Nenda kwa yaliyomo

Hadithi ya Bidh-'ah

Kutoka wikishia
Mchoro wa Hadith ya Bidh-'ah na mwandishi wa maandishi wa Iran Gholam Hussein Amirkhani.

Hadith ya Bidh-'ah (Kiarabu: حديث البضعة), ni moja ya hadithi za Mtume kuhusiana na bibi Fatimah (a.s) ambapo Mtume (s.a.w.w), kupitia Hadithi hiyo alimtambulisha bibi Fatimah (a.s) kama "kipande cha mwili wake" na akaifungamanisha furaha yake (s.a.w.w) na furaha ya binti yake (Fatima) kwa kusema; Furaha yake yeye ndio furaha yangu, na kukereka kwake ndio kukereka kwangu mimi. Hadithi hii imepokewa katika vyanzo vya Shia na Sunni. Hadithi ya (بضْعَةٌ) hutumika katika kuthibitisha mambo kadhaa kama vile; umaasuma (hali ya kutotenda dhambi) wa bibi Fatimah (a.s), mrengo wake wa haki katika tukio la Fadak, pia hutumika katika kuthibitisha ulazima na wajibu wa kuwaheshimu Ahlul-Bait (a.s).

Kwa mujibu wa baadhi ya ripoti kutoka katika vyanzo vya Sunni ni kwamba; Chanzo cha Hadithi hii kinahusiana na kisa cha Imamu Ali (a.s) kumposa binti ya Abu Jahal. Lakini kwa mujibu wa wanachuoni wa Kishia, riwaya hizo ni riwaya za uwongo na wapokezi wake wanatuhumiwa kughushi Hadith na kuwa na uadui na Ahlul-Bait (a.s).

Hadhi na nafasi ya matini ya hadithi

Hadithi hii hutumika kama ndio Hadithi tegemezi inayoandikwa juu ya nguo nyeusi ya msiba inayozungushiwa kaburi la Imamu Hussein (a.s), katika masiku maarufu yajulikanayo kwa jina la Ayyamu Fatimiyyah (Masiku ya Fatimiyyah). Matini yake ni kama ifuatavyo: فَاطِمَةُ بَضْعَةٌ مِنِّی ‏فَمَنْ آذَاهَا فَقَدْ آذَانِی و مَنْ سَرّها فَقد سَرّنی ; “Fatima ni sehemu ya mwili wangu, atakayemuudhi yeye atakuwa ameniudhi mimi na anayemfurahisha yeye amenifurahisha mimi”. Kitabu Al-Amali cha Sheikh Saduq, aliyefariki mwaka 1417 Hijiria, uk.165. Imesemwa katika Hadithi hiyo ya Bidh-'ah ya kwamba; Mtume (s.a.w.w) amesema kuhusu binti yake Fatimah (a.s): “Fatima ni sehemu ya mwili wangu, atakayemuudhi yeye atakuwa ameniudhi mimi na anayemfurahisha yeye amenifurahisha mimi”. [1] Muktadha wa Hadithi hii umepokewa katika vyanzo mbalimbali vya Shia na Sunni [2] Miongoni mwa wasimulizi wa Hadithi hii ni: Imamu Ali (a.s), [3] Ibnu Abbas, [4] Abu Dharri Al-Ghafari [5] na bibi Fatima Al-Zahra (a.s). [6]

Jalal al-Din Suyuti, mfasiri wa Kisunni, ameisimulia Hadithi hiyo na kusema kuwa; Hadithi hiyo inakubalika na pande zote mbili, za Kishia na Kisunni. [7] Mfasiri maarufu wa upande wa Kisunni Fakhru Al-Razi, ameitumia Hadithi hiyo kana ni dalili katika kufasiri baadhi ya Aya za Qur'an. [8]

Neno Bidh-‘ah (بضْعَةٌ) ni neno la Kiarabu lenye maana yake ni kipande cha mwili. [9] kwahiyo, inaposemwa mtu fulani ni "sampuli ya mwili wangu au ni kipande cha mwili wangu" huwa na maana ya sitiari inayomaanisha ukaribu uliopo baina ya mzungumzaji na mzungumzwaji, kana kwamba mtu huyo ni sehemu ya mwili wake. Pia aina hiyo ya sitiari imeonekana kutumiwa na bwana Mtume (s.a.w.w) akiwazungumzia Ali bin Abi Talib [11] na Imamu Ridha (a.s). [12]

Matumizi ya kitheolojia na kisheria (Kifiqhi)

Hadithi ya Bidh-‘ah (بضْعَةٌ) imetumika kuthibitisha baadhi ya mada za kitheolojiakama kama ifuatavyo:

  • Umaasuma wa bibi Fatimah (a.s): wanatheolojia wameitumia Hadith hii katika kuthibitisha umaasumu wa bibi Fatimah (a.s). [13] Kwa maoni ya mmoja wa wanazuoni wa Kishia, Ayatullah Ja'afar Subhani, aliyezaliwa mnamo mwaka wa (308 Shamsia), ni kwamba; Katika Hadithi ya Bidh-‘ah (بضْعَةٌ), Radhi na hasira za bibi Fatima ni sababu ya radhi na hasira za Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w). Kwa kuwa Mwenyezi Mungu anapendezwa na matendo mema tu na wala haridhii dhambi na uasi wa amri zake. Hivyo basi kama bibi Zahra (a.s) atakuwa amefanya dhambi, basi atakuwa ameifanya dhambi hiyo kutokana na kufurahishwa na dhambi hiyo, jambo ambalo Mungu amechukizwa nalo, hali ya kwamba katika Hadithi ya Bidh-‘ah (بضْعَةٌ) ridhaa ya Mwenyezi Mungu zimehusishwa moja kwa moja na ridhaa za bibi Fatima (a.s). [14]
  • Ubora wa bibi Fatimah (a.s) juu ya wanawake wa ulimwengu mzima: Shahabuddin Alusi, mfasiri wa Kisunni (aliyefariki mnamo mwaka wa 1270 Hijiria), kwa kutumia hadithi hii chini ya Aya isemayo: (وَإِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَهَ اصْطَفَاكِ وَطَهَّرَكِ وَاصْطَفَاكِ عَلَىٰ نِسَاءِ الْعَالَمِينَ ; “Na Malaika waliposema, ewe Mariamu, kwa hakika Mwenyezi Mungu amekutewa, na akakutakasa, kisha akakuteuwa juu ya wanawake wa ulimwenguni.") [15] Yeye amethibitisha ubora wa bibi Fatima na bibi Mariam (a.s) juu ya wanawake wa ulimwenguni. [16]
  • Ushahidi juu ya mrengo wa haki wa bibi Fatimah (a.s) katika tukio la Fadak. [17] Baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), bibi Fatima Al-Zahra (a.s) aliitumia Hadithi hii katika maandamano yake dhidi ya Sheikhain (Abu Bakar na Omar). [18]

Pia Hadithi Bidh-‘ah (بضْعَةٌ) imetumika katika kuthibitisha, ulazima wa kuwatukuza Ahlul-Bait (a.s) [19] pamoja na kuthitisha mambo mengine kadhaa kama vile; kutokubalika shahidi wa mtoto kwa baba yake au kinyume chake, [20] kuharamishwa kuwaoa mama pamoja na mabinti wa mtu mwenyewe, [21] ulazima wa kuwaheshimu wazazi [22] pamoja na ruhusa ya kuzuru makaburi kwa wanawake. [23]

Jinsi ya Hadithi ya Bidh-‘ah (حديث البَضْعَة) ilivyotumika dhidi ya Imamu Ali (a.s)

Makala Asili: Hadithi ya posa Imam Ali wa binti ya Abu Jahli

Kwa mujibu wa baadhi ya riwaya, Hadith ya Hadithi ya Bidh-‘ah (بضْعَةٌ) inatokana na kisa cha Imam Ali (a.s) kumposa binti wa Abu Jahli; Kwa mujibu wa riwaya ya Ibnu Hambal (aliyefariki mwaka wa 241 Hijiria) kwamba; Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Zubeir akisema: Pale Ali (a.s) alipozungumza kuhusu kumuoa binti ya Abu Jahli, kisha habari hizo zikamfikia Mtume, ndipo Mtume (s.a.w.w) aliposema: (اِنّما فَاطِمَةُ بَضْعَةٌ مِنِّی یُوذینی ما آذَاها ; Kwa hakika Fatima ni kipande cha mwili wangu, kinaniudihi chenye kumuudhi yeye). [24] Hadithi hii imenukuliwa kupitia ibara tofauti zilizotajwa katika vyanzo tofauti. [25]

Mwanatheolojia wa Kishia Sayyid Murtadha (aliyezaliwa mwaka 436 na kufariki mwaka 355 Hijiria) amezihisabu riwaya hizi kuwa ni riwaya za uwongo. [26] Pia kwa mujibu wa Hadithi kutoka kwa Imam Swadiq (a.s), Hadithi hii ni ya uwongo. [27] Abu Hurairah ni mmoja wa wapokezi wa hadithi hii, ambaye anatuhumiwa kughushi Hadith. [28] Pia, Hussein Karabisi na Miswar bin Mahramah Al-Zuhari, ni miongoni mwa wasimuliaji wengine wa riwaya hii, ambaye vitabu vya elmu al-rijal vimemhisabu yeye kuwa dhaifu asiye aminika katika upokezi wa Hadithi, kwa hiyo riwaya zao hazikubaliki. [29] Sayyied Murtadha amemuhisabu Karabisi kuwa ni adui wa Ahlul-Bait (a.s). [30] Kutoka na mtazamo wake; Kama kisa hicho ni cha kweli, basi kwa nini Banu Umayya na wafuasi wao hawakuitumia kisa hicho kama kisingizio cha kuharibu sura ya Imamu Ali (a.s) katika kufikia malengo yao. [31]

Ja'afar Murtadha Amili (aliyefariki mwaka wa 1441 Hijiria), ambaye ni mmoja wa watafiti wa historia ya Kiislamu, hakutosheka na kuzikadhibisha tu ripoti za Imamu Ali (a.s) kumposa binti ya Abi Jahli bali kapingana nazo na kusimamisha dalili 13 za kuikataa hadithi hii.[32]

Rejea

Vyanzo