  • Dehkhuda, Ali Akbar. Loghatnameh. Tehran: Daneshgah-e Tehran, cet. II, 1377 S.
  • Shahid Thani, Zainuddin bin Ali. Masalik al-Afham ila Tanqih Sharai' al-Islam. Qom: Muassasah al-Ma'arif al-Islamiyah, cet. I, 1413 H.
  • Tusi, Muhammad bin Hasan. Al-Amali. Qom: Dar al-Thaqafah, cet. I, 1414 H.
  • Allamah Majlisi, Muhammad Baqir. Bihar al-Anwar. Beirut: Dar Ihya al-Turath al-Arabi, crt. II, 1403 H.
  • Allamah Majlisi, Muhammad Baqir. Mir'at al-'Uqul fi Sharh Akhbar Āl al-Rasul. Diteliti oleh Hasyim Rasuli Mahallati. Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyah, cet. II, 1404 H.
  • Kulaini, Muhammad bin Yaqub. Al-Kafi. Diteliti oleh Ali Akbar Ghaffari dan Muhammad Akhundi. Teheran: Dar al-Kutub al-Islamiyah, cet. IV, 1407 H.
  • Mazandarani, Muhammad Shalih bin Ahmad. Sharh al-Kafi (al-Ushul wa al-Raudhah). Diteliti dan direvisi oleh Abul Hasan Sya'rani. Teheran: Dar al-Kutub al-Islamiyah, cet. I, 1382 H.
  • Majlisi, Muhammad Taqi. Raudhat al-Muttaqin fi Sharh Man La Yahdhuruhu al-Faqih. Diteliti dan direvisi oleh Husain Musawi Kermani dan Alipanah Isytihardi. Qom: Muassase Farhanggi Eslami Kushanpur, cet. II, 1406 H.
  • Mahmudi, Muhammad Ridha. Manasek-e Haj (Muhassya). Teheran: Nashr-e Mash'ar, 1429 H.
  • Makarim Shirazi, Nashir. Manasek-e Jame'-e Haj. Qom: Madrasah Imam Ali bin AbinThalib as cet. I, 1426 H.
  • Muntazeri, Husain Ali. Mabani Feqhi Hokumat-e Eslami. Terjemahan Mahmud Shalawati dan Abul Fadhl Shakuri. Qom: Muassasah Keyhan, cet. I, 1409 H.
  • Najafi, Muhammad Hasan. Jawahir al-Kalam fi Sharh Sharai' al-Islam. Beirut: Dar Ihya al-Turath al-Arabi, cet. VII, tanpa tahun.
  • Naraqi, Ahamd bin Muhammad Mahdi. 'Awaid al-Ayyam fi Bayan Qawaid al-Ahkam. Qom: Muassasah al-Ma'arif al-Islmiyah, cet. I, 1417 H.
  • Warram, Warram bin Abi Faras. Majmu'ah Warram (Tanbih al-Khawathir wa Nuzhat al-Nawazhir). Qom: Maktabah Fiqhiyah. Cet. I, 1410 H.
  • Sheikh Answari, Sheikh Murtadha. Faraid al-Ushul. Qom: Majma al-Fikr al-Islami, cet. I, 1419 H.
  • Thabathabai Yazdi, Sayyied Muhammad Kazhim. 'Urwah al-Wutsqa fi ma Ta'ummu bihi al-Balwa (Muhassha). Diteliti dan direvisi oleh Ahmad Mohseni Sabzawari. Qom: Daftar Insharat-e Eslami, cet. I, 1419 H.
  • Malik Ahmadi, Ali Ashghar. Darsnameh Rezq-e Halal. Masyhad: Muassasah Muthalaat Rahburdi Ulum wa Ma'arif-e Eslam, cet. I, 1391 S.
  • Nahjul Balaghah. Revisi Subhi Shalih. Qom: Hijrat cet. I, 1414 H.