Nenda kwa yaliyomo

Juwayn bin Malik Taymi

Kutoka wikishia
Makaburi ya Mashahidi wa Karbala katika Haram ya Imamu Hussein (a.s)

Juwayn bin Malik bin Qays Taymi (Kiarabu: جُوَيْنُ بْنُ مَالِك بْنُ قَيسٍ التَّيْمِيُّ) (kuuawa shahidi: 61 H) alikuwa mmoja wa mashahidi wa Karbala waliokuja Karbala kutoka Kufa na Jeshi la Omar bin Sa’d kupigana na Imamu Hussein (a.s), lakini wakati pendekezo la Imamu Hussein (a.s) lilipokataliwa na Ibn Ziyad na vita vikaanza, akiwa na watu saba [1] wa kabila lake kama ilivyoelezwa aliungana na Imamu Husein (a.s) wakati wa usiku. [2]

Katika Ibsar al-Ayn, imesimuliwa kutoka kwa Ibn Shahrashub kwamba, aliuawa shahidi siku ya Ashura katika shambulio la kwanza la jeshi la Ibn Sa'd. [3]

Sheikh Tusi amemuorodhesha miongoni mwa masahaba wa Imam Hussein (a.s). [6] Baadhi wamenukuu jina lake kuwa ni Juwayr bin Malik au Huwai bin Malik. [7] Wengine wamemchanganya na John mtumwa wa Abu Dharr. [8]

Katika Ziyarat al-Shuhadaa, anatajwa kwa ibara ya:«اَلسَّلَامُ عَلَی جُوَینِ بْنِ مَالِک الضُّبَعِی ; Amani iwe juu ya Juwayn bin Malik al-Dhubai».[9]

Rejea

Vyanzo