Nenda kwa yaliyomo

Dua ya saba ya Sahifa Sajjadiyya

Kutoka wikishia
Dua ya Saba ya Sahifa Sajjadiyya
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Ahmad Nayrizi, iliyoandikwa mnamo 1145 AH.
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Ahmad Nayrizi, iliyoandikwa mnamo 1145 AH.
Mtoaji / MwandishiImamu Sajjad (a.s)
LughaKiarabu
Msimulizi / MpokeziMutawakkil ibn Harun
MadaKuomba msaada kuondolewa huzuni, shida na tabu za dunia.
ChanzoSahifa Sajjadiyah
Tafsiri kwa Lugha yaKifarsi

Dua ya Saba ya Sahifa Sajjadiyya (Kiarabu: الدعاء السابع من الصحيفة السجادية) Ni mojawapo ya dua maarufu kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s) ambayo husomwa wakati wa shida, maafa na wakati wa huzuni. Dua hii inaashiria kwamba shida zinawezekana kutatuliwa kwa mkono wa Mungu na kwamba sababu za kurahisisha maisha zinaweza kupatikana kwa uwezo wa Mungu Mwenyewe. Imamu Sajjad (a.s) katika dua hii anamwomba Mungu afungue fundo na mizongo ya maisha. Pia, Imamu wa nne katika dua hii aameashiria kwamba viumbe vyote chini ya utiifu wa Mungu. Pia Imamu Sajjad (a.s) katika dua hii anakiri udhaifu wa kila kiumbe mbele ya mamlaka ya Mwenye Ezi Mungu, pia anakiri kutokuwepo kwa msaidizi na mtu ambaye anaweza kumwokoa au kumsaidia yule aliye dhalilishwa na Mwenye Ezi Mungu amemdhalilisha.

Dua hii Inapendekezwa kusomwa kwa ajili ya kuondoa shida, ambapo inasharitishwa kusomwa kwa adabu na sharti maalum, nazo ni kama vile kusomwa baada ya sala ya asubuhi na katikati ya machomozo mawili (kuchomoza kwa alfajiri na kuchomoza kwa jua).

Dua ya saba ya Sahifa Sajjadiyya imefasiriwa kwa lugha ya Kiajemi katika tafsiri kadhaa za Sahifa Sajjadiyyah, kama vile Diyaru Aashiqaan cha Hussein Ansariyan, pia imechambuliwa kupitia lugha ya Kiarabu kwenye kitabu Riyad al-Salikin cha Sayyid Ali Khan Madani.

Thamani na Nafasi Yake

Dua ya Saba ya Sahifa ya Sajjadiyya ni dua ambayo Imam Sajjad (a.s) aliiomba katika wakati mgumu au wakati wa kushuka kwa majanga makubwa na wakati wa huzuni, ili kuondoa huzuni na shida hizo. Imamu wa nne katika dua hii ameonyesha kwa njia ya nyuma ya pazia nini jukumu la mja wakati wa kutokea kwa majanga.[1] Ayatullah Khamenei, kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, pia aliagiza kusoma dua hii, ili kuondoa virusi vya COVID-19 vilivyokuwa vimeenea nchini Iran na nchi nyingine mnamo Februari 2019. [2]

Mafunzo Yaliomo Ndani Yake

Mafunzo ya Dua ya Saba ya Sahifa ya Sajjadiyya yameorodheshwa kama ifuatavyo:

  • Mungu ndiye anayefungua fundo la kila gumu na shida.
  • Viumbe vyote ni dhaifu na viko chini amri na mamlaka ya Mwenye Ezi Mungu.
  • Utoaji wa visahilishaji vya maisha na sababu zote za maisha ni kupitia fadhila na rehema za Mwenyezi Mungu.[3]
  • Mtiririko na mkondo mzima war Qadhaa na Qadar hutimia kupitia uwezo wa Mwenye Ezi Mungu.
  • Matakwa ya Mwenyezi Mungu ni hatima isiyo epukika.
  • Mwenyezi Mungu ndiye kimbilio la mwanadamu dhidi ya mitihani migumu mbali mbali.
  • Udhaifu wa wote mbele ya uwezo na nguvu za Mwenyezi Mungu.
  • Ombi la kufunguliwa milango ya faraja kutoka kwa Mola Mtakatifu.
  • Ombi la kuonja utamu wa kujibiwa dua.[4]
  • Dua kwa ajili ya kujali na kutilia maanani suala la kufanya amali za wajibu na kujali amali za sunna.
  • Mtiririko wa kila kitu yapo chini ya mamlaka ya Mwenye Ezi Mungu.
  • Yeyote yule aliye dhalilishwa na Mwenye Ezi Mungu, huyo hatakuwa wa kumsaidia.[5]

Jinsi ya Kusoma Dua Hii

Katika baadhi ya maandiko, njia ya kusoma hitima ya dua ya saba ya Sahifa ya Sajjdiyya imenukuliwa kama ifuatavyo:

Mfumo wa kwanza

Muda wa kuanza kwake inatakiwa kuanzia siku ya Jumapili na kudumisha kwa muda wa siku thelathini, kila siku dua hiyo inatakiwa kusomwa mara kumi. Baada ya kumalizika kwa dua, inatakiwa msomaji aseme: Yaa Rabbi Yaa Rabbi hadi pumzi zake zimalizike (zifikie kikomo), kisha asujudu na amwombe Mola wake ombi lake.

Mfumo wa pili

Katika kukamilisha hitima ya mzunguko wa dua hii: Inatakiwa kabla ya mtu kuanza dua yake, kwanza anatakiwa amsalie Mtume Muhammad na Aali zake mara kumi, pia kabla na baada ya dua, aseme mara arobaini: Yaa Allahu. Dua hii inatakiwa kusomwa katikati ya kuchomoza kwa alfajiri na kuchomoza jua, na baada ya sala ya al-Fajiri. Moja ya masharti ya dua hii ni kujiepusha na haramu na kuto kula kupita kiasi kwa muda wa siku thelathini. Pia ni lazima achunge tohara na akae akiwa ameelekea qibla, na la muhimu zaidi ni kuuhudhurisha moyo katika amali hii.[6]

Vitabu vya Uchambuzi wa Dua ya Saba

Ndani ya vitabu chambuzi na maelezo kuhusiana na Sahifa ya Sajida, pia ndani yake mmetolewa uchambuzi na maelezo kuhusiana na “Dua ya Saba ya Sahifa ya Sajida”, ndani ya uchambuzi huu pia maneno yake magumu yamefafanuliwa ndani yake. Dua hii imechambuli na kufasiriwa katika vitabu kama vile; Diyaru Aashiqaan,[7] Shuhudu wa Shenakht,[8] Riyadhatu al-Salikin[9] na fi Dhilali Sahifatu al-Sajjadiyya[10] pia imechambuliwa kwenye kitabu cha Faidhu Kashani kijulikanacho kwa jina la Ta’aliqatu ala al-Sahifati al-Sajjadiyya.[11]

Matini na Tarjama Yake

Maandishi
Maandishi na Tafsiri
Tafsiri

وَ کانَ مِنْ دُعَائِهِ علیه‌السلام إِذَا عَرَضَتْ لَهُ مُهِمَّةٌ أَوْ نَزَلَتْ بِهِ، مُلِمَّةٌ وَ عِنْدَ الْکرْبِ

یا مَنْ تُحَلُّ بِهِ عُقَدُ الْمَکارِهِ، وَ یا مَنْ یفْثَأُ بِهِ حَدُّ الشَّدَائِدِ، وَ یا مَنْ یلْتَمَسُ مِنْهُ الْمَخْرَجُ إِلَی رَوْحِ الْفَرَجِ

ذَلَّتْ لِقُدْرَتِک الصِّعَابُ، وَ تَسَبَّبَتْ بِلُطْفِک الْأَسْبَابُ، وَ جَرَی بِقُدرَتِک الْقَضَاءُ، وَ مَضَتْ عَلَی إِرَادَتِک الْأَشْیاءُ.

فَهِی بِمَشِیتِک دُونَ قَوْلِک مُؤْتَمِرَةٌ، وَ بِإِرَادَتِک دُونَ نَهْیک مُنْزَجِرَةٌ

أَنْتَ الْمَدْعُوُّ لِلْمُهِمَّاتِ، وَ أَنْتَ الْمَفْزَعُ فِی الْمُلِمَّاتِ، لَا ینْدَفِعُ مِنْهَا إِلَّا مَا دَفَعْتَ، وَ لَا ینْکشِفُ مِنْهَا إِلَّا مَا کشَفْتَ

وَ قَدْ نَزَلَ بی‌ یا رَبِّ مَا قَدْ تَکأَّدَنِی ثِقْلُهُ، وَ أَلَمَّ بی‌مَا قَدْ بَهَظَنِی حَمْلُهُ

وَ بِقُدْرَتِک أَوْرَدْتَهُ عَلَی وَ بِسُلْطَانِک وَجَّهْتَهُ إِلَی

فَلَا مُصْدِرَ لِمَا أَوْرَدْتَ، وَ لَا صَارِفَ لِمَا وَجَّهْتَ، وَ لَا فَاتِحَ لِمَا أَغْلَقْتَ، وَ لَا مُغْلِقَ لِمَا فَتَحْتَ، وَ لَا مُیسِّرَ لِمَا عَسَّرْتَ، وَ لَا نَاصِرَ لِمَنْ خَذَلْتَ

فَصَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ افْتَحْ لِی یا رَبِّ بَابَ الْفَرَجِ بِطَوْلِک، وَ اکسِرْ عَنِّی سُلْطَانَ الْهَمِّ بِحَوْلِک، وَ أَنِلْنِی حُسْنَ النَّظَرِ فِیمَا شَکوْتُ، وَ أَذِقْنِی حَلَاوَةَ الصُّنْعِ فِیمَا سَأَلْتُ، وَ هَبْ لِی‏ مِنْ لَدُنْک رَحْمَةً وَ فَرَجاً هَنِیئاً، وَ اجْعَلْ لِی مِنْ عِنْدِک مَخْرَجاً وَحِیاً

وَ لَا تَشْغَلْنِی بِالاهْتِمَامِ عَنْ تَعَاهُدِ فُرُوضِک، وَ اسْتِعْمَالِ سُنَّتِک

فَقَدْ ضِقْتُ لِمَا نَزَلَ بی‌یا رَبِّ ذَرْعاً، وَ امْتَلَأْتُ بِحَمْلِ مَا حَدَثَ عَلَی هَمّاً، وَ أَنْتَ الْقَادِرُ عَلَی کشْفِ مَا مُنِیتُ بِهِ، وَ دَفْعِ مَا وَقَعْتُ فِیهِ، فَافْعَلْ بی‌ذَلِک وَ إِنْ لَمْ أَسْتَوْجِبْهُ مِنْک، یا ذَا الْعَرْشِ الْعَظِیمِ

وَ کانَ مِنْ دُعَائِهِ علیه‌السلام إِذَا عَرَضَتْ لَهُ مُهِمَّةٌ أَوْ نَزَلَتْ بِهِ، مُلِمَّةٌ وَ عِنْدَ الْکرْبِ
Na miongoni mwa dua zake Mtume (a.s) alizokuwa akizisoma anapokuwa katika hali ngumu, anapopata tabu, au anapopata huzuni.
یا مَنْ تُحَلُّ بِهِ عُقَدُ الْمَکارِهِ، وَ یا مَنْ یفْثَأُ بِهِ حَدُّ الشَّدَائِدِ، وَ یا مَنْ یلْتَمَسُ مِنْهُ الْمَخْرَجُ إِلَی رَوْحِ الْفَرَجِ
Ewe ambaye kupitia kwake yeye fundo la dhiki hufunguliwa, Ewe, ambaye kupita kwake yeye ukali wa dhiki unakua butu, na Ewe, aombwaye katika kutafuta mlango wa kutoka katika dhiki na kuelekea katika roho ya faraja.
ذَلَّتْ لِقُدْرَتِک الصِّعَابُ، وَ تَسَبَّبَتْ بِلُطْفِک الْأَسْبَابُ، وَ جَرَی بِقُدرَتِک الْقَضَاءُ، وَ مَضَتْ عَلَی إِرَادَتِک الْأَشْیاءُ.
Magumu yamedhalilika na kuinamisha shingo mbele ya mamlaka yako, na sababu zimesahilika kwa huruma zako, na hatima za makadirio zimeshika mkondo wake, na mambo yametokea kulingana na matakwa yako.
فَهِی بِمَشِیتِک دُونَ قَوْلِک مُؤْتَمِرَةٌ، وَ بِإِرَادَتِک دُونَ نَهْیک مُنْزَجِرَةٌ
Viumbe vyote vimesimama kwenye mamlaka na amri zako bila ya haja ya kutumia lugha ya maneno, na kupitia matakwa yako vimejikanya bila haja ya kukanywa.
أَنْتَ الْمَدْعُوُّ لِلْمُهِمَّاتِ، وَ أَنْتَ الْمَفْزَعُ فِی الْمُلِمَّاتِ، لَا ینْدَفِعُ مِنْهَا إِلَّا مَا دَفَعْتَ، وَ لَا ینْکشِفُ مِنْهَا إِلَّا مَا کشَفْتَ
Wewe pekee ndiye uombwaye faraja katika matatizo, na wewe ndiye kimbilio pekee katika kukimbia kutokana na mabalaa, halikai kando (balaa lolote lile) isipokuwa lile uliepushalo, na wala halipambazuki isipokuwa lile ulipambazualo.
وَ قَدْ نَزَلَ بی‌ یا رَبِّ مَا قَدْ تَکأَّدَنِی ثِقْلُهُ، وَ أَلَمَّ بی‌مَا قَدْ بَهَظَنِی حَمْلُهُ
Nami ewe Mola wangu! Limenishukia balaa ambalo uzito wake umenielemea na kunitia mashakani, na balaa lake limenipa maumivu, ambapo kulivumilia kwake kunanidhiki.
وَ بِقُدْرَتِک أَوْرَدْتَهُ عَلَی وَ بِسُلْطَانِک وَجَّهْتَهُ إِلَی
Na uwezo wako balaa hili umeliingiza kwangu, na kwa mamalaka yako umelielekeza kwangu.
فَلَا مُصْدِرَ لِمَا أَوْرَدْتَ، وَ لَا صَارِفَ لِمَا وَجَّهْتَ، وَ لَا فَاتِحَ لِمَا أَغْلَقْتَ، وَ لَا مُغْلِقَ لِمَا فَتَحْتَ، وَ لَا مُیسِّرَ لِمَا عَسَّرْتَ، وَ لَا نَاصِرَ لِمَنْ خَذَلْتَ
Basi haukuna wa kulitoa ulilo liingiza, wala mwepushaji wa ulilolielekeza, wala mfunguaji wa ulilo lifunga, wala mfungaji wa ulilo lifungua, wala msahilishaji wa ulilo litia ugumu, wala mtoa nusra kwa uliye mdhalilisha.
فَصَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ افْتَحْ لِی یا رَبِّ بَابَ الْفَرَجِ بِطَوْلِک، وَ اکسِرْ عَنِّی سُلْطَانَ الْهَمِّ بِحَوْلِک، وَ أَنِلْنِی حُسْنَ النَّظَرِ فِیمَا شَکوْتُ، وَ أَذِقْنِی حَلَاوَةَ الصُّنْعِ فِیمَا سَأَلْتُ، وَ هَبْ لِی‏ مِنْ لَدُنْک رَحْمَةً وَ فَرَجاً هَنِیئاً، وَ اجْعَلْ لِی مِنْ عِنْدِک مَخْرَجاً وَحِیاً
Basi mshushie sala na salamu Muhammad na Aali zake, na unifungulie ewe Mola wangu mlango wa faraja kwa hisani zako, na uvunje mamlaka ya nguvu za huzuni zilizoko juu yangu kwa mbinu zako, na unifikishe kwenye dhana njema kuhusiana na yale niliyo yashitakia, na unionjeshe ladha ya jawabu katika maombi yangu, na unipe rehema na faraja njema kutoka kwako, na unijaalie njia ya uokovo ya haraka kutoka kwako.
وَ لَا تَشْغَلْنِی بِالاهْتِمَامِ عَنْ تَعَاهُدِ فُرُوضِک، وَ اسْتِعْمَالِ سُنَّتِک
Na usiniache kujishughulisha na matatizo na huzuzi, nisije kuacha kufuata maagizo yako na sunna zako.
فَقَدْ ضِقْتُ لِمَا نَزَلَ بی‌یا رَبِّ ذَرْعاً، وَ امْتَلَأْتُ بِحَمْلِ مَا حَدَثَ عَلَی هَمّاً، وَ أَنْتَ الْقَادِرُ عَلَی کشْفِ مَا مُنِیتُ بِهِ، وَ دَفْعِ مَا وَقَعْتُ فِیهِ، فَافْعَلْ بی‌ذَلِک وَ إِنْ لَمْ أَسْتَوْجِبْهُ مِنْک، یا ذَا الْعَرْشِ الْعَظِیمِ
Ewe Mola wangu Mlezi! Nimechoshwa na Nimepata tabu sana kutokana na mtihani ulio nishukia. Na moyo wangu umejaa huzuni kutokana na ya yale yaliyonipata. Nawe ndiye Mwenye uwezo wa kuliondoa balaa lililonikuta na kuniepushia mtihani ulio niangukia. Nakusihi kwa uwezo wako na nguvu zako niepushie mitihani hii, hata kama mimi sinastahili hayo kutoka kwako, Ewe Mwenye Kiti kikuu cha Enzi.

Na miongoni mwa dua zake Mtume (a.s) alizokuwa akizisoma anapokuwa katika hali ngumu, anapopata tabu, au anapopata huzuni.

Ewe ambaye kupitia kwake yeye fundo la dhiki hufunguliwa, Ewe, ambaye kupita kwake yeye ukali wa dhiki unakua butu, na Ewe, aombwaye katika kutafuta mlango wa kutoka katika dhiki na kuelekea katika roho ya faraja.

Magumu yamedhalilika na kuinamisha shingo mbele ya mamlaka yako, na sababu zimesahilika kwa huruma zako, na hatima za makadirio zimeshika mkondo wake, na mambo yametokea kulingana na matakwa yako.

Viumbe vyote vimesimama kwenye mamlaka na amri zako bila ya haja ya kutumia lugha ya maneno, na kupitia matakwa yako vimejikanya bila haja ya kukanywa.

Wewe pekee ndiye uombwaye faraja katika matatizo, na wewe ndiye kimbilio pekee katika kukimbia kutokana na mabalaa, halikai kando (balaa lolote lile) isipokuwa lile uliepushalo, na wala halipambazuki isipokuwa lile ulipambazualo.

Nami ewe Mola wangu! Limenishukia balaa ambalo uzito wake umenielemea na kunitia mashakani, na balaa lake limenipa maumivu, ambapo kulivumilia kwake kunanidhiki.

Na uwezo wako balaa hili umeliingiza kwangu, na kwa mamalaka yako umelielekeza kwangu.

Basi haukuna wa kulitoa ulilo liingiza, wala mwepushaji wa ulilolielekeza, wala mfunguaji wa ulilo lifunga, wala mfungaji wa ulilo lifungua, wala msahilishaji wa ulilo litia ugumu, wala mtoa nusra kwa uliye mdhalilisha.

Basi mshushie sala na salamu Muhammad na Aali zake, na unifungulie ewe Mola wangu mlango wa faraja kwa hisani zako, na uvunje mamlaka ya nguvu za huzuni zilizoko juu yangu kwa mbinu zako, na unifikishe kwenye dhana njema kuhusiana na yale niliyo yashitakia, na unionjeshe ladha ya jawabu katika maombi yangu, na unipe rehema na faraja njema kutoka kwako, na unijaalie njia ya uokovo ya haraka kutoka kwako.

Na usiniache kujishughulisha na matatizo na huzuzi, nisije kuacha kufuata maagizo yako na sunna zako.

Ewe Mola wangu Mlezi! Nimechoshwa na Nimepata tabu sana kutokana na mtihani ulio nishukia. Na moyo wangu umejaa huzuni kutokana na ya yale yaliyonipata. Nawe ndiye Mwenye uwezo wa kuliondoa balaa lililonikuta na kuniepushia mtihani ulio niangukia. Nakusihi kwa uwezo wako na nguvu zako niepushie mitihani hii, hata kama mimi sinastahili hayo kutoka kwako, Ewe Mwenye Kiti kikuu cha Enzi.

🌞
🔄

Rejea

  1. Mamduhi, Shuhud wa Shenakhte, 1388 S, juz. 1, uk. 425.
  2. Dua ambayo Kiongozi wa Mapinduzi alipendekeza kusoma wakati wa janga.(Persian).
  3. Matini ya Dua
  4. Matini ya Dua
  5. Ansarian, Diyar al-Asheqan, 1371 S, juz. 4, uk. 103-224
  6. Akbari Savji, Ab Hayat, 1392 S, Destur 186.
  7. Ansarian, Diyar Ashiqan, 1371 S, juz. 4, uk. 224.
  8. Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shenakhte, 1385 S, juz. 1, uk. 425-435.
  9. Hussaini Madani, Riyadh al-Salkin, 1409 AH, juz. 2, uk. 301-325.
  10. Mughniyyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 135-141.
  11. Faydh Kashani, Taaliqat Ala al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1407 AH, uk. 32-33.

Vyanzo

  • Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
  • Jazairi, Izu-Din, Sherh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Beirut, Dar al-Taaruf Lil-Matbuat, 1402 AH.
  • Khalji, Muhammad Taqi, Asrar al-Khamushan, Qom, Parto Khorshid, 1383 S.
  • Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
  • Dua ambayo Kiongozi wa Mapinduzi alipendekeza kusoma wakati wa janga.(Persian), Ofisi ya Kuhifadhi na Kuchapisha Kazi za Ayatollah Khamenei, Tarehe ya kuwekwa Machi 3, 2019.
  • Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
  • Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
  • Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
  • Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
  • Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
  • Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.