Nenda kwa yaliyomo

Hotuba ya Khutta al-Maut

Kutoka wikishia

Hotuba ya Khutta al-Maut (Kiarabu: خطبه خُطَّ المَوت), ni moja ya hotuba zilizotolewa na Imamu Hussein (a.s) kuhusu hamu na shauku ya kupata shahada (kujitoa muhanga kwa ajili ya Uislamu). Hotuba hii ilitolewa pale Imamu Hussein (a.s) alipokuwa akiondoka Makka kuelekea Iraq. Katika moja ya sehemu za hotuba hii, Imamu Hussein (a.s) alitaja mahali pa kuuawa kwake kuwa ni kati ya Karbala na Nawawis. Matini ya hotuba ya Khutt al-Maut imepatikana katika vitabu vya al-Malhuf na Kashfu al-Ghumma.

Hotuba hii ni kioo safi kinacho akisi picha na hali halisi ya mandarin ya kidini na kijamii ya zama za Imamu Hussein (a.s). Kioo ambacho kinadhihirisha jinsi hali ilivyokuwa mbaya, kiasi ya kwamba Imamu aliwajibika kujitoa muhanga kwa ajili ya marekebisho ya jamii. Watafiti weengine wameeleza kwamba; hotuba hii ilitolewa katika mji wa Makka, huku wengine wakidai kuwa ilitolewa katika ardhi ya Madina.

Umuhimu Wake

Hotuba ya Khuṭṭ al-Maut iliyo ripotiwa kutoka katika vyanzo mbali mbali vya kihistoria, ni miongoni hotuba umuhimu mkubwa katika jamii za Kiislamu. Hotuba ilitolewa na Imamu Hussein (a.s) akiwa safarini kutoka mji wa Makka kuelekea Iraq. Kulingana na moja ya sehemu za hotuba hii, Imamu Hussein (a.s) alitaja wazi mahali pa kuuawa kwake, ambapo ni eneo lililoko kati ya Nawawis na Karbala.[1] Nawawis ilikuwa ni eneo karibu na kitongoji cha Karbala ambalo lilikuwa na makaburi ya Wakristo ndani yake, au kwa lugha nyengine, Karbala ilikuwa ni mava ya Wakristo.[2]

Hotuba ya Khuttal-Maut inachukuliwa kama ni kielelezo kitoacho picha kamili juu ya hali mandhari ya kidini na kijamii katika zama za Imamu Hussein (a.s), kwani Imamu Hussein (a.s) alitangaza azma yake ya kujitoa muhanga ili kulinda na kuhifadhi sheria ya Kiislamu. Kulingana na maelezo ya Sharif Qurashi katika kitabu chake Hayat Imamu Hussein (a.s), hali ya jamii ya Kiislamu ya wakati huo ilikuwa imefikia kiwango ambapo si rahisi jamii hiyo kutengemaa. Jamii ambayo ilikuwa ni jamii mfu, iliyo hitaji kitendo kikubwa kama kujitoa mhanga ili kuiamsha na kuleta mabadiliko ndani yake.[3] Wengine, kwa kutegemea hotuba hii, wametenganisha kati harakati za Imamu Hussein (a.s) na harakati nyinginezo, wakiona kwamba lengo kuu la harakati za Imam lilikuwa ni kufa shahidi.[4]Kwa Kulingana na mjengeko wa, hotuba ya Khutt al-Maut, inaonyesha wazi kuwa Imamu Hussein (a.s) aliona kuwa kufa kwake shahidi ndiko kungeliokoa na kurekebisha hali ya Uislamu, jambo ambalo linaendelea kuwa kiini cha kumbukumbu na heshima ya harakati aake miongoni mwa Waislamu, hasa wa dhehebu la Shia.

Hotuba ya Khutt al-Maut ni miongoni mwa hotuba zilizoripotia kutoka kwa Imamu Hussein (a.s), hotuba ambayo inapatikana katika vyanzo viwili vya karne ya saba Hijria: al-Malhuf[5] na Kashf al-Ghumma.[6] Allama Majlisi, katika kitabu chake maarufu Bihar al-Anwar, pia amenukuu hotuba hii kutoka vyanzo hivyo viwili.[7] Ingawa kuna tofauti ndogo tu za maneno kati ya matoleo ya al-Malhuf na Kashfu al-Ghumma, ila bado ujumbe wa hotuba hii umebaki kuwa na maana ile ile iliopo katika vyanzo viwili hivyo. [8] Hotuba hii bado inaendelea kuwa muhimu katika kuelewa azma na lengo la Imamu Hussein (a.s) katika harakati zake za Karbala, hasa kwa jinsi inavyoelezea kujitoa kwake muhanga ili kuuhifadhi Uislamu na kuleta mabadiliko ndani ya jamii ya wakati huo.

Maudhui za Hotuba ya Khutta al-Maut

Yaliyomo katika hotuba ya Khutta al-Maut yanajumuisha ufahamu wa dhana kuu ya shahada (kujitoa muhanga) na upendo wa kufa katika njia ya Mwenye Ezi Mungu. [9] Licha ya hayo, khutba hii fupi inawasilifa mambo mbalimbali ndani yake kama ifuatavyo:

  • Maelezo ya uzuri na kutoweza tengana kati kifo na mwanadamu, sawa na mkufu shingoni mwa binti fulani.[10]
  • Uhamasishaji wa Imamu Hussein (a.s) kuhusu kukubiliana na kifo na kuonana mababu zake waliotangulia mbele ya haki.[11]
  • Utoaji habari wa Imamu Hussein (a.s) kuhusiana na shahada [12] yake na jinsi hali itakavyokuwa.[13]
  • Kuwafananisha maadui zake na mbwa mwitu wa mbugani. [14]
  • Kuelezea ulazima wa kutokea kwa tukio hili na kuridhika na matakwa ya Mwenye Ezi Mungu.[15] [Maelezo 1][16]
  • Maelezo juu ya malipo ya Mwenye Ezi Mungu katika kuwalipe wavutao subira.[17]
  • Kueleza nafasi yake katika ujirani wake na bwana Mtume (s.a.w.w) baada ya shahada yake.[18]
  • Kuwahimiza Waislamu kuungana na Imamu Hussein (a.s).[19]

Mahala Ilipotolewa Hotuba Hii

Kwa mujibu wa maoni ya Sayyid Ibn Tawus, hotuba ya Khutta al-Maut ilitolewa na Imamu Hussein (a.s) wakati wa kuondoka kwake akielekea Iraq. Hata hivyo, Sayyid Ibn Tawus hakubainisha wazi mahali ilipotolewa hotuba hiyo.[20] Wakati baadhi ya wanazuoni wakiamini kuwa hotuba hii ilitolewa mjini Madina,[21] huku wengine wakidai kuwa ilitolewa mjini Makka.[22]

Matini na Tafsiri ya Hotuba

اَلْحَمْدُلِلهِ ما شاءَ اللهُ، وَ لا قُوَّةَ إِلاّ بِاللهِ، وَ صَلَّی اللهُ عَلی رَسُولِهِ، خُطَّ الْمَوْتُ عَلی وُلْدِ آدَمَ مَخَطَّ الْقَلادَةِ عَلی جیدِ الْفَتاةِ، وَ ما أَوْلَهَنی إِلی أَسْلافی اِشْتِیاقُ یعْقُوبَ إِلی یوسُفَ، وَ خُیرَ لِی مَصْرَعٌ اَنَا لاقیهِ. کَأَنِّی بِاَوْصالی تَقْطَعُها عَسْلانُ الْفَلَواتِ بَینَ النَّواویسِ وَ کَرْبَلاءَ فَیمْلاََنَّ مِنِّی اَکْراشاً جَوْفاً وَ اَجْرِبَةً سَغْباً، لا مَحیصَ عَنْ یوْم خُطَّ بِالْقَلَمِ، رِضَی اللهِ رِضانا اَهْلَ الْبَیتِ، نَصْبِرُ عَلی بَلائِهِ وَ یوَفّینا اَجْرَ الصّابِرینَ. لَنْ تَشُذَّ عَنْ رَسُولِ اللهِ(صلی الله علیه وآله) لَحْمَتُهُ، وَ هِی مَجْمُوعَةٌ لَهُ فی حَظیرَةِ الْقُدْسِ، تَقَرُّ بِهِمْ عَینُهُ وَ ینْجَزُ بِهِمْ وَعْدُهُ. مَنْ کانَ باذِلا فینا مُهْجَتَهُ، وَ مُوَطِّناً عَلی لِقاءِ اللهِ نَفْسَهُ فَلْیرْحَلْ مَعَنا فَاِنَّنِی راحِلٌ مُصْبِحاً اِنْ شاءَ اللهُ تَعالی[23]


Shukrani na Sifa zote njema ni za Mwenye Ezi Mungu, ayatakayo Mungu ndiyo yawayo, na hakuna uwezo wala nguvu ila kwa msaada wake. Na rehema za Mwenye Ezi Mungu ziwe juu ya Mtume wake, Muhammad (s.a.w.w). Fahamuni kwamba: Kifo ni kama mkufu ulioko shingoni mwa binti. Hamasa yangu ya kukutana na mababu zangu (baba yangu, mama yangu, babu yangu, na kaka yangu) ni sawa na hamu ya Nabii Ya’akubu ya kukutana na Yusuf. Mahala pa Kifo change cha kishahidi tayari pamesha ainisheshwa kwa ajili yangu, na hakika nitakifikia. Na ni kana kwamba naona mbwa mwitu wakali wa porini wakinikata vipande vipande nikiwa baina ya ardhi ya Nawaawis na Karbala, wakishibisha matumbo yao matupu na kujaza viriba vyao vya maji kupitia damu yangu. Hakuna njia ya kuepuka siku hiyo, kwani ni kadari ya Mwenye Ezi Mungu iliyokwisha pita tangu zamani. Ridhaa ya Mwenye Ezi Mungu ni ridhaa yetu, Sisi Ahlul Bait. Sisi tunavumilia majaribio ya Mwenye Ezi Mungu, na Yeye atatulipa thawabu kubwa kwa subira yetu. Kamwe pande ya mwili wa Mtume haitatenganishwa naye, na hatimae itaungana naye katika daraja za juu za Peponi, ambapo macho ya Mtume (s.a.w.w) yatang'ara kwa kukiona kizazi chake, na ahadi zake zitatimizwa kupitia kwao. Yeyote ambaye yupo tayari kutoa damu yake kwa ajili yetu basi anajitayarisha kukutana na Mwenye Ezi Mungu, na afuatane pamoja nasi, kwa kuwa mimi Mwenye Ezi Mungu akipenda, nitaondoka kesho asubuhi.[24]


Maelezo

  1. Sentensi isemayo: (رِضَی اللهِ رِضانا اَهْلَ الْبَیتِ ; Ridhaa ya Mweye Ezi Mungu ndiyo ridhaa yetu sisi Ahlu Al-Bait, inaweza kufasiriwa kwa maana ya kwamba “Limfurahishalo Mungu ndilo litufurahishalo sisi Ahlu Al-Bait) au pia inaweza kuwa na maana sawa na ile iliyoko katika ibara za Qur’ani: (رَضِی اللهُ عَنْهُمْ وَ رَضُوا عَنْهُ. Kwa maana ya kwamba: Ahlul-Bait wamefikia daraja ya kuridhiwa na Mola wao. Kwa maana ya kwamba wao wamemuabudu Mola wao hadi akawaridhia, huku wao pia wakiwa ni wenye kuridhika na Mola wao). Hii itakuwa na maana ya kwamba: Kutafuta radhi za Ahlul-Bait huwa ni sawa na kutafuta radhi Mwenye Ezi Mungu mwenyewe". Maelezo haya yametoka kwenye tovuti ya Waarithun, kwenye Makala ya Sherh Ziarate Jaamie.

Rejea

  1. Sharif Qureshi, Hayat al-Imam al-Hussein, juz. 2, uk. 295, 1385 H.
  2. Baladhuri, Futuh al-Buldan, uk. 179, 1988; Humawi, Mu'jam al-Buldan, juz. 5, uk. 254, 1995 M.
  3. Sharif Qureshi, Hayat al-Imam al-Hussein, juz. 2, uk. 295-296, 1385 H.
  4. Ma'ash, al-Imam al-Hussein 'alaihissalam wa al-Wahhabiyah, juz. 1, uk. 288, 1429 H.
  5. Sayid Ibnu Tawus, al-Malhuf, uk. 126, 1417
  6. Irbili, Kashf al-Ghumah, juz. 2, uk. 239, 1433 H.
  7. Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 44, uk. 366-367, 1403 H.
  8. Sayid Ibnu Tawus, al-Malhuf, uk. 126, 1417 H; Irbili, Kashf al-Ghumah, juz. 2, uk. 239, 1433 H
  9. Muhaddithi, Farhangg Ashura, uk. 161
  10. Sha'rani, Dam'u al-sujum, (tarjamaha kitab Nafs al-Mahmum), uk. 171-172, 1387.
  11. Sha'rani, Dam'u al-sujum, tarjamaha kitab Nafs al-Mahmum, uk. 171-172, 1387.
  12. Ma'ash, al-Imam al-Hussein alaihissalam wa al-Wahhabiyah, juz. 1, uk. 288, 1429 H.
  13. Sharif Qureshi, Hayat al-Imam al-Hussein, juz. 2, uk. 295, 1385 H.
  14. Husseini Tehrani, Lama'at al-Hussein, uk. 37-40.
  15. Yarane Mukhlis dar Qiyam Imam Hussein (a.s)» Paygah Itila'resani, Ayatullah Makarim Shirazi.
  16. Sha'rani, Dam'u al-sujum, tarjamaha kitab Nafs al-Mahmum, uk. 171-172, 1387.
  17. Sha'rani, Dam'u al-sujum, tarjamaha kitab Nafs al-Mahmum, uk. 171-172, 1387.
  18. Sha'rani, Dam'u al-sujum, tarjamaha kitab Nafs al-Mahmum, uk. 171-172, 1387.
  19. Sha'rani, Dam'u al-sujum, tarjamaha kitab Nafs al-Mahmum, uk. 171-172, 1387.
  20. Sayid Ibnu Tawus, al-Malhuf, uk. 126, 1417 H.
  21. Ali Tum'ah, Tarikh Marqad al-Imam al-Hussein wa al-Abbas, uk. 23, 1416 H.
  22. Sharif Qureshi, Hayat al-Imam al-Hussein, juz. 2, uk. 295, 1385 H.
  23. Sayid Ibnu Tawus, al-Malhuf, uk. 126, 1417 H; Irbili, Kashf al-Ghumah, juz. 2, uk. 239, 1433 H
  24. Yarane Mukhlis dar Qiyam Imam Hussein (a.s)» Paygah Itila'resani, Daftar Hazrat Ayatullah Makarim Shirazi; Sha'rani, Dam'u al-sujum, tarjamaha kitab Nafs al-Mahmum, uk. 171-172, 1387.

Vyanzo