Mali iliyochanganyika na haramu

Kutoka wikishia

Mali ya halali iliyochanganyika na haramu (Kiarabu: المال الحلال المخلوط بالحرام) ni mali ambayo, sehemu yake imepatikana kwa njia ya kisheria (halali) na sehemu yake nyingine imepatikana kwa njia isiyo ya kisheria (haramu).[1] Tofauti baina yake na mali yenye utata ni kwamba, mali yenye utata kuna shaka kuhusiana na kuchanganyika kwake na haramu.[2] Kwa maana kwamba, kuna shaka tu, hakuna uhakika wa mia kwa mia kwamba, mali hii imechanganyika na haramu.

Katika fiq’h ya Kiislamu, haijuzu kutumia mali ya halali ambayo imechanganyika na haramu.[3] Kwa mujibu wa mtazamo wa mafakihi wa Kishia, kama kiwango cha haramu na mwenye mali ya haramu vitafahamika, ni wajibu kuirejesha mali hiyo ya haramu kwa mwenyewe.[4] Lakini kama kiwango cha mali ya haramu kitafahamika lakini, mmiliki asifahamike, kwa mujibu wa fat’wa ya kundi la mafakihi, ni lazima kutoa sadaka kiwango hicho kwa niaba ya mmiliki na kwa mujibu wa tahadhari ya wajibu anapaswa kuchukua idhini kutoka kwa mtawala wa kisheria (fakihi aliyekamilisha masharti).[5] Na mkabala wake, kama mmiliki wa mali atafahamika, lakini ikawa haifahamiki kiwango cha mali ambayo ni haramu ambacho kimechangayika na mali hiyo ya halali, kwa mujibu wa kauli ya wazi ya kundi la mafakihi, ni lazima kumridhisha na kama hakuridhia, ni lazima kumpatia kiwango fulani ambacho kitapelekea kupatikana yakini.[6]

Lakini ikiwa haifahamiki mmiliki wake wala kiwango cha mali ya haramu iliyochangayika na halali, mafakihi wa Kishia wanaamini kwamba, mali hiyo itaingia katika moja ya maeneo saba ya wajibu wa khumsi[7]. Fat’wa hii ni mtazanmo na raia mashuhuri ya Mamujitahidi wa Kishia.[8] Imeelezwa pia ya kwamba, kwa Waislamu wa madhehebu ya Kisunni sio wajibu kuitolea khumsi mali ambayo imechanganyika na haramu.[9]

Ikiwa baada ya kuitolea khumsi mali ya halali iliyochanganyika na haramu akatokea mmiliki wake, kwa mujibu wa rai ya baadhi ya Marajii Taqlidi kama Imamu Khomeini, Sayyid Ali Sistani na Makarem Shirazi kwa mujibu wa tahadhari ya wajibu (Ihtiyat Wajib), inapaswa kumpatia mhusika huyo kiwango fulani cha mali, na kwa mujibu wa kundi jingine Marajii kama Sayyid Abu-Qassim Khui, Golpaygani, Araki na Mirza Jawad Tabrizi, sio lazima kumpatia kitu.[10]

Rejea

  1. Muntaẓirī, Mabānī-yi fiqhī-yi ḥukūmat-i Islāmī, juz. 6, uk. 184.
  2. Muntaẓirī, Mabānī-yi fiqhī-yi ḥukūmat-i Islāmī, juz. 6, uk. 184.
  3. Tazama: Sheikh Anṣārī, Kitāb al-khums, uk. 111; Shahīd al-Thānī, Masālik al-ifhām, juz. 3, uk. 141.
  4. Baḥrānī, al-Ḥadāʾiq al-nāḍira, juz. 12, uk. 364; Iṣfahānī, Wasīlat al-najāt, juz. 1, uk. 318.
  5. Imām Khomeinī, Tawḍīh al-masāʾil, Mada ya 1814.
  6. Khomeinī, Tawḍīh al-masāʾil, Mada ya 1815.
  7. Tazama: Najafī, Jawāhir al-kalām, juz. 16, uk. 69; Khomeinī, Tawḍīh al-masāʾil, juz. 2, uk. 47.
  8. Shāhrūdī, Farhang-i fiqh muṭābiq bā madhhab-i Ahl al-Bayt, juz. 3, uk. 499; Iṣfahānī, Wasīlat al-najāt, juz. 1, uk. 318; Khomeinī, Tawḍīh al-masāʾil, Mada ya 1813.
  9. Anṣārī Shīrāzī, Mawsūʿat aḥkām al-aṭfāl wa adillatihā, juz. 1, uk. 470.
  10. Khomeinī, Tawḍīh al-masāʾil, Mada ya 1817.

Vyanzo

  • Anṣārī Shīrāzī, Qudrat Allāh. Mawsūʿat aḥkām al-aṭfāl wa adillati-hā. Qom: Markaz-i Fiqhī-yi Aʾimma Aṭhār, 1429
  • Baḥrānī, Yūsuf al-. Al-Ḥadāʾiq al-nāḍira fī aḥkām al-ʿitrat al-ṭāhira. Edited by Muḥammad Taqī Irawānī and Sayyid ʿAbd al-Razzāq al-Muqarram. Qom: Intishārāt-i Islāmī, 1405 AH.
  • Imām Khomeinī. Tawḍīh al-masāʾil. Edition 8. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1424 AH.
  • Iṣfahānī, Abu l-Ḥasan. Wasīlat al-najāt. Qom: Intishārāt-i Mehr-i Ustwār, 1993.
  • Muntaẓirī, Ḥusayn ʿAlī. Mabānī-yi fiqhī-yi ḥukūmat-i Islāmī. Translated by Maḥmūd Ṣalawātī and Abu l-Faḍl Shakūrī. Qom: Muʾassisa-yi Keyhān, 1409 AH.
  • Najafī, Muḥammad al-Ḥasan al-. Jawāhir al-kalām fī sharḥ sharāʾiʿ al-Islām. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1404 AH.
  • Shahīd al-Thānī, Zayn al-Dīn b. ʿAlī. Masālik al-ifhām ilā tanqīh sharāyiʿ al-Islām. 1st edition. Qom: Muʾassisat al-Maʿārif al-Islāmīyya, 1413 AH.
  • Shāhrūdī, Sayyid Maḥmūd. Farhang-i fiqh muṭābiq bā madhhab-i Ahl al-Bayt. Qom: Muʾassisat Dāʾirat al-Maʿārif al-Fiqh al-Islāmī, 1426.
  • Shaykh Anṣārī, Murtaḍā b. Muḥammad Amīn. Kitāb al-khums. Qom: Kungira-yi Jahānī Buzurgdāsht-i Sheikh Aʿzam Anṣārī, 1415 AH.