Nenda kwa yaliyomo

Haamidaati

Kutoka wikishia

Haamidaati (Kiarabu: الحامدات) ni Sura maalumu za Qur’ani ambazo ni; Fatiha, An'am, Kahf, Saba na Fatir, ambazo neno lake la mwanzo huanza na Alhamdulillah. [1] Sura hizi pia zinajulikana kwa jina la «Haa-aati», «Hamdu», na «Maqaasiri al-Qur’ani». [2] [Maelezo 1] Inasemekana kuwa mada shirikisho ya pamoja ya Sura hizi ni Tawhid, Unabii, na Ufufuo (Wahyi), ambayo ni misingi mikuu ya dini ya Uislamu. [3] Suyuti katika kitabu chake kiitwacho Al-Itqani akinukuu kutoka kitabu cha «Jamalu al-Qurraa» amesema kuwa; katika Qur’ani kuna nyanja «ميادين» (wingi wa neno uwanja «میدان»), mabustani «بساتين» (wingi wa bustani بُستان), maqaasir «مقاصير», maharusi «عرائس» (wingi wa harusi), dabaiji «ديابيج» (wingi wa hariri ambayo inatokana na neno «diba»), na mabustani «و رياض» (wingi wa bustani). Nyanja za Qur’ani ni Sura zinazianza na «Alif Lam Miim». Bustani za Qur’ani ni Sura zinazianza na «Alif Lam Raa». Maqasir ya Quran ni Sura za Hamidat, na maharusi wa Qur’ani ni Sura za Musabbihati, na hariri za Quran ni Sura za Haamiimaati, na mabustani ya Quran ni Sura za Mufassalati. [4]

Maelezo

  1. Maqaasir ni wingi wa neno «maqsurah» linalomaanisha ukumbi, sebule, au roshani. Rejea Farhangnaame ‘Ulume Qur’ani/ Chapa ya Daftare Tabliighat Islami/ Uk. 3442

Rejea

Vyanzo