Nenda kwa yaliyomo

Iltimas al-Dua’

Kutoka wikishia

Iltimas al-Dua (Kiarabu: التماس الدعاء) ni neno linalotumika kumuomba au kuwaomba watu wengine kukuombea dua za kheri. [1] Kwa maana kwamba, wakati wanaomba dua basi wakuombee na wewe. Kikawaida ombi hili hutolewa kwa mtu anayekwenda kufanya ziara katika maeneo matakatifu au ambaye anafanya ibada fulani. [2]

Kwa mujibu wa hadithi mbalimbali mafakihi wa Kishia [3] wanasema kuwa, ni mustahabu kwa anayemtembelea mgonjwa amuombe amshirikishe katika dua zake yaani amuombee. [4] Kadhalika imekokotezwa kwamba, baada ya kumsaidia fakiri umuombe akuombee dua; kwani dua ya fakiri hukubaliwa pale amuombeapo mtu aliyemsaidia. [5]

Baadhi ya mafakihi wamelitambua kuwa ni mustahabu suala la kuwaomba waumini wawaombee wengine dua ya kheri. [6] kwa mujibu wa hadithi, Mwenyezi Mungu alimtaka Nabii Mussa amuombe yeye kwa ulimi ambao haujatenda dhambi na baada ya Nabii Mussa kuuliza kwamba, hilo linawezekana vipi. Allah akambwambia amuombe kupitia kwa asiyekuwa yeye. [7] Sio wajibu kujibiwa takwa la mtu ambaye umemuomba akuombee dua yaani akushirikishe katika dua na maombi yake. [8]

Kwa mujibu wa Aya ya 97 ya Surat Yusuf baadhi ya mafakihi wameitambua iltimas al-Dua (kuomba mtu akuombee) kuwa inajumuisha pia kusamehewa dhambi (maghufira) na Mwenyezi Mungu; [9] kwa mujibu wa Aya hii, ndugu zake Nabii Yusuf (a.s) baada ya kujuta kwa kumtupia Yusuf kisimani walimuomba baba yao Nabii Ya’qub (a.s) awaombee maghufira na msamaha kwa Mwenyezi Mungu. [10]

Kuomba dua kwa wafu

Katika suala la kutaka kuombewa dua na mtu (iltimas al-Dua) Waislamu wa madhehebu ya Shia hawajatofautiasha baina ya aliye hai na aliyekufa na wanaamini kwamba, inajuzu pia kufanya Iltimas al-Duua kwa aliyekufa. [11] Mkabala na wao kuna kundi la Mawahabi ambalo linapinga na kuona kuwa kuomba dua wafu hatakwa Mtume (s.a.w.w) haifai na ni bidaa na uzushi. [12] Hoja ya Mawahabi ni kwamba, maiti hawasikii sauti za walio hai [13] na kwamba, hakuna sahaba yeyote miongoni mwa masahaba wa Mtume (s.a.w.w) ambaye alifanya jambo hili. [14] Wanazuoni na wasomi wa Kishia wanasema kuwa, maiti anasikia sauti za walio hai [15] na masahaba baada ya kuaga dunia Mtume (s.a.w.w) walikuwa wakimuomba dua za kheri. [16].

Rejea

Vyanzo