Aya ya Fitra

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Fitra)
Aya ya Fitra

Aya ya Fitra (Kiarabu: آية الفطرة) ambayo ni Aya 30 ya Surat al-Ruum: Inaonyesha wazi ya kwamba mwanadamu ana asili ya kiroho ni maumbile ya kufungama na dini. Kulingana na maoni ya wafasiri wa dini ya Kiislamu, ni kwamba; dini ya Kiislamu ni dini imefumwa kwa mfumo wa sheria ziendazo sawa na matakwa ya fitra (dhati na asili) ya mwanadamu. Katika kitabu cha majma’u al-Bayani, neno hanifa «حَنیفاً» lililotumika katika Aya hiyo limefasiriwa likiwa na maana ya kuwa imara katika dini; lakini Sayyid Muhammad Hussain Tabataba’i amelifasiri kuwa kwa maana ya kuwa katika hali ya wastani katika dini.

Baadhi ya Hadithi zimeitambua tawhidi kuwa ni mfano halisi wa fitra ya mwanadamu, na baadhi ya Haidthi nyengine zimesema kwamba; mifano halisi ya fitra ya mwanadamu ni kumtambua Mwenye Ezi Mungu, Uislamu, na Wilaya (Kuwatambaua na kuwakubali Maimamu 12 wa Kishia) kuwa ni miongoni mwa maumbile asili (fitra) ya mwanadamu. Wanazuoni kama vile Allamah Tabatabai na Jawadi Amuli wakitegemea Aya ya Fitra, wanachukulia kwamba njia ya uongofu ni moja tu kwa watu wote.

Matini na Tafsiri ya Aya

فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا فِطْرَةَ اللَّهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّهِ ذَلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ


Basi elekeza uso wako kwenye dini ya haki, ambayo ndiyo mfumo wa fitra ya Mwenye Ezi Mungu aliyeumba watu kwayo. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenye Ezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyo thabiti, lakini watu wengi hawafahamu.



(Surat Ar-Rum: 30)


Kuielekea Dini Kiukamilifu

Kwa mujibu wa imani ya Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai; Aya ya fitra inaelezea tija na matokeo yanayotokana na Aya zilizotangulia. Anaandika akisema: “Kwa kuwa katika Aya zilizotangulia, Mwenye Ezi Mungu amethibitisha kufufuliwa na kuhisabiwa kwa watu katika ulimwengu wa akhera, hivyo basi Aya hii inatoa natija kwamba, mtu hatakiwi kumgeukia Mwenye Ezi Mungu, na ni lazima awe ni mwaminifu kwa dini ilioletwa na Mola wake; kwa sababu ni dini hiyo tu inayolingana na uumbaji wake wa Kiungu alioumbwa nao mwanadamu”. [1] Katika tafsiri Noor, imeelezwa kuwa; Aya hii inatufahamisha kwamba, binadamu kimaumbile ni kiumbe mwenye mwelekeo wa kufungamana na dini na ni mpenzi wa haki, na Mwenyezi Mungu amemuumba kwa mfumo wa kufahamu na kupenda haki. [2]

Maana ya Neno Hanifa «حَنیفاً»

Katika tafsiri ya Majma al-Bayan, Tabarsi amelifasiri neno “Hanifa «حَنیفاً» kwa maana ya kuwa na msimamo imara katika dini; yaani kujidhatiti na kuto geuka na kuelekea katika dini nyingine. [3] Ila kwa mujibu wa welewa wa Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai, neno hili linabainisha jinsi ya kutekeleza dini, na kutokana na maana yake ya kilugha, maana yake ni kuwa na msimamo wa wastani katika utekelezaji wa dini ya Mwenye Ezi Mungu. [4]

Tafsiri ya Neno «Fitra»

Kulingana na yaliokuja katika tafsiri ya Majma’u al-Bayani, maana ya neno «fitra» ni Tawhidi na dini ya Kiislamu ambayo watu wameumbwa kwa malengo ya kuitambua na kushikamana nayo. Kuna Hadithi ilionukuliwa kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) akisema kwamba: “Kila mtu huzaliwa kulingana na fitra (ya Tawhidi) mpaka pale wazazi wake wanapombadilisha na kumfanya ima awe Myahudi, Mkristo au Mmajusi (Mzoroastro).” [5]

Katika hadithi nyingi za Kishia, fitra imefasiriwa kama ni Tawhid; [6] lakini katika baadhi ya mifano iliotolewa kuhusiana na fitra, pia neno hili limepewa maana ya; kutambua Mungu, Uislamu na Wilaya (Uongozi wa Ahlul-Bait). [7]

Bwana Zurara amenukuu riwaya kutoka kwa Imamu Baqir (a.s), akisema kwamba; maana ya «فِطْرَتَ اللَّهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْها» (Umbile la Mwenye Ezi Mungu alilowaumba watu kwalo), inamaanisha kwamba, Mwenyezi Mungu aliwaumba watu kwa mfumo wa kumtambua Yeye, vinginevyo watu wasingeze kujua ni nani Mola wao mwenye kuwapa riziki. [8] Katika kitabu cha Manaqibu Ibnu Shahri Ashub, pia imenukuliwa kutoka kwa Imamu Ridha (a.s) akimnukuu Imamu Sadiq (a.s) akisema kwamba; maana ya msemo huo ni Tawhid, Utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), na Wilaya ya Imamu Ali (a.s) (Ukhalifa wa Imamu Ali). [9]

Njia ya Uongofu ni Moja Tu

Allama Tabataba’i na Jawadi Amuli wakitoa ufafanuzi kuhusiana na ibara isemayo; Fitrah ya Allah ambayo amewajenga watu kwayo «فِطْرَتَ اللَّهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْها» wamesema kwamba; kuna njia moja tu ya ya kufuzu kwa wanadamu. [10] Wanazuoni hawa wanaamini kwamba; kulingana na ibara hii, mwanadamu ana asili maalum ya kimaumbile, yaani uwepo wake umejengeka kwa namna maalum ambayo inamwelekeza kwenye njia maalum ya kufikia lengo lililokusudiwa katika kuumbwa kwake. [11] Pia hali iko vivyo hivyo kuhusiana na viumbe wengine, kwani kulingana na Aya za Qur'ani, viumbe vingine pia vinaongozwa kuwekwa kwenye lengo maalumu lililokusudiwa katika kuubwa kwao. Mwenye Ezi Mungu katika Qur’ani anasema: رَبُّنَا الَّذِي أَعْطى‏ كُلَّ شَيْ‏ءٍ خَلْقَهُ ثُمَّ هَدى‏» [12]» (Mola wetu ni Yeye aliyeumba kila kitu kwa mujibu wa umbo lake, kisha akaongoza). [13]

Kwa upande mwingine, kwa kuzingatia kwamba wanadamu wote ni aina moja na wana sifa za jumla na za paomja zinazofanana, hivyo basi hakuna njia zaidi ya moja ya kufuzu kwao. [14]

Maudhui Zinazo Husiana

Rejea

Vyanzo