Kutawasali kupitia wafu

Kutoka wikishia

Kutawasali kupitia wafu (Kiarabu:التوسل بالموتى أو التوسل بالأموات): Makala hii inazungumzia dhana ya tawassul au kutawasali, ambacho ni kitendo cha kutafuta wasila (njia) kupitia kwa watu wema waliokuwa tayari wamesha kufa, hasa Mitume na Maimamu (a.s), ili kufikia mahitaji na matilaba maalumu ya mwenye kutawasali.

Imani hii inategemea kukubalika kwa dhana za Barzakh (uwanja wa maisha uliopo kati ya maisha ya duniani na Akhera), na uwezo wa kuwasiliana na kutafuta msaada kutoka kwa wafu.

Wanazuoni wa Kishia na baadhi ya wanazuoni wa Kisunni wanaiunga mkono "tawassul". Uungaji mkono huo umeegemea kwenye Aya za Qur'an pamoja na mazoea na tabia za Ahlul-Bayt (a.s) na baadhi ya masahaba kutawasali kwa Mtume baada ya kufa kwake. Hata hivyo, Mawahabi wanapinga mazoea hayo na kuyachukulia kuwa ni shirki.

Kulingana na wanazuoni wa Kiislamu, hakuna tofauti kati ya kutawasali kwa waja wa Mwenyezi Mungu katika wakati wa uhai wao na baada ya kufa kwao. Kama ilivyo wakati wa uhai wa Bwana Mtume (s.a.w.w) na waja wengine wa Mwenyezi Mungu, kwamba tunaweza kwenda kuwaomba watusaidie kwa kumwomba Mwenyezi Mungu kwa ajili yetu na kutuombea msamaha. Kwa hivyo, baada ya kufa kwao,pia tunaweza kuwaomba ombi hilo.

Welewa wa dhana

Kutawasali kwa wafu maana yake ni: Kumwomba Mwenye Ezi Mungu kwa kupitia jaha za watukufu wa kidini, watakatifu ambao kutokana na ukamilifu walionao, baada ya kufariki kwao Mwenyezi Mungu amewaweka karibu yake. [1]

Maisha ya Barzakhi na usikivu wa maiti

Ukubalikaji wa suala la kutawasali kutoka kwa wafu lenye maana ya kuomba msaada na kuwasiliana na roho za watu waliokufa, unategemea Imani ya uwepo wa maisha ya Barzakh, maisha ambayo yanaaminiwa kuwepo baina ya ulimwengu huu wa kimwili na ulimwengu wa Akhera, na uwezekano wa kuwasiliana kati ya walio hai na roho zilizoko katika ulimwengu huo na uwezekana wa kusikia sauti za walio hai. [2]

Uhalali

Vile vile tazama: Tawassul

Uhalali ni hali ya kitu kujuzu na kuwa halali au kuwa sahihi kisheria. Katika suala hili, ili kutoa uhalali kwa suala la kutawasali kwa wafu, wanazuoni wa Kiislamu wametoa vielelezo kadhaa vilivyo tegemea Aya za Qur'an, nyenendo za Watu wa nyumba ya Mtume, pamoja na nyenendo za Waislamu kwa jumla. Miongoni mwa vielelezo hivyo ni:

Qur'ani

Kwa ajili ya kusimamisha hoja juu ya uhalali wa kutawasali, wanazuoni wametumia vielelezo vya Aya za Qur'ani katika kuunga mkono hoja ya kumtumia mtu aliyekufa kama mwombezi. Miongoni mwa Aya hizo ni Aya ya 64 ya Surat an-Nisaa ambayo inawahimiza waumini kumwomba Mtume awaombee msamaha. Aya hii haikufunga pendekezo la kumwomba Mtume katika zama maalumu, hivyo wanazuoni wametumia maelezo hayo huria ya Aya hiyo, kama ni ithibati ya uhalali wa kufanya hivyo katika zama za uhai wa Mtume na hata baada ya kufa kwake. [3] Pia wametumia Aya ya 35 ya Surat al-Ma'idah ambayo inaruhusu ruhusa huria ya kutumia mwombezi. Kupitia ruhusa huria (مطلق) hiyo, wao wameweza kuitumia Aya hii kama ni kielelezo cha ruhusa ya kuwatumia wachamungu ambao ni mitume Maimamu na mawalii wa Mungu wawe ni mawakili waombezi wa kutuombea mbele ya Mungu, wawe hai au hata baada ya kufariki kwao. [4]

Nyenendo za Maimamu wa Kishia

Kulingana na baadhi ya vyanzo fulani, Maimamu wa Shia wametawasili kwa bwana Mtume (s.a.w.w) baada ya kifo chake. Imam Ali (a.s) [5] na Imam Hussein (a.s) pia nao wametawasili kwa bwana Mtume (s.a.w.w) baada ya kifo chake. [6] Imam Sajjad (a.s) naye hakutafautisha katika kutawasali kwa Masumina kumi na wanne katika hali ya uhai wao au baada ya kufa kwao. [7] [Maelezo 1]

Pia katika miongoni mwa dua zilizothibiti kutoka kwa Ahlul-Bait (a.s) kama vile dua iitwayo Dua-u Sarii’u al-Ijaabah inaonesha kwamba; kuomba kutawasali kupitia mawalii wa Mwenye Ezi Mungu baada ya baada ya kufa kwao, ni miongoni mwa mambo yaliyo pendekezwa. [8]

Nyenendo za Masahaba

Katika vyanzo vya Sunni, kuna ripoti za baadhi ya masahaba na Waislamu waliokuwa wakitafuta shufaa (wakitawasali) kupitia kwa bwana Mtume (s.a.w.w) baada ya kifo chake. Baadhi yao ni pamoja na:

  • Aisha: Aisha alitawasali kwa Mtume (s.a.w.w) na kaburi lake ili kupunguza ukame na tatizo la njaa. [9]
  • Mtu mmoja: Bwana huyu alitawasali kwa Mtume wakati wa zama ukhalifa wa Othmani, akiongozwa na Othmani bin Hanifu katika kulekea kwenye kaburi la bwana Mtume. [10][Maelezo 2]
  • Bilal bin Harithi: Yeye alitawsali kwa Mtume (s.a.w) ili kuomba mvua. [11]
  • Kulingana na ripoti, Malik ibn Anas alimfundisha Mansur Dawaniqi jinsi ya kumzuru (kumsalia sala maalumu) bwana Mtume (s.a.w.w) na kutafuta shufaa (kutawasali) kutoka kwake (s.a.w.w). [12]

Mtazamo wa Masunni

Wanazuoni wengi wa madhehebu ya Sunni wamejuzisha kutawasali kupitia waumini walikwisha tanguli mbele ya haki, nao walikuwa na kawaida ya kutawasali kupitia mawalii wa Mwenye Ezi Mungu. Kati ya wanazuoni walio fanya hivyo ni:

  • Samhudi, mwanachuoni wa madhehebu ya Shafi'i wa karne ya 10 Hijiria, ameeleza katika kitabu chake Wafā'u al-Wafā' bi-akhbār Dār al-Mustawfā ripoti za watu ambao wamepata mahitaji yao kwa kuomba msaada kwa kwa bwana Mtume (s.a.w.w). Pia yeye Anaamini kuwa; kuomba msaada, kutawasali na kuombea msamaha mbele ya Mwenyezi Mungu, kupitia jaha ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), ilikuwa ni miongoni mwa matendo ya manabii na watu wema. Kwa mtazamo wake, jambo hili lilikuwa likifanywa katika kila zama, hata kabla ya uumbwaji bwana Mtume (s.a.w.w) na baada ya kuumbwa, akiwa duniani na hata akiwa kaburini. [13]
  • Abu Ali Khalali amesema kwamba; kila mara alipopata shida, alikwenda kumtembelea Imamu Kadhim (a.s) na kuomba msaada kwake, na haitimae alikidhiwa shida yake. [14] Pia kuna ripoti isemayo kwamba; Imamu Shafi'i akizungumzia kaburi la Imamu Kadhim (a.s) amesema kwamba; "kaburi lake ni ponyo lenye kuponya maradhi". [15]
  • Alusi naye katika tafsiri yake “Ruhu al-Ma’ani”, baada ya kutaja baadhi ya ripoti za kihistoria na Hadithi kuhusu kuomba msaada (kutawasli) na kuchambua kwa kina suala hilo, amefikia hitimisho lisemalo kwamba; hakuna kizuizi juu ya kumwakilisha Mtume (s.a.w.w) katika kuomba msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa, iwe katika maisha ya bwana Mtume au baada ya kifo chake. Baada ya uchambuzi marefu juu ya mada hii, yeye amekiri kwamba; hata kuomba msaada mbele ya Mwenyezi Mungu kupitia jaha ya mtu mwingine asiyekuwa Mtume (s.a.w.w) pia hakuna inafaa, kwa sharti kwamba awe kweli ni mwenye hadhi mbele ya Mwenye Ezi Mungu. [16]
  • Asqalani, baada ya kutaja kisa cha Omar bin Khatab kumwomba Ibn Abbas aombe dua ya kupata mvua, anakiri kwamba kuomba msaada (kutawasali) kupitia watu wema, na hasa Ahlul Bait (a.s), ni miongoni mwa mambo ya sunna. [17]

Mtazamo wa Kiwahabi

Wahubabi hawaruhusu na hawakubaliani uhalali wa kuomba msaada au kutawasali kupitia watu walio kwisha fariki. Ibn Taymiyyah (ambaye Mawahabi hutegemea maoni yake) anaamini kwamba; kuomba msaada kupitia jaha ya bwana Mtume (s.a.w.w) na watu wema, ni halali tu wakati wa maisha yao, na kuomba msaada kwao baada ya kifo chao, ni jambo la shirki. [18]

Jawabu

Kwa maoni ya wafuasi wa wanaounga mkono uhalali wa kutawasali ni kwamba; hakuna tofauti kati ya kutawasali na kuomba msaada katika zama za maisha ya Mtume (s.a.w.w) na mawalii wa Mungu, na baada ya kifo chao. Kwa hiyo kama ilivyokuwa halali kufanya katika maisha yao basi pia itakuwa ni halali baada ya kufa kwao. [19] Pia, katika kusisitiza hoja yao juu ya suala hili, wametoa kielelezo cha Aya ya 64 ya Surat al-Nisaa isemayo: ((وَلَوْ أنَّهُمْ إذْ ظَلَمُوا أنْفُسَهُمْ جَاءُوک فَاسْتَغْفَرُوا اللهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللهَ تَوَّاباً رَحِیماً Bila shaka, laiti pale walipo jidhulimu nafsi zao (kwa kutenda dhambi), wangelikujia wewe, na wakamuomba Allah msahama (kwa kutawasali kwako) nawe ungeliwaombea msamaha, basi wangelimkuta Allah ni Msamehevu na Mhurumivu.)) Aya hii imetumika kama ni kielelelezo tosha juu ya uhalali wa kutawasali, na kwa kuwa Aya hii imetoa idhini huria ya kutawasali kwa bwana Mtume (s.a.w.w), hii imefanya wanazuoni kujuzisha jambo hilo, iwe ni wakati wa maisha yake au baada ya kifo chake. [20] Pia nyenendo za Masahaba zinaonesha kwamba; jambo la kutawasali lilikuwa ni jambo halali. [21]

Mada zinazo fungamana

Maelezo

  1. (إنا نتوسل إلیک بمحمد صلواتک علیه وآله رسولک، و بعلی وصیه، و فاطمة ابنته، و بالحسن والحسین، وعلی و محمد و جعفر و موسی و علی و محمد وعلی والحسن والحجة علیهم‌السلام أهل بیت الرحمة); “Hakika sisi tunatawasali kwako (tunashika mashiko ya kukufikia wewe Mola wetu) kupitia Muhammad sala na amani yako iwe juu yake pamoja na Aali zake, ambaye ni Mtume wako, na tunatawasali kwako kupitia Ali wasii wa Mtume, na Fatima ambaye ni bint wa Mtume, na kwa kupitia kwa Hassan na Hussein, na Ali pamoja na Muhammad, na Ja’afar, na Musa, na Ali, na Muhammad na Ali na Hassan na kwa kupitia kwa Hujjah (Imamu Mahdi), amani ziwe juu yao watu wa nyumba ya rehema (nyumba ya Mtume)”.
  2. Othman bin Hunifu alimwomba mtu huyo aombe msaada (atawasali) kwa Mtume kupitia maneno haya: اللّهمّ إنّی أسألک وأتوجّه إلیک بنبیک محمّد صلّی اللَّه علیه وسلّم نبی الرحمة، یا محمّد! إنّی أتوجّه بک إلی ربّی فتقضی لی حاجتی ; Ewe Mwenye Ezi Mungu! Ninakuomba na ninaelekea Kwako kupitia mwakilishi Wako Mtume Muhammad (s.a.w.w), Mtume wa Rehema. Ewe Muhammad! Ninakutanguliza wewe mbele ya Mwenye Ezi Mungu, ili unitikie ombi langu (uniombee haja yangu ikidhiwe). Rejea:(Tabrani, Al-Mu'ujam al-Kabir, 1406 AH, juzuu ya 9, ukurasa wa 30.)